"Marriage is our last, best chance to grow up."

Monday, March 9, 2009

Hutazama kwa undani

Ni baby boy au baby girl?
Mwanaume hupenda kujua hilo! Mwanamke siku zote hujihusisha zaidi na undani wa kitu kuliko mwanaume.
Hebu fikiria pale mtoto akizaliwa, mwanaume kitu ambacho atauliza siku zote “je mtoto ni wa kiume au wa kike?”
Hicho ndicho kinachomhusu wakati huo na ndicho kinachomhusu kuhusu mtoto ambaye amezaliwa na mara nyingi akishajua hilo basi imetoka.

Lakini mwanamke atamshika (hold) mtoto wake na kumuangalia (chunguza) kila kila kitu ataanza na vidole vya mkono na miguuni, sura kamili ya mtoto na atajua mtoto anafanana na nani baba (au baba anayemjua yeye mwanamke), nywele za mtoto, midomo, pua, mguu, kila kitu kuhusu mtoto.
Mwanamke huwa sensitive hata kujua hisia mbalimbali za mtoto hadi aina ya mlio anaotoa akilia na zaidi anajiweka tayari kuwa mama na mlezi wa mtoto.

Fikiria suala la harusi, mwanaume anachojua ni kuwa na harusi then mke ndani ya nyumba, lakini mwanamke huwaza na kutaka kujua kila kitu kuhusiana harusi kama vile rangi za nguo za harusi, aina za pete na duka gani wanaweza kupata, aina za nguo, maua, wapi watafanyia sherehe za harusi, aina ya wageni, nani atafungisha ndoa na kwa nini, atataka kujua nani atatoa huduma ya chakula na chakula gani kiwepo nk.
Yupo tayari kuzunguka mji Mzima kujua ni duka gani atapata kile anataka kwa ajili ya harusi yake.
Naamini ukimwachia mwanaume kila kitu kuhusu harusi anaweza ku-ruin au screw siku yako muhimu duniani maana mwanaume anachosubiri ni kukuvalisha pete na mwanamke kuwa ndani ya nyumba.
Wapo wanaume ambao pia wapo makini sana na details za kila kitu ila wanawake wao ni wengi zaidi.

Ukinunua gari mwanamke atataka kujua ni rangi gani. Ingawa mwanaume anaweza kuona rangi ya gari ni rangi tu muhimu ni aina ya gari linalodumu.

Pia wanawake hukumbuka sana mambo yote yanayohusiana na kalenda, kama vile birthday, anniversary na appointments.
kama ni mwanaume ni vizuri kukumbuka siku maalumu za maisha yako na ya mpenzi wako kwani ukijisahau anaweza kuhisi humjali.

Hata mkishaoana mwanamke huwa bado anakumbuka undani wa mwanaume jinsi alivyokuwa anafanya wakati wa wachumba au wakati unafanya juhudi za kumpata, anakumbuka siku amekutana na wewe mwanaume, anaweza kukwambia hata shati ulilokuwa umevaa, kiatu na hata mahali na mpangilio wa vitu ulivyokuwa sehemu mlipokutana mara ya kwanza.

Anakumbuka sana jinsi ulivyokuwa unamkumbatia na kumpa sifa zote kwamba yeye ni mwanamke bora duaniani na hakuna kama yeye.
Anakumbuka sana ulivyokuwa unamsifia mbele za rafiki zako na kila aina ya maneno matamu ulikuwa unamwambia ndiyo maana sasa anashangaa mbona upo hivyo.

Kumbuka mwanamke na mwanaume ni tofauti na hizi tofauti ndizo zinatufanya tuwe na mahusiano mazuri ya ya kudumu na yanayoridhisha kiroho, kimwili na kiakili na pale tunapojisahau ndipo tunarudisha nyumba maendeleo ya kukua kwa mahusiano yetu na matokeo yake kila mmoja anaanza kushangaa vipi upendo mbona unapoa.

Pia kumbuka vitu vidogo sana ambavyo zamani ulikuwa unafanya ni muhimu sana nab ado unahitaji kufanya tena na tena bila kuacha.
Upendo daima!

2 comments:

Anonymous said...

kaka lazarua naomba uliza, hivi kwanini wanaume wengi wanapenda watoto wa kiume? mi nilidhani sisi tu tunaoishi afrika tu, kumbe hata mataifa ya magharibi pia, mimi mume wangu ni african american nakumbuka wakat tunapanga khs watoto nikamuuliza unapenda tuzae wangapi akajibu alaf akasema wa kiume wa kwanza nikasema moyoni heeeh ina maana hii tabia sio tu ya ktz hata USA na Kwingineko ipo?

wanaume tusaidieni kwanini mnapendelea sana watoto wa kiume?

Virginia

Lazarus Mbilinyi said...

Mmmm!
Kwa kweli binafsi naamini mtoto wa kiume au wa kike wote ni watoto tu na tuntakiwa kumshukuru Mungu, hata hivyo tukikaa kijiweni na kuanza kuulizana wanaume wengi huja na jibu kwamba mtoto wa kiume huendeleza familia kwa maana kwamba ataendeleza jina la ukoo kwani mtoto wa kike akiolewa basi na jina la ukoo linakufa.
Pia wanaume wengi hujisikia vizuri kuwa na mtoto wa kiume kwa maana kwamba kuwa na mwanaume ambaye atamlea na kuwa kama yeye.
Hata hivyo hili suala nchi kama India ni gumu sana kwani mwanamke akizaa mtoto wa kike huweza hata kupoteza maisha acha kupoteza ndoa.

Upendo daima