"Marriage is our last, best chance to grow up."

Thursday, March 5, 2009

Kabla hujaolewa!

Ndege wa tabia moja huruka pamoja! Ujana ni fahari pia ni wakati wa kufanya maamuzi muhimu kumchagua yule utatumia muda wako wote unaobaki duniani.
Pia mapenzi ni matamu, na kupendwa kutamu, wakati mwingine mapenzi huanza polepole na inafika siku yanakuja yanakufagia miguu yote, hata kabla hujajitambua vizuri unajikuta tayari upo kwenye ndoa kupitia kasi ya ajabu kwa jina la "Love is Blind"

Ndoa ni kupenda, ni commitment ya maisha, kukubali ndoa maana yake ni kukubali kwamba upo tayari kutoa kila kitu na kijikabidhi kwa mtu mmoja tu maisha yako yote, ndoa ni ahadi na agano la kumpenda yeye sasa na hadi kifo kitakapo watenganisha.

Ndoa ni zaidi ya unavyojisikia (feelings) ni zaidi ya mguso unaoupata ndani ya nafsi yako, ndoa ni kuudhihirishia ulimwengu kwamba umechagua kumpenda mtu mmoja, maisha yako yote, na kabla hujaanza kuvuna unachopanda sasa ni vizuri kufikiria kwanza huku ukiwa na akili timamu ili usije siku ukamlaumu mtu hahaha nisikutishe hakuna kitu kitamu kama ndoa!

UMERIDHIKA NA TABIA YAKE?
Naamini mpenzi wako ni the sweetest, cutest, lovable, barafu la moyo wako, is a real honey na majina mengine mengi tu, anakupa raha na unajisikia hakuna mwanaume kama yeye duniani anayekupa ridhiko la moyo ila ni yeye tu, kweli uchumba ni mtamu, ukitaka chochote anakupa, anapenda akuone kila wakati.

Kabla hujafika mbali na kutoa maamuzi jaribu kufikiria kwanza kwa makini zaidi zile tabia ambazo unahisi hujaridhika nazo.
Unajifariji kwa kuwa anakupenda basi ukiolewa naye utambadilisha au ataacha tu.

Uzoefu unaonesha kwamba vitu vingi ambavyo unaona sasa ndiyo vinakuvutia kwake kama vile jinsi anavyoongea, jokes zake, n.k vinaweza kukupa raha kwa muda mfupi sana wakati huu lakini ukishazoena naye baada ya kuoana naye, utatamani awe na kitu kipya kitu ambacho kwake haitawezekana na wewe utaanza kuwa bored.

Utani na jokes ni raha kwa unaposikia kwa mara ya kwanza au kwa mtu unayekuwa naye kwa mara ya kwanza, ila akishazoeleka ukajua kila kitu kuhusu yeye inakuwa kwisha kabisa anakukinai.
Kama ni mwanaume mwenye utani na jokes basi inabidi uwe una develop new skills za jokes zako kila baada ya muda fulani kabla ya expire date.

Vile vitu umekuwa unavipenda kwake sasa vinaweza kuwa usumbufu miaka 2 ijayo.

Ni vizuri kuangalia tabia endelevu ambazo hata baada ya miaka 10, 15 au 20 bado kwako hazitaleta shida.

Wazo kuu ni kwamba angalia miaka 10 ijayo maisha na yeye yatakuwaje kama unaona yatakuwa supper basi ingia kichwakichwa maana hakuna shida ila ukihisi unaona mawingu please think twice!

Inawezekana anamwamini mama yake kuliko wewe mke mtarajiwa na amekwambia bayana linapokuja suala la maamuzi mama yake ndiye top,
Inawezekana amekuahidi kwamba yupo tayari kuacha dini yake kwa ajili yako, hata hivyo uwe makini kwani suala la dini ndilo linafanya watu wauane duniani,
Inawezekana anajua kuutwika na sasa ametulia kidogo anasubiri uingie ndani ya 18 na wewe umejifariji kwamba utambadilisha, mara nyingi baada ya kuingia kwenye ndoa wanawake ndio hubadilika.
Inawezekana anavuta sana sigara na kwa sasa anavuta sigara moja kwa siku kwa sababu anakupenda, kumbuka wote wanaovuta sigara ukiwauliza watakwambia wanataka kuacha kuvuta sigara, fikiria maana bedroom inaweza kuwa tray vipisi vya sigara zake.

Inawezekana unajidanganya eti anakupenda hivyo tabia zake mbovumbovu ataacha unajifariji tu au unawezekana ume-fall in love na image, au hisia zako (feelings) ambazo zimezikosa upendo wa mwanaume.

Ndoa si 50/50 wala 100/100 bali ni 150/150 yaani kujitoa kwa ajili ya mwenzako zaidi ya asilimia mia, kwamba umechagua kazi ya kumpenda huyo mwanaume hapa duniani yeye tu bila kujali amefanya nini.

Pia usikubali kuolewa kwa sababu ndugu zako wanakushauri kwamba uolewe au kwa sababu sasa unahisi mwili unawasha sana unahitaji mume wa kukuridhisha au kwa sababu rafiki zako wanakusema sana kwamba mbona huolewi.
Au kwa sababu kiongozi wako wa dini anasema uolewe, olewa kwa sababu ni wakati wako na kwamba umekubali mwenyewe baada ya kukaa na kufikiria kwa makini na kumkubali mwanaume huyo.
Kawaida dunia nzima inaweza kukushauri na kukusema hata hivyo mwamuzi wa mwisho ni wewe maana wewe ndiye utakaye kuwa na huyo mwanaume siku meli yenu ya ndoa itakapokuwa inapita kwenye kina kirefu cha maji wakati wa dharuba kali, usiwategemee wanadamu kwani ndivyo walivyo ni vigeugeu.

Zaidi omba Mungu akupe amani ya kweli na huyo mwanaume ili uwe na uhakika na uamuzi unaenda kuutoa.

“Marriage is a school in which the pupil learns too late.”

Kama hupo makini kuchagua partner mzuri wakati wa kuolewa basi hiyo sentensi inaweza kuwa ni ukweli mtupu.

9 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Swali:- sasa kama umeolewa na baadaye unaona huyu uliyeolewa naye siye. Aliyetakiwa uolewe naye amejitokeza je ni haki kumwacha yule uliyeolewa naye?

Lazarus Mbilinyi said...

Asante kwa swali zuri!

Inabidi turudi kwenye maana ya ndoa tena kwamba ndoa si ahadi tu bali ni agano kati yako, mumeo na Mungu hivyo basi kuachana hadi kifo kitakapowatenganisha.
Kuachana pia si jibu wala suluhisho zaidi sana ni kubadilisha shape ya mwanaume, size na kutafuta matatizo mapya makubwa zaidi.
Kila ndoa ambayo huwa inaonesha dalili za kuvunjika bado huwa kuna kuwa na uwezekano wa kuirudisha kwenye mstari ni wewe na mume ambaye unadhani si yeye tena kukaa pamoja na kuondoa tofauti na kusameheana na kuendelea na maisha.
Kuachana kuna maumivu makali kuliko kifo.
Inawezekana hata huyo unayesema amejitokeza ikafika siku naye ukachokana naye ile mbaya hadi kutamani kurudi kwa yule umeachana naye.
Ndiyo maana mkazo mkubwa ni kuwa makini pale unataka kuolewa kwanza kwani unaweza kufall in love na image ya mtu badala ya mtu mwenyewe na ukiwa ndani ya ndoa unakuja kugundua uliuziwa mbuzi kwenye gunia.

Upendo daima

Yasinta Ngonyani said...

Asante kwa jibu kakangu. siku njema na kazi au masomo mema.

ellycs said...

huyo anaye uliza hilo shwali , Hivi ukilala na ukaota kuwa unalala unatakiwa uamke mara mbili?

Anonymous said...

Na ww ELLYCS ulieuliza hilo swali, kwani ukilala na ukaota umelala utakuwa umelala mara ngapi?

Anonymous said...

NDOA, km ilivyo mikataba mingine inaweza kuvunjika. Msemo wa alicho kiunganisha Mungu hakiwezi kutenganishwa na binadamu ni kuelewa vibaya, kwani mungu ndiye anaefungisha ndoa? Hata kama anayefungisha ni kwa niaba yake Mungu basi huyo huyo aivunje kwa niaba yake.

Vinginevyo itakuwa ni kuishi kinyume na maumbile, mtu hampendani lkn mwalazimishwa kuishi pamoja.

Hii ni aina nyingine ya ufisadi na uvunjwaji wa haki za binaadam.

Lazarus Mbilinyi said...

Ukishaamini kwamba haki za binadamu zipo juu kuliko sheria na taratibu za aliyekuumba basi umeshachanganya mambo na umeshapoteza mwelekeo.
Pia unapomwambia mtu unampenda kwa hiari yako na kwamba unakubali kuishi naye halfu kesho unakuja kusema unalazimishwa kuishi na mtu ambaye humpendi lazima ubongo wako una matatizo yanayohitaji nguvu zaidi ya zile za haki za binadamu ili kuweza kujua unaenda kinyume na maumbile.

Kabla ya kumpenda mtu na kumpa ahadi fikiria kwanza ili usije singizia haki za binadamu!

Upendo daima

Anonymous said...

ndoa ni paradise na si ndoano kama wengine wanavyodhani.ni commintment ya maisha na utaiona paradise kweli kweli pale mnapopendana haswa na kumfanya Yesu ndo kiongozi wa ndoa.yani Yesu ni kila kitu jamani.

Ms GBennett

Lazarus Mbilinyi said...

Ms GBennett,
Hapo umeongea point ya maana, unavyozidi kumjua Yesu na kuishi sawasawa na mapenzi ya Mungu ndoa huwa imara na raha zaidi, ni kweli kuna siri kubwa kwa ndoa zilizo katika Kristo na hakuna kitu kizuri duniani kama ndoa.
Mungu akubariki sana