"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, March 18, 2009

Katika afya njema na Ugonjwa!

Nilienda Muhimbili hadi siku ya mwisho wake! Ndoa ni kazi na wakati mwingine huweza kuwa kazi nzito nay a ziada.
Watu wengi hukumbana na wakati mgumu kwenye ndoa wakati fulani inawezekana hata wewe msomaje upo kwenye wakati mgumu sana wa ndoa yako, hata hivyo swali gumu ambalo linahitaji majibu ni
je, mume wako au mke wako anapokuwa amepata tatizo kubwa la kiafya kwa mfano hawezi kushiriki tendo la ndoa na wewe, hawezi kula mwenyewe, ameharibika sura kwa sababu ya ugonjwa au inabidi umbebe kwa ajili ya haja zote ndogo na kubwa,
Je, utakimbia?, utakaa naye?,
utamuomba Mungu?
Utaomba talaka?
Utakimbilia kwenye kifua cha mwanaume au mwanamke mwingine?
Au ndo wakati wako wa kujirusha?

Unaweza kuangalia maswali hayo na kujiuliza
hivi ni nani anaweza kufikiria kufanya vitu kama hivyo?”

Ukweli kuna mifano hai ambapo baada ya mmoja ya wanandoa afya kuzolota mwingine amefanya moja ya hayo hapo juu.

Wakati wanandoa wapo mbele ya kanisa na mbele ya mchungaji, kutoa viapo vyao mara nyingi ni rahisi sana kusema
“katika afya au ugonjwa nakubali”
au
‘Katika utajiri na umaskini nakubali”,
Wakati wote mna afya njema ni rahisi sana kukubali lakini wakati ukifika umaskini ukaanza kuwakalia kwa kasi ya ajabu, au mmoja afya kuzolota ndipo unaweza kukumbuka kile kiapo kilikuwa kina maana gani.

Moyo wangu ulikufa ganzi pale niliposikia mume wangu mpenzi ana Cancer na ipo hatua ya 4 ambayo hakuna dawa duniani.
Hadi hapa tulikuwa wanandoa wazuri na wenye raha pamoja na watoto wetu na tulipenda na kila mmoja kujisikia raha kwa mwenzake.
Mume wangu mpenzi alianza kuugua alianza kupunguza uwezo wa kwenda kufanya kazi kila siku hadi ikafika siku hawezi kula chakula mwenyewe hadi nimlishe huku amelazwa Hospitalini.
Wengine waliona ni udhaifu wa mume wangu kshindwa hata kula mwenyewe ila mimi nilimuona jinsi anavyojitahidi kutumia nguvu zake na ilishindikana, niliona anavyoteseka kwa maumivu hadi nikamuomba Mungu anipe nguvu kuvumilia kuona mume wangu katika ugonjwa namna hii.
Ilibaki mimi kuwa pembeni kwake usiku na mchana na kumuonesha mume wangu upendo mkuu na kwamba bado namuhitaji kuliko wakati mwingine hata kama alikuwa kwenye kitanda cha mgonjwa, Mungu aliniwezesha kunipa nguvu na ujasiri kuendelea kumuona mume wangu bado ni mume wangu hata kama alikuwa amebadilika sana kwa jinsi ugonjwa ulivyomharibu.

Ili niweze kupita katika haya yote nilikuwa namuomba Mungu ili niwe strong na anilinde kupita katikati ya kipindi hicho kigumu na Mungu alinionesha njia ya kumsaidia mume wangu na njia pekee ilikuwa ni mimi kuendelea kumhudumia “Kama Mume wangu” bila kujali alikuwa katika hali gani.
Alikuwa anaongea mama mmoja kwa uchungu na moyo wa machozi kuonesha kwamba kweli ndoa ni kujitoa na alikuwa anajua kuwepo wakati mumewe afya imezolota".

Swali Je utakuwa pamoja na mume wake au mke wako akiwa katika ugonjwa?

Jibu ni
Endelea kumpenda kama ulivyokuwa unampenda
Omba Mungu akupe uwezo na nguvu na uvumilivu,
Uwe pamoja nay eye,
Usikimbie,
Usikate tama,
Simama na toa upendo wako maalumu na
Mpende mpende na endelea kumpenda.

No comments: