"Marriage is our last, best chance to grow up."

Friday, March 6, 2009

Kumbe mnawaza chakula!

Picha kwa hisani ya Dada A. Hamidu Ripoti mpya imedhihirisha kwamba wanawake hutumia muda mwingi kufikiria kuhusu chakula kuliko sex na wanaume hutumia muda mwingi kufikiria kuhusu sex kuliko chakula.

Uchunguzi uliofanywa na tume ijulikanayo kama Weight Watchers, iligundua kwamba asilimia 58 ya wanawake huko Uingereza waliweza kufikiria kuhusu sex angalau mara 1o kwa siku na asilimia 70 walikiri kwamba walikuwa wanafikiria kuhusu chakula.
Pia ilidhihirika kwamba wanawake wengi walikuwa wanafikiria kuhusu body image (mwonekano wa miili yao) kama walikuwa hawafikiria (waza) kuhusu chakula.

Chakula ni complex issue kwa wanawake, hii haina maana sana wanwake wanakula sana bali inadhihirisha kwamba linapokuja suala la nini ale mwanamke huhusisha sana mawazo yake kuliko masuala ya sex ambapo mwanaume hujihisisha zaidi kufikiria.

Wanawake wengi hutumia muda mwingi kufikira chakula na body image kwa maana kwamba wengine hushinda njaa wakiogopa kunenepeana na kuonekana wana sura na miili ya ajabu.
Na wengine huishia kula chocolate tu au biscuits siku nzima wakiogopa kuwa na miili ya ajabu.

Source:
YellowBrix, The Scotsman

No comments: