"Marriage is our last, best chance to grow up."

Thursday, March 19, 2009

Mume kutoweka!

Kwa mwanamke ambaye alikuwa na ndoto za maisha bora ya ndoa kuondokewa na mume huleta maumivu makali sana, ni janga na hasara kubwa sana kwake.
Kuachwa mwenyewe ni badiliko kubwa katika maisha linalokuacha unahangaika mwenyewe na kujikuta ghafla unahusika kifedha, kulea watoto na kuendeleza taaluma kama si kuanza taaluma mpya.

Kama umepitia hali hii au unapitia hali hii ya kutalikiwa au mume kufa au mume kutoweka na kukuacha wewe na watoto au hata namna yoyote basi fahamu kwamba si nina yangu kutonesha kidonda ulichonacho bali ni katika kusaidiana ili uweze kukabiliana na kushinda na hatimaye kusimama katika changamoto hii kubwa uliyonayo.

Kumbuka hukuchagua iwe hivyo, na mume kutoweka si mwisho wa yote (end of the road), bado kuna uamuzi na chaguo wawezafanya.

Kila mwanamke mwenye ndoa ni mjane mtarajiwa hivyo hata kama una mume bado unahitaji kusoma na kuelewa na zaidi sana kujifahamu wewe ni nani na lolote laweza kutokea.

Inawezekana unajisikia kila kitu hakiendi, unajiona maisha ni shagalabagala, asilimia 80 ya uwezo wako na nguvu zako unatumia kutafakari emotions zako zilivyoharibiwa, ndiyo maana unajisikia kuwa confused na pia umepoteza self esteem or self image, hujiamini tena, marafiki wote wanakukwepa na unajiona mpweke na depressed and stressed.

Hata hivyo mara nyingi ukiachwa na mume marafiki wengi ulikuwa nao hukimbia na hilo linakufanya uwe mpweke na kukaliwa na msongo wa mawazo maana hata ndugu nao hawaoni thamani yako tena.
Umeshaanza kupata matatizo ya ajira na fedha pia.

Kumbuka kutoweka kwa mume wako hakujabadilisha kitu chochote ambacho Mungu alikuumba kuwa, thamani yako ipo palepale, kuachwa ni uamuzi wake si wako na hiyo haiwezi kuondoa kile unastahili kuwa (worth).
Bado wewe ni mwanamke tofauti (unique), mzuri, mrembo, mwanamke mwenye malengo, mipango kamili, mwenye talents na mawazo mazuri ya kukufanya kuwa vyovyote unataka kuwa, wewe ni mbunifu, mwanamke mwenye ndoto na mwenye uwezo wa kufanya vitu vya uhakika na tofauti duniani.

Nakutia moyo kwamba achana na mawazo yanayoongea ndani yako kwamba
Huna lolote, maisha kwisha, maisha hayana maana tena, hakuna mtu anakujali tena, unataka kukata tama”

Anza kuchukua hatua madhubuti kuwa na uamauzi mpya ili uweze kukua na kuendelea kusonga mbele katika mwelekeo sahihi na halisi kwa furaha na ujasiri.
“Hakuna mtu anaweza kuondoa furaha yako ndani yako hadi uamue mwenyewe”

Jaribu kufanya yafuatayo:
Pata ushauri kwa mtu unayemwamini kama vile mchungaji wako.
Andika kwenye karatasi hisia na kila linalokusumbua hata kama utaandika kwa machozi utajisikia kupata relief.
Kama huna ajira tafuta ajira/kazi yoyote ya kufanya hasa ile unapenda.
Weka malengo – long term or short term na anza kuyatimiza.

Kubali kwamba maisha yako ni changamoto na zitazame changamoto kwa jicho la opportunities kwako kukua kiimani na kupata new skills za maisha hata kuweza kufundisha wengine.
Kubali kwamba huna mume kwa sasa na kwamba usijiingize haraha haraka kutafuta mwanaume mwingine kuziba pengo unaweza kuingia kwenye moto mkali zaidi.

Katika jambo gumu kama hili Mungu anaweza kukurejesha kwenye matumaini na wewe kuwa strong baada ya kuvunjika moyo.

Tambua kwamba Mungu anaweza kutenda kazi hata katika giza nene, anaweza kujibu maombi yako na kukurejesha katika maisha mapya pole pole na baadae kujenga msingi imara kimaisha na kiroho ili kuweza kugundua baraka, hazina mpya na hata wewe kuwa mtu mpya kabisa.

Ubarikiwe na Bwana!

3 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Ni kweli pigo kubwa sana na maumivu makali sana kuondokewa na mume/mke. Na pia yeyote umpendaye.Kuna wengine wanaamua kuishi maisha ya ujane maisha yote.Sijui kama ni uamuzi mzuri

Lazarus Mbilinyi said...

Katika mapenzi ya kweli mmoja kutoweka ni maumivu makali sana, hata hivyo wengine kutokana na upendo alikuwa naye kwa aliyetoweka huamua kubaki kama alivyo kwani huamini hakuna binadamu anaweza kuwa sawa na mume/mke ambaye ametoweka, hata hivyo data nyingi zinaonesha wanawake ndo wanakuwa hivyo ila kwa wanaume wengine baada ya mwezi utasikia tayari kapata mke mwingine.
Bottom line hili jambo ni gumu mno!

Upendo daima!

Anonymous said...

Simply wish to say your article is as surprising. The
clarity for your publish is simply nice and i can think you are knowledgeable on this subject.
Fine together with your permission allow me to seize your feed to keep up to date with imminent post.
Thank you a million and please carry on the gratifying work.


Here is my homepage; Christian Louboutin Toronto