"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, March 25, 2009

Ni nguvu ya ajabu!

Baada ya kupendana watu huoana, hata hivyo wakati mwingine baada ya kuoana watu hupendana, usishangae muulize babu yako na bibi yako kama si baada ya kuoana ndipo walianza kupendana.

Hebu fikiria umewakutanisha watu wawili mume na mke, baada ya muda wataanza kila mmoja kutaka kumjua zaidi mwenzake.
Hata kama hawana uzoefu wowote kimahusiano, wataanza kila mmoja kuvutiwa na mwenzake kikemia, wasiwe na ukaribu wa damu, hakikisha unazidi kuwaweka pamoja kama mawe mawili unayoyatupwa sehemu hadi somethings happens.

Wataanza kila mmoja kujawa na mawazo na kuanza kumfikiria mwenzake, concentration itaongezeka kila mmoja kwa mwenzake kama tiger anayekimbiza kasungura.
Matokeo yake wataanza kutumia muda pamoja kuongea, kucheka na kutembea, wakati mwingine hawajui hata wakikutana watafanya kitu gani au kila mmoja anataka kufanya nini kwa mwenzake ila wanajisikia nguvu ya ajabu inayomfuta kila mmmoja kwa mwenzake.

Kila wanachofanya hakina maana, kitu chenye maana ni kuwa pamoja, wanaanza kujisikia nguvu ya ajabu ya kutaka kurukia kitandani pamoja, kila mmoja sasa anahamu ya kumgusa mwenzake, wanatamani kuanza kuziondoa layers moja badi nyingine kuanzia nguo walizovaa nje hadi za ndani, kila mmoja anataka kumjua mwenzake hahaha yaani hadi awe uchi wawe wawili tu.
Kila wakiwa karibu kila mmoja ni raha na kila mmoja anapenda kuendelea kugundua hazina za uzuri wa mwenzake, wanahangaika kuwa pamoja tu hata for doing nothing muhimu wapo pamoja.

Unaonaje ukiwasambaratisha na kila mmoja kwenda kuishi nchi tofauti kama vile Finland na Tanzania?
Kama wana mapenzi ya kweli hapo itakuwa disaster na watakuchukia maisha yao yote na baada ya dakika chache wataanza kuwa depressed kwa kila mmoja kumkosa mwenzake.

Romantic love is composed of some very strong human fibers, once formed, it is not easily broken.
(Song of Solomon 8:6 -7)


1 comment:

Yasinta Ngonyani said...

Nakubaliana nawe ni kweli kupenda ni "nguvu ya ajabu"! kazi kwelikweli