"Marriage is our last, best chance to grow up."

Monday, March 30, 2009

Nimeachwa, nimepata mwingine!

Mimi na wewe milele Duniani kuna wakati wa kutoa machozi, wakati wa kucheka, wakati wa kuhuzunika, wakati wa kufurahi, wakati wa kuchukiwa, wakati wa kupendwa, wakati wa kuponya nk.

Kama umewahi kupendwa na mwanaume au mwanamke then akakupiga chini bila sababu za msingi au kwa mgogoro mkubwa, ukweli hali hii huumiza na huweza kuzidi maumivu ya operation hospitalini kama si kuwa na mawazo hadi unanusurika kugongwa na magari barabarani.


Kupendwa kutamu na kuacha kuchungu !


Ni kawaida kujisikia huzuni, kuvunjika moyo, kujisikia hatia na hata kuwa na siku za machozi na hata kushindwa kufanya kazi kama kwenda kazini maana love is greater than faith and hope.


Ni kweli uliwekeza muda wako wote hata rasilimali zako kuhakikisha unampa umpendaye kile ambacho kinatoka ndani ya moyo wako, hata hivyo amekukimbia na kukuacha.


Ni kweli umeumizwa, umekasirishwa, hata unajiuliza una tatizo gani hata hivyo jambo la msingi ni kumshukuru Mungu kwamba sasa una nafasi ya kusahihisha makosa na kwamba alikuacha kabla ya kuwa ndoa hivyo una nafasi nzuri zaidi kufanya maamuzi ya kweli.

Wengine akishaachwa, kwa haraka anajiingizwa mahusiano na mtu mwingine ili kuziba pengo au nafasi iliyoachwa wazi moyoni na kuendelea kumlaumu aliyeachana naye kwamba ndiye alikuwa chanzo na sababu.

Kabla ya kuingia kwenye mahusiano mapya ni jambo la msingi kuwa makini zaidi kwani unaweza kuingia kwenye mahusiano mapya na ukagundua kwamba umefanya terrible mistake kuliko mara ya kwanza ukaishia kujuta zaidi nakujikuta umebadilisha sura, rangi, kimo na shape hata hivyo mwanaume au mwanamke ni yuleyule na tabia zake.

Data zinaonesha kwamba ukiwa na mahusiano na yakavunjika ukienda haraka unaweza kuishia kwa mtu wa aina ile ile na kuendelea kuumizwa zaidi.

Maswali mawili ya msingi kujiuliza kabla ya mengine ni kwanza je, nitawezaje kumpata mwingine ambaye hataniumiza kama yule wa kwanza?

Na pili je, nitawezaje kubadilika na kuwa mtu mwingine tofauti na nilivyokuwa mara ya kwanza kabla ya mahusiano kuvunjika?

Tunatakiwa kujifunza kutokana na mahusiano ya kwanza na kujua tulihusika vipi kusababisha mahusiano kushindikana au je ni kitu gani kinatakiwa kubadilisha?

Yafuatayo ni maswali ya kujiuliza kabla hujaingia kwenye mahusiano mapya
Je, nimekuwa na muda wa kutosha kuponya (heal) majeraha yangu kabla sijajiingiza kwenye mahusiano mapya?
Je, nimefahamu kwa nini mahusiano ya kwanza yalivunjika?
Je, nimebadilika katika tabia, mitazamo, maneno, kufikiria na mawazo yangu kabla ya mahusiano haya?
Je, nipo wazi na huru katika mahusiano haya ninayotaka kuanza?

Tumeshaongelea malengo ya baadae, dini, pesa?
Je, nataka kuanza mahusiano mapya kwa sababu ni mpweke au nataka kufanya naye mapenzi au namuhitaji sana kifedha, au ni mtu sahihi kwangu?

Je, nimemuomba Mungu?

4 comments:

Anonymous said...

kaka lazarus kwa kweli hii picha sio powa kabisa itoe kabisa kwa ushauri wangu.

Ms GBennett

Lazarus Mbilinyi said...

Dada GBennett,

Pole sana ukweli nilitaka kujua watu wakiona nyoka huogopa kiasi gani hasa nyoka mwenyewe vichwa viwili, hahaha inatisha!
Nimeiondoa naamini sasa utajisikia raha zaidi pamoja na wengine ambao wametishika kiasi cha kuogopa kurudi tena.

Niambie sasa huogopi?

Anonymous said...

sasa siogopi tena

asante kwa kuiondoa

Ms GBennett

Lazarus Mbilinyi said...

Hongera!

Nimefurahi kama huogopi tena.
Ubarikiwe

Lazarus