"Marriage is our last, best chance to grow up."

Tuesday, March 24, 2009

Sikujua kuna Upweke!

Binadamu si kisiwa!
Unahitaji watu ili ku-socialize na hatimaye kuondokana na upweke.
Pichani ni Kole, Gloria, Lilly, Emmanuel na Jody.Kujisikia upweke ni suala la wote, umeolewa, hujaolewa au umeoa au hujaoa.

Swali muhimu je upweke ni kwa wanawake peke yao?
Ukweli hata wanaume hujisikia upweke ingawa matokea ya upweke hutofautiana kwani mwanaume akishakuwa na mahusiano ya kijamii (social network) huweza kuondokana na upweke wakati mwanamke anaweza kuwa na mahusiano ya jamii (social network) na bado akawa na upweke emotionally.

Linapokuja suala la emotions wanawake ni sawa na barabara yenye njia 8 (8 lanes) wakati wanaume ni mfano wa barabara iliyotota inayoenda msituni (forest access road).

Pia jinsi tunavyowasiliana wanawake na wanaume ni tofauti, wanaume tupo direct to the point wakati wanawake hupendelea kuongea kunakoelewesha, kitu amacho automatically mwanamke akiongea na mwanaume hujikuta mpweke maana jamaa yupo mkatomkato tu.

Pia kama umeolewa inawezekana ndoa yako ipo kwenye stage ya repair, huwa tunajidanganya kwamba tukiolewa au kuoa basi kila kitu kitakuwa shwari kama mwindaji nyikani hakuna milima wala mabonde bali tambarare.
Hata tukikutana na matatizo badala ya kushambulia tatizo tunashambuliana wenyewe kwa nini tusiwe wapweke?
Kujua tatizo ni mtaji wa ushindi wa tatizo lolote katika ndoa.

Kawaida watu hukutana na upweke wa aina mbili ule wa kijamii (social) na ule wa tukuko (emotional)
Upweke wa kijamii hutokana na kukosa mtandano wa kijamii, kila mmoja anahitaji wmingine awe mwanaume au mwanamke pasipo suala la sex, hakuna mtu ni kisiwa kwamba hahitaji mwingine.
Wanawake ambao wapo active kijamii ni mara chache sana huwa na upweke wa kijamii, hata hivyo wapo wengine kutokana na kuwa na aibu, au kuwa wapya katika eneo jipya hawana mtandao wa marafiki na hujikuta wapweke.

Hivyo jambo la kwanza mahali popote ni kutengeneza mtandao wa marafiki ili kuondoa upweke wa kijamii.

Kwa upande mwingine upweke wa tukuko (emotions) ni upweke unaotokana na kukosa ukaribu wa kihisia katika mahusiano, hata kama upo socially active bado kuna nafasi ya ndani ambayo lazima ujazwe na mtu wako wa karibu mume umpendaye au mke umpendaye.
Ndiyo maana watu wanaweza kulala wanafanya party, lakini bado ndani yao asubuhi wakajikuta ni wapweke wa ajabu.

Pia kujenga emotional relationship ni ngumu kwani watu huogopa unaweza kujiachia kwa mwanaume au mwanamke then akaja akakuumiza (rejection factor) kwani lazima ujiweke wazi kwake ili muwe na mahusiano ya karibu kabisa.
Pia kumpata mtu ambaye anakufaa emotionally kuna hitaji kazi kubwa kumfahamu na zaidi chemistry ziendane.

Hata wanawake ambao wameolewa bado wakati mwingine hujikuta kwenye upweke wa kupindukia kwa sababu wanaume walionao bado hawajazi nafasi ile ya ndani ambayo mwanamke anahitaji kujisikia ili upweke umtoke.

Wanawake wengine ni wapweke kwa sababu hawapo wazi kwa waume zao na kwa kuwa wanaume kihisia ni tofauti na mwanamke basi huwa hawajui kwamba something is wrong ni ngumu mwanaume kusoma uso na kujua mwanamke anahitaji kitu gani kwenye mahusiano ingawa wengine wapo smart ila si wote.
Ni vizuri mwanamke ambaye ameolewa kuongea na mumewe jinsi anavyojisikia kwani kubaki kimya na kudhani kwamba mume atajua jinsi unavyojisikia na kwamba atajirekenisha huwezi jua ndo imetoka hiyo.
Siku njema....................................

1 comment:

Anonymous said...

Wow! thanks for this. Glory looks big, happy and cute