"Marriage is our last, best chance to grow up."

Tuesday, March 17, 2009

Wenye Wallet nzito!

Mwanaume akiwa na wallet kubwa basi wakiwa kwenye sita kwa sita mwanamke hufika haraka kileleni.
Je, ni kweli sex pleasure anayopata mwanamke ina uhusiano mkubwa na ukubwa wa wallet ya mzee ?
Je, ni kutafsiri kwamba mwanamke hupunguza uwezo wa kufika kileleni akiwa na mwanaume ambaye akilala naye bado anaendelea kuwaza shida ya pesa na jinsi ya kulipa bills na manunuzi ya vitu mbalimbali anavyohitaji?

Wanawake 1,534 huko China walifanyiwa utafiti (Chinese Health and Family Life Survey) wanawake 121 walikiri kufika kileleni kila wakati, 408 mara kwa mara, 762 mara chache na 243 hawakuweza kufika kileleni kabisa.
Hata hivyo iligundulika kwamba kuongezekana kwa kipato cha mwanaume kulikuwa na matokeo ya kuongezeka kwa mwanamke kufika kileleni.
Mwanaume alivyozidi kuwa na pesa mwanamke alifika haraka kileleni.

Hata hivyo utafiti wa aina hii umetoka matokeo yanayofanana si kwa wachina tu bali hata Ulaya na Amerika sijui hapa Afrika utafiti kama huu ukifanyika matokeo yatakuwaje.

Hata hivyo utafiti haokuonesha je, hawa wanawake wanaofika kileleni haraka kwa sababu mzee ana pesa furaha yao hudumu kwa muda gani?
au ni kuwadanganya wanaume waone mwanamke anajituma na kwamba ameridhika?

Hapa nahisi wanaume hudanganywa tu na mwanamke kwamba amefika kileleni ili atoe pesa.

Ila hata hivyo kuna kaukweli fulani ndani yake fikiria mwanaume ana pesa na amemwambia wakitoka hapo atamkabidhi funguo za gari, mwanamke akishafikiria jinsi atakavyoringa na usafafiri wake, kwa nini usifike kileleni!
Kazi kwelikweli!

No comments: