"Marriage is our last, best chance to grow up."

Thursday, April 30, 2009

Busu (2)

(Picha kwa hisani ya Makky) Ukweli busu ni kitu kinachoshangaza hasa kutokana na raha yake, wengi hufurahia sana kutoa na kupokea busu na bado tunakumbukumbu halisi za busu la kwanza lilivyokuwa.
Inawezekana na wewe ni moja ya wale wanaotafakari ladha ya busu la kwanza itakuwaje, Please relax kila jambo na wakati wake na majira yake.
JINSI YA KUBUSU KATIKA BUSU LA KAWAIDA

Angalia machoni kwa mpenzi wako:
Kwamba anategemea kumbusu lazima uelekeze macho yako kumuangalia yeye,
“Eyes are windows to personal soul”
Ukimwangalia usoni utajua kama anahisia (feelings and emotions) kwamba yupo tayari na anakupa ujumbe unaoelekeza kwamba yupo tayari for intimacy.
Pia kumuangalia usoni na kwenye macho yake ni kupeleka ujumbe kwamba unataka kumkaribia kwa ajili ya busu.

Tabasamu
Tabasamu kidogo hupendekeza unataka kufanya kitu, kama unataka kujua kama partner wako anataka kiss unapotuma ujumbe kwa kutabasamu utajua kama yupo tayari au la.
Kama aki-respond kwa tabasamu unaweza kuendelea na ukiona anaangalia chini au pembeni au hali fulani ya kuonesha hayupo tayari unaweza kuacha.

Karibia kabisa
Sasa unajua unataka busu, ni wakati kuelekea kwenye tendo lenyewe, karibia polepole na wakati unazidi kuwa close hakikisha huna papara

kama ni mwanaume unaweza sasa kumgusa au kumshika (hold) mwili wake au uso wake huku ukikaribia polepole na hapo atajisikia kama vile yupo tayari na comfortable.
Elekeza kichwa chako ili midomo iwe rahisi kukutana kwa ajili ya kubusu.
Pia hakukisha upo usawa wa partner wako ili wakati una busu iwe sawasawa usije ukamiss

Relax lips zako, Hakikisha lips zako zipo relax na hazipo tight kabisa na zake, kutanisha lips kwa ulaini kabisa bila nguvu
Hakikisha lips zako siyo kavu.
Kwani lips kavu hazileti raha yenyewe.
Wengine hupenda kufumba macho na wengine hawapendi.
Kwa leo fumba macho na ukishakutanisha lips achia hisia zimalizie kila kitu

BAADHI YA AINA ZA MABUSU

Butterfly kiss
Huku uso upo distance zero na mpenzi wako, fungua kope (eyelids) za macho funga fungua kwa speed huku unagusisha kwenye shavu lake.
Hili ni busu lisilohusisha lips na hutoa mtekenyo wenye kusisimua kwenye shavu.

Eskimo kiss
Huku mpo distance zero na mpenzi wako sugua pua yako kwenye pua yake kama sekunde 10 hivi, raha sana.

Finger kiss
Wakati mmelala wote na mpenzi wako, chukue kidole kimoja cha mkono wake na kubusu kwa kukinyonya.

French kiss
Hili ni busu linalohusisha ulimi wengine huita “soul kiss” kwa sababu uhai na nafsi hupita kwenda kwa mwingine kupitia kupumua kwa kinywa kupitia ulimi “wet
Kitu cha kushangaza ni kwamba wafaransa huiita “English kiss
Huhusisha maeneo yote ya mdomo na husisimua maeneo yote ya mwili.

Fruit kiss
Chukua kipande cha tunda (hasa fruit juice kipande cha nanasi, embe au zabibu) ng’ata nusu na yeye nusu na kunyang’anyana hadi linavunjika na juice kutelemka midomoni romantically.

Tiger kiss
Kama tiger huku akiwa hajui ukiwa mgongoni mshike na kumbusu kwa kung’ata shingo (angalie usijemuumiza mimi simo nazungumzia kung’ata kimahaba)

Angel Kiss
Ni tamu, kumfariji kwa kumbusu kwenye lips delicately.

Earlobe Kiss
Polepole ingiza ulimi kwenye masikio na kuyanyonya, usifanye kwa kusababisha sauti sana kwani masikio ni sensitive sana kwa sauti.

Tuesday, April 28, 2009

Busu

Busu hiloooooooo pokea!Busu husaidia kuwezesha moto wa mahaba kuendelea kuwaka kati ya wapenzi.
Kumbuka mpenzi wako huhitaji kujisikia yupo appreciated na zaidi anapata mapenzi (love and affection) kutoka kwako na njia nzuri ni kumpa busu.

Bahati mbaya ni kwamba wanandoa wengi wameshikwa na kunaswa na mtego wa u-busy hadi imefika wanasahau kuwabusu wapenzi wao.
Niambie wewe unayesoma sasa hivi hapa umembusu mke wako au mume wako lini?
Nahisi umesahau!
Plainly; mahusiano yanahitaji kazi, hasa kwa huyo special someone wako in your life kama ulifanya kazi kumpata kwa nini sasa ulegeze kamba, kaza uzi hakikisha uzi uleule uliotumia kumpata ndo huohuo unatumia kudumisha penzi na si kudumu tu bali linakuwa sustainable.

Kubusu hujenga intimacy kati ya mke au mume pia hufanya bonding iwe strong na kuhufanya wewe mwenyewe ujisikia vizuri na afya njema.
Nini faida za kubusu kiafya?
Busu ni afya kwa meno yako, wataalamu wamefanya tafiti na kugundua kwamba busu kuzuia plague kujijenga kwenye meno na hii ina maana utapunguza safari kwa daktari wa meno.

Busu ni afya kwa moyo wako (heart) kwani wakati wa kubusiana mnazalisha adrenaline ambazo husababisha moyo kuongeza speed na damu kwenda sehemu zote za mwili.

Kila mwanaume au mwanamke ambaye humuaga mwenzake asubuhi kwa busu utafiti unaonesha anaongeza miak 5 zaidi kuishi duniani.
Kama huwa hubusu wakati unaagana na mwenzi wako asubuhi unajipiga panga miaka 5 kuishi.

Kubusu hukuongezea self esteem na kujisikia upo appreciated kwani busu ni tamu na raha.

Mabusu hupunguza kuzeeka (aging) kwani mnapobusiana huhusisha misuli zaidi ya 29 kwenye eneo la mashavu na shingo.

Kubusu huchoma calories kati ya 6 – 12 na mkiongeza na love making huweza kufikia 300 na utajisikia raha.

Kubusu huondoa stress, huweza kutoa ocytocin, homoni ambayo hufanya mtu kujisikia vizuri.

Hakikisha unapobusu ni zaidi ya sekunde 10 ili kupata matokeo.

Hivyo basi wewe na mpenzi wako go ahead, kwa afya na furaha sherehekea kila siku kwa kupigana mabusu.
Je, kuna aina ngapi za mabusu?
Tutaendelea.............................................................

Bikira (2)

Eti unaweza kumjua mwanamke bikira kwa kumwangalia jinsi anavyotembea! Kutokana na maandiko ya agano la Kale (Biblia) (Kumbukumbu la torati 22:13 17)
Wanaume wa kiisraeli walikuwa wanatahiriwa (circumcision) na hiki kitendo cha kutahiriwa au kukata govi (foreskin) kilikuwa ni agano (covenant) na Mungu wao, agano la damu kwa maana kwamba ubikira wa mwanaume ulitolewa kwa Mungu.
Hii ilikuwa na maana kwamba mwanaume sasa alikuwa ni mali ya Mungu (belong to God).
Kwa kutahiriwa damu ilitoka na damu kutoka ni kuonesha kutoa bikira na yeye kuwa na mahusiano na Mungu.

Mwanaume aliunganishwa na Mungu ambaye sasa anakuwa chanzo cha uwezo wake.
Agano la mwanaume na Mungu lilihitaji damu kutoka katika govi la uume na si katika sehemu nyingine ya mwili wa mwanamke kwa sababu uume ndiyo ulitumika pia kwa kuvunja kizinda (hymen) mwanamke kutoka damu kwa ajili ya agano kati ya mwanaume na mwanamke mbele za Mungu kuwa kitu kimoja.

Hii ina maana kwamba kwa mwanamke bikira kutoa damu ni muhuri wa agano kati ya mwanaume na mwamke mbele za Mungu.

Je, katika agano jipya bado tunahitaji damu ya binadamu kwa ajili ya agano?
Baada ya Yesu Kristo kuja yeye alitoa damu ya thamani msalabani ambao hutuunganisha wanadamu wote na Mungu.
Mwanaume na mwanamke wote wanaunganishwa na damu ya Kristo na wao kwa pamoja wanakuwa bikira (bibi harusi mtarajiwa) hadi siku Yesu akija kulichukua kanisa na kila mmoja ambaye atakutwa hana bikira maana ataachwa.
(Kama umeokoka utanielewa nazungumzia kitu gani)
Hivyo basi suala la msingi hapa si mwanamke kuwa bikira na kutoa damu ya agano kwa mume au mume kutahiriwa kutoa damu ya agano kwa Mungu bali kuikubali damu ya agano jipya ambayo ni Yesu Kristo.
Kumpokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi ndiyo ubikira wa kweli

Je, inawezekana mwanamke bikira kuwa na mimba?
Ndiyo inawezekana, ikitokea sperms zinkawa deposited nje ya uke hata kama hakukuwa na penetrative sex kwani sperm ni genius au smart sana zikipata mwanya hasa kutokana na kufunguka kwa vitundu kwenye kizinda (hymen)

Je, ukiwa Bikira muda mrefu unaweza usizae watoto?
Uwongo mtu hasa kama mwanaume bado ana uwezo wa kuzalisha sperms na kama mwanamke bado anapata siku zake.

Je, unaweza kujua bikira kutokana na anavyotembea?
Thubuti! Hakuna external signal ambayo huweza kukufahamisha kama kweli mwanamke ni bikira au mwanaume ni bikira ukweli anajua yeye.

Je, Ukisubiri sex hadi uolewe au uoe ni mshamba kama si msenge?
Ukweli ni kwamba wewe ni smart sana kuliko wajinga wote wanaojiingiza kwenye masula ya sex kabla ya ndoa, Wazinzi na waasherati hawana nafasi katika ufalme wa Mungu.
Pia kusubiri kunakufanya uishi kwa amani na kutimiza malengo ya maisha bila hofu ya UKIMWI.

Je, Ukiwa in love na mtu lazima mfanye mapenzi?
Kuwa na mpenzi haina maana sex lazima, Pia inatokana na mipaka mliyowekeana.

Je, kwa mwanamke kudumisha urafiki na mwanaume sex ni muhimu?
Ukweli unajidanganya, kama urafiki wako ok shaky kiasi hicho kumbuka sex si tiketi ya kukufanya akupende zaidi bali tiketi ya kukupiga chini muda wowote na yeye kubeba kitu kipya kabisa.
Kama huamini nitumie email nitakupa mifano zaidi ya 100.

Friday, April 24, 2009

Bikira

Mabinti wa kizulu huko Lamontville Afrika kusini wakisubiri kukaguliwa kama bado ni mabikira huku nyuso zikiwa zimepakwa udongo.
(Picha kwa hisani ya Ellen Emendorp wa NYT)
Kutokana na desturi za huko Sri Lanka bibi harusi ni lazima athibitishe kwamba ni bikira usiku wa harusi yake.
Kila bibi harusi hutakiwa kubeba kitambaa cheupe ambacho huwekwa chini wakati wa tendo la ndoa kwa mara ya kwanza usiku wa kwanza kwa maharusi ili kuthibitisha kwamba bibi harusi alikuwa bikira.
Kitamba kuwa na damu ni certificate kwamba bibi harusi alikuwa bikira.
Na wapo mabibi harusi hukutana na wakati mgumu baada ya kujikuta hawakutoa damu yoyote ingawa ni kweli wao ni mabikira.
Hii ni kwa sababu wasri Lanka kama jamii zingine duniani bado wanaamini bikira yeyote hutoa damu siku ya kwanza na Yule ambaye hakutoa damu huonekana alijihusisha na ngono kabla.

Hiki ni kipimo cha kitambaa kuwa na damu ni kipimo potofu kwani na unscientific, wanawake wengi innocent huumizwa na kuonekana hawana quality ya kuitwa bikira wakati ni bikira.
Ni vizuri watu kujua uhusiano uliopo kati ya kizinda (hymen) na ubikira (virginity)

Bikira ni nani?
Bikira ni mwanamke au mwanaume ambaye hajawahi kufanya mapenzi (penetrative sex) na si lazima awe mwanamke ambaye atatoa damu siku ya kwanza ya tendo la ndoa.
Ni vizuri kufahamu kwamba asilimia 20% - 25% ya mabikira huwa hawatoi damu yoyote kutokana na muundo wa kizinda (hymen)
Wakati mwingine kizinda huondolewa kwa kufanya mazoezi mazito, kupanda baiskeli, kukwea miti na ifahamike kwamba kufanya mazoezi hakuwezi kuondoa ubikira.
Kizinda ni nini?
Kizinda ni ngozi nyembamba sana (membrane) ambayo huziba entrance kwenye uke.
Ina matundu ambayo hutofautiana kwa size ambapo damu ya mwezi kwa mwanamke huweza kupita kila mwezi.

Kuna aina Nne za vizinda
1. Kizinda cha kawaida (normal hymen),
2. Kizinda kisicho na tundu lolote [huhitaji surgery wakati mwingine] (Imperforated hymen),
3. Kizinda chenye tundu dogo sana (Microperforated hymen)
4. Kizinda chenye tishu za ziada na kufanya matundu mawili (septate Hymen)

Bado haijajulikana kazi ya kizinda ni nini, kwani baada ya sex mara ya kwanza huchanika na kuachana na kubaki historia.

Kizinda kiligunduliwa mwaka 1544 na Daktari wa kiarabu Ibn Sinna hata hivyo kufika karne ya 16 watu walikuwa wana imani potofu kwamba kizinda ni ugonjwa na dawa yake ilikuwa ni sex inayofuatana na mwanamke kuolewa.

Kutokuwa na kizinda au kutokutoa damu siku ya kwanza ya sex si evidence kwamba mwanamke si bikira wapo wanazaliwa hawana wengine nyembamba sana na wengine huweza kutoka kutokana na aina ya mazoezi au accidentally.
Damu ambayo hutoka siku ya kwanza ya sex ni kidogo sana linaweza kuwa tone hakuna mwanamke amewahi kutoa damu na kulazwa au kuhatarisha maisha yake kwa sex mara ya kwanza.
Pia ifahamike kwamba mwanamke huweza kujisikia maumivu kidogo au discomfort wakati wa tendo la ndoa.
Hata hivyo maumivu mengi huhusiana na woga na ignorance (knoweledge is power), wakati mwanamke anakuwa na hofu, woga wakati wa tendo la ndoa misuli ya uke hukaza na uke huwa tight na mwembamba na wakati mwingine hushindwa kutoa lubricants kwenye uke kutokana kuwa na hofu na matokeo yake ni kusikia maumivu wakati wa penetration.
Pia inawezekana mwanaume hakumuandaa vya kutosha na pia inawezekana wakati wa kumuandaa mwanamke mwenyewe hakuwa relaxed na kuwa tayari kupokea tendo zuri la sex akihofia kuumizwa.

Je, mwanamke kutunza bikira hadi wakati wa kuolewa kuna heshima au fahari yoyote?

Kwa nini suala la kuwa bikira kwa wanaume katika jamii zote linakuwa halina uzito bali wanawake tu?

Je, wakati wa kuoa au kuolewa karne hii ya 21 suala la bikira ni muhimu kuzingatiwa?

Tutaendelea…………………………..

Thursday, April 23, 2009

Wororo!

Mwanamke huwa kama pasi huchelewa kupata joto na hutunza joto kwa muda zaidi hata baada ya kumaliza kupiga pasi.Inatoke mwanaume anafika nyumbani kutoka kazini anamkuta mke naye yupo nyumbani anamsalimia then anaenda zake chumbani kubadilisha nguo za kazini.
Anapata chakula cha usiku (Dinner) then anaanza kutazama TV au kupitia magazeti yake na kuyasoma.
Muda wa kulala umefika anaenda kuoga na kuvaa pajama zake; mke naye anaenda kuoga na kufanya sawa na mume.
Wanapanda kitandani, mume anampapasa mke, mke naya anajua mzee anataka maana ndiyo sex code yake akinigusa kwa mtindo huu maana yake anataka tuwe mwili mmoja na anajisikia kama kusumbuliwa maana alikuwa hajui kama mzee atataka kutokana na kutowasiliana hata hivyo anamkubalia.
Baada ya dakika chache wamemaliza, wapo kimya na mzee anapiga usingizi.
Mke anajiona kama ametumiwa tu kwani hakukuwa na raha yoyote ni kuumizwa tu kwani mwili haukuwa connected hisia.

Kuna tofauti gani na chura hapa?
Kuwa na mahusiano na kimapenzi kwa mtindo huu ni sawa na kuiba akili ya asili ya chura (Frog’s love making instinct)

Mwanaume ni rahisi kusisimka kimapenzi wakati mwanamke huhitaji kusisimuliwa. Mwanaume husisimuliwa na moja ya mlango wake wa fahamu kupitia kuona (sight) wakati nwanamke husisimuliwa kupitia milango yote mitano ya fahamu Kuguswa, kusikia, kuona, kuonja, kunusa na wororo (tenderness) wa mwanaume.

Mwanaume ni mfano wa bulb ya umeme uki-switch tu mara moja inawaka wakati mwanamke ni mfano wa pasi ya umeme ambayo huchukua muda hadi ipate joto na hutumia muda zaidi to cool off.
Hii ni muhimu sana ukitaka kuwa mpenzi mzuri na mpenzi mzuri hujua na kuzingatia jinsi ya kumridhisha mwenzake.

Mwanamke anaongozwa na highway ya emotions, atajisikia vizuri sana kama alikuwa na idea kwamba kutakuwa na kuwasha pasi yake ya umeme mapema.
Itakuwaje kama wakati wa kuondoka asubuhi mume akampa mke busu la uhakika na kumnong’oneza mkewe kwamba “vipi unaonaje leo usiku ukawasha pasi mapema kwani nina hamu sana kupiga pasi nguo kwani naona bulbu yangu ina mwanga wa uhakika leo".
Nahisi mke atashinda anaweza jinsi ya kuhakikisha pasi yake inawaka chapchap usiku na ikitokea na mchana akaambiwa neon linguine mwororo inaweza kuwa jioni yenye mwako wa mahaba.

Kwa mawasiliano mazuri na kupeana quality time mwanamke huweza kufunguka kiakili, kimwili na kiroho na kuwa tayari kwa usiku wa kufurahisha na kuridhishana.
Ndiyo maana wakati mwingine ukipapasa usiku unaambiwa “baba nanii leo kichwa kinaniuma sana” au “nimechoka sana” au “unapata zero participation na kuambiwa maliza haraka” au pasi inakuwa kavu kabisa matokeo yake ni pasi inagoma kuwaka na kuanza kuumizana.

Jifunze kuwa mwanaume mwororo (tenderness) wasiliana na mke, tafuta muda wa kumsikiliza, cheka naye, cheza naye, ongea naye, mpe mgusu (touch), mkumbatie na kumbusu hata kama si wakati wa sex ni wako na ni wewe uliamua kuishi naye.

Mwanaume humtengeneza mwanamake!

Nitajuaje ni Yeye?

Uchumba ni mtamu acha kabisa, ila kumbuka ndoa ni kitu halisi!
(Picha kwa hisani ya YM - Arusha Tanzania)
Kumekuwa na maswali mengi sana naulizwa na vijana wengi wa kike na wakiume ambao wanataka kujua ni yupi anaweza kuwa mchumba halisi ambaye atakuwa mke au mume wake.

Ukizingatia kwamba kuoa au kuolewa ni uamuzi ambao unaweza kupelekea kuwa mtu wa furaha katika maisha yako au mtu huzuni na kujuta siku zote katika maisha yako.
Mambo ya msingi kuangalia ni haya:

MAHUSIANO HUWA RAHISI TANGU SIKU YA KWANZA:
Tangu siku ya kwanza nilipojikuta naonana uso kwa uso upendo uliokuwa kati yangu na yeye ulikuwa natural, nilijihisi nimemuona mwanamke ambaye namfurahia kila kitu, namkubali kama alivyo, nilihisi kama tulizaliwa tuishi pamoja na sasa nimempata mtu ambaye nimekuwa namtafuta, nilijiona atanitosheleza kimwili na kiroho, ninapoongea nayenaridhika kwa mvuto alionao.
Kila kitu katika mahusiano na urafiki wetu kilikuwa natural na kutupa hisia mpya kabisa hapa duniani.

Wapo ambao katika safari ya uchumba hadi ndoa hufikia kuzipiga na kugombana mara nyingi sana, leo wanazipiga au kununiana au hugombana na kesho wanapatana tena na kurudiana.
Wanaendelea na kasheshe hizo hizo mara kwa mara hadi wanaoana.

Inawezekana unarudiana naye labda kwa kuogopa ukiachana naye hutapata mtu mwingine wa kuoana naye, au umri unaona umeenda sana, au unataka kuondoa nuksi ili na wewe ujulikane uliolewa, au rafiki zako watakucheka au una hamu sana na sex, Kumbuka ni busara kuachana wakati wa uchumba kuliko kuachana ikiwa ndoa.
Ukiingia kwenye ndoa utakumbana na storm ambayo itakuja kupima kama sababu zako za kuoana zilikuwa strong kuliko storm yenyewe na kama zilikuwa weak storm itakuchukua bila huruma.

UHUSIANO MZURI NA FAMILIA, NDUGU NA MARAFIKI:
Inaweza kuwa tofauti kidogo hasa linapokuja suala la dini, kabila, nk kwani mara nyingi wazazi na familia nyingi huwa na lao kuhusu kabila au dini.
Ikitokea kwamba mchumba wako ni kabila moja, dini moja na bado ndugu zako, familia yako au marafiki zako hawaelewani naye ni vizuri kufikiria upya.
Wewe umelelewa na familia na kutokana na hayo malezi ndivyo ulivyo na umempata huyo mchumba kutokana na tabia yake aliyokulia au kulelewa na hiyo familia na kama bado hakubadilika maana yake hapo kuna bendera nyekundu inawaka na inaashiria kuna kitu hakipo sawasawa.

Kawaida ukishaingia kwenye mapenzi (fall in love) huweza kupunguza uwezo wako wa kuamua na kuona kasoro ndiyo maana wanasema love is blind.
Hii haina maana kwamba unatakiwa kuvunja mahusiano eti kwa sababu ya ndugu, familia au marafiki hawakubaliani na huyo mchumba wako ila ni kawaida kwamba inawezekana kuna kitu ndugu zako na familia yako wanakiona na wewe hukioni ambacho mbele ya safari mkiwa kwenye ndoa unaweza kukumbana nacho na bahati mbaya umewakana wazazi ndugu na marafiki.
Utaenda kwa nani kuomba ushauri maana umekuwa kichwa ngumu.

Jaribu kuchunguza kile ambacho ndugu zako au familia au marafiki wanasema vibaya kuhusu huyo mtu wako inawezekana ni kweli.
Ni kawaida kama umepata mtu wa kufanana na wewe basi huweza kujichanganya kirahisi sana na ndugu zako, familia yako na marafiki zako.

HUTAONA KITU KIKUBWA CHA KUMBADILISHA:
Kawaida, hata kama mnapendana kuliko binadamu yeyote chini ya jua, bado tofauti ndogondogo zitakuwepo; hata migogoro itajitokeza pia.
Ila kama kuna jambo kubwa sana unaona ni muhimu sana yeye abadilike basi hiyo ni ishara kwamba fikiria kwa makini.

Tatizo ukishashambuliwa na chemicals za love unaweza kujikuta unadhania kwamba haina shida kwa tatizo au kasoro alizonazo na utavumilia.
Ukiingia kwenye ndoa chemistry ya mapenzi hushuka na kupanda kutokana na jinsi mnavyojitahidi kuimarisha ndoa yenu; hapo ndipo sasa utagundua kwamba ulichemka and too late.
Usiingie kwenye ndoa ukidhania utambadilisha mtu sana sana wewe ndo utabadilishwa.
Kama umegundua kuna kitu ambacho ni tatizo kubwa sana mbele ya safari na hutaweza kuishi nacho ni vizuri ku move out kuliko kupoteza muda wako na kujifariji na baada ya miaka 3 ya ndoa ujikute upo kwenye jehanamu yako mwenyewe na upweke uliokithiri.
Watu hupata upweke lakini upweke wa kwenye ndoa ni mbaya kuliko upweke mwinghine wowote duniani.

NI RAFIKI
Mvuto wake ni kitu muhimu sana katika mahusiano.
Ndani ya mahusiano lazima kuwa na mzizi mkuu wa urafiki ambao hata mkiwa wawili sehemu yoyote duniani bado mnajiona hamjapungukiwa na pia bado mnajiona ndiyo marafiki bora duaniani.
Je, unajiona unahitaji kutumia muda na yeye tu?
Je, unajisikia raha kuwa na yeye wawili tu?
Je, unahisi yeye ndiye anastahili wewe kumwambia siri zako na kwamba ni yeye tu anakufahamu kuliko mtu yeyote duniani, kama ni NDIYO, basi mshike vizuri.
Kuwa best friends hata baada ya kuoana ni raha sana, na ndoa hudumu, maana hakuna anaye bore mwenzako.

UNAPOFIKIRIA KUOANA NAYE HAIKUPI SHIDA:
Kama unajikuta unapofikira kuoana naye huna wazo lingine la kuhisi ndoa inaweza kuwa na matatizo na unajisikia amani ya kweli moyoni na kwamba future yako na yeye itakuwa sawa basi umepatia.

Mwisho Kumbuka Kumuomba Mungu akupe amani ya kweli na huyo mtu wako maana yeye ndiye anajua liubavu lako lipo wapi.

“Marriage is not about finding a person you can live with, it’s about finding the person you can’t live without.”

Tuesday, April 21, 2009

Wapo wengi!

Kuna maboksi mengine kabla ya kuyabeba fikiria kwanza!Wakati mwingine huwa tunajikuta tumebeba maboksi ambayo tunadhani ni yetu na kwa furaha kubwa huwa tunawaringishia wengine hasa kutokana uzuri wa boksi kwa nje tukitegemea na ndani litakuwa na kitu kizuri.
Hata hivyo tukifika majumbani tunashangaa kuku vitu vilivyomo ndani ya boksi ni kinyume chake.

Maisha ya mahusiano nayo wakati mwingine ni kama kubebeshana maboksi tena kwa hiari kabisa.
Tatizo huanza pale box lenyewe likijua kwamba wewe ni mbebaji mzuri basi utachakaa kwa kubeba hili boksi.
Na linaweza kuwa ni boksi lililokuja na viboksi vingi ndani yake kama vile hasira, ukari, au manyanyaso ya kila aina, maneno magumu na mazito ambayo hukuumiza zaidi ya kupigwa ngumi na mateke, yaani unajikuta umeruka majivu na kukanyaga moto.

Kuna kitu kinaitwa “Narcissism” hili ni neno la kigiriki lenye maana ya mtu kuipenda zaidi nafsi yake kuliko kawaida (extreme self-loving).
Hili Neno linaendana na story ya kijana wa Kigiriki ambaye alivutiwa na taswira yake mwenyewe kwenye bwawa kiasi cha kushindwa kuondoka hadi alifia hapo.

Hili tatizo huanzia wakati mtu bado mtoto mdogo hasa baada ya kukosa upendo na anapokuwa mtu mzima anakuwa hajui maana ya kupenda na kupendwa.

Utafiti unaonesha ni asilimia 75 wana kaasili ka narcissists.
Na Adolph Hitler alikuwa kinara wa hizi tabia ingawa huyu alikuwa hatari hata hivyo tunao akina Hitler wengi sana kwenye mahusiano yetu ya kila siku.

Hawa akina Hitler wanachofanya ni kukubebesha kiboksi cha wewe Kujiona una hatia, wanakupa hofu, woga, mashaka, wanakufanya usijiamini ili wakupelekesha wanavyotaka wao.
Hawa wanaweza kukudhalilisha kimwili, kimapenzi, kihisia na pia wanaweza kuzira kuongea (silence) na wanachofanya ni kuku-control wewe idara zote za maisha yako unakuwa kama mfungwa fulani kwa kuwa umeingia kwenye anga zao.

Hata unapoishi nao unakuwa unaishi maisha ya mateso, mtindo wa jela na kunyimwa uhuru.
Hii aina ya mahusiano ni hatari tupu na huhitaji msaada wa ushauri kwa wataalamu wa masuala ya ndoa na mahusiano.
Wengine ni watu wenye status kubwa katika jamii zetu anaweza kuwa mameneja, wahadhiri wa vyuo vikuu, matajiri, wabunge au mawaziri na hawa watu huonekana watu wa heshima kubwa sana mbele ya jamii kwani ni wapole, wema, watii, ni marafiki, wastaarabu, wamevaa ngozi ya kondoo huku ndani ni mbwa mwitu wakali na wenye njaa.
Hawa watu ni lethal.
Ukifanya kosa moja tu kwao unastahili kupewa adhabu ambayo utajuta kuwa naye katika maisha.
Hawa wanaume au wanawake hufurahia sana kutesa wake zao au waume zao, hawana huruma na hawafai kabisa katika jamii.

Tupendane katika ndoa zetu

Monday, April 20, 2009

Nani kakwambia

Hata gari jipya wakati mwingie huwa garage kwa muda mrefu!Eti mahusiano mazuri hayana sexual problems.
Wanandoa wote kuna wakati hupitia matatizo kuhusiana na sex na hii haina maana kwamba uhusiano wako na mume au mke basi umeota mabawa.
Hata hivyo kama tatizo linabaki kwa kula jiwe kati yako na mwenzako ni kweli linaweza ku ruin ndoa yenu na mahusiano.
Signal yoyote ya kuwepo tatizo katika mahusiano linapokuja suala la sex si alama ya kuwa ninyi ni failure ni sehemu katika mahusiano.
Inawezekana sexual needs za mume wako au mke wako zimebadilika, hasa katika dunia ya leo ambayo watu wanakimbizana na maisha bila mafanikio.
Umenunua gari ukimbize maisha lakini wapi, umejenga nyumba ukimbize maisha lakini wapi, umeoa mke mzuri kukimbiza maisha lakini wapi na wewe unayesoma hapa umeolewa na mwanaume mzuri lakini maisha wapi bado ni kukimbizana tu, mimi simo!
Hata hivyo kubadilika kwa hamu, kuridhika nk vinahitaji muda ili muweze kufanya adjustment na kurudi kwenye mstari na kuendelea na maisha kwa raha zenu.

Eti mwanamke lazima afike kileleni kwa intercourse peke yake (uume kuingia kwenye uke)
Wanawake wengi hawawezi kufika kileleni kwa hicho kitendo peke yake hata kama unatumia ukuni mkubwa kiasi gani au jogoo anawika kwa muda mrefu kiasi gani kwa sababu uume hauwezi kutoa stimulation ya kutosha hadi kufika kileleni isipokuwa kisimi (soma post ya nyuma inayoitwa “kitufe”)
Pia kutumia milalo ya aina tofauti hasa ile inayoweza kusisimua kitufe (kisimi) au G- spot huwezi kusaidia kwa wengine.
Pia kumbuka forplay ni muhimu kuliko sex yenyewe na hilo ni muhimu kuhakikisha kila mmoja anafika kileleni kwa raha zake hata hivyo muhimu zaidi ni mood hasa kwa mwanamke.
Ni busara ya hali ya juu kwa mwanaume kuacha kufanya sex kama mwanamke unahisi hana mood.

Eti mke wangu au mume wangu atajua mwenyewe tu jinsi ya kunipa raha hata nisipomwambia wakati wa mahaba.
Mkeo au mumeo si mind reader hana scanner yoyote ya kujua unajisikia raha wapi na aongeze efforts kwenye hilo eneo huku wewe umelala kama gogo.
Kukosa mawasiliano wakati wa sex ni moja ya factor kubwa inayochangia kuwa na tendo la ndoa lisiloridhisha kwa kila mmoja.
Kila mmoja anajua sex ni kitu gani kila mtu hili eneo ni genius hata hivyo kila mtu ana sexual needs tofauti na mwingine.
Ni lazima umwambia partner wako nini unahitaji, acha aibu tena mwambia kwa details na kuwa huru hata kama yeye huwa bubu au huchanganyikiwa kabisa ukishamwambia twende south pole.

Love is the greatest food for an emotional starving world.

Thursday, April 16, 2009

Kitufe (2)

"Ni round siyo square"Kabla ya wiki 8 za kwanza za mimba sehemu za viungo vya uzazi; mtoto (fetuses) wa kike na kiume huonekana sawa kimaumbile katika uzazi, baada ya hapo mtoto wa kiume huanza kutoa testosterone ambazo husaidia huwezesha uume kujitokeza zaidi kuliko motto wa kike.
Hivyo basi kilivyo kisimi na uume hufanana na vyote hufanya kazi sawa kutoa raha ya mapenzi na kufika kileleni (orgasm) linapokuja suala la mahaba.

Kama kisimi ni zaidi ya uume kwa raha ya mapenzi kwa nini baadhi ya wanawake wakisisimuliwa kisimi bado huwa hawajisikii raha?
Utangulizi:

Jibu:
Hakuna tatizo lolote na hao wanawake ingawa ni kweli kisimi/kinembe ni kiungo maalumu na cha tofauti sana kwenye mwili wa mwanamke.
Ila kumbuka kila mwanamke na mwili wake ni tofauti na mwanamke mwingine, wengine hupenda na kujisikia raha kisimi kikiguswa kwa nguvu, wengine si kwa nguvu sana, wengine kubusiwa, wengine kunyonywa, wengine kikilambwa, wengine kikisuguliwa na wengine hawawezi kupata raha hadi kifanyiwe mazoezi kwa muda zaidi (baada ya miezi na miaka kadhaa).

Pia kumbuka wapo wanawake amabo huwa hawasikii raha hasa mwanaume akiwahi kisimini kabla ya kusisimuliwa sehemu zingine kama matiti nk kwani huko kuna nerves 8,000 so ukigusa haraka anaweza kurusha rocket mwezini.
Pia kuna wanawake ambao ni mbumbu kuhusu sexuality na miili yao mfano kama anaamini unampotezea muda kuhangaika na kisimi chake, je unadhani atapata raha yoyote?

Sex huanza kwenye mind kama ameweka password kwenye mind yake utafungua vipi?
Kumsisimua mwanamke huhusika moja kwa moja na ubongo wake au nini unaongea naye wakati mwingine hata kabla ya kuingia chumbani au kitandani.
Ili asisimke inategemea sana nini unaongea kwenye sikio lake, kile unamnong’oneza kina maana sana katika kuuandaa mwili wake, kama hujajua kuongea maneno fulani fulani ambayo huongelewa kwenye sikio la mwanamke kabla ya sex basi huna budi kujifunza.
Jinsi unavyoweza kumsisimua kabla hata nguo hajavua utakuwa na kazi rahisi sana wakati akiwa hana hata nguo moja na hii itakurahisishia yeye kutaka zaidi.

Kama umeoa mwanamke ambaye hajijui mwili wake na kisimi kina kazi gani kwake jaribu hii na unaweza kuwa mbunifu zaidi ukiongeza skills inazozijua wewe.
Kwa kuwa unajua kisimi ni nini na kipo wapi hongera maana umeshapiga hatua kubwa on this game, hakikisha ame-relax, ungana naye kuhakikisha miili inapata joto la mahaba kimwili, kiroho na kiakili.
Jisikia comfortable, hakikisha unapumua vizuri na ukitaka hakikisha mnapumua pamoja sare na deep , ukiweza mfanyie massage mwili mzima kuanzia kichwa hadi vidole vya miguu, anza kwa kutumia ncha za vidole vyako na baadae kwa kupalaza viganja na mikono yote.
Sasa hakikisha unalishikilia vizuri hekalu lako, uso, shingo, masikio, mabaga, mikono, kifua, matiti, tumbo, mgongo, mapaja na miguu hadi vidole.
Huku ukimchunguza kama vile umewahi fanya kazi FBI angalia kama yupo relax na amesisimuka ( anapumua kwa nguvu zaidi, chuchu zimesimama, na south pole kunalowa kimbiza mikono yako kwenye kuta za uke na kisimi.
Ukiaona bado hajisikii raha kwenye kisimi chake, rudi ground zero kichwani tena kwa kumbusu sawa kama ulivyompa massage.
Then rudi tena kwenye kuchezea kisimi kwa skills zote
Then fanya unachojua wewe!

Jinsi ya kusisimua kisimi.
Vidole:
Kwanza mikono lazima iwe safi na kucha fupi zilizokatwa vizuri zisizo na mikwaruzo yoyote wala ncha mpya kali.
Na kabla hujatujuliza vidole au kidole chako hapo hakikisha unapita kwanza kusalimia sehemu zingine kama mapaja na eneo zima la south pole (uke).
Kujua ni pressure kiasi gani utumie wewe si bubu muulize mkeo anaweza kukujibu kwa kukunong’oneza au kwa kukupa signal, kumbuka kuna aina ya kuchezesha vidole au kidole iwe duara au square na kama hukusoma geometry au vector basi rudi shule maana hapo ndo application yake.
Kumbuka hilo ni eneo sensitive kuliko eneo lolote katika mwili wa binadamu hivyo usicheze rough.

Kinywa.
Wapo ambao kwao sex si uchafu na huweza kutumia viungo vyao nyote katika mwili na kwao kufanya hivyo ni kuwa karibu zaidi kati ya mke na mume na ni mwili mmoja na zaidi tendo la ndoa ni kuwaunganisha wawili kimwili, kiakili na kiroho hivyo si kuingiliana tu bali kuwa kitu kimoja.
Kwa kuwa ulimi ni kiungo au msuli imara (strong) kuliko yote katika mwili wa binadamu basi kisimi kikikutana na ulimi mbingu hufunguka na watu kurushwa International Space Station bila kujijua basi kama umejazwa Roho Mtakatifu unaweza kunena kwa lugha kwa raha inayotokea.
Lubricant ya asili iliyopo kweny ulimi na joto la kinywa hutoa sensation ambayo ni kama dream team pamoja na kuzungusha ulimi kwa skills zote mke wako atakutana na lift itakayomnyenyua hewani kuelekea kileleni.
Kumbuka
Cleanness is second to godliness

Uume
Uume ni toy la mwanamke yeyote ambaye ameolewa, this is favorite toy; uume unaweza kuingia kwenye game la kuchezea kisimi.
Ila jiangalie usije maliza haraka kwani kusugua kisimi kwa uume huweza kuupa uume sensation za kupelekea kumaliza haraka.
Conclusion
Kufahamu kuhusu kisimi kwa mwanaume au mwanamke ni kuonesha kwamba ume-invest vya kutosha kuhusiana na raha ya mapenzi ya mke au mume wako, kitu cha msingi ukijua utakuwa na tendo la ndoa ambalo linaridhisha na zaidi kila mmoja atamuhitaji mwenzake kila mara.

Kumbuka ukiwa na mwanamke anayeridhika kimapenzi na yeye atahakikisha anakuwa na mwanaume anayeridhishwa kimapenzi pia na hutauliza hili kwake maana anajua.

Without geography we are no where,
bila kujua geography ya mwanamke huwezi kumfikisha pale anahitaji kufika kimapenzi.

Ubarikiwe!

Wednesday, April 15, 2009

Kitufe

Utangulizi
Kuchua / kusugua baadhi ya sehemu za mwili kunaleta raha na kumaliza ashki ya tendo takatifu la ndoa.
Kwa wanawake wengi kinembe/kisimi ndiyo sehemu haswa inayoleta raha.
Hii ni kwa sababu sehemu hii ina mishipa mingi ya kusisimua mara ikiguswa.
Njia moja ya kupata raha na kumaliza ashki ni kuchua taratibu sehemu hii.
Hii ni njia moja ya kutoshelezana kimahaba.

Kinembe au kisimi au clitoris au clit au joy button, hot spot nk ni moja ya kiungo ambacho humsisimua mwanamke zaidi kuliko kiungo chochote katika mwili wake unaovutia. Hiki kiungo kipo eneo la juu zinapounganika kuta za ndani za uke (Labia minora).
Ni rahisi kukipata kiungo hiki kwa macho na kwa kugusa au kupapasa.
Kisimi hutofautiana kati ya mwanamke na mwanamke, wengine ni kidogo sana na wengine huwa kikubwa zaidi.

Kipoje?
Kisimi kina sehemu muhimu 18 na kile tunaona na kugusa kwa nje ni kitu kidogo sana ukilinganisha na siri iliyofichwa ndani.
Kwa nje kisimi kimejigawa katika sehemu kuu tatu kichwa, msukano (shaft) na mfuko ambao hufunika kichwa na msukano.
Mwanamke akisisimka kimapenzi kisimi hudinda au huongezeka au kutuna na kimfuko hurudi kwa nyuma na kichwa ambacho ni very sensitive hujitokeza na kuwa kigumu.
Kisimi kipo eneo la juu baada ya tundu la kibofu cha mkojo na chini ya tundu la kibofu cha mkojo kuna tundu la uke.
Ngozi laini inayofunika kisimi huwa na stimulation ya uhakika na kuna baadhi ya milalo huwezesha kusugua hii ngozi na mwanamke hujisikia raha zaidi wakati wa sex.

Kazi yake ni nini?
Kisimi ni powerful organ kwa ajili ya raha ya sex kwa mwanamke, kina nerves zaidi ya 8,000 kuliko sehemu yoyote katika viungo vya binadamu; why? Ukweli ni kwa ajili ya kumpa mwanamke raha kimapenzi.
Kisimi kazi yake ni moja tu kumpa mwanamke raha ya mapenzi.
Na wanasayansi wamegundua kwamba chini ya kisimi kuna network ya tishu za msisimko, misuli, nerves na mishipa ya damu ambayo kwa pamoja huitikia na kujikunja wakati wa sex na kupelekea mwanamke kufika keleleni.

Tofauti na uume ambao hutoa mlipuko mmoja wa kufika kileleni kwa sekunde chache, kisimi hutoa mlipuko wa muda mrefu wa aina zaidi ya 100 za raha, Hii ina maana kisimi ni zaidi ya uume kwa kutoa raha ya kimapenzi.
Ole wenu mnaowafanyia ukeketaji wanawake, mna kesi ya kujibu! Kwani mnawanyima haki yao ya kuzaliwa kupata raha ya kimapenzi.

Je, wengi wanajua umuhimu wa kisimi katika raha ya tendo la ndoa?
Wanaume na wanawake wengi tunapozungumzia suala la sex huchukulia kwa mtazamo wa kiume (mfumo dume) kwa maana kwamba sex ni nzuri sana kwa wanaume na si wanawake na kwamba jukumu la nani aanze ni mwanaume na kwamba wanawake hawapo powerful kwenye sex kama wenzao wanaume.

Hata hivyo mwanamke akifahamu utendaji wa mwili wake kiungo baada ya kiungo anaweza kugundua na kuimarisha furaha ya tendo la ndoa akisaidiana na mume wake na moja ya viungo muhimu ni kisimi.
Na pia anaweza kufahamu ni namna gani anaweza kufika haraka kileleni kwa kujua kisimi kilivyo muhimu kwake.

Je, nini umuhimu wa kisimi wakati wa tendo la ndoa?
Wanawake wengi ili kufika kileleni (orgasm) ni muhimu sana kusuguliwa, kuchezewa kisimi.
Hii ni kwa sababu uke hauwezi kumpa direct stimulation wakati wa sex na pia mwanaume hawezi kusugua uke kiasi cha mwanamke kufika kileleni bali uke huweza kumpa mwanaume msuguano ambao humuwezesha yeye mwanaume kufika kileleni haraka.

Hii ina maana mwanaume anatakiwa kuelekeza nguvu nyingi kuhakikisha anasisimua kisimi kwa muda wa kutosha kuliko uume wake kuwa kwenye uke na kuusugua kwa skills zote badala ya kuelekeza skills zote kwenye kisimi.

Hii ina maana kwamba kama mwanaume anataka kufika kileleni haraka ni kwa mwanamke kumruhusu mwanaume kuingiza uume wake kwenye uke na mwanaume akitaka kumfikisha mwanamke haraka kileleni ni kumshughulikia mwanamke kisimi kwa skills zote.
Hii haina maana kwamba mwanamke hawezi kufika kileleni bila kisimi la hasha kwani anaweza kufika hata kwa busu, au kumpa mguso kwenye sehemu zingine za mwili, hapa tunazungumzia kisimi.

Tutaendelea.......................................


Tuesday, April 14, 2009

Chains do not hold a marriage together.
It is threads, hundreds of tiny threads which sew people together through the years.
~Simone Signoret

Monday, April 13, 2009

Eti hatuwasikilizi!

Etu huwa hatuwaelewi!
Wanaume tunapigiwa kelele sana kwamba mkiongea huwa hatuwaelewi na hata tukiwaelewa tunafanya tofauti na tukifanya tofauti tunakuwa wakali kukubali ukweli.
Ukweli ni kwamba mnapoongea mnaongea kwa maneno mengi mno na kama si hivyo basi mnalalamika mno (kefyakefya) au mnasisitiza mpaka tuhisi umekuwa mama enzi za utoto wetu au wakati sisi ni watoto wa shule ya msingi.
Mwanaume gani anataka kuwa mtoto wa shule?
thubutu hakuna!
Pia lazima mfahamu kwamba ile sehemu iyotunza maneno mnayotuambia mkiwa mmekasirika ni sehemu ileile tunatunza kumbukumbu za mechi (au mambo ya sports) za ligi kuu ya Uingereza (Chelsia ilivyomfunga Liverpool) sasa hapo utajua mwenyewe.

Eti anawaangalia sana wanawake wengine.
Baadhi ya wanawake huendelea kuwasuta waume zao maswali kwa nini huwa hanawaangalia wanawake wengine mfano wakiwa njiani, dukani, au mitaani. Sidhani kama kuna kosa kwa mwanaume kumuangalia mwanamke mwingine na kumpa heshima zake kama amependeza au ni mzuri as long awe anampa credit na mke wake katika maisha yao.
Ukweli wanaume tunawapenda wake zetu to death, hata hivyo kuwaangalia wanawake wengine haina maana kwamba tunawatamani na kwamba tuna tamaa sana.
Pia wewe mwanamke unayesoma hapa mwanaume akikuangalia hadi unastuka ujue mumeo amepata mke bomba!

Eti huwa wanaume hatuwasifii wake zetu;
Ukweli graph ya kukua kimapenzi wanaume hukua kila mwaka, hii ina maana kwamba kama mwaka huu au mwaka uliopita nilikuwa zikupi sifa kutokana na kazi unafanya hii haina maana kwamba sikupendi, nakupenda sana (I love u to death or from earth to the moon) huwa tunakua polepole na tunabadilika hivyo tuombee tu.
Pia tuna nafasi kubwa sana katika emotional chart yetu kujifunza na kubadilika hivyo tupe muda na utaona mabadiliko.

Eti unataka kujua mahusiano yake ya zamani yalikuwaje?
Kuna watu wengine hushangaza sana kwani mmekubaliana kuoana na sasa mpo kwenye ndoa, kuingia tu unanza sasa kuchokonoa na kutaka kujua mahusiano ya nyuma ya partner wako ili um-control vizuri.
Mwache awe kama alivyo ndo maana umependana naye na mkakubaliana kuoana kitendo cha kuanza kutaka kujua kila kitu kuhusu yeye yuko nyuma unaweza kujikuta unaanza kumsahihisha na kumkosoa au kukasirika na vitu ambavyo vilipita na ameshabadilika.
Jisikia vizuri tu jinsi alivyo sasa, hizo kumbukumbu za zamani unazoingiza kwenye memory disk yako ya ubongo zinaweza kukupa hisia mbaya ukaanza kumuona hafai wakati amebadilika.
Kawaida past huwa inadanganya kwa sababu haipo sasa hivi, hata hivyo let the past be the past and it will stay there.

Eti tunapenda sana michezo
Ni kweli tunapenda sana michezo ila wakati mwingine hatupendi kukaa mahali ambapo mke wako mwenyewe amekasirika, hachangamki, kila wakati kulaumu tu, kelele mtindo mmoja, mara hujafanya hiki au kile, yaani mwanamke unajua kila kitu nakumsemesha mwanaume hadi anashindwa kupumua. Ndiyo maana huwa tunaenda kuangalia michezo mbalimbali wakati mwingine mnakuwa mmetuchosha hahaha!

Eti tukiahidi hatutekelezi!
Ukweli ni kwamba kuna wakati hata tukiwaeleza ukweli humuamini so inabidi tuwaahidi mambo makubwa makubwa na kweli tukiwaahidi mnafurahi hadi hadi mnaenda kuwaambia rafiki zenu na siku hiyo ukiwahidiwa kila kitu nyumbani kinakuwa kama kusuma mlevi.
Kama mnataka tusiwaahidi mambo makubwa muwe mnaridhika na kutotaka mambo makubwa.
Just kidding!
Thursday, April 9, 2009

Kumaliza haraka (mwisho)

Maji yakiisha kabla moto haujazima kasheshe!Mwanaume kuwahi kumaliza (Premature Ejaculation - PE) ni jambo muhimu linalomhusu mke na mume, karibu mwanaume mmoja kati ya wanawaume watatu mmoja huwa na tatizo la kuwahi kumaliza mapema.
Nitatumia Neno PE kumaanisha mwanaume kuwahi kumaliza mapema au kwa kingereza (Premature Ejaculation)
Kwa njia zingine kuwahi kumaliza kwa mwanaume ni kitu ambacho kimejificha kwani huwezi kumtambua mwanaume ambbaye ana PE kwa kumwangalia sura, pia ni mara chache sana au ni ngumu sana kwa wanaume kupeana story za mambo kama haya wakiwa wenyewe kwani mwanaume huhofia kuonekana si lolote kwa wenzake (kupoteza ego) sana sana anayejua ni mke wake ambaye anajua inamuathiri kiasi gani na kupata usumbufu kiasi gani kwani wapo wanaume ambao hata huruma hana ile kumaliza tu basi usimguse.

Kwa kuwa hakuna mwanaume anapenda kuwa na PE hii ina maana kwamba kuwa na PE siyo huathiri mwenendo wa sex tu bali hupelekea kuathiri maeneo yote ya maisha kwani mwanaume akiwa na hili tatizo huogopa kushiriki na matokeo yake huwa mtu mwenye masumbufu na mpweke na baadae hukosa ujasiri (self esteem) na huathiri maisha kwa ujumla hadi taaluma yake.

Mambo mengine ya msingi ambayo yanaweza kukusaidia mwanaume ni jinsi ya kutumia akili, mawazo (thoughts and mind)
"You are by what you think"
Amua kwamba utaweza kuthibiti hiyo hali, jiamini, jitolee, uwe na imani ile ya kuhamisha milima na kwamba wakati umefika unataka kubadilisha uwezo wako katika tendo la ndoa.
MAZOEZI
Pia ni muhimu kuwa mtu wa kufanya mazoezi, kama una misuli ambayo hata kama ulikuwa unakojoa (urinate) ukashindwa kuziba mkojo ghafla basi hii ina maana misuli yako ya PC imelegea na jambo la msingi ni kujifunza kuikaza kwa kufanya mazoezi.
Kuwa na misuli ya PC iliyokaza ni siri kubwa katika kufanikisha furaha ya mapenzi kwa mume na mke.
Nini Imani Potofu kuhusiana na PE?
Eti PE ni kitu ambacho huwezi kuthibiti.
Ukweli ni kwamba unaweza kuthibiti na mwanaume yeyote anaweza kujifunza kuthibiti PE kama vile ile njia alitumia kubana mkojo wakati mtoto na sasa akilala hakojoi ovyo kitandani.

Eti PE huathiri wanaume wenye umri mkubwa.
Ukweli ni kwamba PE huathiri wanaume wa umri wowote, ingawa wanaume wenye umri mkubwa huwa na tatizo na kushindwa kusimamisha na hutumia muda mrefu ili uume usimame na kuwa tayari kwa tendo la ndoa.

Eti PE huweza kusababisha kuwa na matatizo ya kuchelewa kusimamisha.
Ukweli ni kwamba huwezi kukojoa (ejaculate) bila uume kusimama hii ina maana kuliacha tatizo kwa muda mrefu kunaweza kupelekea kuwa na matatizo ya jogoo kushindwa kuwika kabisa.

Eti PE haiwezi kuathiri maisha yako ya kimapenzi na mke wako.
Ukweli ni kwamba kama una experience PE wakati unafanya mapenzi kawaida unakuwa umejawa na mawazo kwamba unaweza kumaliza mapema na matokeo yake huwezi kufurahia sex na huwezi ku-relax, pia mke wako anaweza kuwa haridhiki na matokeo yake atakuwa anakwambia kichwa kinauma kila siku ukitaka kuwa mwili mmoja hahaha!

Eti PE haiwezi kuathiri kujiamini kwako.
UKweli ni kwamba kila mwanaume huwa anapenda kuwa mzuri kitandani, PE na kutomfikisha mke pale anahitaji kufika ni sababu tosha ya kupoteza confidence zako.

Eti PE huathiri wanaume wachache sana
Ukweli ni kwamba wanaume wengi ni wahanga wa hili jambo kuliko watu wanavyodhani.
Hivyo si wewe unayesoma hapa ndo unahusika, huko nje kuna wanaume wengi tu wanakumbana na hii kasheshe, ila wengi wamechukua hatua na kuondokana na hili tatizo.

Eti ukiwa na PE huwezi kubadilika kabisa hivyo ishi nayo ni kilima chako.
Ukweli ni kwamba kukubali kwamba ni kilema chako ni kosa kubwa sana (terrible and biggest mistake on earth)
Kufikiria hivyo ni kosa ambalo litakufunga wewe na mpenzi wako kwenye jela ya wale ambao ni wapweke wakati wapo kwenye ndoa.
Siri kubwa ni wewe kuweza kuthibiti PE (piga ua lazima uweze, kama wengine wanaweza kwa nini wewe ushindwe?)
Ukifanikiwa unaweza kuwa ni mwanaume smart sana kitandani ambaye hajawahi kutokea kwani utakuwa ni mwanaume unayejali, uliyejifunza na kugundua feelings zako na hisia zako na jinsi ambayo huwa unasisimka kwa muda wote kitandani na hii itakupa ujasiri wa kuwa mwanaume kiongozi kitandani na kila mwanamke huhitaji mwanaume kiongozi na ambaye ni caring.
================================

Wednesday, April 8, 2009

Kumaliza haraka (ii)

Kawaida baada ya mwanaume kuwa na tabia ya kumaliza haraka kinachofuata ni kuanza kukwepa sex kitu ambacho inakuwa ngumu zaidi kuthibiti tatizo, mwanaume akiwa anauwezo wa kuthibiti kumaliza mapema pia huweza kuwa na hamu zaidi ya kufanya mapenzi.

Wengine hutumia njia ya kuondoa mawazo kujihusisha na tendo lenyewe kwa kuwaza vitu vingine hata hivyo hapo ni kujinyima raha na huweza kupelekea vitu kuwa ovyo zaidi.
Si vema kuhamisha mawazo yako kutoka kwenye akili zako wakati wa tendo la ndoa kwani ni sex muunganiko wa roho, mwili na nafsi.
Jambo la msingi ni kuwa na ufahamu wa viwango tofauti vya msisimko (sensation) wa kimapenzi kuhusiana na kiungo chako (uume).
Unatakiwa kujua ni namna gani unajisikia (feel) unapokaribia kufikia hatua ambayo hakuna kurudi nyuma (ejaculatory inevitablility kifupi EI).

Ukishakuwa umefahamu unavyojisikia kuelekea point of No return hapo haitakuwa vigumu kufanya marekebisho ambayo yatakuruhusu kubaki umesisimka lakini bila kumaliza (kukojoa).

Kusisimka kimapenzi huwa ni mzunguka wa hatua 4 muhimu ambazo kwanza ni kupanda kwa mdadi (excitement phase) huu ni wakati ambao kupumua huongezeka, uume husimama (hudinda), hatua ya pili ni kilimani (plateau stage) hii ni hatua ambayo uume huwa umebaki umesisimka kwa kiwango cha juu, hatua inayofuata ni hatua ya tatu ambayo ni kumaliza au kukojoa au (orgasmic with ejaculation) na hatua ya mwisho ambayo kupumua hurudi kama kawaida na uume hurudi na kuwa kawaida (resolution phase).
Ufunguo muhimu katika kuthibiti kumaliza mapema ni ku-maintain hatua ya pili (plateau phase) yaani kubaki hapo kilimani bila kupiga risasi hata kama umelenga vizuri na unajisikia kuachia, hapa ndipo panahitaji imani na kujikana maana huwa ni kuelekea kwenye raha kamili ya sex kwa mwanaume, ila kumbuka uliye naye anahitaji uendelee zaidi.

Nini kifanyike kuthibiti hii hali?
Usitumie drugs au kilevi eti ndo unaweza kuthibiti hii hali, vitu kama hivi huweza kukupa interference na kupunguza uwezo wa kuelewa wakati muhimu wa wewe kuthibiti kumaliza mapema.
Kwanza jikubali, wanaume wengi huamini kwamba sex ni kwenye uume tu na pia kufanya mapenzi ni pale uume ukiingia kwenye uke tu.
Kufikiria hivyo ni tiketi ya moja kwa moja ya mwanaume kuwahi kukojoa au kumaliza.

Kufanya mapenzi kunakoridhisha (best sex) ni pamoja na kupeana mahaba, romance kuanzia juu kichwani kwenye nywele hadi kwenye kucha za vidole miguuni.
Mwanaume anayejifunza kujipa raha kimapenzi kupitia sehemu zote zinazompa raha (chuchu, lips, shingo, midomo, ulimi, nk) huweza kurelease tension kupitia hizo sehemu na kutosubiri sehemu moja tu yaani uume ndo iwe sehemu ya kupata raha ndo maana huweza kukojoa mapema.
Ni kwamba mwanaume anakuwa amefunga outlet zingine na kubaki na uume tu hivyo ni rahisi kufikia point ya no return tena kwa haraka mno.
Ukishajifunza kupata raha ya mapenzi (sexual pleassure) kuanzia nywele kichwani hadi kucha miguuni maana yake mwili mzima unachukua raha ya mapenzi badala ya uume peke yake na matokeo yake utabaki ndani ya mke wako kwa muda mrefu.

Kujipa raha ya mapenzi ya mwili mzima ni njia ya ku-relax na kurelax ni moja ya njia muhimu za kujipa good sex.
Kwa mfano kuoga pamoja kwanza au kufanyiana massage kwanza kabla ya kuanza kwa tendo la ndoa husaidia mwanaume kurelax na zaidi kuupa mwili mzima sexual pleassure matokeo yake ni kufanya mapenzi kwa muda unaotosha na bibie kuridhika.

Kuwa na uwezo wa kupumua vizuri (deep breath) hii haina maana kwamba wakati unafanya mapenzi huwa hupumui, la hasha bali upumuaji wako inawezekana si ule usiotakiwa kwani wanaume wengi huzuia kupumua wakiwa kwenye sex.
Wengine huogoa kusikika wanapumua tofauti, sex ni kazi kama kazi zingine sasa usipopumua unadhani kitatokea nini, ikiwezekana pumua huku unatoa visauti, achia kupumua usijivunge kwani unapoficha kupumua maana yake unakaribisha uume ukusaidie kupumua na njia sahihi kwa uume kupumua ni kukojoa mapema.
Wengi baada ya kujifunza kupumua kwa kujiachia wamefanya mabadiliko makubwa sana katika muda wa kuwa ndani bila kumimina risasi.
· .
Ukishajua kuutumia mwili mzima kuhusika na raha ya mapenzi pamoja na kupumua sasa inakuja technic nyingine ya kujipiga stop.
Unaweza kuwasiliana na partner wako jinsi ya kupeana signal kwamba nakaribia kile kituo ambacho nikifika sitarudi tena, hakuna break.
Unaweza kutoa uume nje huku ukiendelea kupumua na ukiona unapata zile feelings kwamba huwezi kukojoa basi unaweza kurudi na kuendelea tena, kiasi cha kujipiga stop na kuendelea ni uamuzi wa ninyi wawili mnaohusika hasa baada ya mke kuridhika.

Kwa wwale ambao kufanya mapenzi kupo katika level nyingine (oral sex) wanaweza kutumia oral sex kuthibiti mwanaume kumaliza mapema kwa mwanaume kujipa stop akiona anakaribia kumaliza kwa oral sex hii ni baada ya kupata mafanikio hasa baada ya kuona sasa mwanaume anaweza kwenda mbali zaidi ya kawaida yake.

Pia aina ya milalo wakati wa mapenzi huchangia mwanaume kumaliza mapema, kwa mfano missionary position (mwanaume juu mwanamke chini) huu huwezesha mwanaume kumaliza haraka kuliko mwanamke kuwa juu na mwanaume chini, otherwise mwanaume ni vizuri ukafanya utafiti wako kujua ni mlalo gani huwa unajisikia kuchelewa kumaliza na mke wako kuwahi kufika kileleni.

Pia ni vizuri kufanya mapenzi bila kuwa mabubu,kufanya mapenzi huku mnaongea husaidia mwanaume kurelax (na mwanamke pia) na husaidia mwanaume kuchukua muda mrefu kumaliza
Kujifunza kuthibiti kumaliza mapema kunaweza kuchukua muda mrefu na mazoezi ya kutosha, unaweza kujisikia ksumbuka tu wakati unajitahidi kuthibiti hata hivyo kwenye nia njia ipo na wewe utaweza tu nakuamini.

Mwisho, kujifunza mwanaume kumaliza mapema kutampa mpenzi wako raha (enjoyment) kubwa sana kimapenzi. Wanawake hupenda good sex ambayo ni leisure, playful, whole body, massage kwa wingi.
Na wanawake wengi hulalamika kwamba wanaume huwa na haraka tukiwa kwenye miili yao, tupo too much mechanical, tunakimbilia kule chini tuingiza tumalize na tuishie zetu kwa usingizi, tuna focus matiti na maeneo ya uke tu.
Wanawake hujisikia mwili mzima ni uwanja wa kucheza kimapenzi na hushangazwa na wanaume kugundua visehemu kidogo tu katika uwanja mzima na kuvipenda.
Hata uume pia umeumbwa kwa ajili ya leisure, kuchezewa, mapenzi ya mwili mzima, massage ya mwili mazima ndipo sex, kuwa focused kwenye uume peke yake huweza kuupa uume mgandamizo ambao hupelekea kutoa risasi mapema.

Kimsingi kama wanaume wangekuwa wanafanya mapenzi kwa namna ambayo wanawake wanapenda basi kusingekuwa na malalamiko na wanaume wangekuwa na matatizo kidogo yanayohusiana na tendo la ndoa.
Tutaendelea ............................................

Tuesday, April 7, 2009

Kumaliza haraka!

Baada ya kupeana mabusu na romance hadi kila mmoja anakuwa amesisimka kiasi cha kuwa tayari kwa kurushwa hadi kufika kileleni, ghafla baada ya msuguano mmoja tu mwanaume ameshamaliza na tayari hoi anageuka na kulala zake usingizi mzito wakati huohuo bibie bado kwanza ndo alianza kupata raha na sasa ameachwa kwenye mataa anazubaa akiugulia kukosa raha yenyewe.

Jambo la kuhuzunisha ni kwamba baadhi ya wanaume huweza kufika kileleni haraka mno; dakika chache tu baada ya kuingiza uume kwenye uke, ingawa hii humpa mwanaume raha ya ajabu hata hivyo anaweza kumwacha mke wake katika kukatishwa tamaa na kutoridhika hasa kama ni mwanamke ambaye kufika kwake kileleni hutegemea msuguano (thrusting) wa uume kwenye uke wake.

Kawaida mwanaume huweza kuwa tayari kufika kileleni kila baada ya mipigo 50 (kuingiza na kutoka ndani ya uke) [thrusting] na wakati huohuo inachukua zaidi ya dakika 10 kwa mwanamke kufikia kileleni (siyo wanawake wote wengine huwahi).

Mwanaume anapokuwa hana uwezo wa kujizuia kukojoa (ejaculate) mapema huweza kukosa kiwango cha raha ya kutosha anayostahili yeye mwenyewe na mke wake pia, vilevile hukosa raha halisi ya kuwa ndani ya mke wake kwa muda mrefu (mwili mmoja) na hapati zile hisia za ukaribu (intimacy), mapenzi na muunganiko ambao huweza kuwaunganisha wawili wapendanao kupitia tendo takatifu la ndoa ambalo Mungu alilifanyia ubunifu kwa ajili ya mwanaume na mwanamke duniani kuwa pamoja na kufurahia uumbaji wake.
Wanawake wengi huhitaji mume kukaa ndani ya uke kwa muda mrefu unaotosha kwa kadri wanavyohitaji raha na utamu wa hii zawadi ya mwili.
Na njia sahihi ya kuweza kufanikisha hili ni pale tu mwanaume anapokuwa na uwezo wa kuhimili kutokojoa mapema na kuwa na uwezo wa kuwa na hiari wakati gani aweze kukojoa au kutokukojoa.


Fikiria raha inayopatikana kwa mwanaume ambaye anaweza kumhakikishia mpenzi wake anapata raha kwa muda anaoutaka maana tendo la ndoa ni haki yake ya msingi ya kuzaliwa.

Kwa kujifunza unaweza kuwa na uwezo wa kufika muda mrefu vyovyote unataka na kukupa ridhiko la kimapenzi wewe pamoja na mpenzi wako.

Mwanaume anapokuwa kwenye mahaba asipokuwa makini huweza kufika mahali mambo yakawa matamu kiasi kwamba hakuna kurudi nyuma (no point of return) kwa maana kwamba lazima mwanaume akojoe, hana chaguo bali kumaliza hata hivyo kumbuka mke wako ni muhimu pia na mwitikio wa mapenzi kati yako na yeye ni tofauti, ili kumtanguliza yeye unahitaji kufanya kitu nacho ni kuthibiti kutowahi kujokoa kabla yeye hajaridhika.


Habari njema ni kwamba mwanaume yeyote pamoja na wewe unayesoma unaweza kuwajifunza na kuwa mwanaume anayeweza kufika kileleni wakati anaotaka yeye.
Naamini ni ndoto ya kila mwanaume kuwa mzuri katika mapenzi na kuhakikisha mke wake mpenzi anapata kile anastahili wakiwa faragha na zaidi kuweza kumfikisha mwanamke katika kiwango cha juu kabisa cha raha ya mapenzi ambayo ni ndoto ya binadamu yeyote duniani ambaye ana hisia kamili za kimapenzi.

Je, nini kifanyike kuweza kuthibiti kumaliza mapema?
Tutaendelea…………..

Monday, April 6, 2009

Coolidge Effect

Panya dume huwa tayari kwa sex muda wowote kama binadamu mwanaume na panya jike huhitaji mood kuwa sawa ili kujihusisha na sex kama binadamu mwanamke.
Panya jike akiwa akiwa anajisikia vizuri huwa hana shida wakati panya dume akimsogelea kwa ajili ya sex huupeleka mkia wake pembeni kumrahisishia panya dume kumuingilia bila wasiwasi, hata hivyo baada ya dakika chache tu (maskini panya dume) huishiwa nguvu kabisa kwa kuchoka na tendo hilo (mating).
Huku panya jike akiwa bado hajachoka na anahitaji panya dume huwa amelala kama vile amepooza na hutoa mlio kama wa filimbi (mluzi) ambao huashiria kwamba ondoka nimechoka, basi panya jike huridhika, hujivuta na kuondoka kukaa mbali na panya dume ambalo linaugulia uchovu wa sex.

Kitu cha kushangaza ni kwamba akija panya jike mwingine na awe tayari kwa sex, panya dume yuleyule aliyekuwa choka mbaya haijalishi alikuwa amechoka namna gani ataanza sex upya na panya jike mpya na baada ya in and out mara tatu tu anakuwa hoi bin taabani kwamba hawezi tena kuendelea, hata hivyo ukimleta kike mwingine ataendelea na kitendo chake cha kuchangamkia hadi unaweza kumpoteza kwa kufia mwilini mwa panya jike wapya!
Hii huitwa Coolidge Effect, jina ambalo linatokana na rais wa Marekani ambaye wakati wake aliwahi kutembelea shamba la Kuku, na mke wa rais alipata muda kuongea na mtunza shamba ambaye alimwambia tuna huyu jogoo ambaye huwapanda tetea hata elfumoja kwa siku.
Na mke wa rais alimuomba mtunza shamba kumwambia rais (mumewe) hicho kisa hata hivyo huyu rais aliuliza
"je, jogoo huyo humpanda tetea mmoja?"
Na mtunza shamba akasema "hapana," huwapanda tetea tofauti.

Tabia kama hii imeonekana kwa wanyama (males) na kwamba wakati mwingine imeleta shida kidogo.

Pia imejulikana kwamba baadhi ya wanaume huwa jogoo hawiki wakiwa na wake zao ila akifanya cheating jogoo wake huwika kama si yeye.
Wapo mabinti ambao bada ya kupata wachumba wakaamua kufanya nao mapenzi hata kabla ya ndoa na baada ya moja, mbili, tatu na nne siku ameachwa kwenye mataa maana mchumba kapata binti mwingine.
Hata hivyo Binadamu ni tofauti na wanyama wengine, yeye anaongozwa kwa ufahamu, malezi, taratibu za maisha, dini nk,

Pia jambo la msingi kufahamu ni kwamba Mungu ndiye aliyefanya ubunifu wa binadamu kuwa na sex, si binadamu ambao wameumba sex; hivyo Mungu ndiye mwenye uwezo wa maamuzi yoyote tunayojisikia kuhusu miili yetu kuhusu sex na yeye ndiye mwenye blue print halisi ya sex iweje na si hilo tu bali ukipata matatizo yanayohusiana na mahusiano, ndoa, mapenzi nk yeye ndiye anaweza kutupa majibu ya kudumu.

Friday, April 3, 2009

Weekend Njema!

Love is a temporary insanity, curable by marriage.
===========================
All married couples should learn the art of battle as they should learn the art of making love.
Good battle is objective and honest--never vicious or cruel.
Good battle is healthy and constructive, and brings to a marriage the principle of equal partnership.
wwwwwwwwwwwwwwwwwwwww

Thursday, April 2, 2009

Mapenzi ni sanaa, huelezea maisha, leo ni tofauti na jana na jinsi binadamu wanafanya mapenzi kufanya mapenzi hubadilika kila siku, mtazamo wa kufanya mapenzi enzi za bibi yako na babu yako ni tofauti na leo.
suala la kufurahia raha ya mapenzi halina mipaka katika ubunifuna huwezi kupima raha ambayo mtu anapata kutokana na kufanya mapenzi.
Huwezi kuweka mapenzi kwenye box au kujenga fence au kuweka mipaka.
Unaweza kuwa na sanaa bora katika mapenzi au sanaa ovyo katika mapenzi.
Unaweza kujidhania wewe ni bora katika sanaa ya mapenzi hata hivyo ukashangaa mpenzi wako hawezi hata kusisimka kutokana na usanifu wako na unaweza kukatishwa tama na kile ulitarajia.

Wakati mwingine unaweza kushangaa jinsi sanaa yako ya mapenzi inavyopata kibali kwa mpenzi wako kama vile maji yanavyotiririka kwenye mto uliozungukwa na ndege wanaoimba sauati ya asili.

Kila mmoja anatakiwa kufungua nafasi yake kupokea raha mpya ya kimapenzi ilimradi unaishi na upo hai.

Je, ni nini siri ya mahusiano (ndoa) yanayodumu na kumfanya mtu aridhike?
-Kuwa na vicheko?
-Kufanya mapenzi?
-Pesa?
-Uaminifu?
-Urafiki?
-Kufanana?
Kila mtu anaweza kuwa na jibu lake hapo.

Wednesday, April 1, 2009

Ajisikia vizuri kwanza!

Kuna tofauti kubwa sana ya maana na mwitikio wa mapenzi kati ya mwanaume na mwanamke.
Wanaume kawaida wanauwezo wa kutenganisha mwili na moyo
(Body and Heart)

Kwa upande wa wanawake tunaweza kusema wao wamekomaa kimapenzi kuliko wanaume kwa sababu kwao kutenganisha mwili na moyo inakuwa vigumu na wakati mwingine haiwezekani.
Mwanamke anapompenda mwanaume huanza na hisia za ndani za moyo wake then hisia za nje za mwili wake;
wakati mwanaume anapompenda mwanamke huanza kupenda kuanzia hisia za nje za mwilini mwake then hisia za ndani za moyo wake.

Ni rahisi mwanaume kukwambia anakupenda kumbe hakupendi bali anakutamani tu na wanawake wamekuwa wanaumizwa sana na wanaume kutokana na hii style yao ya kupenda kwa kumuweka mtu moja kwa moja kwenye moyo wake.

Utafiti mwingi unaonesha kwamba wanawake wengi huwa hawafurahii kufanya mapenzi na mwanaume asiyempenda;
wakati wanaume wanaweza kufurahia na kupata raha ya mapenzi (kufika kileleni) hata kwa mwanamke asiyempenda.
Ndiyo maana mwanaume anaweza kutembea na mwanamke yeyote hata kama ni mbaya kila idara ukilinganisha na mke wake.
Ndiyo maana matukio mengi ya ubakaji hufanywa na wanaume.
Ndiyo maana nyumba ndogo nyingi (wanawake) si wazuri kama nyumba kubwa (wake zao halisi)

Wanaume wanaweza kutenganisha upendo na kufanya mapenzi (love and sex).
Wanawake hutazama kufanya sex ni kitendo cha ziada baada ya upendo wa kweli na wakati mwingine hufanya mapenzi ili kuimarisha mapenzi kwa mwanaume, wakati wanaume sex ni kwa ajili ya kufurahia tu siyo lazima awe anampenda mwanamke anataka kufanya naye sex.

Kwa mwanaume kufanya sex ni kitu kinachofanywa nje ya mwili (out-of-body experience) kwa sababu viungo vyake vya kufanyia vya sex vipo nje na anapofanya mapenzi anakuwa anafanya kitu kwa mtu mwingine (mwanamke) kama vile kupigilia msumari kwenye ukuta;

Kwa upande wa wanawake viungo vya sex vipo ndani ya mwili na kwao kufanya mapenzi ni kama kumkaribisha mtu ndani ya nafasi ya ndani yake, hivyo inakuwa ngumu kutenganisha mwili, moyo na hisia zake.

Kama ilivyo kwa watu wote kwamba mtu mgeni akiingia nyumbani kwako hutajisikia raha kwanza au hutajisikia salama hadi ufahamiane naye, ndivyo wanawake walivyo.Kwa mwanamke kufanya mapenzi na mwanaume asiyemfahamu au mgeni au asiyempenda ni sawa na mtu anayeingilia mipaka ya shamba lake, (trespacing)

Kumvamia mwanamke bila kuonesha upendo wa kweli ni sawa na kuvamia mipaka ya mashamba ya watu, au ni sawa na kuingia kwenye nyumba za watu bila kukaribishwa.
Wanawake hupenda kuwa na ukaribu na upendo wa kweli ili kumruhusu mwanaume kuwa naye kitandani na kuingia kwenye nafasi yake ya siri kufanya mapenzi.Ndiyo maana huwa wanajisikia kutumiwa na kuumizwa na mwanaume ambaye haoneshi upendo wa kweli.

Wanahitaji mwanaume anayewasililiza, anayewapenda, anayewajali, anayekuwa tayari wakati wanamuhitaji, mwanaume anayebembeleza, mwanaume ambaye anajua kuwahudumia wao kama viumbe rasmi na maalumu ambao Mungu ametoa zawadi kwa wanaume duniani.
Hii ndiyo sababu mwanamke hupenda kujisikia vizuri kwanza ili afanye mapenzi wakati mwanaume hujisikia vizuri baada ya kufanya mapenzi.

Kukagua Msingi!

Katika kujenga au kusimamisha jengo lolote duniani kawaida kuna taratibu ambazo ni sharti zifuatwe ili jengo lisimame, liwe imara na lidumu.

Tumekuwa tukishuhudia majengo mengi yakiporomoka hii ni kutokana na kutofikia viwango hasa uzembe wakati wa kufanya ukaguzi wa ujenzi tangu msingi (foundation).
Pia hata kama jengo likiimarishwa juu wakati msingi ni ovyo au haujafikia viwango bado jengo zima lipo hatarini na haliwezi kufika mbali kwa sababu msingi hautaweza kuhimili kila aina ya dharuba, mitikisiko, upepo na wakati mwingine hata mvua.

Tunaporudi kwenye suala la mahusiano wakati wa uchumba ndiyo wakati wa kuchunguza msingi, ni wakati wa kufanyia inspection msingi kuhakikisha ni kweli una standards zinazotakiwa kuhakikisha jengo linadumu karne hadi karne.

Mtu unayechagua kuoana naye na kujenga maisha yako yaliyobaki hapa duniani ni vizuri akawa na imani, values, interest, standards, mitazamo unayoridhika nayo na kufikia uamuzi wa kukubali kupitisha hati ya kusaini kwamba msingi umefikia viwango vinavyotakiwa (engagement ring) ingawa bado unaweza kuahirisha ujenzi ukigundua kwamba bado jengo linaweza lisisimame kwani kuachana katika uchumba ni kiroho na pia afadhari kuvunja uchumba kuliko Ndoa.
Ni busara kuvunja msingi kuliko kumaliza jengo la ghorofa 25 then linavunjwa.

Wakati unaendelea na inspection ya msingi kama unaona kuna dalili na umethibitisha kwamba nyufa zilizopo zinaweza kusababisha jengo lisisimame, deal with it!,
Usifanye terrible mistake kwani kufikiria kwamba nitaishi naye hata kama ana matatizo hayo au hata kama hili ni tatizo ambalo nitasaidiana naye hadi nambadilisha; thubutu! kawaida hatuwezi na hatutaweza kumbadilisha mtu hata kama upo smart namna gani au una skills za ajabu za kushawishi, suala la ndoa na mapenzi ni gumu utajuta!

Binadamu ni wazuri sana kwa kutoa ahadi hasa katika mapenzi, (at the touch of love, everyone becomes a poet) ingawa ahadi nyingi ni kwa ajili ya kukupata wewe hivyo ni juu yako wewe kuamini kama kweli atakununulia gari wakati kazi hafanyi na mvivu, hana tatizo na dini yako wakati haitambui dini yako, atakupenda milele wakati juzi ulikutana naye ana kwa ana amekaa na rafiki yako katika mkao wa hasara uliotikisa moyo wako kiasi kwamba ile picha ikikurudia unajisikia he is the wrong person.
Anakwambia anakumiss wakati huohuo kuwasiliana na wewe hadi umkumbushe maana hakuna cha simu wala sms wala email wakati simu anayo.
Hapa unafanya uamuzi wa aina yake katika maisha yako na watu wanaweza kukushauri ila mwamuzi ni wewe.
Pia hata kama umeachwa na mchumba inawezekana huo ni muujiza wa kumpata aliyesahihi kwako hivyo usiumize kichwa.

“Don't cry for a man who's left you, the next one may fall for your smile.”