"Marriage is our last, best chance to grow up."

Tuesday, April 28, 2009

Bikira (2)

Eti unaweza kumjua mwanamke bikira kwa kumwangalia jinsi anavyotembea! Kutokana na maandiko ya agano la Kale (Biblia) (Kumbukumbu la torati 22:13 17)
Wanaume wa kiisraeli walikuwa wanatahiriwa (circumcision) na hiki kitendo cha kutahiriwa au kukata govi (foreskin) kilikuwa ni agano (covenant) na Mungu wao, agano la damu kwa maana kwamba ubikira wa mwanaume ulitolewa kwa Mungu.
Hii ilikuwa na maana kwamba mwanaume sasa alikuwa ni mali ya Mungu (belong to God).
Kwa kutahiriwa damu ilitoka na damu kutoka ni kuonesha kutoa bikira na yeye kuwa na mahusiano na Mungu.

Mwanaume aliunganishwa na Mungu ambaye sasa anakuwa chanzo cha uwezo wake.
Agano la mwanaume na Mungu lilihitaji damu kutoka katika govi la uume na si katika sehemu nyingine ya mwili wa mwanamke kwa sababu uume ndiyo ulitumika pia kwa kuvunja kizinda (hymen) mwanamke kutoka damu kwa ajili ya agano kati ya mwanaume na mwanamke mbele za Mungu kuwa kitu kimoja.

Hii ina maana kwamba kwa mwanamke bikira kutoa damu ni muhuri wa agano kati ya mwanaume na mwamke mbele za Mungu.

Je, katika agano jipya bado tunahitaji damu ya binadamu kwa ajili ya agano?
Baada ya Yesu Kristo kuja yeye alitoa damu ya thamani msalabani ambao hutuunganisha wanadamu wote na Mungu.
Mwanaume na mwanamke wote wanaunganishwa na damu ya Kristo na wao kwa pamoja wanakuwa bikira (bibi harusi mtarajiwa) hadi siku Yesu akija kulichukua kanisa na kila mmoja ambaye atakutwa hana bikira maana ataachwa.
(Kama umeokoka utanielewa nazungumzia kitu gani)
Hivyo basi suala la msingi hapa si mwanamke kuwa bikira na kutoa damu ya agano kwa mume au mume kutahiriwa kutoa damu ya agano kwa Mungu bali kuikubali damu ya agano jipya ambayo ni Yesu Kristo.
Kumpokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi ndiyo ubikira wa kweli

Je, inawezekana mwanamke bikira kuwa na mimba?
Ndiyo inawezekana, ikitokea sperms zinkawa deposited nje ya uke hata kama hakukuwa na penetrative sex kwani sperm ni genius au smart sana zikipata mwanya hasa kutokana na kufunguka kwa vitundu kwenye kizinda (hymen)

Je, ukiwa Bikira muda mrefu unaweza usizae watoto?
Uwongo mtu hasa kama mwanaume bado ana uwezo wa kuzalisha sperms na kama mwanamke bado anapata siku zake.

Je, unaweza kujua bikira kutokana na anavyotembea?
Thubuti! Hakuna external signal ambayo huweza kukufahamisha kama kweli mwanamke ni bikira au mwanaume ni bikira ukweli anajua yeye.

Je, Ukisubiri sex hadi uolewe au uoe ni mshamba kama si msenge?
Ukweli ni kwamba wewe ni smart sana kuliko wajinga wote wanaojiingiza kwenye masula ya sex kabla ya ndoa, Wazinzi na waasherati hawana nafasi katika ufalme wa Mungu.
Pia kusubiri kunakufanya uishi kwa amani na kutimiza malengo ya maisha bila hofu ya UKIMWI.

Je, Ukiwa in love na mtu lazima mfanye mapenzi?
Kuwa na mpenzi haina maana sex lazima, Pia inatokana na mipaka mliyowekeana.

Je, kwa mwanamke kudumisha urafiki na mwanaume sex ni muhimu?
Ukweli unajidanganya, kama urafiki wako ok shaky kiasi hicho kumbuka sex si tiketi ya kukufanya akupende zaidi bali tiketi ya kukupiga chini muda wowote na yeye kubeba kitu kipya kabisa.
Kama huamini nitumie email nitakupa mifano zaidi ya 100.

15 comments:

Anonymous said...

BROTHER LAZARUS...NAKUUNGA MKONO KABISA KTK MADA HII.

This is what i believe about being a virgin woman till u get marry.


Here are three perfectly good ressons I believe;

Yes. Sex is worth waiting until marriage. You know the feeling if you know that you can't a chocolate bar until tomorrow? And waiting for it makes u anxious and excited? Well, dont you know how much better tasting it is when you get it the next day just because you waited. If you ate it yeseterday it wouldnt be exciting because you didnt wait for it. Having sex too soon may ruin it for you.

Also, think of it like this. Everytime you have sex b4 marriage or have a serious relationship it takes a piece of your heart away. So by time your married you have like no heart left for your true love.

The last reason is basically if you believe in God it's totally agaist his will.

By
Shyrose USA

Yasinta Ngonyani said...

Mimi nina swali Je ni msichana tu anatakiwa kuwa BIKIRA? Yaani je? kijana hatakiwi kuwa BIKIRA pia?

Lazarus Mbilinyi said...

Dada Yasinta,
Tangu mwanzo mwanaume na mwanamke walitakiwa kuoana wakiwa mabikira hadi sasa bado mwanaume na mwanamke wanatakiwa kuoana wakiwa mabikira.

Ubikira wa mwanamke ni fahari ya mume wake na ubikira wa mwanaume ni fahari ya mke wake.

Upendo daima.

fikirikwanza said...

Hii somo kubwa na safi sana ,labda kwa kusaidia kujibu swali la yasinta ni hivi.Kama wasichana wote ambao hawajaolewa ni bikira basi ni logic kwamba wanaume wote ambao hawajao ni bikira nao.

Anonymous said...

hi kaka, naona kiswahili sahihi ni govi na si gomvi
nawasilisha

Lazarus Mbilinyi said...

Samahani kwa kiswahili kibovu, nashukuru kwa kunisahihisha.

Next time nitajaribu kuangalia zaidi hata hivyo namini niliruka wakati narudia spellings check kwa kishwahili.

Upendo daima

Anonymous said...

Asante sana kaka Lazarus kwa mada hii! naomba kuuliza maswali madogo 2,,je kama msichana anafanya romantic love hadi anafika kileleni bila kuingiziwa uume (yaani anakuwa mtupu na ananyonywa kila milango mitano ya fahamu hadi kisimi chake)je huyo ni bikira? na je msichana hajawahi kufanya mapenzi hata siku moja na akabakwa siku moja na akasababishiwa maumivu makali sana je huyo atajiesabia ni bikira au sio? ni hayo tu napenda kujua kaka
mdau Singida

Lazarus Mbilinyi said...

Mdau wa Singida,
Asante sana kwa maoni yako, kuhusu maswali yako mawili ukweli kwa ufupi ni kwamba definition tuliyonayo ya maana ya bikira bado haitoshelezi.
Kwa mtazamo wangu suala la kupoteza bikira linahusisha sehemu mbili yaani Emotional and Physical na kwangu kitendo chochote kinachopelekea mwanamke au mwanaume kusisimka, na kufika kileleni (intimate sex) hata bila penetration nmi sex na mtu anakuwa amevunja bikira.
Kama unatoa mwili kwa mtu mwingine na akakupa stimulation hadi ukafika kileleni au hata usipofika ile intention ni sex na hakuna bikira hapo.
Pia wale ambao wanabakwa au kunajisikiwa ukweli bado emotionally wapo bikira ingawa wamefanya sex na bado wanajitunza.
Kuwa bikira ni kitu ambacho mtu anakitunza na hukitoa mwenyewe na si kupoteza.

Ingawa life style ya sasa kwa definition ya zamani ni kweli unaweza kukuta mwanamke anajiita bikira ila kashafanya mapenzi bila penetration kitu ambacho ni kweli huyu ni Bikira kwani amefanya sex tayari.

Upendo daima

Anonymous said...

asante sana kaka,majibu mazuri sana
mdau
Singiga

Zeddie said...

Dah Bro Lazarus nimekukubali ukweli kwa hii mada kweli nilikuwa nyuma ila sasa naweza kuwa mtu kati ya watu baada ya kusoma hii

big up sana Bro

by Zeddie

Lazarus Mbilinyi said...

Zeddie,

Asante sana kwa hongera, nami nakupa hongera kwa kupita hapa na kupata tips ambazo naamini zinaweza kukufanya uwe bora zaidi linapokuja suala la mahusiano na yule unayempenda.

Thank you so much

ibrahim juma said...

thanx kaka kwa xom zur bt inakuwaje kwa m2 alyefkxha umr wa miaka20 na hajafanya chchte na kabla ya kuoa/kuolewa inakuwaje ktk sex

ibrahim juma said...

thanx kaka kwa xom lako bt naomba nxaidie je inakuwaje kwa mwanaume alyefkxha miaka20 bla kufanya tendo la ndoa?

ibrahim juma said...

hvi je kjana kama hajawah kufanya sex mpaka anaoa af ictoxhe anakutana na bint bikra hpo inakuwaje ktk ufunguz wa suala hlo? nxaidie bro

Anonymous said...

Bwana Mbilinyi hii apa email yangu nitumie hio mifano 100
(abasandrewshiguta@gmail.com)