"Marriage is our last, best chance to grow up."

Friday, April 24, 2009

Bikira

Mabinti wa kizulu huko Lamontville Afrika kusini wakisubiri kukaguliwa kama bado ni mabikira huku nyuso zikiwa zimepakwa udongo.
(Picha kwa hisani ya Ellen Emendorp wa NYT)
Kutokana na desturi za huko Sri Lanka bibi harusi ni lazima athibitishe kwamba ni bikira usiku wa harusi yake.
Kila bibi harusi hutakiwa kubeba kitambaa cheupe ambacho huwekwa chini wakati wa tendo la ndoa kwa mara ya kwanza usiku wa kwanza kwa maharusi ili kuthibitisha kwamba bibi harusi alikuwa bikira.
Kitamba kuwa na damu ni certificate kwamba bibi harusi alikuwa bikira.
Na wapo mabibi harusi hukutana na wakati mgumu baada ya kujikuta hawakutoa damu yoyote ingawa ni kweli wao ni mabikira.
Hii ni kwa sababu wasri Lanka kama jamii zingine duniani bado wanaamini bikira yeyote hutoa damu siku ya kwanza na Yule ambaye hakutoa damu huonekana alijihusisha na ngono kabla.

Hiki ni kipimo cha kitambaa kuwa na damu ni kipimo potofu kwani na unscientific, wanawake wengi innocent huumizwa na kuonekana hawana quality ya kuitwa bikira wakati ni bikira.
Ni vizuri watu kujua uhusiano uliopo kati ya kizinda (hymen) na ubikira (virginity)

Bikira ni nani?
Bikira ni mwanamke au mwanaume ambaye hajawahi kufanya mapenzi (penetrative sex) na si lazima awe mwanamke ambaye atatoa damu siku ya kwanza ya tendo la ndoa.
Ni vizuri kufahamu kwamba asilimia 20% - 25% ya mabikira huwa hawatoi damu yoyote kutokana na muundo wa kizinda (hymen)
Wakati mwingine kizinda huondolewa kwa kufanya mazoezi mazito, kupanda baiskeli, kukwea miti na ifahamike kwamba kufanya mazoezi hakuwezi kuondoa ubikira.
Kizinda ni nini?
Kizinda ni ngozi nyembamba sana (membrane) ambayo huziba entrance kwenye uke.
Ina matundu ambayo hutofautiana kwa size ambapo damu ya mwezi kwa mwanamke huweza kupita kila mwezi.

Kuna aina Nne za vizinda
1. Kizinda cha kawaida (normal hymen),
2. Kizinda kisicho na tundu lolote [huhitaji surgery wakati mwingine] (Imperforated hymen),
3. Kizinda chenye tundu dogo sana (Microperforated hymen)
4. Kizinda chenye tishu za ziada na kufanya matundu mawili (septate Hymen)

Bado haijajulikana kazi ya kizinda ni nini, kwani baada ya sex mara ya kwanza huchanika na kuachana na kubaki historia.

Kizinda kiligunduliwa mwaka 1544 na Daktari wa kiarabu Ibn Sinna hata hivyo kufika karne ya 16 watu walikuwa wana imani potofu kwamba kizinda ni ugonjwa na dawa yake ilikuwa ni sex inayofuatana na mwanamke kuolewa.

Kutokuwa na kizinda au kutokutoa damu siku ya kwanza ya sex si evidence kwamba mwanamke si bikira wapo wanazaliwa hawana wengine nyembamba sana na wengine huweza kutoka kutokana na aina ya mazoezi au accidentally.
Damu ambayo hutoka siku ya kwanza ya sex ni kidogo sana linaweza kuwa tone hakuna mwanamke amewahi kutoa damu na kulazwa au kuhatarisha maisha yake kwa sex mara ya kwanza.
Pia ifahamike kwamba mwanamke huweza kujisikia maumivu kidogo au discomfort wakati wa tendo la ndoa.
Hata hivyo maumivu mengi huhusiana na woga na ignorance (knoweledge is power), wakati mwanamke anakuwa na hofu, woga wakati wa tendo la ndoa misuli ya uke hukaza na uke huwa tight na mwembamba na wakati mwingine hushindwa kutoa lubricants kwenye uke kutokana kuwa na hofu na matokeo yake ni kusikia maumivu wakati wa penetration.
Pia inawezekana mwanaume hakumuandaa vya kutosha na pia inawezekana wakati wa kumuandaa mwanamke mwenyewe hakuwa relaxed na kuwa tayari kupokea tendo zuri la sex akihofia kuumizwa.

Je, mwanamke kutunza bikira hadi wakati wa kuolewa kuna heshima au fahari yoyote?

Kwa nini suala la kuwa bikira kwa wanaume katika jamii zote linakuwa halina uzito bali wanawake tu?

Je, wakati wa kuoa au kuolewa karne hii ya 21 suala la bikira ni muhimu kuzingatiwa?

Tutaendelea…………………………..

10 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Tamaduni9 nyingine jamani kweli ni potofu. Kuna mambo mpaka dunia hii bado watu wanayafuata na kutaamini. kazi kwelikweli

Yasinta Ngonyani said...

Tamaduninyingine jamani kweli ni potofu. Kuna mambo mpaka dunia hii bado watu wanayafuata na kutaamini. kazi kwelikweli

Anonymous said...

Nasikia kwanza kuna wanawake huwawanafanya ujanja tuu hadi mbuzi alipwe kumbe hawana chochote. Na wengine hujitete eti michezolakini nasikia si rahsi sana kutokea kitu kamahicho . hata hivyo naamini wanaume walio ona wake zao wana bikira huwa na imani na wake zaokuliko wale ambao waliona patupu.
edmund.

Lazarus Mbilinyi said...

Ni kweli bado suala la bikira linachukuliwa jambo la msingi sana katika kuoana kwa baadhi ya tamaduni hadi leo.
Pia bado kuna kudanganyana kwingi sana kuhusiana na suala la bikira pia wapo wanaume ambao bila mwanamke kukiri kwamba ni bikira hakuna ahadi ya kuoana.

Kila mtu ana mtazamo wake!

Upendo daima

Anonymous said...

mie binafsi naona wanawake nasijidangaje ,naona ni heri mwanamke ajitunze hadi siku yake kuliko kuolewa na miwasiwasi kibao. sisemi kuwa wanaume sii muhimu ila mwanamke bkira ni fahari na anakuwa na ujasiri mbele ya mumewe. naogopa sana kuoa mwanamke ambaye siye bikira kwa sababu atakuwa hajiamini; na hata kama akiniambia hawezi kujua kama kweli nitampenda kwa asilimia zote. nakumbuka katika somo moja uliandika mwanamke kumpa ruhusa mtu afanye naye mapenzi ni kama kumpa mtu funguo angia ndani ya nyumba. kwa hiyo ni vyema walio bikira waendelee kuwa ikira ni zawadi nzuri kwa wale watakao bahatika kuoa. edmund.

Lazarus Mbilinyi said...

Ni kweli,
NI vizuri kwa aliyebikira kuzidi kujitunza kuwa bikira hadi siku ambayo anapata mume au mke (ndoa au harusi)
Kwenda dukani na kung'ata chungwa eti unaonja kama lina ladha nzuri ili ununue hakuna muuzaji anayeweza kukubali pia suala la ndoa ni muhimu sana na si kama kununua gari kwamba uendeshe kwanza ndo ujue linafaa au hapana, Kumbuka ukiwa unajitunza na kuishi maisha matakatifu hukuwezesha kuwa na amani ya kweli na Mungu na unayempenda.

Upendo daima

Bongo Pixs said...

Juzi nilikutana na jamaa ananadi dawa za kurejesha bikira, kuongeza makalio na kusimamisha chuchu kwa kina mama.


Lakini kabla ya hapo nilipata kusikia kuwa kuna binti ambaye alikuwa mwingi wa mambo kiasi cha kuchoropoa mimba kadhaa eti alikutwa na bikira siku ya ndoa yake!! nilipigwa na butwaaaa


Je ni kweli kuna bikira za kutengeza?????

Lazarus Mbilinyi said...

Bongo pix,

Ni kweli dawa za kurudisha bikira zipo si Africa tu bali hata huku America naamini hata ulaya na Asia zipo.

Hata sijajua lengo linakuwa kitu gani kwani Bikira ina uhusiano mkubwa na kuwa hujafanya mapenzi kwa njia yoyote.

Kazi kwelikweli

Anonymous said...

Mimi ni bikira,namwekea bwanangu mtarajiwa zawadi ya pekee isiyo na substitute

Fadhili Moperon said...

Yehova Mungu Hajaruhusu Ngono Kabla Ya Ndoa Hata Karne Hii.