"Marriage is our last, best chance to grow up."

Tuesday, April 28, 2009

Busu

Busu hiloooooooo pokea!Busu husaidia kuwezesha moto wa mahaba kuendelea kuwaka kati ya wapenzi.
Kumbuka mpenzi wako huhitaji kujisikia yupo appreciated na zaidi anapata mapenzi (love and affection) kutoka kwako na njia nzuri ni kumpa busu.

Bahati mbaya ni kwamba wanandoa wengi wameshikwa na kunaswa na mtego wa u-busy hadi imefika wanasahau kuwabusu wapenzi wao.
Niambie wewe unayesoma sasa hivi hapa umembusu mke wako au mume wako lini?
Nahisi umesahau!
Plainly; mahusiano yanahitaji kazi, hasa kwa huyo special someone wako in your life kama ulifanya kazi kumpata kwa nini sasa ulegeze kamba, kaza uzi hakikisha uzi uleule uliotumia kumpata ndo huohuo unatumia kudumisha penzi na si kudumu tu bali linakuwa sustainable.

Kubusu hujenga intimacy kati ya mke au mume pia hufanya bonding iwe strong na kuhufanya wewe mwenyewe ujisikia vizuri na afya njema.
Nini faida za kubusu kiafya?
Busu ni afya kwa meno yako, wataalamu wamefanya tafiti na kugundua kwamba busu kuzuia plague kujijenga kwenye meno na hii ina maana utapunguza safari kwa daktari wa meno.

Busu ni afya kwa moyo wako (heart) kwani wakati wa kubusiana mnazalisha adrenaline ambazo husababisha moyo kuongeza speed na damu kwenda sehemu zote za mwili.

Kila mwanaume au mwanamke ambaye humuaga mwenzake asubuhi kwa busu utafiti unaonesha anaongeza miak 5 zaidi kuishi duniani.
Kama huwa hubusu wakati unaagana na mwenzi wako asubuhi unajipiga panga miaka 5 kuishi.

Kubusu hukuongezea self esteem na kujisikia upo appreciated kwani busu ni tamu na raha.

Mabusu hupunguza kuzeeka (aging) kwani mnapobusiana huhusisha misuli zaidi ya 29 kwenye eneo la mashavu na shingo.

Kubusu huchoma calories kati ya 6 – 12 na mkiongeza na love making huweza kufikia 300 na utajisikia raha.

Kubusu huondoa stress, huweza kutoa ocytocin, homoni ambayo hufanya mtu kujisikia vizuri.

Hakikisha unapobusu ni zaidi ya sekunde 10 ili kupata matokeo.

Hivyo basi wewe na mpenzi wako go ahead, kwa afya na furaha sherehekea kila siku kwa kupigana mabusu.
Je, kuna aina ngapi za mabusu?
Tutaendelea.............................................................

6 comments:

Mwanasosholojia said...

Kaka Mbilinyi, kweli hapa ni The Hill of Wealth!najifunza mengi sana, shukrani..Hii ya busu, maana na aina zake imenikosha sana. Nafikiria cha kuandika, umenipa changamoto!

Anonymous said...

Nashukuru sana brother kwa somo lako big up napendelea sana blog yaka inanielimisha sana

Lazarus Mbilinyi said...

Mwanasosholojia,
Hongera sana kwa maoni yako ni kweli tukiwa wazuri kubusu kila siku kwa wale tumeamua kuishi nao inaleta raha pia kubusu ni lugha kama lugha zingine kwa busu lako naweza kujua mume wangu au mke wangu leo mood yako ipoje.

Kujifunza ni moja ya kazi au efforts za kuimarisha ndoa zetu na "Knowledge is Power"

Upendo daima

Anonymous said...

Asante sana kaka Mbilinyi kwa somo lako zuri,nakubaliana na wewe kwa yote uliyoyaelezea,lakini bali ya yote kuna hii ya kunyonyana ulimi na kubadilishana mate inakera sana,japo ni tamu nahisi kuliko zote,na usipofanya hivyo mpenzi au mwanandoa wako atahisi humpendi...je naweza sema mapenzi ni uchafu? au laa?ni hayo tu maoni yangu
Asante sana
Mdau
Singida

Lazarus Mbilinyi said...

Mdau wa Singida,

Hongera sana kwa maoni yako, kwa ujumla tunapozungumzia mapenzi ndani ya Ndoa kwa kuwa ni baraka na makusudi ya Mungu mapenzi (sex) iwe ndani ya ndoa hivyo mapenzi kwa ujumla si uchafu bali ni utakatifu, hayo mabusu na kila aina za flavor zote ni utakatifu, ila mapenzi nje ya ndoa ni uchafu pia mapenzi kinyume na maumbile ni dhambi kubwa.
Ukitaka kujua ukweli soma kitabu cha wimbo uliobora ndo utajua mapenzi si uchafu bali utakatifu.

Upendo daima.

Anonymous said...

Kaka asante sana kwan unatupa shule ya maana kwan hya mambo n kufundishana wengine n washamba kwa kwel asante mwanalizombe pamoja sana.chacha