"Marriage is our last, best chance to grow up."

Monday, April 6, 2009

Coolidge Effect

Panya dume huwa tayari kwa sex muda wowote kama binadamu mwanaume na panya jike huhitaji mood kuwa sawa ili kujihusisha na sex kama binadamu mwanamke.
Panya jike akiwa akiwa anajisikia vizuri huwa hana shida wakati panya dume akimsogelea kwa ajili ya sex huupeleka mkia wake pembeni kumrahisishia panya dume kumuingilia bila wasiwasi, hata hivyo baada ya dakika chache tu (maskini panya dume) huishiwa nguvu kabisa kwa kuchoka na tendo hilo (mating).
Huku panya jike akiwa bado hajachoka na anahitaji panya dume huwa amelala kama vile amepooza na hutoa mlio kama wa filimbi (mluzi) ambao huashiria kwamba ondoka nimechoka, basi panya jike huridhika, hujivuta na kuondoka kukaa mbali na panya dume ambalo linaugulia uchovu wa sex.

Kitu cha kushangaza ni kwamba akija panya jike mwingine na awe tayari kwa sex, panya dume yuleyule aliyekuwa choka mbaya haijalishi alikuwa amechoka namna gani ataanza sex upya na panya jike mpya na baada ya in and out mara tatu tu anakuwa hoi bin taabani kwamba hawezi tena kuendelea, hata hivyo ukimleta kike mwingine ataendelea na kitendo chake cha kuchangamkia hadi unaweza kumpoteza kwa kufia mwilini mwa panya jike wapya!
Hii huitwa Coolidge Effect, jina ambalo linatokana na rais wa Marekani ambaye wakati wake aliwahi kutembelea shamba la Kuku, na mke wa rais alipata muda kuongea na mtunza shamba ambaye alimwambia tuna huyu jogoo ambaye huwapanda tetea hata elfumoja kwa siku.
Na mke wa rais alimuomba mtunza shamba kumwambia rais (mumewe) hicho kisa hata hivyo huyu rais aliuliza
"je, jogoo huyo humpanda tetea mmoja?"
Na mtunza shamba akasema "hapana," huwapanda tetea tofauti.

Tabia kama hii imeonekana kwa wanyama (males) na kwamba wakati mwingine imeleta shida kidogo.

Pia imejulikana kwamba baadhi ya wanaume huwa jogoo hawiki wakiwa na wake zao ila akifanya cheating jogoo wake huwika kama si yeye.
Wapo mabinti ambao bada ya kupata wachumba wakaamua kufanya nao mapenzi hata kabla ya ndoa na baada ya moja, mbili, tatu na nne siku ameachwa kwenye mataa maana mchumba kapata binti mwingine.
Hata hivyo Binadamu ni tofauti na wanyama wengine, yeye anaongozwa kwa ufahamu, malezi, taratibu za maisha, dini nk,

Pia jambo la msingi kufahamu ni kwamba Mungu ndiye aliyefanya ubunifu wa binadamu kuwa na sex, si binadamu ambao wameumba sex; hivyo Mungu ndiye mwenye uwezo wa maamuzi yoyote tunayojisikia kuhusu miili yetu kuhusu sex na yeye ndiye mwenye blue print halisi ya sex iweje na si hilo tu bali ukipata matatizo yanayohusiana na mahusiano, ndoa, mapenzi nk yeye ndiye anaweza kutupa majibu ya kudumu.

No comments: