"Marriage is our last, best chance to grow up."

Monday, April 13, 2009

Eti hatuwasikilizi!

Etu huwa hatuwaelewi!
Wanaume tunapigiwa kelele sana kwamba mkiongea huwa hatuwaelewi na hata tukiwaelewa tunafanya tofauti na tukifanya tofauti tunakuwa wakali kukubali ukweli.
Ukweli ni kwamba mnapoongea mnaongea kwa maneno mengi mno na kama si hivyo basi mnalalamika mno (kefyakefya) au mnasisitiza mpaka tuhisi umekuwa mama enzi za utoto wetu au wakati sisi ni watoto wa shule ya msingi.
Mwanaume gani anataka kuwa mtoto wa shule?
thubutu hakuna!
Pia lazima mfahamu kwamba ile sehemu iyotunza maneno mnayotuambia mkiwa mmekasirika ni sehemu ileile tunatunza kumbukumbu za mechi (au mambo ya sports) za ligi kuu ya Uingereza (Chelsia ilivyomfunga Liverpool) sasa hapo utajua mwenyewe.

Eti anawaangalia sana wanawake wengine.
Baadhi ya wanawake huendelea kuwasuta waume zao maswali kwa nini huwa hanawaangalia wanawake wengine mfano wakiwa njiani, dukani, au mitaani. Sidhani kama kuna kosa kwa mwanaume kumuangalia mwanamke mwingine na kumpa heshima zake kama amependeza au ni mzuri as long awe anampa credit na mke wake katika maisha yao.
Ukweli wanaume tunawapenda wake zetu to death, hata hivyo kuwaangalia wanawake wengine haina maana kwamba tunawatamani na kwamba tuna tamaa sana.
Pia wewe mwanamke unayesoma hapa mwanaume akikuangalia hadi unastuka ujue mumeo amepata mke bomba!

Eti huwa wanaume hatuwasifii wake zetu;
Ukweli graph ya kukua kimapenzi wanaume hukua kila mwaka, hii ina maana kwamba kama mwaka huu au mwaka uliopita nilikuwa zikupi sifa kutokana na kazi unafanya hii haina maana kwamba sikupendi, nakupenda sana (I love u to death or from earth to the moon) huwa tunakua polepole na tunabadilika hivyo tuombee tu.
Pia tuna nafasi kubwa sana katika emotional chart yetu kujifunza na kubadilika hivyo tupe muda na utaona mabadiliko.

Eti unataka kujua mahusiano yake ya zamani yalikuwaje?
Kuna watu wengine hushangaza sana kwani mmekubaliana kuoana na sasa mpo kwenye ndoa, kuingia tu unanza sasa kuchokonoa na kutaka kujua mahusiano ya nyuma ya partner wako ili um-control vizuri.
Mwache awe kama alivyo ndo maana umependana naye na mkakubaliana kuoana kitendo cha kuanza kutaka kujua kila kitu kuhusu yeye yuko nyuma unaweza kujikuta unaanza kumsahihisha na kumkosoa au kukasirika na vitu ambavyo vilipita na ameshabadilika.
Jisikia vizuri tu jinsi alivyo sasa, hizo kumbukumbu za zamani unazoingiza kwenye memory disk yako ya ubongo zinaweza kukupa hisia mbaya ukaanza kumuona hafai wakati amebadilika.
Kawaida past huwa inadanganya kwa sababu haipo sasa hivi, hata hivyo let the past be the past and it will stay there.

Eti tunapenda sana michezo
Ni kweli tunapenda sana michezo ila wakati mwingine hatupendi kukaa mahali ambapo mke wako mwenyewe amekasirika, hachangamki, kila wakati kulaumu tu, kelele mtindo mmoja, mara hujafanya hiki au kile, yaani mwanamke unajua kila kitu nakumsemesha mwanaume hadi anashindwa kupumua. Ndiyo maana huwa tunaenda kuangalia michezo mbalimbali wakati mwingine mnakuwa mmetuchosha hahaha!

Eti tukiahidi hatutekelezi!
Ukweli ni kwamba kuna wakati hata tukiwaeleza ukweli humuamini so inabidi tuwaahidi mambo makubwa makubwa na kweli tukiwaahidi mnafurahi hadi hadi mnaenda kuwaambia rafiki zenu na siku hiyo ukiwahidiwa kila kitu nyumbani kinakuwa kama kusuma mlevi.
Kama mnataka tusiwaahidi mambo makubwa muwe mnaridhika na kutotaka mambo makubwa.
Just kidding!
No comments: