"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, April 8, 2009

Kumaliza haraka (ii)

Kawaida baada ya mwanaume kuwa na tabia ya kumaliza haraka kinachofuata ni kuanza kukwepa sex kitu ambacho inakuwa ngumu zaidi kuthibiti tatizo, mwanaume akiwa anauwezo wa kuthibiti kumaliza mapema pia huweza kuwa na hamu zaidi ya kufanya mapenzi.

Wengine hutumia njia ya kuondoa mawazo kujihusisha na tendo lenyewe kwa kuwaza vitu vingine hata hivyo hapo ni kujinyima raha na huweza kupelekea vitu kuwa ovyo zaidi.
Si vema kuhamisha mawazo yako kutoka kwenye akili zako wakati wa tendo la ndoa kwani ni sex muunganiko wa roho, mwili na nafsi.
Jambo la msingi ni kuwa na ufahamu wa viwango tofauti vya msisimko (sensation) wa kimapenzi kuhusiana na kiungo chako (uume).
Unatakiwa kujua ni namna gani unajisikia (feel) unapokaribia kufikia hatua ambayo hakuna kurudi nyuma (ejaculatory inevitablility kifupi EI).

Ukishakuwa umefahamu unavyojisikia kuelekea point of No return hapo haitakuwa vigumu kufanya marekebisho ambayo yatakuruhusu kubaki umesisimka lakini bila kumaliza (kukojoa).

Kusisimka kimapenzi huwa ni mzunguka wa hatua 4 muhimu ambazo kwanza ni kupanda kwa mdadi (excitement phase) huu ni wakati ambao kupumua huongezeka, uume husimama (hudinda), hatua ya pili ni kilimani (plateau stage) hii ni hatua ambayo uume huwa umebaki umesisimka kwa kiwango cha juu, hatua inayofuata ni hatua ya tatu ambayo ni kumaliza au kukojoa au (orgasmic with ejaculation) na hatua ya mwisho ambayo kupumua hurudi kama kawaida na uume hurudi na kuwa kawaida (resolution phase).
Ufunguo muhimu katika kuthibiti kumaliza mapema ni ku-maintain hatua ya pili (plateau phase) yaani kubaki hapo kilimani bila kupiga risasi hata kama umelenga vizuri na unajisikia kuachia, hapa ndipo panahitaji imani na kujikana maana huwa ni kuelekea kwenye raha kamili ya sex kwa mwanaume, ila kumbuka uliye naye anahitaji uendelee zaidi.

Nini kifanyike kuthibiti hii hali?
Usitumie drugs au kilevi eti ndo unaweza kuthibiti hii hali, vitu kama hivi huweza kukupa interference na kupunguza uwezo wa kuelewa wakati muhimu wa wewe kuthibiti kumaliza mapema.
Kwanza jikubali, wanaume wengi huamini kwamba sex ni kwenye uume tu na pia kufanya mapenzi ni pale uume ukiingia kwenye uke tu.
Kufikiria hivyo ni tiketi ya moja kwa moja ya mwanaume kuwahi kukojoa au kumaliza.

Kufanya mapenzi kunakoridhisha (best sex) ni pamoja na kupeana mahaba, romance kuanzia juu kichwani kwenye nywele hadi kwenye kucha za vidole miguuni.
Mwanaume anayejifunza kujipa raha kimapenzi kupitia sehemu zote zinazompa raha (chuchu, lips, shingo, midomo, ulimi, nk) huweza kurelease tension kupitia hizo sehemu na kutosubiri sehemu moja tu yaani uume ndo iwe sehemu ya kupata raha ndo maana huweza kukojoa mapema.
Ni kwamba mwanaume anakuwa amefunga outlet zingine na kubaki na uume tu hivyo ni rahisi kufikia point ya no return tena kwa haraka mno.
Ukishajifunza kupata raha ya mapenzi (sexual pleassure) kuanzia nywele kichwani hadi kucha miguuni maana yake mwili mzima unachukua raha ya mapenzi badala ya uume peke yake na matokeo yake utabaki ndani ya mke wako kwa muda mrefu.

Kujipa raha ya mapenzi ya mwili mzima ni njia ya ku-relax na kurelax ni moja ya njia muhimu za kujipa good sex.
Kwa mfano kuoga pamoja kwanza au kufanyiana massage kwanza kabla ya kuanza kwa tendo la ndoa husaidia mwanaume kurelax na zaidi kuupa mwili mzima sexual pleassure matokeo yake ni kufanya mapenzi kwa muda unaotosha na bibie kuridhika.

Kuwa na uwezo wa kupumua vizuri (deep breath) hii haina maana kwamba wakati unafanya mapenzi huwa hupumui, la hasha bali upumuaji wako inawezekana si ule usiotakiwa kwani wanaume wengi huzuia kupumua wakiwa kwenye sex.
Wengine huogoa kusikika wanapumua tofauti, sex ni kazi kama kazi zingine sasa usipopumua unadhani kitatokea nini, ikiwezekana pumua huku unatoa visauti, achia kupumua usijivunge kwani unapoficha kupumua maana yake unakaribisha uume ukusaidie kupumua na njia sahihi kwa uume kupumua ni kukojoa mapema.
Wengi baada ya kujifunza kupumua kwa kujiachia wamefanya mabadiliko makubwa sana katika muda wa kuwa ndani bila kumimina risasi.
· .
Ukishajua kuutumia mwili mzima kuhusika na raha ya mapenzi pamoja na kupumua sasa inakuja technic nyingine ya kujipiga stop.
Unaweza kuwasiliana na partner wako jinsi ya kupeana signal kwamba nakaribia kile kituo ambacho nikifika sitarudi tena, hakuna break.
Unaweza kutoa uume nje huku ukiendelea kupumua na ukiona unapata zile feelings kwamba huwezi kukojoa basi unaweza kurudi na kuendelea tena, kiasi cha kujipiga stop na kuendelea ni uamuzi wa ninyi wawili mnaohusika hasa baada ya mke kuridhika.

Kwa wwale ambao kufanya mapenzi kupo katika level nyingine (oral sex) wanaweza kutumia oral sex kuthibiti mwanaume kumaliza mapema kwa mwanaume kujipa stop akiona anakaribia kumaliza kwa oral sex hii ni baada ya kupata mafanikio hasa baada ya kuona sasa mwanaume anaweza kwenda mbali zaidi ya kawaida yake.

Pia aina ya milalo wakati wa mapenzi huchangia mwanaume kumaliza mapema, kwa mfano missionary position (mwanaume juu mwanamke chini) huu huwezesha mwanaume kumaliza haraka kuliko mwanamke kuwa juu na mwanaume chini, otherwise mwanaume ni vizuri ukafanya utafiti wako kujua ni mlalo gani huwa unajisikia kuchelewa kumaliza na mke wako kuwahi kufika kileleni.

Pia ni vizuri kufanya mapenzi bila kuwa mabubu,kufanya mapenzi huku mnaongea husaidia mwanaume kurelax (na mwanamke pia) na husaidia mwanaume kuchukua muda mrefu kumaliza
Kujifunza kuthibiti kumaliza mapema kunaweza kuchukua muda mrefu na mazoezi ya kutosha, unaweza kujisikia ksumbuka tu wakati unajitahidi kuthibiti hata hivyo kwenye nia njia ipo na wewe utaweza tu nakuamini.

Mwisho, kujifunza mwanaume kumaliza mapema kutampa mpenzi wako raha (enjoyment) kubwa sana kimapenzi. Wanawake hupenda good sex ambayo ni leisure, playful, whole body, massage kwa wingi.
Na wanawake wengi hulalamika kwamba wanaume huwa na haraka tukiwa kwenye miili yao, tupo too much mechanical, tunakimbilia kule chini tuingiza tumalize na tuishie zetu kwa usingizi, tuna focus matiti na maeneo ya uke tu.
Wanawake hujisikia mwili mzima ni uwanja wa kucheza kimapenzi na hushangazwa na wanaume kugundua visehemu kidogo tu katika uwanja mzima na kuvipenda.
Hata uume pia umeumbwa kwa ajili ya leisure, kuchezewa, mapenzi ya mwili mzima, massage ya mwili mazima ndipo sex, kuwa focused kwenye uume peke yake huweza kuupa uume mgandamizo ambao hupelekea kutoa risasi mapema.

Kimsingi kama wanaume wangekuwa wanafanya mapenzi kwa namna ambayo wanawake wanapenda basi kusingekuwa na malalamiko na wanaume wangekuwa na matatizo kidogo yanayohusiana na tendo la ndoa.
Tutaendelea ............................................

19 comments:

Anonymous said...

Nimekubali kaka Mbilinyi na mimi kila siku lazima nitembelee blog yako inaelimisha sana,,,sasa ndoa yangu nikirudi TZ nakwenda kuiweka sawa maana nilikuwa na tatizo la kumaliza mapema sana


elibaraka

Lazarus Mbilinyi said...

Kaka,

Ndoa ni kujifunza kila siku na kila siku zinavyoongezeka na kwenda ndo wanandoa wanakuwa smart zaidi na kufurahia zaidi uumbaji wa Mungu.

Upendo daima

Lazarus

Anonymous said...

Kaka Mbilinyi,
Tunashukuru sana kwa yote na pia Mungu akubariki wewe na familia yako, marafiki na wote.
Pasaka njema kwa sote.
Msafiri

Anonymous said...

Mungu we tu na aliyekuumba akuzidishie pumzi maana kila iitwayo leo maana unatujenga sana.
Mungu na akubariki usichoke kutufundisha ingawa hatutoi maoni ila ujumbe unafika na tunajifunza kaka yangu.
Real Post zako zinajenga na kurudisha matumaini na kukata tamaa katika ndoa Mungu afungue njia na kukupa mwanga
Be blesed
AM

Lazarus Mbilinyi said...

Dada AM,
Asante sana kwa baraka zako na wewe Mungu akubariki na zaidi ufanikiwe na kuwa na furaha ya kweli kila eneo la maisha yako na mumeo.

Upendo daima

Anonymous said...

jamani unajua mnawafanya wasio oa hasa wanaume waanze kuogopa ,hata kuaahirisha kabisa swala la kuwa na mke?
Unajua wao wanajua mambo yapo poa sana ni mwendo mmoja hadi mwisho sasa mnapo sema sometimes ni moto wa nyasi? mmm kazi ipo.

Lazarus Mbilinyi said...

Wewe Unayesema wasio na waume wataanza kuogopa kuolewa pole sana,
sidhani kama ni busara kutokumwambia mtu ukweli ili akiingia na kukutana na hilo tatizo awe anajua jinsi ya kukabiliana nalo, kuliko kula jiwe kwamba ukiingia kwenye ndoa mambo ni tambarare wakati kuna matuta ambayo bila kukutana nayo pia ndo haiwezi kuwa imara.
Haina haja kuwa mwoga au kuogopa, Hakuna mafanikio yasiyo na kukutana na shida na matatizo na si katika ndoa tu bali hata maeneo mengine ya maisha bila kuwa mtu strong huwezi kupata mafanikio yoyote, na waoga wote huishia kulalamika tu wenzao wakifanikiwa.

Upendo daima

Anonymous said...

Ni kweli kaka ,,asante kwa ushauri,ni mie niliye andika kuhusu kuogopa ,inavyo onyesha swala hili ni kikwazo sana ndani ya ndoa lina boa. japo ni ukweli kuwa ukiwa hujaoa unafikiri vingine na ukisha oa unakutan,a na mengine. lakini swali ni hili. je wanawake nao wanapenda kufanya mapenzi au wao ni passive hadi waambiwe na wanaume? . Na kama wao nao wanapenda kufanya hiyo kitu je wananafasi gani kuhakikisha jamaa moto hauwaka mapema na kuzimika ghafla. edmund

Lazarus Mbilinyi said...

Kaka Edmund,

Asante sana kwa changamoto zako, ni kweli ambaye hayupo kwenye ndoa hajui nini kipo ndo maana wanahangaika ili waingie kwenye ndoa na wenye ndoa wanajua nini kimo na wengine wanafurahi na wengine wanajuta, nisikutishe ukweli inatokana na umetumia efforts kiasi gani kuhakikisha unapata partner ambaye tabia mtaendana.
Kuhusu mwanamke kuhusika kuhakikisha mwanaume hamalizi mapema naamini wanawake wanahusika sana na kwa kweli mwanamke anayejua raha ya mapenzi huhusika kikamilifu kuhakikisha mume anafanikiwa katika hili na ukweli ni kwamba kuchelewa kumaliza kwa mwanaume ni raha zaidi kwa mwanamke. Mwanamke anayependa usimalize haraha atakusaidia kuwa na muda wa kutosha kumsisimua yeye ikiwezekana yeye kifika kileleni hata kabla ya intercourse (uume kuingia kwenye uke) au romance kwanza kuhakikisha mwanaume unasisimka na kulerax huku mzee amesimama kwa muda unaotakiwa.
Si kwamba wanawake wapo passive sana ila kila ndoa ila sex code yake kwa mfano ukiona bibie kajifunga kagha tu ujue leo anataka, au ukiona anasema leo tukavue samaki boti ipo order ujue ni lugha rahisi kwamba leo anakutaka na inatokana na mume na mke wapo wazi kiasi gani kwenye suala la mapenzi, kumbuka mwanaume ni mwanaume na kwa tabia zako unaweza kucreate aina ya mke unataka. Mwanaume Ukiwa wazi anakuwa wazi, ukiwa mkorofi na yeye atakuwa mkorofi nk.

Upendo daima

Anonymous said...

Jibu bomba sana ,lakini ebu niembie mshuikemshike wa siku ya kwanza huko honeymoon, si ugovu mtupu au ainabidi muwe na likizo hadi siku chache ndoo mzindue. aunini kifanyike ili uzinduzi uwe bomba.
edmund

Lazarus Mbilinyi said...

Kaka Edmund,

Asante sana kwa maswali mazuri yanayoonesha ni kweli unataka kutimiza ndoto zako za kufanikiwa katika idara zote hahaha!

Kuhusu honeymoon tumeshaongea sana hapa unaweza kusoma post za nyuma kwenye hii link http://mbilinyi.blogspot.com/2008/04/honeymoon-fungate-4.html kama ni mara ya kwanza sex na pia kujua mambo muhimu kuzingatia wakati ukiwa huko na mpenzi wako kwa mara ya kwanza na zaidi ili msiharibu mambo.

Anonymous said...

hallo bomba sana , nimefurahi kujua kuwa kuna asali some where. sasa mkubwa ni hili shwali langu na kama mtu mwingine pia anajua anaweza kunisaidia hasa wanawake wanatembelea blog hii. Ni hivi: Unajua umeandika somewhere kuwa kuuliza uliza mwenzi kuhusu maisha yakesi vizuri na ninakubaliana nawe. lakini kwenye swala la kitu kina itwa bikira kwa kweli naomba sana mnisaidie. Sipendi kujaji mtu kwa sababu ya kitu kama hiki lakini mambo mado naona yananikoroga.Najua kuwa bikira si kitu muhimu kwani yaweza kutokuwepo bila mahusiano lakini bado kuna familia nasikia inabidi upeleke mbuzi kuwashukuru kwa kumtunza mwanao hadi ameolewa bila kumjua mtu na wakati huo huo nisipo pele maana yake nitakuwa nimegundua kuwa hana bikira na nikimwambia ataniona kama namhisi si mwaminifu na yeye kuniambia anaogopa pengine nitamwuliza nani nalihusika na akiniambia ukweli nani alihusika pengine aliye husika namjua na sipendi anadanganye. sasa nimambo gani yamsingi ya kufanya ili nisiingie kwenye matatizo ya kifikra na kuharibu ndoa ambayo nilidhani itakuwa bora. najua wapo wanawake ambao huwadanganya wake zao na sipendi nionekane si jali mambo .
asante
edmund.

Lazarus Mbilinyi said...

Kaka Edmund,
Asante sana kwa maswali yako na ulivyo creative kuhakikisha unapata kile unastahili.
Kwanza kuhusu kuuliza uliza mke au mpenzi wako kuhusu maisha yake ya nyuma haina maana ukweli nazungumzia pale ukiwa tayari umefunga naye ndoa kwani umeshafunga ndoa na zaidi umetoa ahadi kwamba hadi kifo. Kama ni wachumba kuchunguza ni muhimu sana tena nasema chunguza kwa nguvu zako zote maana hapa unajenga mnsingi na lazima msingi bora uwe na inspection kuhakikisha viwango ni sahihi, hapa kama siku ya harusi inakaribia na unahisi kwenye inspection yako mambo hayajakamilika please usiharakishe kwenda mbele ya pastor kutoa ahadi maana utajuta. Chunguza chunguza na chunguza. Ila ukishaoa anza kufurahia maisha na kuangalia ndoa yako Mbele nakuwekeza kwa kila kitu ili uwe na ndoa yenye afya na si kuchunguzana tena.
Kuhusu Bikira mmm kazi kwelikweli ni kweli kuna jamaa wamelipa mbuzi au pesa kushukuru wazazi kwa kutunza binti yao hata hivyo baada ya kuolewa siku ya kwanza jamaa wamekuta jamaa walishapita tena kwa kasi ya light> muhimu achana na hayo mawazo na wazee kama hao wanaishi karne gani. Kama watakwambia utoe mbuzi au pesa toa tu kwa sababu umependa binti yao lakini si kwa sababu ya bikira.
Awe na bikira au asiwe nayo si haina maana. Wote mwanaume na mwanaume Mungu aliwaumba hadi kuoana wote wana bikira hahahaha.

Upendo daiama

Anonymous said...

Hallo asante sana kwa jibu lako umenitia moyo sana. Niljisahau uchumba kumba siyo ndoa !!!. Lakini hilo la bikira kweli bado sijajua maana ni siri kubwa nahitaji nyongeza zaidi. all in all Mungu awabariki wana blog nisaidiane mwenzenu safari ikaribu nisije nidandia ghari gari lisilo nihusu. Hivi ebu niambie hivi mwanamke ambaye anajijua hana bikira na hajambambia mumewe kisa si atakuwa na hatia somewhere na kuna mambo fulani yakiongelewa atakuwa anajisuta. Sipendi nioe mke mwenye siri ambayo inafukuta moyoni mwake. Au nifanyaje ili nihakikishe ananiambia evrything ili awe huru ? . Au huwa wanasema siri zao kiurahisi ? Edmund

Lazarus Mbilinyi said...

Kaka,

Hongera sana kwa kutaka kuwa mwanaume mzuri katika ndoa.
Ukweli kuna mambo jamii inatufundisha kuwa ni mambo ya msingi wakati si kweli. Moja ni suala la bikira.
Binafsi sioni umuhimu wa kufikiria sana kuhusu bikira kama msichana ambaye unataka kumuoa una uhakika na njia zake na historia ya maisha yake kwani bikira na two way street yaani wote mwanaume na mwanamke kwa maana kwamba kama unataka mwanamke mwenye bikira wewe je?
Hata hivyo itabidi nitoe somo la bikira ili kila mmoja tuone anasemaje.

Asante sana

Upendo daima

Anonymous said...

Borother mie nipo gado ,sijue kabisa yaani mshamba !!hahahahaha!! lakini naungana nawe kweli si jambo la msingi na nimepata jibu moja kwa mtu yeye anasema mlevi utamkuta na walevi wenzio!! . Nasubiri somo hilo la bikira ,ikiwezekana wiki hii ,na hamu sana kujua watu wanawaza nini na ikiwezekana weka polls kwenye blog yako ili kujua wangapai wanawaza nini na wangapai hawawazi hivyo. asanet lakini samahani kwa muda wako!
wako mtiifu edmund.

Lazarus Mbilinyi said...

Kaka,
Usijali sana, leo sina darasa nilikuwa na mitihani jana so leo nipo napumzika tu so kupata muda wa kuongea na mtu kama wewe kwangu ni faraja sana.

Hata hivyo naamini wiki ijayo tutajadili hii isuue na pia nashukuru sana kwa maoni yako kuhusu polls.

Siku njema na ubarikiwe na Bwana.

fikirikwanza said...

Nimependa mazungumzo yenu hapa ,ni tabia njema endeleeni.Mnafumbua macho ya wengu hata kina fikiri kwanza. Somo lijalo nitakaa bench la kwanza!!
asanteni wadau.

Lazarus Mbilinyi said...

Fikiri kwanza,

Ni kweli inafurahisha sana na zaidi tunajifunza.

Ubarikiwe