"Marriage is our last, best chance to grow up."

Tuesday, April 7, 2009

Kumaliza haraka!

Baada ya kupeana mabusu na romance hadi kila mmoja anakuwa amesisimka kiasi cha kuwa tayari kwa kurushwa hadi kufika kileleni, ghafla baada ya msuguano mmoja tu mwanaume ameshamaliza na tayari hoi anageuka na kulala zake usingizi mzito wakati huohuo bibie bado kwanza ndo alianza kupata raha na sasa ameachwa kwenye mataa anazubaa akiugulia kukosa raha yenyewe.

Jambo la kuhuzunisha ni kwamba baadhi ya wanaume huweza kufika kileleni haraka mno; dakika chache tu baada ya kuingiza uume kwenye uke, ingawa hii humpa mwanaume raha ya ajabu hata hivyo anaweza kumwacha mke wake katika kukatishwa tamaa na kutoridhika hasa kama ni mwanamke ambaye kufika kwake kileleni hutegemea msuguano (thrusting) wa uume kwenye uke wake.

Kawaida mwanaume huweza kuwa tayari kufika kileleni kila baada ya mipigo 50 (kuingiza na kutoka ndani ya uke) [thrusting] na wakati huohuo inachukua zaidi ya dakika 10 kwa mwanamke kufikia kileleni (siyo wanawake wote wengine huwahi).

Mwanaume anapokuwa hana uwezo wa kujizuia kukojoa (ejaculate) mapema huweza kukosa kiwango cha raha ya kutosha anayostahili yeye mwenyewe na mke wake pia, vilevile hukosa raha halisi ya kuwa ndani ya mke wake kwa muda mrefu (mwili mmoja) na hapati zile hisia za ukaribu (intimacy), mapenzi na muunganiko ambao huweza kuwaunganisha wawili wapendanao kupitia tendo takatifu la ndoa ambalo Mungu alilifanyia ubunifu kwa ajili ya mwanaume na mwanamke duniani kuwa pamoja na kufurahia uumbaji wake.
Wanawake wengi huhitaji mume kukaa ndani ya uke kwa muda mrefu unaotosha kwa kadri wanavyohitaji raha na utamu wa hii zawadi ya mwili.
Na njia sahihi ya kuweza kufanikisha hili ni pale tu mwanaume anapokuwa na uwezo wa kuhimili kutokojoa mapema na kuwa na uwezo wa kuwa na hiari wakati gani aweze kukojoa au kutokukojoa.


Fikiria raha inayopatikana kwa mwanaume ambaye anaweza kumhakikishia mpenzi wake anapata raha kwa muda anaoutaka maana tendo la ndoa ni haki yake ya msingi ya kuzaliwa.

Kwa kujifunza unaweza kuwa na uwezo wa kufika muda mrefu vyovyote unataka na kukupa ridhiko la kimapenzi wewe pamoja na mpenzi wako.

Mwanaume anapokuwa kwenye mahaba asipokuwa makini huweza kufika mahali mambo yakawa matamu kiasi kwamba hakuna kurudi nyuma (no point of return) kwa maana kwamba lazima mwanaume akojoe, hana chaguo bali kumaliza hata hivyo kumbuka mke wako ni muhimu pia na mwitikio wa mapenzi kati yako na yeye ni tofauti, ili kumtanguliza yeye unahitaji kufanya kitu nacho ni kuthibiti kutowahi kujokoa kabla yeye hajaridhika.


Habari njema ni kwamba mwanaume yeyote pamoja na wewe unayesoma unaweza kuwajifunza na kuwa mwanaume anayeweza kufika kileleni wakati anaotaka yeye.
Naamini ni ndoto ya kila mwanaume kuwa mzuri katika mapenzi na kuhakikisha mke wake mpenzi anapata kile anastahili wakiwa faragha na zaidi kuweza kumfikisha mwanamke katika kiwango cha juu kabisa cha raha ya mapenzi ambayo ni ndoto ya binadamu yeyote duniani ambaye ana hisia kamili za kimapenzi.

Je, nini kifanyike kuweza kuthibiti kumaliza mapema?
Tutaendelea…………..

4 comments:

Anonymous said...

Ebana Mbilinyi nakupa hongera sana kwa blog yako imenisaidia sana,,,nasubiri kwa hamu sana maana mimi nikiweka tu nakojoa sina breki

Anonymous said...

hongera sana kwa kazi nzuri unatuletea mauhondo na kutufundisha

Anonymous said...

Kaka Mbilinyi nakupongeza kwa kuwasaidia wanaume wenzio kufurahia raha ambayo ni haki yao!!!
Picha hiyo umetoka vizuri.
Salimia wote.

Msafiri

Lazarus Mbilinyi said...

Hata kama suala la sex limetawala sana kwenye media, bado kuna mambo ya msingi ambayo bila hayo wakati mwingine maisha yetu na wale tunaowapenda huwa kwenye kigiza fulani hata hivyo kujifunza na kuongeza maarifa ni silaha muhimu sana na si kujifunza tu bali kufanyia kazi yale tunajifunza. Ndipo tutafanya ndoa zetu na wale tunaowapenda waridhike na kukubali kwamba hawakufanya makosa kutupa nafasi muhimu katika maisha yao.
Hivyo karibu sana hadi somo lieleweke.

Upendo daima