"Marriage is our last, best chance to grow up."

Thursday, April 2, 2009

Mapenzi ni sanaa, huelezea maisha, leo ni tofauti na jana na jinsi binadamu wanafanya mapenzi kufanya mapenzi hubadilika kila siku, mtazamo wa kufanya mapenzi enzi za bibi yako na babu yako ni tofauti na leo.
suala la kufurahia raha ya mapenzi halina mipaka katika ubunifuna huwezi kupima raha ambayo mtu anapata kutokana na kufanya mapenzi.
Huwezi kuweka mapenzi kwenye box au kujenga fence au kuweka mipaka.
Unaweza kuwa na sanaa bora katika mapenzi au sanaa ovyo katika mapenzi.
Unaweza kujidhania wewe ni bora katika sanaa ya mapenzi hata hivyo ukashangaa mpenzi wako hawezi hata kusisimka kutokana na usanifu wako na unaweza kukatishwa tama na kile ulitarajia.

Wakati mwingine unaweza kushangaa jinsi sanaa yako ya mapenzi inavyopata kibali kwa mpenzi wako kama vile maji yanavyotiririka kwenye mto uliozungukwa na ndege wanaoimba sauati ya asili.

Kila mmoja anatakiwa kufungua nafasi yake kupokea raha mpya ya kimapenzi ilimradi unaishi na upo hai.

Je, ni nini siri ya mahusiano (ndoa) yanayodumu na kumfanya mtu aridhike?
-Kuwa na vicheko?
-Kufanya mapenzi?
-Pesa?
-Uaminifu?
-Urafiki?
-Kufanana?
Kila mtu anaweza kuwa na jibu lake hapo.

No comments: