"Marriage is our last, best chance to grow up."

Tuesday, April 21, 2009

Wapo wengi!

Kuna maboksi mengine kabla ya kuyabeba fikiria kwanza!Wakati mwingine huwa tunajikuta tumebeba maboksi ambayo tunadhani ni yetu na kwa furaha kubwa huwa tunawaringishia wengine hasa kutokana uzuri wa boksi kwa nje tukitegemea na ndani litakuwa na kitu kizuri.
Hata hivyo tukifika majumbani tunashangaa kuku vitu vilivyomo ndani ya boksi ni kinyume chake.

Maisha ya mahusiano nayo wakati mwingine ni kama kubebeshana maboksi tena kwa hiari kabisa.
Tatizo huanza pale box lenyewe likijua kwamba wewe ni mbebaji mzuri basi utachakaa kwa kubeba hili boksi.
Na linaweza kuwa ni boksi lililokuja na viboksi vingi ndani yake kama vile hasira, ukari, au manyanyaso ya kila aina, maneno magumu na mazito ambayo hukuumiza zaidi ya kupigwa ngumi na mateke, yaani unajikuta umeruka majivu na kukanyaga moto.

Kuna kitu kinaitwa “Narcissism” hili ni neno la kigiriki lenye maana ya mtu kuipenda zaidi nafsi yake kuliko kawaida (extreme self-loving).
Hili Neno linaendana na story ya kijana wa Kigiriki ambaye alivutiwa na taswira yake mwenyewe kwenye bwawa kiasi cha kushindwa kuondoka hadi alifia hapo.

Hili tatizo huanzia wakati mtu bado mtoto mdogo hasa baada ya kukosa upendo na anapokuwa mtu mzima anakuwa hajui maana ya kupenda na kupendwa.

Utafiti unaonesha ni asilimia 75 wana kaasili ka narcissists.
Na Adolph Hitler alikuwa kinara wa hizi tabia ingawa huyu alikuwa hatari hata hivyo tunao akina Hitler wengi sana kwenye mahusiano yetu ya kila siku.

Hawa akina Hitler wanachofanya ni kukubebesha kiboksi cha wewe Kujiona una hatia, wanakupa hofu, woga, mashaka, wanakufanya usijiamini ili wakupelekesha wanavyotaka wao.
Hawa wanaweza kukudhalilisha kimwili, kimapenzi, kihisia na pia wanaweza kuzira kuongea (silence) na wanachofanya ni kuku-control wewe idara zote za maisha yako unakuwa kama mfungwa fulani kwa kuwa umeingia kwenye anga zao.

Hata unapoishi nao unakuwa unaishi maisha ya mateso, mtindo wa jela na kunyimwa uhuru.
Hii aina ya mahusiano ni hatari tupu na huhitaji msaada wa ushauri kwa wataalamu wa masuala ya ndoa na mahusiano.
Wengine ni watu wenye status kubwa katika jamii zetu anaweza kuwa mameneja, wahadhiri wa vyuo vikuu, matajiri, wabunge au mawaziri na hawa watu huonekana watu wa heshima kubwa sana mbele ya jamii kwani ni wapole, wema, watii, ni marafiki, wastaarabu, wamevaa ngozi ya kondoo huku ndani ni mbwa mwitu wakali na wenye njaa.
Hawa watu ni lethal.
Ukifanya kosa moja tu kwao unastahili kupewa adhabu ambayo utajuta kuwa naye katika maisha.
Hawa wanaume au wanawake hufurahia sana kutesa wake zao au waume zao, hawana huruma na hawafai kabisa katika jamii.

Tupendane katika ndoa zetu

2 comments:

Mwanasosholojia said...

Mbilinyi umenena ndugu yangu!Nimefurahi kuingia ukumbini humu kupitia kwa kibaraza cha Maisha cha dada Yasinta!Hongera mkuu kwa uchambuzi huu!Tuendeleze Libeneke hili, nakukaribisha pia kijijini kwangu http://mwanasosholojia.blogspot.com.Nitakuwekea na link ili niwe naingia ukumbini kwako kirahisi. Hongera tena na tena!

Lazarus Mbilinyi said...

Kaka mwanasosholojia,
Wewe ndo tunakutafuta sana maana una taaluma ambayo ni nzuri sana kwenye jamii yoyote kuishi vizuri iwe dini, ndoa, jami nk

Asante sana kwa kunikaribisha na kwa kweli nitakuwa napita hapo na kupumzika kidogo kupata elimu ya maisha ili niwe mtu bora katika mahusiano na watu wengine duniani.

Asante sana kwa kunitembelea nakykaribisha sana kwani wewe ni mtu muhimu sana ushauri wako unahitaji sana.

Upendo daima