"Marriage is our last, best chance to grow up."

Saturday, May 30, 2009

Maji yameingiliwa na Mdudu!

CHIMBA KISIMA CHAKO MWENYEWE
By Faustin Munishi:

Uchimbe kisima wewe mwenyewe unywe maji yako peke yako na usiyashiriki nao wengine ni hatari kubwa eeh!
Maji ya kisima cha watu wengi yameingiliwa na mdudu ukiwa na kiu usiyaonje utaambukizwa eeh.
Na kiu ya maji imeongezeka watu wanayanywa kila wakati na yanauzwa kote barabarani nani atapona eeh?
Kwa sababu maji yana mdudu yanapatikana kirahisi ukipita kote utayaona wacha kuyachota eeh.

Ukiwa na njaa ni ya chakula huwa ni vigumu upatiwe lakini sigara na hata pombe watakupatia eeh.
Unajua kwa nini?
kwa sababu pombe na sigara zinaua wanataka na wewe ufe na wao wanakupatia eeh.
Tena na siku hizi na hayo maji yaliyo yaliyoingiwa na mdudu utapewa bure bila kuomba ili mfe wote eeh.
Yapo kwenye chupa kubwa na ndogo watu wanazipenda zile ndogo wanafikiliria zipo salama wamedanganyika eeh.
Wanazifunika nusunusu wamefanya hivyo makusudu ili waamushe kiu ya maji usidanganyjike eeh!

Ndugu jihadhari na maji ya rahisi kachimbe kisima wewe mwenyewe ukiwa na kiu uyanywe maji uliypoyachimba heri.
Dawa ya mdudu hawajaipata wanaitafuta kotekote umwamini Yesu akuokoea amalize kiu

Unaweza kusikiliza wimbo hapa chini

Mithali 5: 15 – 19
Unywe maji ya birika lako mwenyewe, na maji yenye kububujika kwenye kisima chako.
Chemichemi yako ibarikiwe nawe umfurahia mke wa ujana wako!

Sometimes

Sometimes adults are just tall children.
Some come with childhood baggage in marriage.
Understanding your mate’s history sometimes is vital.

Lazarus Mbilinyi

Friday, May 29, 2009

Tunaenda ICU!

Baadhi ya Wanaume baada ya tendo la ndoa hujikuta hoi bin taabani.
Na wanawake wengi hulalamika sana na hii tabia ambapo mwanaume akishamaliza tu hujikoka usingizi na kuanza kukoroma within seconds.
Na hali huwa mbaya zaidi kwani kabla ya sex mwanamke hakuandaliwa kwa muda wa kutosha na mwanaume anamaliza haraka hata kabla mwanamke hajafikishwa popote na kitu cha ajabu zaidi mwanaume akimaliza analala fofofo.

Pia Wanaume wenyewe hawawezi kuondokana na hili kwani ni suala la kisaikolojia na lipo nje ya uwezo.
Hata hivyo akijifunza anaweza kuwa tofauti.

Mwanaume huweza kutengeneza mbegu (semen) kila baada ya masaa 42 hadi 72 na hiki kitendo husababisha mgandamizo wa kimwili wa kutaka kuzitoa kwa njia ya sex.
Pia wanasayansi wanasema kwamba kila drop moja la majimaji ya mbegu za kiume (seminal fluid) huwa kunakuwa na zaidi ya mbegu za kiume milioni 300 na mwanaume ana uwezo wa kutoa hizo mbegu kupitia sex (ejaculation) mara 2 au 3 kwa siku.

Kitendo cha kutoa hizo mbegu huhusisha nguvu za kimwili na kihisia na huwa na pressure kubwa sana wakati zinatoka na kumfanya mwanaume kuwa hoi kabisa.
Huo utoaji wa nguvu ni kama mlipuko wa nje wa bomu (outward explosion) tofauti na mwanamke ambaye kwake huwa internal/ inward/inside explosion.

MENGINEYO
Pia wanaume wanaoishi vijijini Utafiti unaonesha kwamba wao hushiriki tendo la ndoa mara nyingi zaidi kuliko wanaume wa mijini, hii ni kutokana na wanaume wa mijini kukumbana na misukosuko ya maisha na kuathirika kisaikolojia hivyo kuathiri mwili kutaka sex.

Wanaume huwa frustrated sana na wanawake kwa sababu wanawake mara nyingi hawapendi sex.
Wanawake nao huwa frustrated sana na wanaume kwa sababu wanaume kila wakati wao wanataka sex.
Wanawake wanawalaumu wanaume kwa sababu hawajui kupenda.
Wanaume nao wanawalaumu sana wanawake kwa sababu wanaongelea sana upendo lakini hawataki kuweka katika vitendo (sex)
Binadamu hufanya mapenzi kwa sababu ya homoni ya testosterone ambayo kwa kiasi kikubwa ni kwa wanaume.
Mwanaume wa kawaida huzalisha hii homoni mara 20 kuliko mwanamke, ndiyo maana mwanaume anakuwa na drive kubwa ya sex.
Hii ina maana kwamba jinsi mwanaume anavyojisikia kukosa sex kwa siku moja ni sawa na mwanamke anavyojisikia kukosa sex kwa siku 20.

Mwanaume anaweza kuzalisha mtoto kila anapofanya mapenzi wakati mwanamke anaweza kuzaa watoto kwa kila baada ya miaka miwili, hii ina maana kwamba mwanamke anatakiwa kuchagua nani anatakiwa kuwa baba wa mtoto.Wanaume siku zote wanatafuta quantity wakati wanawake siku zote wao ni kutafuta quality.

Ndiyo maana wanaume hutafuta sex kwenye mahusiano na wanawake hutafuta upendo.
Kwa mwanamke upendo ni proof kwamba mwanaume atabaki kwake na kuwa naye wakati wanaume wao baada ya sex ndiyo hujisikia mwanamke anampenda.

Men fall in love through sex; women fall in sex through love.

Wednesday, May 27, 2009

Hatua za Ndoa na mahusiano (mwisho)

"Mimi na wewe tumetoka mbali" HATUA YA NNE NI KUUNGANISHWA:(Connection stage)Jambo linalohuzunisha ni kwamba nusu ya mwanaume na mwanamke wanaoamua kuishi pamoja hushindwa kufikia hii hatua ambayo mateso, maumivu, uchungu na kuvumilia kote huanza kulipa.
Asilimia kubwa ya ndoa zinazovunjika sababu kubwa ni kukosa maarifa (knowledge) hasa kabla ya wawili kuamua kuishi pamoja hivyo huingia kwenye ndoa wakitegemea ndoa itakuwa tambarare kama nyikani au watakutana na vichuguu kumbe kuna milima na mashimo.

Hapa mnakuwa mmeshirikiana kutengeneza historia na kwa pamoja mnakubaliana kwamba kweli ndoa haikuwa rahisi hata hivyo mnajisikia proud kwa kuwa mmeshinda hurricanes na storms zote pamoja.

Kila mmoja anamshukuru mwenzake kwa commitment kubwa na dedication aliyoiweka kuhakikisha ndoa inafika mwisho kwa uvumilivu wa hali ya juu, pia mkiangalia mlikotoa mnajisikia ni kweli ninyi ni wanandoa wa tofauti.
Kila mmoja anajiskia yupo karibu na mwenzi wake na more connected kimwili, kihisia na kiroho, pia kila mmoja hujisikia amepata hamu mpya na kubwa kwa mwenzi wake hasa Kutokana na kupoteza muda mwingi wa kuwa intimate kwa kushughulikia migogoro kila mmoja anajiskia yupo nyumbani tena.

Hujikuta zile qualities ambazo uliziona mwanzo kabisa kumbe bado anazo na unaanza kujiunganisha kihisia upya kwa kuwa sasa mnafahamiana vizuri pande zote za maisha yaani strength na weakness.Hii ni hatua ya furaha, hatua ya mapenzi ya kweli, true love, divine love, unconditional love.

Wanandoa wa hatua hii hata watu wengine huwa-admire kutokana na jinsi walivyoshinda aina zote za majaribu.
Wanakuwa role model kwa jamii.

Kama wanandoa wote wangejua kwamba ndoa huwa katika hatua mbali mbali na kwamba mbele ya safari inalipa, basi wangekuwa tough kuhakikisha wanavumilia na kushinda.

Hata hivyo wengi huamini stage (kama kuna matatizo) waliyopo itakuwa ya kudumu na kwamba watakuwa hapo forever, ni kweli ukiwa na wakati mgumu huumiza na hukatisha tama lakini kumbuka “No situation is permanent” hata kama ndoa imefikia hali mbaya kabisa bado huwa na dalili za kuiokoa ni muhimu kuelekeza nguvu hapo.

Ndoa imara si ile isiyokutana na dhoruba bali ni ndoa ambayo inazishinda aina zote na dhoruba nakuendelea mbele kwa kasi ya ajabu.

NB:
Si lazima ndoa yako ipitie hatua zote 4 unaweza kuwa kwenye hatua ya kwanza miaka yako yote huku kukiwa na vimsuguano vidogo vidogo kama utaruhusu Kristo kuwa kiongozi wa ndoa yako kwani kama yeye anavyolipenda kanisa basi mume na mke wanahitaji kuishi kwa mfano wa Kristo na kanisa.

Tuesday, May 26, 2009

Hatua za Ndoa na Mahusiano

Hivi nilikuwa nawaza nini?Kila mmoja anajua raha ya falling in love or siku za honeymoon je, nini hufuata baada ya hayo?
Wengi hawajui emotional terrain iliyo mbele, au hills zilipo mbele au bonde utakayopita katika kuendelea na ndoa yako.
Hapa kuna hatua predictable ambazo ndoa nyingi hupita, naamini ukiijua hii ramani basi utaweza kufika mahali unapoenda.
Leo tunaendelea na hatua ya pili na ya tatu

HATUA YA PILI NI MAUZAUZA(Nilikuwa nawaza nini)
Ile hali ya kudondokea kwenye mapenzi (fall in love) huchakaa na ukweli halisi huanza kuonekana.
Hii ni hatua ngumu kwa sababu unakumbana na anguko kubwa sana la ndoto zako kuhusiana na mpenzi wako.
Zile tofauti na tumakosa tudogo ambato tulikuwa si kitu sasa huanza kusumbua na kuudhi, mfano kama mwenzi wako alikuwa mzembe kupanga vitu hasa nguo chumbani sasa utaanza kuudhika kwani utajisikia umevulia mno, kama anakoroma sasa utaona usumbufu, kama ana kikwapa sasa unaona kinasumbua, kama ana harufu mbaya mdomoni asubuhi itaanza kukusumbua, tayari sasa vitu vidogo vimekuwa mambo makubwa yanayokuudhi.

Kila mmoja huanza kulalamika kwamba mwenzake hawi kama anavyotegemea.
Kunakuwa na disagreement nyingi kuliko agreement na unagundua kwamba mnatofautiana sana katika mitazamo ya vitu vingi.
Wewe unataka kula hotel unaipenda mwenzako anataka mle nyumbani ili ku save pesa, unapenda usikivu usiku nyumbani mwenzako anataka kusikiliza muziku kwa sauti kubwa.

Ule kuwa mwenzi wangu ni perfect huanza kupotea na imani yako kwake huanza kupotea kwamba mmm kumbe ni mkali kiasi hiki, kumbe ni mchoyo kiasi hiki, kumbe hapendi sex kiasi hiki, kumbe anajua kukalia mwenzake kiasi hiki nk.
Hapa tofauti za malezi, tamaduni, dini, kuamini, tofauti kati ya mwanamke na mwanaume hujitokeza na kuwa wazi.
Katika hatua hii mtu halisi huanza kuonekana na ukweli ni kwamba ndoa huanza kujengwa hapa.
Wengi huanza kujiuliza mbona watu hawakuniambia kwamba ukioa au kutolewa inakuwa hivi kwani anayaanza kuona ni kinyume na matarajio na wengine huanza kujiuliza kwa nini nilioana naye.
Wapo ambao huanza kufikiria wachumba wengine (misri) kwamba labda ningeoana na Fulani alikuwa afadhari kuliko huyu.
Wengi huanza kujiuliza hivi nilikuwa nafikiria nini hadi nikakubali kuoana naye.
Walio na hekima huanza kumuomba Mungu na kupata ushauri wa watu wanaowaamini

HATUA YA TATU NI MATESO, MAJONZI NA TABU(Miserable stage)
Wanandoa hushangaana kwa nini kila mmoja amejiweka gundi kwenye njia zake bila kumjali mwenzake.
Na kila mmoja humwambia mwenzake ungebadilika kila kitu kingekuwa kizuri.
Kama ni mlevi basi hujichimbia mizizi na kuwa mlevi wa kupindukia, kama ni mlevi wa kazi (workaholic) basi ataondoka nyumbani asubuhi na mapema na kurudi midnight eti ana andaa future.
Hata akirudi nyumbani hukuta mke amelala na watoto wamelala na yeye mwenyewe yupo exhausted kiasi kwamba hawezi hata kumuhudumia mkewe.
Hapa ndipo affair nyingi huzaliwa, na ndoa huwa ni vilio, majonzi, Stress, BP, pressure, kukosa usingizi, you name it!Wanasheria wa mambo ya ndoa wengi hutajirika kwenye hatua hii ya ndoa hasa nchi zilizoendelea ambako kuachana ni jambo la kawaida tu (divorce)

Watoto wengi huachwa njia panda na kutojua nini cha kufanya maana mara kwa mara baba na mama hawaelewani.
Hapa ndipo tunafahamu kwamba kupigiana kelele, kulaumiana, kusuguana, kutishiana hakuwezi kubadilisha wapenzi wetu bali kukubaliana kwamba kuna tofauti na kushirikiana kutatua tatizo kwa hekima na busara hupeleka ndoa kwenda hatua nzuri zaidi.

Hii ni discovery stage ambayo wanandoa hujuana na ni opportunity ya kujifunza na kuzalisha true love.Wale wanaokimbia au kuomba talaka au kutoa talaka huenda kutafuta wapenzi wapya ambao hujikuta wameangukia the same boat na matatizo mapya na makubwa zaidi.

Na ndoa nyingi huvunjika hapa na kukosa kufikia stage inayofuata ambayo ni true love kati ya wanandoa.
Ndiyo maana tafiti nyingi zinaonesha kwamba baadhi ya walioachana kwa talaka kuna wakati hutamani kurudiana na wataliki wao au wangejitahidi kuvumilia na hatimaye kutatua matatizo kuliko njia ya kupeana talaka waliochukua.

Wapo ambao huona haina haja kuendelea na hii cold war na huamua kuchukua uamuzi wa kufanya investigation na kuchukua njia sahihi za kujenga mahusiano imara na yenye afya.
Hata hivyo wanaoamua kuchukua huu uamuzi bora wa imani huwa na milima na mabonde ya kupita kufikia hatua ya mwisho ambayo huwapa raha na experience ya ndoa mpya.

Monday, May 25, 2009

Hatua za Ndoa na Mahusiano

Upendo wa kweli ni kusherehekea raha na shida pamoja.Ndoa ni mahusiano yanayoweza na yanayotakiwa kuwa ndiyo kitu kinacholeta raha na kuridhisha katika maisha kuliko kitu chochote.
Tafiti nyingi zinaonesha kwamba watu walio kwenye ndoa huishi maisha marefu kuliko singles (sina maana kutaka kukuumiza kwa sababu wewe ni single au ukimbilie kuolewa au kuoa ili uishi miaka mingi, be carefull unaweza kufupisha maisha huo ni utafiti tu na si lengo kuongelea mtu kuwa single)
Kwa kuwa nusu ya ndoa zinazofungwa huvunjika katika baadhi ya nchi, ni muhimu sana kufahamu vizuri package nzima ya mambo ya ndoa katika pande zote.
Knowledge is power!
Pia ni vizuri kukumbuka kwamba (kama hujaolewa au kuoa bado) yale unakutana nayo muda wote wa uchumba hadi honeymoon (unaweza kuwa na honeymoon ya siku kadhaa au miezi kadhaa au mwaka) ni asilimia 10 tu ya masuala ya ndoa na asilimia 90 ni kazi iliyo mbele yako na hii kazi itakupasa kuendelea kuifanya siku zote unavyoendelea na ndoa.
HATUA YA KWANZA NI KUDONDOKEA KWENYE MAPENZI
(Infatuation)
Kibailojia kuna asili ambayo miili yetu huwa msingi katika hatua mbalimbali ambazo hutufanya kuvutiwa na mtu wa jinsia nyingine na kufika hatua tukaona maisha bila huyo mtu hayana maana.
Kuna aina tatu za kemikali (Phenylethylamine, dopamine na norepinephrine ) ambazo huhusika moja kwa moja na kuwafanya wawili wapendanao kwa mara ya kwanza kujikuta wamedondoka kwenye mapenzi (fall in love).

Kwa pamoja hizi kemikali huweza kuzalisha na kutibua matokeo ya kushangaza hadi mtu kuwa na positive attitude na anayempenda, piga ua hukubali kumuacha maana umempenda, watasema usiku watalala kwani nimempata anayenipenda.
Hizi kemikali hutufanya kuwa na nguvu kubwa ya kumpenda mtu na kujisikia tunajisikia very excited na mpenzi mpya.

Hizi kemikali kama nguvu ya hurricane au storm huweza kuufunika ubongo (amygdale) sehemu inayohusika na kutoa tahadhari.
Amygdale huweza kutoa tahadhari au onyo kwamba partner uliyempata anaweza kukuumiza hata hivyo kutokana nguvu iliyopo ya falling in love mhusika hupuuzia.

Mhusika hajui kuonywa ni kitu gani, haogopi watu wanavyosema maana yeye amependa, yupo blind.

Wengi huangukia kwa wapenzi wasiowajua vizuri na hujishangaa kwa nini wanawapenda kwa kasi ya ajabu kiasi hicho.
Kuna powerful attraction kiasi kwamba huweza kusababisha hadi mtu kutoa maamuzi ya ajabu kama vile kukana dini, kukana wazazi kukana ndugu na kukubaliana na huyo amempenda.
Katika hatua hii ya mahusiano wengi hujiona wamefikia na kutimiza ndoto zao.
Kila kitu huwezekana na kukufanya uridhike maana mpenzi anakupa kile unakihitaji amabcho hata wazazi hawawezi kukupa.

Ni hatua natural ambayo mke na mume huvutiana na hupelekea kuoana
Katika hii hatua maisha ni matamu, ahadi kubwa na kedekede kutolewa,
I miss u,
I love u,
You are mine,
I love u from earth to the moon,
Nakupenda kwa moyo wangu wote,
Sina mwingine ila wewe tu.
Wakiwa wamelala hukumbatiana kama vile amelala mtu mmoja (mwili mmoja) ni raha ni kuhitajiana kwa kiu ya ajabu.
Wahusika huwa blind na hata kama mwingine ana makosa au vitu fulani anaudhi huonekana si tatizo, na hukubaliana kuoana hivyo hivyo.

Watafiti wengi wanauona huu upendo katika hatua ya kwanza si upendo wa kweli (not true love) kwani huongozwa na hizo kemikali tatu na kukupa nguvu za attraction za ajabu. Pia haujajaribiwa bado, haujakumbuna na kasheshe bado.

Hii hatua katika mahusiano ya ndoa huitwa hatua ya ghururi (infatuation, self deceit, arrogance, presumption)
Hapa ndipo kunapatika vitu vinaitwa uchumba na honeymoon
Hii natua huweza kudumu hadi miezi 30 muda ambayo hutosha wahusika kuwa na mtoto.

Je, ni hatua zipi hufuata na kupelekea wanandoa kuwa na true love?
Je, mahusiano mengi au ndoa nyingi huvunjika katika hatua ipi?
Na je, ni jambo gani la busara kufanya katika hatua ambayo ndoa nyingi huangukia kwenye shimo?

Tutaendelea………………………

They say it takes a village to raise a child.

That may be the case,
but the truth is that it takes a lot of solid, stable marriages to create a village.
Diane Sollee

Saturday, May 23, 2009

Ni Afya!

Wengi huja na sababu lukuki linapokuja suala la kuwa mwili mmoja (kwenye ndoa) “mara kichwa kinaume” au “nimechoka sana leo” au “sijisikiii vizuri”lengo ni kukwepa sex.
Hata hivyo tafiti nyingi zinaonesha kuwa kuna faida kubwa sana kupata huduma ya tendo la ndoa angalau mara mbili au tatu kwa wiki, kumbuka too much is harmful

FAIDA SEX KWA AFYA YA MWILI
Huimarisha immune system kwenye mwili.
Wanandoa ambao hushiriki angalau mara mbili kwa wiki walionesha kiwango kikubwa cha antibody zinazosaidia kupigana na magonjwa.

Huongeza umri wa kuishi.
Wanaume ambao walikuwa wanafika kileleni (orgasm) zaidi ya miaka 10 wali- boost uwezo wa kuishi miaka zaidi kuliko wale ambao walikuwa na hawafiki kileleni.

Hupunguza uwezokano wa kupata prostate cancer.
Wanaume ambao wali ejaculate zaidi ya miaka 35 walikuwa na asilimia 33 pungufu kupata prostate cancer.

Hupunguza cholesterol (mafuta)
Kutokana na zoezi la kufanya mapenzi (sex) ni zoezi tosha kuweza kupunguza cholesterol na kuondokana na kupata magonjwa ya moyo.

Huimarisha mzunguko wa damu mwilini
Tunapofanya mapenzi mapigo ya moyo huongezeka na mzunguko wa damu huwa na speed zaidi na damu huongezekana maradufu kwenye ubongo na sehemu zingine za mwili na matokeo ni mzunguko wa damu kuwa mzuri mwili mzima.

Huongeza uwezo wa kukua (growth)
Watafiti wengi wanakiri kwamba sex huongeza uwezekano wa mifupa kukua na kuimarisha repair ya tishu kwenye mwili.

Huimarisha uwezo wa kunusa
Baada ya sex, kuzalishwa kwa homoni ya prolactin huongezeka na huwezesha stem cells zilizopo kwenye ubongo kuzalisha neurons ambazo husaidia kunusa vizuri.

Hupunguza maumivu (pain relief)
Unapokaribia kufika kileleni kiwango cha homoni za oxytocin huongezeka mara tano zaidi kuliko kiwango cha kawaida, matokeo ni kutolewa kwa endorphins ambayo hupunguza maumivu ya kila kitu kuanzia kichwa, arthritis nk.

Huimarisha kibofu cha mkojo
Wakati wa sex unatumia muscles zile zile unatumia kukojoa (urine), kutumia mara kwa mara kwa hii misuli huwezesha kuwa na uwezo wa kuthibiti kibofu cha mkojo.

Huimarisha uke
Wanawake ambao huamua kutoshiriki sex wanakuwa na uwezekano wa kujisikia maumivu wakati wa sex (vaginal atrophy) kwa kushiriki mara kwa mara uke huwa mwepesi kutoa lubricant na hakuna maumivu.
Hapa kuna kanuni “use it or lose it!

Husaidia healing ya vidonda
Baadhi ya evidence zinapendekeza kwamba sex huweza kusaidia vidonda kupona haraka, ushahidi ni kwamba homoni za oxytocin husaidia vidonda kupona kwa regeneration ya seli mwilini na oxytocin huzalisha pale ukishiriki sex.

Hupunguza uwezekano wa kupata cancer ya matiti.
Wanawake ambao hawajawahi kuzaa walionekana kuwa na uwezekano mkubwa wa kupata cancer ya matiti, hii ina maana kwamba kujihusisha na sex hupunguza kupata cancer ya matiti.

FAIDA YA SEX KWA AFYA YA AKILI

Hupunguza stress
Sex huweza kupunguza stress kwa kupunguza kiwango cha masumbuko (anxiety) na kuongeza relaxation na kusaidia kuwa na usingizi mzuri.

Hupambana na depression
Wanawake ambao walijihusisha na sex kwa kuwa contact na semen walikuwa less depressed kuliko wale wambao hawakufanya.

Hupambana na kuthibiti alama za kuzeeka
Sex hufanya mtu kuonekana kijana zaidi.
Katika utafiti mmoja watu ambao walishiriki sex zaidi ya mara 3 kwa wiki walionekana ni vijana zaidi ya miaka 10 pungufu ukilinganisha na wale ambao walikwepa sex.

Huimairsha kujisikia upo fit
Dakika 30 za kufanya mapenzi huweza kuchoma kiasi cha 150 calories.
Na mtu anayeshiriki sex kila mara 3 kwa wiki huweza kupunguza kilo 2.5 za uzito kwa mwaka. Pia sex huweza kunyumbua misuli na kupelekea mtu kuwa fit, pia hekaheka za milalo mbalimbali huweza kufanya contractions ya mapaja, mikono, mabega, shingo, tumbo, kifua, mgongo, matako, miguu, kiuno na pia sex huzalisha testosterone ambayo huimarisha mifupa na misuli.

Husaidia nywele kung’aa na ngozi kuwa imara
Sex huongeza kiwango cha estrogen ambayo husaidia nywele kung’aa na ngozi kuwa imara kwa mwanamke.

Husaidia meno kuwa imara
Mara nyingi kabla ya sex wahusika hujitahidi kusafisha meno (brushing) kwa njia hii una kuwa imeimarisha afya ya kinywa.
Pia wakati wa sex hasa maandalizi huhusisha kissing ambayo hufanya kazi nzuri kusafisha meno na fizi.
Seminal plasma zinazozalishwa huwa na zinc, calcium na madini mengine muhimu kwa afya ya meno.


FAIDA YA SEX KWA AFYA YA UZAZI
Husaidia kuwa na mzunguko mzuri za siku za mwanamke.
Wanawake ambao hujihusisha na sex angalau siku moja kwa wiki huwa na mzunguko wa siku uliosawa tofauti na wale ambao hutoa visingizio.

Huimarisha fertility
Kwa kuwa kushiriki sex hufanya mzunguko kuwa regular inakuwa rahisi mwanamke kushika mimba na kuzaa tofauti na mwanamke akiwa na mzunguko wa siku ambao ni irregular.

FAIDA KATIKA KIROHO
Watafiti wengi wanakiri kwamba kuna sexual energy kama energy zingine ambayo wakati wa sex ikiunganishwa kati ya mwanaume na mwanamke hasa wakati wa kufika kileleni huweza kuwaunganisha wawili in deepest part of of selves.
Na hii energy (non physical) huweza kuimarisha maeneo mengine ya maisha yetu, hutufanya kujisikia ni kitu kimoja na kuwa stronger zaidi katika nafsi na mahusiano kwa ujumla.
Hivyo matokeo ni kujisikia vizuri wewe mwenyewe, mwenzi wako na maisha kwa ujumla.

TAHADHARI:
Hii mada ni kwa ajili ya kupeana habari tu (ndiyo maana hakuna reference links, ingawa unaweza mwenyewe ku- Google),
Jambo la msingi ni kwamba kuna umuhimu wa hali ya juu sana kuzingatia kwamba hapa tunazungumzia sex katika ndoa tu na si zaidi ya hapo.
Pia ni muhimu kuzingatia kwamba ili kushiriki sex ni muhimu kuangalia afya ya mwenzi wako, maadili na kutii sheria na amri za Mungu otherwise badala ya sex kukupa afya inaweza kukuua kimwili na kiroho.
Upendo daima!

Friday, May 22, 2009

Lugha za upendo

Wakati mwingine ukikosa kuguswa unapata "skin hunger" MGUSO (physical touch)
Kukumbatia, kubusu, kushikana mikono na sex (ktk ndoa) ni njia ya mawasiliano ya hisia za upendo au kupendwa.
Watafiti wengi hasa wa maendeleo ya watoto wamethibitisha kwamba kukumbatia, kumbusu na kumshika mtoto kunampa afya njema kihisia.
Kuguswa ni kitu muhimu sana katika mawasiliano ya ndoa hasa linapokuja suala la mahaba, kwa kushikana mikono, kubusu, kukumbatiana na kutekenyana kule kunakonyegesha huleta raha sana kwa mke na mume.

Inawezekana mume wako au mke wako kwake kupendwa ni kukumbatiwa au kupata busu kabla hujaondoka asubuhi na unapokutana naye tena baada ya shughuli za kujenga familia au kutembea mmeshikana naye mikono, pia inawezekana kwako ni jambo gumu na unaona kama ushamba fulani hivi au ulimbukeni.
Jambo la msingi fahamu kwamba kila mmoja wetu ana aina ya kujisikia anapendwa na ni kitu kidogo lakini kinaweza kufanya ndoa au mahusiano yako kuwa matamu au machungu.

Unaweza kutumia muda mwingi kumpikia chakula kitamu, au kununulia mizawadi ya gharama, hata hivyo kama mwenzi wako kupendwa ni kupokea mguso wa kimwili bado zawadi zako hazitamkuna vizuri kama ungempa mguso wa kimwili.
Ktk milango ya mitano fahamu, kugusa ndiyo peke yake kunahusisha mwili mzima ingawa kuna sehemu zingine zikiguswa ni balaa zaidi na zinahusisha watu walio katika ndoa tu.
Kuona tunatumia macho, kunusa tunatumia pua, kusikia tunatumia masikio, kuonja tunatumia ulimi lakini kugusa ni mwili mzima.

Sex ni physical touch, ndiyo maana kuna wanawake au wanaume bila kumpa sex anaona bado humpendi hata kama utamnunulia gari au kumpeleka vacation North pole hata hivyo hapa tunazungumzia sex ndani ya ndoa na si vinginevyo.
Mwili ni kwa ajili ya kuguswa,
Unaonaje mtu akigoma kukusalimia mikononi?
Naamini utatambua kwamba kuna mushkeli.Inawezekana mume wako au mke wako kupata mguso wa mwili ni lugha yake ya msingi kuonesha unampenda na anategemea utamgusa mwili wake kila siku kwa kutekenya nywele zake, au kutembea umemshika mkono au kumpa busu na kumkumbatia kila unapoondoka home asubuhi au unaporudi na pia kumpa romance ya uhakika kabla ya sex mkiwa faragha,

KUSAIDIANA KAZI
Hii ni kufanya vitu ambavyo mke wako au mume wako anatarajia au anategemea ungefanya kuonesha unampenda na kumjali na kuwa wewe na yeye ni kitu kimoja.

Inawezekana anategemea ungemsaidia kutandika kitanda, kusafisha nyumba, kupika, kufua nguo, kumsafisha mtoto, kuosha gari, kufyeka majani nk hiyo mnaweza kufanya pamoja na ni njia nzuri ya kueleza kwamba unampenda kwa vitendo.
Tatizo linakuja kutokana na jamii zetu za kitanzania asilimia kubwa ya familia zetu ni extended, hivyo kwa mfano baba akiamka asubuhi na kuanza kufanya usafi wa nyumba au kupika au kufua nguo za wife nahisi hata majirani wataandamana kuuliza kulikoni kwani yawezekana hapo kwako kuna timu ya watu kutoka kijijini au ndugu zako kama dada, kaka, shemeji, wajomba, baba mdogo, ndugu wa shangazi zako au wafanyakazi ulionao kama house girl, house boy na wale wageni waliokuja kutoka kijijini bila kukupa taarifa nahisi watashangaa.

Point hapa ni wewe kumsaidia mwenzi wako kazi hasa mwenzi ambaye kwake kupendwa ni kusaidiana kazi.

MANENO YA SIFA
(Kusifia, kutia moyo na kushukuru)
Je ni mara ngapi umesema Asante au kumsifia spouse wako kwa jinsi alivyofaanya kitu ambacho kilionekana kizuri?
Na je kawaida unapomsifia au ku-appreciate vitu anafanya huwa anajisikiaje?
Hayo maswali ni ya msingi sana mtu kujiuliza hasa kama unataka kujua mwenzi wako kwake maneno matamu ndiyo KUPENDWA.
Maneno mazuri au yanayotia moyo au yanayomsifia ambayo ni matamu husababisha mambo yafuatayo kwa mwenzi wakoHuleta upamoja na ukaribu zaidi (intimacy)Huleta uponyaji kwenye majeraha ya hisia zake kama kuna maumivu moyoni mwake (healing) na kumfarijiMwenzi hujisikia kulindwa zaidi na anajisikia yupo katika mikono salama.

Fahamu kwamba wewe ndiye mtu muhimu kuliko mtu yeyote duniani kwake, hivyo maneno unayoongea either yanamjenga au yanambomoa na si kubomoa tu bali na kumuumiza na unampa wakati mgumu.
Lengo la upendo si kulalamika kwa kile ambacho hupati
bali ni kufanya kile ambacho kitamsaidia yule unayempenda,
yule umechagua uishi naye hadi kifo kitakapowatenganisha.

Mojawapo la hitaji kuu la ndani la mwanadamu ni kuwa appreciated na kile mtu anafanya.
Je umewahi kuwa na boss mkali na mwenye maneno ovyo na mtu wa amri?
Huwa unajisikiaje?
Fikiria unaishi na mke au mume wa aina hiyo.

Nami mwenzi wangu yupo kwenye hili kundi, kwake kumpenda ni pamoja na kumpa appreciation ya yale anafanya hadi jinsi anavyovaa, mwanzo wa ndoa ilikuwa ngumu kujua ila nilishangaa ananiambia mbona wenzako wananiambia nimependeza na wewe husemi chochote?
Kwa kutojua nilikuwa namjibu “ndiyo maana nilikuoa ni kweli unampendeza na hilo najua.

Hata hivyo sasa nimejifunza kusema asante na kumshukuru na kumpa sifa kwa kila anachovaa hata akivaa akapendeza nakuwa mtu wa kwanza kumwambia bibie leo umependeza na unawake.

Tutaendelea!

Thursday, May 21, 2009

Lugha za Upendo

Love is the most powerful weapon for good in the world. Wakati mwenzi (Spouse) wako anajisikia kuridhishwa kimapenzi (emotionally na romantically) hujisikia salama kihisia na hujiona ulimwengu unampa vyote na matokeo yake hujitoa zaidi kuhakikisha anajiweka katika kiwango cha juu kwako kuimarisha upendo na mahusiano kwa ujumla.
Na anapojisikia kutoridhishwa kabisa kimapenzi, hujisikia mweupe, empty na kama vile anatumika au unamtumia tu kufanikisha na kutimiza hitaji lako la mapenzi.
Moja ya tatizo kubwa katika kuonesha upendo (love) tumeshindwa kufahamu kwamba mke na mume huongea lugha tofauti za upendo.
Kila mmoja huwa na namna tofauti jinsi anavyojisikia unampenda kwa mfano mwingine ukimpa zawadi yoyote hujisikia unampenda na ukimsifia anaona ni maneno matupu na mwingine ukimsifia basi hujiona raha na hujisikia unamthamini na kumpenda.
Kuonesha upendo kuna lugha kama zilivyo lugha za mawasiliano na utamu wa lugha ni pale unapoifahamu kwa kuisikia na kwa kuiongea, pia utamu wa upendo katika ndoa au mahusiano ni pale unapofahamu lugha ya upendo kati yako na mpenzi wako.

Itakuwa vigumu sana kwa anayejua kibena kuanza kuongea na anayejua kimasai na wote wakawa wanadhani inawezekana.
Kumbuka Babeli haikujengwa ikaisha kwani baaada ya lugha kuharibiwa kila kitu kilisambaratika.
Kimsingi ili kuelewana na mpenzi wako kuna lugha za msingi tano ambazo kati ya hizo moja wapo inaweza kuwa ni maalumu kwa ajili ya mpenzi wako na kuifahamu au kuzifahamu lugha zake basi unaweza kujenga mahusiano imara.

Hata hivyo mahusiano bora huanza kwanza na Hofu ya Mungu (Christ in you)
Lugha tano muhimu ambazo mara nyingi wapendanao hutumia ni:
1. Kuwa na muda na mwenzi wako (Quality time)
2. Kupeana zawadi (Receiving gifts)
3. Kusaidia kazi (Acts of services)
4. Kumpa maneno ya kumsifia, kumtia moyo kwa kile anafanya (words of Affirmation)
5. Mguso wa kimwili (physical touch)

KUWA NA MUDA NA MWENZI WAKO
(Quality time)
Msingi wa kuwa na muda na mwenzi wako ni upamoja (togetherness) pamoja na kuwa kimawazo, kimwili na kiakili.
Kukaa na kuangalia TV pamoja si kuwa na muda na mwenzi wako kwani hapo mnaipa TV qulity time.
Kuwa na muda na mwenzi wako ni kukaa pamoja na kumpa attention yote, anaongea na wewe unamsikiliza tena ninyi wawili tu. Ni kutembea pamoja yaani mmeamua kwenda kutembea kwa ajili ya kwenda kutembea wewe na yeye tu si kwa sababu mnaenda kanisani au mnaenda kazini.

Kupeana muda wa pamoja ni kama vile kwenda kula pamoja (outing) ninyi wawili na mkifika hapo kwenye hoteli mnaongea kwa kuangaliana ninyi.

Kama mpenzi wako yupo kwenye hili kundi yaani kwake kupendwa ni kuwa pamoja basi ni dhahiri ukifanya haya mara kwa mara anatajisikia raha sana na atajisikia unampenda sana.

Hata hivyo kama mpenzi wako kwake lugha ya upendo ni zawadi ataanza kulalamika why unakuwa na mimi tu muda wote hata zawadi huniletei?
Maana kwake kupokea zawadi ndo kuonesha unampenda na si kufuatana kila mahali.

KUPEANA ZAWADI
(Receiving gifts)
Zawadi ni kitu chochote unachoweza kukishika kwa mikono na kinakupa hisia kwamba aliyenipa zawadi alikuwa ananifikiria na ananipenda.
Zawadi huelezea upendo kwamba alikuwa ananiwaza na kuniona mtu wa maana sana kwake.

Wanandoa wengi hupuuza na kuona kwamba zawadi siyo kitu muhimu ktk mapenzi, pia wapo wengine hudhani zawadi kwa mpenzi hadi kiwe kitu kikubwa kama gari au nyumba, vitu vidogo sana kama pipi, Chocolate au maua ni zawadi za msingi sana na zina maana kubwa sana katika kuimarisha mapenzi katika ndoa.
Nahisi hata wewe msomaji ulikuwa maarufu sana kutoa zawadi wakati wa uchumba na sasa umeacha, Bisha!

Zawadi muhimu pia ni wewe kuwepo au kupatikana pale mke wako au mume wako au mpenzi wako anakuhitaji anapokuwa na shida (wapo wakiona shida hukimbia wapenzi), uzoefu inaonesha zawadi hata za kutoa muda wako hukaa ktk kumbukumbu za mhusika kwa miaka mingi bila kusahau na pia huongeza level ya mapenzi kwako.

Inawezekana mke wako au mumeo ni watu ambao akipewa zawadi basi yeye ndo kupendwa yaani ndo anaguswa zaidi, moyo wake unaamini ukipewa zawadi ndo unapenda.
Kama mpenzi wako kupewa zawadi ndo lugha yake ya upendo basi ikitokea wewe unampa sifa kwa mambo mazuri anafanya usishangae akikwambia punguza maneno zawadi zipo wapi? Atakwambia anataka matendo si maneno!

Tutaendelea ........................................................

Wednesday, May 20, 2009

Usimfananishe na wengine!

James (si jina lake halisi) ana mshangaa mke wake ambaye baada ya kuzaa mtoto ambaye sasa ana miaka miwili amekuwa akikwepa kuvua nguo na kubaki uchi wakiwa pamoja chumbani wakati haikuwa kawaida yake.
Bila kusita James anaamua kumuuliza mke wake mpenzi
vipi mbona siku hizi ni kama unanikwepa nisikuone upo uchi?”
Mke wake Beatrice anajibu
Naogopa utaniona nilivyo na umbo baya kwani nimenenepa sana na najisikia hutanifurahia kuniona na hizi nyama uzembe nilizonazo”

James kwa mshangao huku ana tabasamu anamjibu
Sikutegemea kama unaweza kuwaza hivyo kwani mwili wako ni wa thamani sana kwani umenizalia mtoto mzuri sana hivyo ni faraja na najisikia fahari sana kuuona mwili wako katika umbo lolote kwani nikiuona mwili wako najiona fahari kwani kwa mwili wako tumepata mtoto mzuri sana duniani"

Je, ni wanawake wangapi wanaweza kutegemea majibu ya hekima kama ya James kutoka kwa waume zao hasa pale wakiwa wamebadilika maumbo yao?

John baada ya kuona mke wake amenenepa ghafla baada ya kuzaa watoto wawili akaaamua kununua jarida (magazine) linaloonesha wanawake wembamba wanamitindo na akaliweka kitandani ili akiona asome na ajifunze na kama inawezekana aweze kufanya juhudi kuiga au kurudi kwenye umbo lake zamani na kuonekana sawa na wale wanawake kwenye jarida.

Je, unadhani approach aliyotumia John kuweka jarida ambalo litaonesha wanawake wembamba itasaidia mke wake kujirekebisha?

Jambo la msingi si kutaka kuwaridhisha au kuwapa kichwa wanawake ambao hunenepa baada ya kuzaa na kwamba waridhike na kujiachia, hapana jambo la msingi ni kwamba approach ambayo mwanaume hutumia inaweza kufanya mwanamke kujisikia amedharauliwa na huishia kuumia na kukwazika.

Kutumia kipimo cha wanawake wa kwenye majarida si sahihi kwani wengi hawajawahi kuzaa hata mtoto mmoja na wengine wamefanyiwa plastic surgery baadhi ya viungo vyao kama matiti na hips, na pia picha zao hupitia processs za kuzisafisha ili zionekane nzuri zaidi na kuvutia hivyo ukitaka mke awe kama hao una kazi ya kufanya na si kumsukumia gazeti asome awe kama wao.

Pia ifahamike kwamba ukitaka kufikisha ujumbe mara nyingi kwa mwanamke jambo la msingi ni jinsi unavyowakilisha ujumbe wako unaweza kuwa na nia nzuri hata hivyo jinsi unavyowakilisha huweza kufikisha ujumbe mwingine ambao matokeo ni kuumizana hisia.
Wapo wanaume ambao huenda mbali zaidi kwa kuwalinganisha na wanawake wengine kwa mfano
"Huoni mwenzako Anna sasa amepungua na wewe bado umebaki umenenepeana"
Hakuna kitu kinaumiza kama hicho!
Kuwa positive huweza kusaidia kutatua tatizo kuliko kuwa negative au kulalamika tu,
anyway kwanza ni mke wako hata aweje ni wewe uliyekubali kusema "hadi kifo kitakapo tutenganisha!"
Hivyo kitunze kidumu na kipendeze na si kwa kulaumu na kumlalamikia tu bila kusaidiana.
"Usione vinaelea vimeundwa kwa mawazo positive na kwa upendo wa kweli"

Saturday, May 16, 2009

Kuvuta sigara!

Kushoto na kulia wote wanavuta sigara, wanasema wataacha kuvuta muda wowote;
Je, ni lini?Tumbaku ni drug hatari sana, maelfu ya watu hufa duniani kwa sababu ya kuvuta sigara na viko (pipes).
Matokea ya nicotine iliyopo kwenye sigara na gesi zingine vikiingia kwenye mapafu huongeza tatizo kubwa sana la afya.

Kuvuta sigara kumekuwa na link ya moja kwa moja na cancer ya mapafu na ugonjwa wa moyo.
Pia imejulikana kwamba passive smoking (kuvuta moshi wa wavutaji wakati huvuti) huweza kusababisha risk kwa afya ndiyo maana sehemu nyingi wamezuia kuvuta sigara in public.

Kwa data zilizopo kiwango cha vijana wanaovuta sigara kimeongezeka mara dufu kwa nchi zilizoendelea kama Canada na Britain.

Uvutaji wa sigara katika ndoa:
Wake au waume wa wanandoa ambao wanavuta sigara wamekuwa na wakati mgumu sana katika hisia zao hasa kutokana na tabia ya kuvuta sigara kwa hao partners wao.
Hisia huweza kuwa ni za hofu, mashaka na kujisikia kutothaminiwa au kuwa disappointed na hata kuumizwa na hiyo tabia.

Wapo partners ambao hutafsiri kwamba kitendo cha kutoacha kuvuta sigara ni kuonesha kutojali afya yake mvutaji na familia kwa ujumla yaani mke, mume na watoto.

Anyway, kila mvutaji hupenda kuacha kuvuta sigara hata hivyo hamu na uhitaji wa kuvuta sigara huwa mkubwa zaidi kuliko makali ya kifo hii ina maana mvuta sigara akiwa na hamu ya sigara huwa ladhi kukubali kuvuta sigara kuliko kutovuta kwa kuogopa kifo.

Ukishajiingiza kwenye kuvuta sigara na kuwa addicted na nicotine iliyomo utakuwa ladhi kukubali kifo kuliko kuacha kuvuta.

Wakati mnaoana ulimuahidi partner wako kwamba utampenda, utamheshimu na zaidi mtasaidiana kuhakikisha ndoa yako inalindwa kiroho na kimwili na njia mojawapo ya kutimiza ahadi zako ni kuacha kuvuta sigara.

Pia kama unataka kujifunza kuvuta sigara achana kabisa na hiyo tabia maana kuanza ni rahisi lakini kuacha ni ngumu mno.
Kumbuka
Wavuta sigara huwa na magonjwa mengi kuliko wasiovuta.
Wavuta sigara huishi muda mfupi kuliko wasiovuta.
Nchi zingine kama unavuta sigara; Health Insurance huwa kubwa zaidi kuliko wasiovuta.
Magari au nyumba za wavuta sigara (ambao huvuta ndani ya gari au nyumba) kuuza ni ngumu sana kwani watu hukatishwa tamaa na harufu ya sigara.

Ukivuta sigara kwa zaidi ya miaka 30 unaweza kuwa umekula pesa yenye thamani ya zaidi ya TSh. millioni 200.

Sources
http://www.quitsmoking.com/info/articles/costofsmoking.htm

Friday, May 15, 2009

Inakuwaje!

Hisia
katika mji fulani mwanamke analalamika kwa kuwa mume wake anatembea na mke nje (sex) hata hivyo mwanamke anashangazwa sana kwani mume wake anatembea na mwanamke ambaye ni ugly idara zote kuliko yeye mwenye mume.
"Hilo limwanamke kwanza ni overweight na sura ndo hivyo tena" analalama huyo mwanamke.
Mume akiulizwa kulikoni kutembea na mwanamke kama huyo jibu sahihi na mkato eti
“she has time for me!

Je, hujashuhudia mwanaume anaacha mke mzuri nyumbani na kwenda kutembea na mwanamke ambaye ni garbage?
Je, uzuri wa mwanamke ni sura au elimu yake au kiwango cha hisia na muda anaokupa mwanaume katika ndoa?
Naamini jibu unalijua!

Hata hivyo katika mji mwingine mwanaume (professional/mtaalamu fulani shule imakubali) analia kwani mkewe mrembo wa uhakika anatembea na kijana ambaye ni kibarua wao (sijajua ni house boy au shamba boy maana jamaa analia hata hasemi nilihisi kama ana kizunguzungu vile)
Huyu mwanamke akiulizwa vipi mbona unatembea na kibarua wenu, anajibu
“Ananifanya nijisikie vizuri na tena ananifanya nijisikia mimi ni mwanamke muhimu na wa maana”

Kwa ujumla hawa watu wanaweza kuwa na matatizo gani? na inawezekana mimi na wewe yaakatufika tusipokuwa makini, sitegemei kama wewe ni msomaji wa hii blog maana hapa ni the Hill of Wealth tukianza na ndoa.

Moja
Hawa watu wamewaacha wapenzi wao si kwa sababu ya ubaya wa sura au uzuri wa sura bali ni zaidi ya hapo.

Pili
Inaonesha kuna feelings/hisia ambazo hawa wanandoa hukosa kwa mwenzake na kuamua kwenda kutafuta sehemu zingine au wamekuwa wakizipata kwa hawa watu wamekuwa na affairs nao.

Tatu
Watu wanaotembea (sex) nao wanaonekana wapo smart sana kujua hawa wenzetu (wanandoa) wanakosa kitu gani kwenye ndoa zao.

Nne
Hawa wanaotembea nao wanajua jinsi ya kuwahudumia hawa wanandoa kitu wanakosa katika ndoa zao na kitu wanachokosa ni hisia na mapenzi yanayopelekea kila mmoja kuguswa na mwenzake.

Tano
Unaweza ku- fall in love na hisia za mtu na si mtu mwenyewe, kwa maana kwamba mtu kama ni mwanaume unakosa hisia maalumu kutoka kwa mke wake na kazini kukawa na mwanamke ambaye anajua kile anakosa na akaamua kumpa basi unaweza kufall in love naye hata kama yeye kama mwanamke huna haja naye ila feelings zina nguvu za kuweza kufanya kuwe na affair.
Mfano mume wapati muda wa kukaa na mke wake na mke kila siku yeye ni semina na kusafiri tu na huko ofisini mzee anakaa na secretary wake na wanaokuwa na muda (intimate) hadi kuanza kupeana siri za maisha.
Mwanaume au mwanamke ambaye ametumbukia kwenye tatizo kama hili huweza kurudi haraka kwenye mstari kama mke wake au mume wake akaamua kubadirika kwani ukweli hakumpenda mtu nje bali alizipenda hisia za mtu wa nje.

Suala la kumpa mpenzi wako muda wa pamoja ili aridhike ni muhimu sana kumbuka wewe usipo mpa muda mwingine atampa.

Tumeona wasichana wa kazi, vijana wa kazi, mabosi na kila aina za watu wakifanya vitu vya ajabu na wale tunaowapenda hata hivyo je, sisi tumefanya jitihada gani kutosababisha wao kukosa kile ambacho tungewapa hadi wapewe na wengine?
Hili dudu linaitwa hisia achana nalo kabisa na usifanye mchezo hasa likivaa nguo zinazoitwa mapenzi, halishikiki na linaweza kuleta maafa katika jamii.
Mungu akubariki!

Wednesday, May 13, 2009

Ni Bank Account

Ndoa au Mahusiano Yoyote ya Kimapenzi
ni mfano wa Bank Account tulizonazo.
Unapopata mwenzi wako ni kama vile umefungua Bank Account na katika kuendelea na maisha au relationship kila siku unafanya transaction ambazo ni either Kuweka pesa (Deposits) au Kutoa pesa (Withdraw)

Pia ni muhimu sana kujua hali ya Account yako bank ipoje; kwani unaweza kwenda kuchukua pesa ukakuta hakuna kitu, kumbe huko nyuma uli-overwithdraw zaidi kuliko ulivyotakiwa.
Hakikisha kila Wakati Account Yako Ina Pesa ndipo uzichukue pesa zako.
Love Bank Account ni muhimu sana katika maisha ya kila siku ya mahusiano na kama vile mti au mmea wowote unahitaji kutunzwa ili uweze kustawi na Love bank Account pia inahitaji kuwa na Pesa muda wote ili iweze kudumu.Unapomkubali mtu kuwa mwenzi wako (Soulmate) maana yake umefunguwa Love Bank Account kwake.

Ni jukumu lako kuhakikisha kila siku Kuna Balance ya pesa za kutosha ili inapotokea unahitaji kufanya manunuzi yoyote basi kuna akiba ya kutosha.
Unapompa feelings (hisia) nzuri za kukuhitaji wewe zaidi maana yake unafanya deposits, unaweka pesa za kutosha.
Kuna mambo mengine katika mahusiano watu hudhani ni vitu vidogo sana lakini ni muhimu sana na vina maana kubwa,
Unapo mwamini (trust),
unapompa zawadi haijalisha ni nini na kiasi gani,
unapompa muda, unapo mpa busu,
unampa maneno ya sifa na kutia moyo,
unampomsikiliza,
na kumjali hapo
unafanya Deposit na Account yako kwake inajaa.
Lakini unapokuwa humjali, unampa maneno mazito na magumu yanayoumiza (criticism),
Ignore, hutunzi ahadi zako wala kumlinda na kumpa kile anahitaji
hapo una withdraw kwa kiasi kikubwa na inawezekana unafanya over withdraw ya hiyo Account na siku mambo yakiwa mambo kuna kuwa hakuna balance, na zogo linaanza.
Please Hakikisha Love Bank Account ya Mkeo, Mumeo, Mchumba Wako, Mpenzi Wako Umeifanyia Deposits za Uhakika then Tutajua wewe Unajua Kupenda.
Ubarikiwe na Bwana!

Tuesday, May 12, 2009

Zingatia Haya!

Kumpata mwenza au mke au mume ambaye utaishi naye maisha yako yaliyobaki hapa duniani ni jambo la msingi sana katika maisha ya binadamu.
Na kwa kupenda wenyewe hupelekana hadi kwa viongozi wa dini na kutangaza hadharani kwamba mimi na mwenzangu tunataka kuwa mke na mume na ulimwengu ujue.
Huwa tunakuwa tumejawa na mioyo yenye furaha na kutaka siku ifike upesi ili nianza kuishi na mwenzangu haraka iwezekanavyo.

Mungu bariki mioyo ya maharusi wapya maana hawajui kazi halisi wwanayoenda kuianza kazi halisi (real life) na kuachana na maisha ya uchumba ambayo mengi ni tambarare kama nyikani.
Baada ya honeymoon tu wengine siku ya pili tu, wengine mwezi wa kwanza tu na wengine mwaka wa kwanza tu wa ndoa huanza kujiuliza hili swali;
Lakini hakuna aliyeniambia itakuwa kama hivi?

Alikuwa anaacha mialiko ya watu kwa ajili yako lakini baada ya kukuoa si hivyo tena, unadhani kwa kuwa alikuwa ana cancel mialiko ya kwenda kufanya mambo yake kwa ajili yako kabla hamjaona na mkioana itakuwa the same?
You are wrong!

Ili usipoteze matarajio ya mahusiano yako ya ndoa jaribu kuzingatia mambo yafuatayo (kama unategemea kuoa au kuolewa please print na kafiche haya unaenda kuyasoma na baada ya kuanza ndoa soma tena na pia ukiyaweka moyoni na ukizingatia utakuwa candidate mzuri sana)

Hakuna binadamu anaweza kutimiza mahitaji yako yote:
Mtu ambaye anaweza kutimiza mahitaji yako yote ni BWANA, na ilimpasa kufa ili aweze kukutimizia yote.
Usitegemee ndoa au uliyeoana naye atakutimizia mahitaji yako yote au ahadi zake zote alizoahidi kabla hamjaoana.

Kiwango cha mapenzi hakiwezi kuwa juu kama ilivyo mwanzo wa ndoa.
Jinsi anavyokwambia ‘I love you” huweza kupungua hadi ukashangaa kadri ziku zinaenda ingawa neno “I love u” huleta raha sana kwa mwanamke akisikia kutoka kwa mumewe hata hivyo siku zinavyoenda mwanaume hujisahau na kuanza kula jiwe kusema " I love u"
je, utadai?
Pia wanawake nao (wachache sana) akishazaa huanza kujisahau na kujiona mama na si mrembo bado. Huku ni kukosa ustaarabu na kinyume cha maadali.
shame on you!

Mwanaume anaweza kuwa anakupenda mno lakini bado hatajua unahitaji kitu gani.
Wanawake wengi huja na sentensi ‘ Kama ananipenda angefanya kile napenda afanye” kumbuka usiposema na kumwambia ujue hawezi kujua unataka kitu gani au nini kinakusumbua.
If you don’t ask the answer is NO.
Men read newspapers not minds!

Si mara zote uliyeoana naye atapenda kuimarisha mahusiano.
Katika mazingira ya kawaida wanawake hupenda hata kuimarisha kitu kizuri (mfano ndoa ambayo hata haina mgogoro) hata hivyo wanaume wana msemo wao
“If it is not broken, don’t fix it”
Hivyo tumia hekima na kuomba Mungu ili Mungu awape moyo wa umoja na juhudi ya kuishi kwa amani.

Ndoa haiwezi kukufanya uwe umekamilika.
Si mara zote ukiongeza nusu na nusu unapata kitu kizima.
Wengi ambao ni ‘Single’ hudhani wakioa au kuolewa watakamilika na kujiona complete na kuwa na furaha ya kweli.
Na wengine hufika mbali zaidi kwa kujinyima vacation, kununua vitu vizuri wakisubiri kufanya hivyo wakioa au kuolewa.
Unapoteza muda wako anza kukamilika kwanza kabla ya kuolewa au kuoa na ingia ukiwa si tegemezi kwamba mwenzako atakukamilisha hadi kukupa furaha.
Ndoa ni kuunganisha strength na ku-balance weakness siyo kukaa tu kutegemea mwenzako akukamilishie furaha yako.

Usitegemee kufanya kila kitu pamoja
Kufanya kazi pamoja, kupanga mipango pamoja, kuweka malengo pamoja ni suala zuri sana hata hivyo kila mmoja huhitaji breathing room.
Usitegemee kila kile unapenda basi na mwenzio atakuwa excited nacho si kweli hivyo kuna wakati utahitaji kuwa mwenye na yeye kuwa mwenyewe.
Nakwambia mapema ili siku ikifika usiseme hakuna aliyeniambia, mimi nimekwambia!

Mtu ambaye anaweza kumbadilisha ni yeye mwenyewe si wewe.
Kama unategemea ukioa au kuolewa utambadilisha (change) mpenzi wako basi utakuwa very much disappointed.
Kama kuna vitu vinasumbua kwa mpenzi wako kabla humjaona viangalia vizuri, kutegemea kwamba utamsaidia kubadilika baada ya honeymoon ni kujidanganya kulikokithiri.
Ndoa si mahali pa kulaumiana, kukefyakefya (nagging), hasira na kukosoana.
Kama mpenzi wako hajui UCHAFU ni kitu gani hakikisha anafahamu kabla hamjaoana, na kama unategemea utambadilisha aache ulevi, kuvuta sigara, kuwa mwongo nk shauri yako!

Maswali ya kujadili
Wewe ambaye upo kwenye ndoa sasa je, unaona maratajio yako yote ya ndoa yalitimia?
Je, una matarajio yoyote ambayo unahisi yalikusumbua zaidi?
Je, una ushauri gani kwa wanandoa wapya?

Friday, May 8, 2009

You can’t run way from problems; there is no running away, no place to hide.
Whether rich or poor, you will have to cope.
How well you cope and adapt makes a big difference.

Remember:
Champions never quit!
Kidding!

Thursday, May 7, 2009

Zawadi


Kutoa zawadi ni tendo la upendo.
Lakini wakati mwingine kupeana zawadi huleta kasheshe na kufikia mahali watu kuumizana.
Unapotoa zawadi kwa mpenzi wako ni vizuri kuzingatia yafuatayo:
Toa kile ambacho mpenzi wako anakipenda siyo kile wewe unakipenda vinginevyo kutoa kunaweza kuwa ni kitendo cha uchoyo uliopindukia kama utatoa kila wewe unapenda.
Wengine huwapa wapenzi wao zawadi ambazo wao wanazipenda wakidhani kwamba kwa kuwa wao wanazipenda na wapenzi wao watazipenda, ni vizuri kuchunguza mpenzi wako anapenda kitu gani. Hata kama zawadi ni zawadi.

Zawadi si biashara.
Kutoa si deal kwamba ukitoa basi na yeye lazima atoe. Na kuna wengine akikupa zawadi na wewe usipompa ni kununiana tu.
Unatoa hata kama hutapokea in return ( hata hivyo watoaji hupokea)

Toa zawadi nzuri.
Inawezekana mpenzi wako amekuwa anahitaji Digital Camera na inaonekana kama vile ni usumbufu maana kila wakati anakukumbushia.
Huhitaji kununua bora Digital Camera isipokuwa nunua Digital Camera bora zaidi ya ile alikuwa anahitaji na tofauti na vile alikuwa anategemea.

Toa kwa furaha;
Kutoa kwa furaha (smile) huongeza value ya zawadi. Usitoe kwa kushurutishwa kwa sababu bila kutoa zawadi mpenzi wako anakuwa mkali, toa kutoka moyoni na kwa furaha.

Wednesday, May 6, 2009

Rangi si Kitu sasa!

Miaka 60 iliyopita ilikuwa ni illegal kwa mweusi na mweupe kuoana katika states 40 za USA.
Watu walioamua kuoana huku wakiwa na race tofauti walitumikia kifungo cha miaka 2 au 1 na aliyehusika kufungisha hiyo ndoa aliweza kupata fine inayomtosha.

Kwa mfano katika jimbo la Virginia, Supreme Court iliwahukumu wahusika kwenda jela mwaka mmoja na wakishamaliza kifungo kuondoka Virginia bila kurudi kwa miaka 25 na Jaji aliwahukumu kwa kipengele kinachosema
Mungu aliumba races tofauti kama vile white, black, yellow, malay na red na akawaweka kila race kwenye continent yake na kwa hiyo Mungu alifanya hivyo kwa makusudi ili watu wasichanganyane au kuona”.

Hata hivyo Supreme Court of USA ilikatisha hiyo hukumu na kuwaruhusu watu kuoana race tofauti tarehe 12/06/1967 kwa maana kwamba kukataza mixed marriages si suala la kikatiba kuanzia hapo sasa kuna biracial marriage za kumwaga duniani kote ingawa bado baadhi ya jamii zina mashaka na hili.
Tunaitumia marekani kama mfano kwa sababu ndiyo nchi yenye mchanganyiko wa rangi zote za ngozi kuliko nchi yoyote na kwamba wamepita katika machungu mengi kuhusiana na races.

Biblia haina tatizo na watu wa races tofauti kuona ingawa wapo wakristo vipofu ambao wanadhani kuona rangi tofauti za ngozi ni kinyume cha Biblia.

Hata hivyo binadamu wote wametokana na mtu mmoja Adamu hivyo tangu Mwanzo hadi Ufunuo hakuna mstari unaokataza kuoana races tofauti.

Musa mwenyewe alioa mwanamke wa kiafrika kutoka Ethiopia (Hesabu 12:1) hata Mfalme Sulemani ambaye alivunja rekodi ya kuoa wanawake wengin duniani bado Mungu hakasirikia kwa kuoa wanawake wageni (race tofauti) bali alimkataza kuoa wanawake wanaoamini Mungu tofauti na Jehova.
Hata hivyo unapoamua kuoana na mtu ambaye ni rangi ya tofauti ni muhimu kukumbuka sana kwamba suala la kubaguana lipo na utakumbana nalo ila kama mkishikana vizuri mume na mke na watoto athari huwa kidogo.
Watoto huweza kutaniwa sana na baadhi ya jamii ingawa kwa sasa kuna kukubalika kwa kiwango cha juu sana duniani.

Sasa mambo yamebadilika mweupe anamtaka mweusi (chocolate colour) na kizazi cha sasa kinaona rangi si kitu.

Hata hivyo kabla ya kuoana lazima ufikirie vizuri suala la tamaduni maana tamaduni zingine job description kwa mwanaume ni tofauti, angalia usije ukajuta ni muhimu kuangalia mbali zaidi miaka 30 au 50 ijayo kuliko kuangalia sasa.

Tuesday, May 5, 2009

Ni kuingia tu!

Kawaida ikiona kuna alama ya NO EXIT kuingia humo lazima ufikiria mara mbiliKitendo cha kutoa ahadi kwamba Hadi kifo kitakapotutengenisha ukweli binadamu unakuwa ume –launch moja ya ahadi za pekee duniani.
No turning back, no escape route kulia au kushoto, wawili mnaingia kwenye life boat, hakuna kwa kwenda zaidi ya kubaki na huyo umemkubali.

Ukweli ni kwamba mtu mwenye akili timamu akiambiwa nyumba unayoingia haina EXIT atafikiria kwa makini zaidi na zaidi ya mara mbili.

Kazi yako ipo well defined hakuna kutoka, hapa nazungumzia mtu ambaye kweli yupo serious kwanza kuhakikisha ndoa yake inampa Mungu utukufu na kwamba Kristo ni Bwana katika maisha yake.
Na kwamba suala la dini na imani ni muhimu sana kwake otherwise hakuna shida.
Mambo ambayo wakati mwingine huleta shida sana kwenye ndoa ni dini, rangi (race) na taifa hata hivyo linaloweza kuwa mwiba mkali ni suala la dini.

General rule ni kwamba
“The more couples have in common the better the chance of success”

Ukweli unabaki palepale kwamba waumini wa kweli wa dini tofauti (let say muislam wa swala tano na mkristo aliyeokoka) wakioana kuna uwezekano mkubwa kukumbwa na matatizo yanayohusiana na dini katika ndoa yao.
(Najua ukianza kuzungumzia dini unaweza kuwasha moto ambao kuzima ni ngumu hata hivyo lazima kuongea ukweli)

Watu ambao hupuuza hiki kipengele baada ya kuoana wanayo ya kusimulia kwa masikitiko.
Jambo la msingi kabla ya kuoa au kuolewa ni vizuri kupata solution ya suala la dini au suala la imani, usijidangany kwamba mkioana utanyoosha kwa pasi ya umeme kirahisi suala la hili la dini, hapa unahitaji kuwa genius tumia akili zako zote kuhakikisha umejua nini hatima yake.

Unaweza kuvuka mito mingi tu lakini mto wa dini ni lazima uvuke ukiwa makini kabisa maana unaweza kuzama mbele ya safari.

Je, mtasali wapi na kivipi, na watoto wakizaliwa watakuwa dini gani na dini ya mwenzako ina amini vipi kuhusu ndoa?
Ni maswali ya msingi sana.

Wengi huona hii ni issue ndogo sana na tutakabiliana nayo tukiona sasa muhimu ni love maana nampenda kuliko suala la dini.
Ukweli vitu vidogo ndo hupelekea ndoa kwenda shimoni.
Na kuacha kujadili sasa haiwezi kumaliza tatizo baadae, kumbuka
the sooner the better”
au niseme
“the more you solve now the greater your compatibility later.

Imani ya dini ni moja ya njia mke na mume huwa connected, dini ni big deal na zaidi ili ndoa iwe strong haina budi kuwa na 3 layers yaani connection ya kimwili, kihisia (emotions) na kiroho na bond ambayo hushika ndoa (siyo sex) mara nyingi ni kiroho.

"Marriage is not a trial like foreign dish sampled to see if it is tasty"

Monday, May 4, 2009

Ni mwili mzima!

Haina haja kuchezea kipande tu cha uwanja wakati mnaruhusiwa kiwanja chote na kuonesha skills zote kwa pasi za mbali na karibu loo! Kisaikolojia wanaume wengi (si wote) ni genital aroused (wakiwa kwenye sita kwa sita huwaza sana south pole na kupeleka mkono sharp kama kupokea pesa bank), hata akiwa na Mwanamke anaweza kusisimua matiti na uke tu then akaendelea kuchimbua dhahabu yake na kwa namna na style zote anajua.
Wanawake wao ni “Generally aroused” kwa maana kwamba kwao foreplay ni mwili mzima na mwili mzima kwake ni “one big sex organ” hivyo wana uwanja mkubwa sana wa mwanaume kuchezea kabla ya kwenda bondeni kuchimbua gold habari njema ni kwamba wanawake wanajua kwamba wanahitaji mwanaume mwenye mikono slow kuchezea uwanja mzima kabla ya south pole.

Kwa Mwanamke erogenous zones si matiti na between the legs bali ni entire body, huwa Inaumiza sana wakati mwingine Mwanamke anakuta mwanaume hata kukisi tu anasahau na moja kwa moja anakimbilia kwenye clit.. kwa kuwa ni joy button, ni vizuri lakini unahitaji kuuandaa mwili mzima kwanza hadi mind yake ifunguke na kuwa ready kwa shughuli ndipo ukimbilie kwenye kisimi then nice sex moments.

Wengi katika kujifunza masuala ya mapenzi (hasa wanaume) na hasa suala la kufanya maandalizi (foreplay) anajua kitu cha msingi ni kwenda moja kwa moja kubusu, kuchezea matiti kidogo (geresha tu) then anakimbilia bondeni na kuanza kupima kuona kama kuna unyevu wa kutosha ili mtambo uanze kuchimbua dhahabu huku anasahau kwamba lazima mwili mzima wa mwanamke lazima uhusike kupata matokeo mazuri ya dhahabu unataka kuchimbua, sex ni mwili, mood, ubongo na lazima vyote vijui kwamba kuna mitambo ya kuchimba dhahabu imefika.

Mwanaume kukimbilia bondeni haraka hupelekea sex kuwa na utaratibu unao bore ambao mwisho husababisha Mwanamke kuepukwa sex kwani anajiona unamtumia kutimiza raha zako bila kumpa yeye raha.
Kumpa mguso (emotional touch) kwa kumhudumia mwili mzima ambao kwa mwanamke ni kiungo kimoja cha mapenzi.

Fikiria mwanaume umechelewa kurudi na unakuta mkeo kalala fofofo, kwa kuwa unahamu na kuwa mwili mmoja bila kusema chochote wala kujua mwenzio ameshindaje wewe moja kwa moja na mkono wako sharp unakimbilia kuanza kusugua clit.. yake, huo si ustaarabu kabisa, ni kukosa maadili ya ndoa (immoral) na unahitaji kufahamu kwamba kila kitu kina utaratibu wake huwezi kuweka unga kwenye maji kabla hayajachemka ukitegemea ugali utaiva na kuwa mtamu shauri yako utaishia kujaza unga hadi kiwe kitu kingine na si ugali tena.

Pia kuna wanawake ambao maumbo yao huwa na kasoro kama unene sana, au kifua Kuwa flat kama mwanaume au matiti kuwa makubwa mno (Nido au mtindi, watermelon), huwa hawajisikii vizuri au kutojiamini (bad self image) na huwa na mtazamo negative so akiona wewe ume concentrate hapo anaanza kujisikia vibaya na husababisha kutojiamini (insecurity) then kutosisimka.
Ni vizuri kujifunza strength na weakness za maeneo ya mke au mume wake ili kutosababisha kuharibu mambo pia ni muhimu mtu kujiamini kwamba wewe ni mzuri na kama ulivyo unaweza kuwa mtaalamu na kurishika na kurishisha mwenzako.
Ni wewe so unaogopa nini na mume au mke ni wako.
Wapo wanandoa ambao ni waoga na hawajiamini kiasi cha kushindwa kabisa kuwa uchi mbele ya mwenzake. Ni aibu na kupitwa na wakati.

Pia utafiti unaonesha kwamba wanaume wengi waliooa ni wagumu sana lipokuja suala la kubusiana na wake zao wakati wa maandalizi ya tendo la ndoa, wengi walikuwa wazuri sana kubusu wakati ndoa zilikuwa mpya na miaka inavyoenda basi wanazidi kupunguza skills na muda wa kubusu ingawa wanaonekana kwa sex ndo wenyewe skills zimeongezeka.

Upendo daima!


Jose Eduard KATIKA Moja Moja

Ni jambo la msingi kukumbuka kwamba mlikuwa wawili sasa ni mmoja na si wawili tena sasa ni kufanya mambo kwa umoja

Saturday, May 2, 2009

Ni moto

Sex ni zawadi murua kutoka kwa Mungu yenye makusudi ya ajabu.
Sex hutufanya kuzaliana, kujenga upendo (mutual love au one flesh) pia ili tujisikia raha (pleasure).
Sex ni God given drive kama vile tunavyojisikia njaa, ili tule Mungu aliweka ndani yetu kujisikia njaa. Na ili tuzaliane, kujenga upendo na ku-enjoy kati ya mume na mke katika ndoa Mungu aliumba sex, Mungu ndiye ame-innovate sex si binadamu.
Sex ni kitu ambacho kina nguvu sana na uwezo wa ajabu (powerful) kinachoweza kuharibu na pia kupotoshwa na binadamu.

Sex ni kama moto, uweza kukufanya ujisikie joto kama kuna baridi ila huo moto ukishindwa kuithibiti unaweza kuchoma nyumba yako au misitu na kuweza kukuua.
Watu wengi sasa wamekufa kwa sababu ya sex kama vile magonjwa ya zinaa kama UKIMWi, Kisonono, Kaswende nk.

Wengine wameachwa na wake zao au waume zao na kuzifikisha familia nje ya ndoto zao na maumivu makali wka watoto.
Wengine wamekatwa mapanga na wengine kupata ngeu za kila aina kwenye miili yao.
Wengine hawana amani maana siri walizoziweka ndani ya mioyo yao kuhusiana na sex zinawatafuna kila siku.
Ni kama vile aibu kuona watu wanapata maafa na wengine kufa kutokana na bado decisions kuhusian na sex.

Kama hujaolewa au kuoa kumbuka kusubiri (abstinence) ni uamuzi wa busara kuliko kujiingiza kwenye mapenzi kabla ya ndoa.
Kama umeoa au kuolewa kumbuka mapenzi nje ya ndoa ni janga kubwa kuliko unavyofikiria.

Kwa Mungu hakuna lisilowezekana:

(Luka 1:37)

Friday, May 1, 2009

The man who finds a wife finds a treasure, and receives favor from the LORD.
Proverbs 18:22 (NLT)