"Marriage is our last, best chance to grow up."

Monday, May 25, 2009

Hatua za Ndoa na Mahusiano

Upendo wa kweli ni kusherehekea raha na shida pamoja.Ndoa ni mahusiano yanayoweza na yanayotakiwa kuwa ndiyo kitu kinacholeta raha na kuridhisha katika maisha kuliko kitu chochote.
Tafiti nyingi zinaonesha kwamba watu walio kwenye ndoa huishi maisha marefu kuliko singles (sina maana kutaka kukuumiza kwa sababu wewe ni single au ukimbilie kuolewa au kuoa ili uishi miaka mingi, be carefull unaweza kufupisha maisha huo ni utafiti tu na si lengo kuongelea mtu kuwa single)
Kwa kuwa nusu ya ndoa zinazofungwa huvunjika katika baadhi ya nchi, ni muhimu sana kufahamu vizuri package nzima ya mambo ya ndoa katika pande zote.
Knowledge is power!
Pia ni vizuri kukumbuka kwamba (kama hujaolewa au kuoa bado) yale unakutana nayo muda wote wa uchumba hadi honeymoon (unaweza kuwa na honeymoon ya siku kadhaa au miezi kadhaa au mwaka) ni asilimia 10 tu ya masuala ya ndoa na asilimia 90 ni kazi iliyo mbele yako na hii kazi itakupasa kuendelea kuifanya siku zote unavyoendelea na ndoa.
HATUA YA KWANZA NI KUDONDOKEA KWENYE MAPENZI
(Infatuation)
Kibailojia kuna asili ambayo miili yetu huwa msingi katika hatua mbalimbali ambazo hutufanya kuvutiwa na mtu wa jinsia nyingine na kufika hatua tukaona maisha bila huyo mtu hayana maana.
Kuna aina tatu za kemikali (Phenylethylamine, dopamine na norepinephrine ) ambazo huhusika moja kwa moja na kuwafanya wawili wapendanao kwa mara ya kwanza kujikuta wamedondoka kwenye mapenzi (fall in love).

Kwa pamoja hizi kemikali huweza kuzalisha na kutibua matokeo ya kushangaza hadi mtu kuwa na positive attitude na anayempenda, piga ua hukubali kumuacha maana umempenda, watasema usiku watalala kwani nimempata anayenipenda.
Hizi kemikali hutufanya kuwa na nguvu kubwa ya kumpenda mtu na kujisikia tunajisikia very excited na mpenzi mpya.

Hizi kemikali kama nguvu ya hurricane au storm huweza kuufunika ubongo (amygdale) sehemu inayohusika na kutoa tahadhari.
Amygdale huweza kutoa tahadhari au onyo kwamba partner uliyempata anaweza kukuumiza hata hivyo kutokana nguvu iliyopo ya falling in love mhusika hupuuzia.

Mhusika hajui kuonywa ni kitu gani, haogopi watu wanavyosema maana yeye amependa, yupo blind.

Wengi huangukia kwa wapenzi wasiowajua vizuri na hujishangaa kwa nini wanawapenda kwa kasi ya ajabu kiasi hicho.
Kuna powerful attraction kiasi kwamba huweza kusababisha hadi mtu kutoa maamuzi ya ajabu kama vile kukana dini, kukana wazazi kukana ndugu na kukubaliana na huyo amempenda.
Katika hatua hii ya mahusiano wengi hujiona wamefikia na kutimiza ndoto zao.
Kila kitu huwezekana na kukufanya uridhike maana mpenzi anakupa kile unakihitaji amabcho hata wazazi hawawezi kukupa.

Ni hatua natural ambayo mke na mume huvutiana na hupelekea kuoana
Katika hii hatua maisha ni matamu, ahadi kubwa na kedekede kutolewa,
I miss u,
I love u,
You are mine,
I love u from earth to the moon,
Nakupenda kwa moyo wangu wote,
Sina mwingine ila wewe tu.
Wakiwa wamelala hukumbatiana kama vile amelala mtu mmoja (mwili mmoja) ni raha ni kuhitajiana kwa kiu ya ajabu.
Wahusika huwa blind na hata kama mwingine ana makosa au vitu fulani anaudhi huonekana si tatizo, na hukubaliana kuoana hivyo hivyo.

Watafiti wengi wanauona huu upendo katika hatua ya kwanza si upendo wa kweli (not true love) kwani huongozwa na hizo kemikali tatu na kukupa nguvu za attraction za ajabu. Pia haujajaribiwa bado, haujakumbuna na kasheshe bado.

Hii hatua katika mahusiano ya ndoa huitwa hatua ya ghururi (infatuation, self deceit, arrogance, presumption)
Hapa ndipo kunapatika vitu vinaitwa uchumba na honeymoon
Hii natua huweza kudumu hadi miezi 30 muda ambayo hutosha wahusika kuwa na mtoto.

Je, ni hatua zipi hufuata na kupelekea wanandoa kuwa na true love?
Je, mahusiano mengi au ndoa nyingi huvunjika katika hatua ipi?
Na je, ni jambo gani la busara kufanya katika hatua ambayo ndoa nyingi huangukia kwenye shimo?

Tutaendelea………………………

6 comments:

Anonymous said...

Dear brother , hope you are fine am fine too ,
it is now almost six month since i came to know that educative blog and to me i wish and sincerely appreciate your effort to impart the knowledge and understanding in that area. may HE grant you wisdom for his glory
Thank you Mbilinyi
Daniel.

Lazarus Mbilinyi said...

Hello Daniel,

Thank you so much for the prayers and comments.

For sure I real need wisdom from God to continue blogging on this crucial area of our life.

God bless you

Anonymous said...

Bro uko juu... Naomba umalizie ile ya "LUGHA ZA UPENDO".
Dada M.

Lazarus Mbilinyi said...

Dada M,
Asante sana kwa maoni yako, naamini nilishamaliza kuhusu Lugha za upendo ambazo ni 1. Kupokea zawadi 2. mguso (physical touch) 3. Maneno ya kutia moyo na kusifia 4. muda wa pamoja (quality time) 5. kusaidiana kazi
Soma http://mbilinyi.blogspot.com/2009/05/lugha-za-upendo_22.html

kila mmoja wetu hujisikia vizuri zaidi kama atafanyiwa moja kati ya hivyo vitu vitano (hujisikia umempenda zaidi) ingawa hivyo vyote vitano ni muhimi sana kwa kila mmoja suala ni kwamba kila mmoja ana lugha yake kujisikia unampenda.

Asante sana kama unahitaji ufafanuzi zaidi basi unaweza kuniandikia lazarusmbilinyi@gmail.com

Upendo daima

Yasinta Ngonyani said...

Naanza na Upenda daima kama usemavyo we mwenyewe. zaidi mmependeza sana kama familia itakiwavyo.salimia familia yako

Anonymous said...

Yeah bro, saw the 2nd part of lugha ya Upendo, sijui ilikuaje haikufunguka that day.
Well nice time.
Upendo daima

Dada M.