"Marriage is our last, best chance to grow up."

Tuesday, May 26, 2009

Hatua za Ndoa na Mahusiano

Hivi nilikuwa nawaza nini?Kila mmoja anajua raha ya falling in love or siku za honeymoon je, nini hufuata baada ya hayo?
Wengi hawajui emotional terrain iliyo mbele, au hills zilipo mbele au bonde utakayopita katika kuendelea na ndoa yako.
Hapa kuna hatua predictable ambazo ndoa nyingi hupita, naamini ukiijua hii ramani basi utaweza kufika mahali unapoenda.
Leo tunaendelea na hatua ya pili na ya tatu

HATUA YA PILI NI MAUZAUZA(Nilikuwa nawaza nini)
Ile hali ya kudondokea kwenye mapenzi (fall in love) huchakaa na ukweli halisi huanza kuonekana.
Hii ni hatua ngumu kwa sababu unakumbana na anguko kubwa sana la ndoto zako kuhusiana na mpenzi wako.
Zile tofauti na tumakosa tudogo ambato tulikuwa si kitu sasa huanza kusumbua na kuudhi, mfano kama mwenzi wako alikuwa mzembe kupanga vitu hasa nguo chumbani sasa utaanza kuudhika kwani utajisikia umevulia mno, kama anakoroma sasa utaona usumbufu, kama ana kikwapa sasa unaona kinasumbua, kama ana harufu mbaya mdomoni asubuhi itaanza kukusumbua, tayari sasa vitu vidogo vimekuwa mambo makubwa yanayokuudhi.

Kila mmoja huanza kulalamika kwamba mwenzake hawi kama anavyotegemea.
Kunakuwa na disagreement nyingi kuliko agreement na unagundua kwamba mnatofautiana sana katika mitazamo ya vitu vingi.
Wewe unataka kula hotel unaipenda mwenzako anataka mle nyumbani ili ku save pesa, unapenda usikivu usiku nyumbani mwenzako anataka kusikiliza muziku kwa sauti kubwa.

Ule kuwa mwenzi wangu ni perfect huanza kupotea na imani yako kwake huanza kupotea kwamba mmm kumbe ni mkali kiasi hiki, kumbe ni mchoyo kiasi hiki, kumbe hapendi sex kiasi hiki, kumbe anajua kukalia mwenzake kiasi hiki nk.
Hapa tofauti za malezi, tamaduni, dini, kuamini, tofauti kati ya mwanamke na mwanaume hujitokeza na kuwa wazi.
Katika hatua hii mtu halisi huanza kuonekana na ukweli ni kwamba ndoa huanza kujengwa hapa.
Wengi huanza kujiuliza mbona watu hawakuniambia kwamba ukioa au kutolewa inakuwa hivi kwani anayaanza kuona ni kinyume na matarajio na wengine huanza kujiuliza kwa nini nilioana naye.
Wapo ambao huanza kufikiria wachumba wengine (misri) kwamba labda ningeoana na Fulani alikuwa afadhari kuliko huyu.
Wengi huanza kujiuliza hivi nilikuwa nafikiria nini hadi nikakubali kuoana naye.
Walio na hekima huanza kumuomba Mungu na kupata ushauri wa watu wanaowaamini

HATUA YA TATU NI MATESO, MAJONZI NA TABU(Miserable stage)
Wanandoa hushangaana kwa nini kila mmoja amejiweka gundi kwenye njia zake bila kumjali mwenzake.
Na kila mmoja humwambia mwenzake ungebadilika kila kitu kingekuwa kizuri.
Kama ni mlevi basi hujichimbia mizizi na kuwa mlevi wa kupindukia, kama ni mlevi wa kazi (workaholic) basi ataondoka nyumbani asubuhi na mapema na kurudi midnight eti ana andaa future.
Hata akirudi nyumbani hukuta mke amelala na watoto wamelala na yeye mwenyewe yupo exhausted kiasi kwamba hawezi hata kumuhudumia mkewe.
Hapa ndipo affair nyingi huzaliwa, na ndoa huwa ni vilio, majonzi, Stress, BP, pressure, kukosa usingizi, you name it!Wanasheria wa mambo ya ndoa wengi hutajirika kwenye hatua hii ya ndoa hasa nchi zilizoendelea ambako kuachana ni jambo la kawaida tu (divorce)

Watoto wengi huachwa njia panda na kutojua nini cha kufanya maana mara kwa mara baba na mama hawaelewani.
Hapa ndipo tunafahamu kwamba kupigiana kelele, kulaumiana, kusuguana, kutishiana hakuwezi kubadilisha wapenzi wetu bali kukubaliana kwamba kuna tofauti na kushirikiana kutatua tatizo kwa hekima na busara hupeleka ndoa kwenda hatua nzuri zaidi.

Hii ni discovery stage ambayo wanandoa hujuana na ni opportunity ya kujifunza na kuzalisha true love.Wale wanaokimbia au kuomba talaka au kutoa talaka huenda kutafuta wapenzi wapya ambao hujikuta wameangukia the same boat na matatizo mapya na makubwa zaidi.

Na ndoa nyingi huvunjika hapa na kukosa kufikia stage inayofuata ambayo ni true love kati ya wanandoa.
Ndiyo maana tafiti nyingi zinaonesha kwamba baadhi ya walioachana kwa talaka kuna wakati hutamani kurudiana na wataliki wao au wangejitahidi kuvumilia na hatimaye kutatua matatizo kuliko njia ya kupeana talaka waliochukua.

Wapo ambao huona haina haja kuendelea na hii cold war na huamua kuchukua uamuzi wa kufanya investigation na kuchukua njia sahihi za kujenga mahusiano imara na yenye afya.
Hata hivyo wanaoamua kuchukua huu uamuzi bora wa imani huwa na milima na mabonde ya kupita kufikia hatua ya mwisho ambayo huwapa raha na experience ya ndoa mpya.

2 comments:

Anonymous said...

Hii mada imenigusa sana, nipo kwenye ndoa miaka kama 3 hivi na inafika mahali tabia za mwenzangu zinanifanya nijiulize hivi niliwaza nini hadi tukaoana, hata hivyo wakati mwingine najirudi Kutokana na anavyojitoa kwa ajili yangu na pia hakuna mtu ambaye ni perfect.
Nasubiri hatua zingine za ndoa ili nijifunze zaidi.
Ubarikiwe

Lazarus Mbilinyi said...

Ni kweli wakati mwingine unaweza kumshangaa jinsi partner wako anavyofanya tofauti na ulivyotegemea pia inawezekana na yeye anajisikia the same kwako.

Jambo la msingi kumbuka kwamba hiyo ndiyo hatua muhimu sana inayofanya muwe connected na baada ya hapo mtakuwa na true love kwani kila mmoja atamkujua vizuri mwenzake maana mnakuwa mmpeita katika hali zote (shida na raha)
Jambo la msingi ni kwamba unatakiwa kutumia busara na hekima ili muweze kuvuka na kwenda hatua ya mbele ambayo ni nzuri zaidi na si kukata tamaa na kuwa negative na kujiona ulifanya uamuzi potofu.

Utasemaje tumetoka mbali kama hamjavumiliana na kupita katika shida na raha?

Mungu akupe nguvu na mafanikio

Upendo daima