"Marriage is our last, best chance to grow up."

Friday, May 15, 2009

Inakuwaje!

Hisia
katika mji fulani mwanamke analalamika kwa kuwa mume wake anatembea na mke nje (sex) hata hivyo mwanamke anashangazwa sana kwani mume wake anatembea na mwanamke ambaye ni ugly idara zote kuliko yeye mwenye mume.
"Hilo limwanamke kwanza ni overweight na sura ndo hivyo tena" analalama huyo mwanamke.
Mume akiulizwa kulikoni kutembea na mwanamke kama huyo jibu sahihi na mkato eti
“she has time for me!

Je, hujashuhudia mwanaume anaacha mke mzuri nyumbani na kwenda kutembea na mwanamke ambaye ni garbage?
Je, uzuri wa mwanamke ni sura au elimu yake au kiwango cha hisia na muda anaokupa mwanaume katika ndoa?
Naamini jibu unalijua!

Hata hivyo katika mji mwingine mwanaume (professional/mtaalamu fulani shule imakubali) analia kwani mkewe mrembo wa uhakika anatembea na kijana ambaye ni kibarua wao (sijajua ni house boy au shamba boy maana jamaa analia hata hasemi nilihisi kama ana kizunguzungu vile)
Huyu mwanamke akiulizwa vipi mbona unatembea na kibarua wenu, anajibu
“Ananifanya nijisikie vizuri na tena ananifanya nijisikia mimi ni mwanamke muhimu na wa maana”

Kwa ujumla hawa watu wanaweza kuwa na matatizo gani? na inawezekana mimi na wewe yaakatufika tusipokuwa makini, sitegemei kama wewe ni msomaji wa hii blog maana hapa ni the Hill of Wealth tukianza na ndoa.

Moja
Hawa watu wamewaacha wapenzi wao si kwa sababu ya ubaya wa sura au uzuri wa sura bali ni zaidi ya hapo.

Pili
Inaonesha kuna feelings/hisia ambazo hawa wanandoa hukosa kwa mwenzake na kuamua kwenda kutafuta sehemu zingine au wamekuwa wakizipata kwa hawa watu wamekuwa na affairs nao.

Tatu
Watu wanaotembea (sex) nao wanaonekana wapo smart sana kujua hawa wenzetu (wanandoa) wanakosa kitu gani kwenye ndoa zao.

Nne
Hawa wanaotembea nao wanajua jinsi ya kuwahudumia hawa wanandoa kitu wanakosa katika ndoa zao na kitu wanachokosa ni hisia na mapenzi yanayopelekea kila mmoja kuguswa na mwenzake.

Tano
Unaweza ku- fall in love na hisia za mtu na si mtu mwenyewe, kwa maana kwamba mtu kama ni mwanaume unakosa hisia maalumu kutoka kwa mke wake na kazini kukawa na mwanamke ambaye anajua kile anakosa na akaamua kumpa basi unaweza kufall in love naye hata kama yeye kama mwanamke huna haja naye ila feelings zina nguvu za kuweza kufanya kuwe na affair.
Mfano mume wapati muda wa kukaa na mke wake na mke kila siku yeye ni semina na kusafiri tu na huko ofisini mzee anakaa na secretary wake na wanaokuwa na muda (intimate) hadi kuanza kupeana siri za maisha.
Mwanaume au mwanamke ambaye ametumbukia kwenye tatizo kama hili huweza kurudi haraka kwenye mstari kama mke wake au mume wake akaamua kubadirika kwani ukweli hakumpenda mtu nje bali alizipenda hisia za mtu wa nje.

Suala la kumpa mpenzi wako muda wa pamoja ili aridhike ni muhimu sana kumbuka wewe usipo mpa muda mwingine atampa.

Tumeona wasichana wa kazi, vijana wa kazi, mabosi na kila aina za watu wakifanya vitu vya ajabu na wale tunaowapenda hata hivyo je, sisi tumefanya jitihada gani kutosababisha wao kukosa kile ambacho tungewapa hadi wapewe na wengine?
Hili dudu linaitwa hisia achana nalo kabisa na usifanye mchezo hasa likivaa nguo zinazoitwa mapenzi, halishikiki na linaweza kuleta maafa katika jamii.
Mungu akubariki!

3 comments:

angel said...

hy mi naitwa angel,i really enjoy ur blog,inanifundisha mambo mengi.i am a graduate,hard working and i do have a relationship of 6 years hope 2 get married soon,thanx and please kip it up.
cheers!

Lazarus Mbilinyi said...

Congratulations dada Angel,

Inapendeza kwamba utaolewa very soon tunakuombea Mungu akufanuikisha kwani naamini upo katika pilikapilika nyingi hata hivyo usisahau kupita hapa ili tuweze kujifunza pamoja mambo mazuri kwa ajili ya wale tunawapenda.

Upendo daima

Anonymous said...

Habari kaka Lazarus.
Mimi naitwa Maryam, ni fun mkubwa wa blog yako.
Kuna rafiki yangu alinitumia article ya heading ya Hisia. Nikaisoma then chini yake kukawa na link yako.
Napenda kukupongeza kwa kazi nzuri unayoifanya kutuelimisha na kutupa mwanga wa maisha ya ndoa.
Articles zako zinanisaidia sana. Nimeziprint zote 4 future use as natarajia kufunga ndoa mwezi wa July.

Plse usichoke kututumia articles za kutuelimisha wana ndoa watarajiwa ili tuweze kuleta mabadiliko katika jamii.

Big up sana

M.