"Marriage is our last, best chance to grow up."

Saturday, May 16, 2009

Kuvuta sigara!

Kushoto na kulia wote wanavuta sigara, wanasema wataacha kuvuta muda wowote;
Je, ni lini?Tumbaku ni drug hatari sana, maelfu ya watu hufa duniani kwa sababu ya kuvuta sigara na viko (pipes).
Matokea ya nicotine iliyopo kwenye sigara na gesi zingine vikiingia kwenye mapafu huongeza tatizo kubwa sana la afya.

Kuvuta sigara kumekuwa na link ya moja kwa moja na cancer ya mapafu na ugonjwa wa moyo.
Pia imejulikana kwamba passive smoking (kuvuta moshi wa wavutaji wakati huvuti) huweza kusababisha risk kwa afya ndiyo maana sehemu nyingi wamezuia kuvuta sigara in public.

Kwa data zilizopo kiwango cha vijana wanaovuta sigara kimeongezeka mara dufu kwa nchi zilizoendelea kama Canada na Britain.

Uvutaji wa sigara katika ndoa:
Wake au waume wa wanandoa ambao wanavuta sigara wamekuwa na wakati mgumu sana katika hisia zao hasa kutokana na tabia ya kuvuta sigara kwa hao partners wao.
Hisia huweza kuwa ni za hofu, mashaka na kujisikia kutothaminiwa au kuwa disappointed na hata kuumizwa na hiyo tabia.

Wapo partners ambao hutafsiri kwamba kitendo cha kutoacha kuvuta sigara ni kuonesha kutojali afya yake mvutaji na familia kwa ujumla yaani mke, mume na watoto.

Anyway, kila mvutaji hupenda kuacha kuvuta sigara hata hivyo hamu na uhitaji wa kuvuta sigara huwa mkubwa zaidi kuliko makali ya kifo hii ina maana mvuta sigara akiwa na hamu ya sigara huwa ladhi kukubali kuvuta sigara kuliko kutovuta kwa kuogopa kifo.

Ukishajiingiza kwenye kuvuta sigara na kuwa addicted na nicotine iliyomo utakuwa ladhi kukubali kifo kuliko kuacha kuvuta.

Wakati mnaoana ulimuahidi partner wako kwamba utampenda, utamheshimu na zaidi mtasaidiana kuhakikisha ndoa yako inalindwa kiroho na kimwili na njia mojawapo ya kutimiza ahadi zako ni kuacha kuvuta sigara.

Pia kama unataka kujifunza kuvuta sigara achana kabisa na hiyo tabia maana kuanza ni rahisi lakini kuacha ni ngumu mno.
Kumbuka
Wavuta sigara huwa na magonjwa mengi kuliko wasiovuta.
Wavuta sigara huishi muda mfupi kuliko wasiovuta.
Nchi zingine kama unavuta sigara; Health Insurance huwa kubwa zaidi kuliko wasiovuta.
Magari au nyumba za wavuta sigara (ambao huvuta ndani ya gari au nyumba) kuuza ni ngumu sana kwani watu hukatishwa tamaa na harufu ya sigara.

Ukivuta sigara kwa zaidi ya miaka 30 unaweza kuwa umekula pesa yenye thamani ya zaidi ya TSh. millioni 200.

Sources
http://www.quitsmoking.com/info/articles/costofsmoking.htm

4 comments:

ashura said...

yes kaka...ni true.sasa hivi wanamlizwa na price plus tax ya sigara.si utani.....shy

Anonymous said...

UONGOZI wa Kanisa la Efatha jijini Dar es Salaam, umewapiga marufuku waumuni wake hususani wanawake na mabinti wanaovaa mavazi ambayo huleta vishawishi kwa wanaume na kuamua kushona majoho ili kuwadhibiti wale wanaokiuka sheria.


Akizungumza katika kikao cha wanawake na mabinti, mke wa Mtume na Nabii wa kanisa hilo, Eliakunda Mwingira alisema lengo la kushona majoho ni kuhakikisha wanawahifadhi wanawake au mabinti watakaokuja wamevaa vituko katika nyumba ya ibada.


Alisema majoho hayo yatakuwa yakihifadhiwa kanisani hapo na pindi muumini atakayefika kanisani hapo na nguo ambazo hazistahili kuvaliwa mahala hapo patakatifu wanamuhifadhi kwa kumpa joho.


"Baadhi ya waumini hawajui ni mavazi gani yanafaa kwenda nayo kanisani na yapi hayafai.. hivyo ni vyema mwanamke akajiheshimu kwa kuvaa nguo za heshima ambazo, hazitaleta kikwazo kwa wanaume", alisema Eliakunda na kuongeza;


"Mavazi ambayo hayafai kuvaa kanisani ni pamoja na suruali za jeans, mashati ambayo yanaonyesha mgogo, pamoja na nguo fupi (vimini), hizi ni nguo ambazo mtu unapaswa kuvaa akiwa kwenye disko au sherehe na siyo kanisani,"alisisitiza.


Hata hivyo Eliakunda alifafanua kwamba, wanawake na mabinti wanapaswa kuwa kielelezo bora katika jamii, kwa kujiheshimu kimavazi na kitabia ili kuweza kupunguza vishawishi kwa wanaume.

Mwanasosholojia said...

Kaka, ahsante kwa post hii, mimi sijawahi kabisa kuvuta, ila nina marafiki kibao ambao wanavuta, huwa nawashauri mara kibao kuachana na sigara, lakini haiwaingii akilini!Hapo ndipo nashindwa kuwaelewa. Madhara ya hii kitu yanaonekana, wanayaona lakini hawajali!

Lazarus Mbilinyi said...

Mwanasosholojia,

Hongera sana kwa ushauri wako ni kweli hawa watu wanashangaza sana, anyway kila mmoja ukimuuliza lini ataacha anakwambia muda wowote hata hivyo muhimu kama hujawahi vuta sigara acha kabisa kujaribu maana ukiingia ni gereza hatari sana.

Pia bei ya sigara imepanda sana hivyo inaathiri sana kipato cha familia.

Kuachana na kuvuta sigara ni moja ya kuonesha unajali familia yako na wale unaowapenda.

Upendo daima!