"Marriage is our last, best chance to grow up."

Thursday, May 21, 2009

Lugha za Upendo

Love is the most powerful weapon for good in the world. Wakati mwenzi (Spouse) wako anajisikia kuridhishwa kimapenzi (emotionally na romantically) hujisikia salama kihisia na hujiona ulimwengu unampa vyote na matokeo yake hujitoa zaidi kuhakikisha anajiweka katika kiwango cha juu kwako kuimarisha upendo na mahusiano kwa ujumla.
Na anapojisikia kutoridhishwa kabisa kimapenzi, hujisikia mweupe, empty na kama vile anatumika au unamtumia tu kufanikisha na kutimiza hitaji lako la mapenzi.
Moja ya tatizo kubwa katika kuonesha upendo (love) tumeshindwa kufahamu kwamba mke na mume huongea lugha tofauti za upendo.
Kila mmoja huwa na namna tofauti jinsi anavyojisikia unampenda kwa mfano mwingine ukimpa zawadi yoyote hujisikia unampenda na ukimsifia anaona ni maneno matupu na mwingine ukimsifia basi hujiona raha na hujisikia unamthamini na kumpenda.
Kuonesha upendo kuna lugha kama zilivyo lugha za mawasiliano na utamu wa lugha ni pale unapoifahamu kwa kuisikia na kwa kuiongea, pia utamu wa upendo katika ndoa au mahusiano ni pale unapofahamu lugha ya upendo kati yako na mpenzi wako.

Itakuwa vigumu sana kwa anayejua kibena kuanza kuongea na anayejua kimasai na wote wakawa wanadhani inawezekana.
Kumbuka Babeli haikujengwa ikaisha kwani baaada ya lugha kuharibiwa kila kitu kilisambaratika.
Kimsingi ili kuelewana na mpenzi wako kuna lugha za msingi tano ambazo kati ya hizo moja wapo inaweza kuwa ni maalumu kwa ajili ya mpenzi wako na kuifahamu au kuzifahamu lugha zake basi unaweza kujenga mahusiano imara.

Hata hivyo mahusiano bora huanza kwanza na Hofu ya Mungu (Christ in you)
Lugha tano muhimu ambazo mara nyingi wapendanao hutumia ni:
1. Kuwa na muda na mwenzi wako (Quality time)
2. Kupeana zawadi (Receiving gifts)
3. Kusaidia kazi (Acts of services)
4. Kumpa maneno ya kumsifia, kumtia moyo kwa kile anafanya (words of Affirmation)
5. Mguso wa kimwili (physical touch)

KUWA NA MUDA NA MWENZI WAKO
(Quality time)
Msingi wa kuwa na muda na mwenzi wako ni upamoja (togetherness) pamoja na kuwa kimawazo, kimwili na kiakili.
Kukaa na kuangalia TV pamoja si kuwa na muda na mwenzi wako kwani hapo mnaipa TV qulity time.
Kuwa na muda na mwenzi wako ni kukaa pamoja na kumpa attention yote, anaongea na wewe unamsikiliza tena ninyi wawili tu. Ni kutembea pamoja yaani mmeamua kwenda kutembea kwa ajili ya kwenda kutembea wewe na yeye tu si kwa sababu mnaenda kanisani au mnaenda kazini.

Kupeana muda wa pamoja ni kama vile kwenda kula pamoja (outing) ninyi wawili na mkifika hapo kwenye hoteli mnaongea kwa kuangaliana ninyi.

Kama mpenzi wako yupo kwenye hili kundi yaani kwake kupendwa ni kuwa pamoja basi ni dhahiri ukifanya haya mara kwa mara anatajisikia raha sana na atajisikia unampenda sana.

Hata hivyo kama mpenzi wako kwake lugha ya upendo ni zawadi ataanza kulalamika why unakuwa na mimi tu muda wote hata zawadi huniletei?
Maana kwake kupokea zawadi ndo kuonesha unampenda na si kufuatana kila mahali.

KUPEANA ZAWADI
(Receiving gifts)
Zawadi ni kitu chochote unachoweza kukishika kwa mikono na kinakupa hisia kwamba aliyenipa zawadi alikuwa ananifikiria na ananipenda.
Zawadi huelezea upendo kwamba alikuwa ananiwaza na kuniona mtu wa maana sana kwake.

Wanandoa wengi hupuuza na kuona kwamba zawadi siyo kitu muhimu ktk mapenzi, pia wapo wengine hudhani zawadi kwa mpenzi hadi kiwe kitu kikubwa kama gari au nyumba, vitu vidogo sana kama pipi, Chocolate au maua ni zawadi za msingi sana na zina maana kubwa sana katika kuimarisha mapenzi katika ndoa.
Nahisi hata wewe msomaji ulikuwa maarufu sana kutoa zawadi wakati wa uchumba na sasa umeacha, Bisha!

Zawadi muhimu pia ni wewe kuwepo au kupatikana pale mke wako au mume wako au mpenzi wako anakuhitaji anapokuwa na shida (wapo wakiona shida hukimbia wapenzi), uzoefu inaonesha zawadi hata za kutoa muda wako hukaa ktk kumbukumbu za mhusika kwa miaka mingi bila kusahau na pia huongeza level ya mapenzi kwako.

Inawezekana mke wako au mumeo ni watu ambao akipewa zawadi basi yeye ndo kupendwa yaani ndo anaguswa zaidi, moyo wake unaamini ukipewa zawadi ndo unapenda.
Kama mpenzi wako kupewa zawadi ndo lugha yake ya upendo basi ikitokea wewe unampa sifa kwa mambo mazuri anafanya usishangae akikwambia punguza maneno zawadi zipo wapi? Atakwambia anataka matendo si maneno!

Tutaendelea ........................................................

1 comment:

Anonymous said...

Sawa mtaalamu!
Nimekubali

USA