"Marriage is our last, best chance to grow up."

Friday, May 22, 2009

Lugha za upendo

Wakati mwingine ukikosa kuguswa unapata "skin hunger" MGUSO (physical touch)
Kukumbatia, kubusu, kushikana mikono na sex (ktk ndoa) ni njia ya mawasiliano ya hisia za upendo au kupendwa.
Watafiti wengi hasa wa maendeleo ya watoto wamethibitisha kwamba kukumbatia, kumbusu na kumshika mtoto kunampa afya njema kihisia.
Kuguswa ni kitu muhimu sana katika mawasiliano ya ndoa hasa linapokuja suala la mahaba, kwa kushikana mikono, kubusu, kukumbatiana na kutekenyana kule kunakonyegesha huleta raha sana kwa mke na mume.

Inawezekana mume wako au mke wako kwake kupendwa ni kukumbatiwa au kupata busu kabla hujaondoka asubuhi na unapokutana naye tena baada ya shughuli za kujenga familia au kutembea mmeshikana naye mikono, pia inawezekana kwako ni jambo gumu na unaona kama ushamba fulani hivi au ulimbukeni.
Jambo la msingi fahamu kwamba kila mmoja wetu ana aina ya kujisikia anapendwa na ni kitu kidogo lakini kinaweza kufanya ndoa au mahusiano yako kuwa matamu au machungu.

Unaweza kutumia muda mwingi kumpikia chakula kitamu, au kununulia mizawadi ya gharama, hata hivyo kama mwenzi wako kupendwa ni kupokea mguso wa kimwili bado zawadi zako hazitamkuna vizuri kama ungempa mguso wa kimwili.
Ktk milango ya mitano fahamu, kugusa ndiyo peke yake kunahusisha mwili mzima ingawa kuna sehemu zingine zikiguswa ni balaa zaidi na zinahusisha watu walio katika ndoa tu.
Kuona tunatumia macho, kunusa tunatumia pua, kusikia tunatumia masikio, kuonja tunatumia ulimi lakini kugusa ni mwili mzima.

Sex ni physical touch, ndiyo maana kuna wanawake au wanaume bila kumpa sex anaona bado humpendi hata kama utamnunulia gari au kumpeleka vacation North pole hata hivyo hapa tunazungumzia sex ndani ya ndoa na si vinginevyo.
Mwili ni kwa ajili ya kuguswa,
Unaonaje mtu akigoma kukusalimia mikononi?
Naamini utatambua kwamba kuna mushkeli.Inawezekana mume wako au mke wako kupata mguso wa mwili ni lugha yake ya msingi kuonesha unampenda na anategemea utamgusa mwili wake kila siku kwa kutekenya nywele zake, au kutembea umemshika mkono au kumpa busu na kumkumbatia kila unapoondoka home asubuhi au unaporudi na pia kumpa romance ya uhakika kabla ya sex mkiwa faragha,

KUSAIDIANA KAZI
Hii ni kufanya vitu ambavyo mke wako au mume wako anatarajia au anategemea ungefanya kuonesha unampenda na kumjali na kuwa wewe na yeye ni kitu kimoja.

Inawezekana anategemea ungemsaidia kutandika kitanda, kusafisha nyumba, kupika, kufua nguo, kumsafisha mtoto, kuosha gari, kufyeka majani nk hiyo mnaweza kufanya pamoja na ni njia nzuri ya kueleza kwamba unampenda kwa vitendo.
Tatizo linakuja kutokana na jamii zetu za kitanzania asilimia kubwa ya familia zetu ni extended, hivyo kwa mfano baba akiamka asubuhi na kuanza kufanya usafi wa nyumba au kupika au kufua nguo za wife nahisi hata majirani wataandamana kuuliza kulikoni kwani yawezekana hapo kwako kuna timu ya watu kutoka kijijini au ndugu zako kama dada, kaka, shemeji, wajomba, baba mdogo, ndugu wa shangazi zako au wafanyakazi ulionao kama house girl, house boy na wale wageni waliokuja kutoka kijijini bila kukupa taarifa nahisi watashangaa.

Point hapa ni wewe kumsaidia mwenzi wako kazi hasa mwenzi ambaye kwake kupendwa ni kusaidiana kazi.

MANENO YA SIFA
(Kusifia, kutia moyo na kushukuru)
Je ni mara ngapi umesema Asante au kumsifia spouse wako kwa jinsi alivyofaanya kitu ambacho kilionekana kizuri?
Na je kawaida unapomsifia au ku-appreciate vitu anafanya huwa anajisikiaje?
Hayo maswali ni ya msingi sana mtu kujiuliza hasa kama unataka kujua mwenzi wako kwake maneno matamu ndiyo KUPENDWA.
Maneno mazuri au yanayotia moyo au yanayomsifia ambayo ni matamu husababisha mambo yafuatayo kwa mwenzi wakoHuleta upamoja na ukaribu zaidi (intimacy)Huleta uponyaji kwenye majeraha ya hisia zake kama kuna maumivu moyoni mwake (healing) na kumfarijiMwenzi hujisikia kulindwa zaidi na anajisikia yupo katika mikono salama.

Fahamu kwamba wewe ndiye mtu muhimu kuliko mtu yeyote duniani kwake, hivyo maneno unayoongea either yanamjenga au yanambomoa na si kubomoa tu bali na kumuumiza na unampa wakati mgumu.
Lengo la upendo si kulalamika kwa kile ambacho hupati
bali ni kufanya kile ambacho kitamsaidia yule unayempenda,
yule umechagua uishi naye hadi kifo kitakapowatenganisha.

Mojawapo la hitaji kuu la ndani la mwanadamu ni kuwa appreciated na kile mtu anafanya.
Je umewahi kuwa na boss mkali na mwenye maneno ovyo na mtu wa amri?
Huwa unajisikiaje?
Fikiria unaishi na mke au mume wa aina hiyo.

Nami mwenzi wangu yupo kwenye hili kundi, kwake kumpenda ni pamoja na kumpa appreciation ya yale anafanya hadi jinsi anavyovaa, mwanzo wa ndoa ilikuwa ngumu kujua ila nilishangaa ananiambia mbona wenzako wananiambia nimependeza na wewe husemi chochote?
Kwa kutojua nilikuwa namjibu “ndiyo maana nilikuoa ni kweli unampendeza na hilo najua.

Hata hivyo sasa nimejifunza kusema asante na kumshukuru na kumpa sifa kwa kila anachovaa hata akivaa akapendeza nakuwa mtu wa kwanza kumwambia bibie leo umependeza na unawake.

Tutaendelea!

No comments: