"Marriage is our last, best chance to grow up."

Saturday, May 30, 2009

Maji yameingiliwa na Mdudu!

CHIMBA KISIMA CHAKO MWENYEWE
By Faustin Munishi:

Uchimbe kisima wewe mwenyewe unywe maji yako peke yako na usiyashiriki nao wengine ni hatari kubwa eeh!
Maji ya kisima cha watu wengi yameingiliwa na mdudu ukiwa na kiu usiyaonje utaambukizwa eeh.
Na kiu ya maji imeongezeka watu wanayanywa kila wakati na yanauzwa kote barabarani nani atapona eeh?
Kwa sababu maji yana mdudu yanapatikana kirahisi ukipita kote utayaona wacha kuyachota eeh.

Ukiwa na njaa ni ya chakula huwa ni vigumu upatiwe lakini sigara na hata pombe watakupatia eeh.
Unajua kwa nini?
kwa sababu pombe na sigara zinaua wanataka na wewe ufe na wao wanakupatia eeh.
Tena na siku hizi na hayo maji yaliyo yaliyoingiwa na mdudu utapewa bure bila kuomba ili mfe wote eeh.
Yapo kwenye chupa kubwa na ndogo watu wanazipenda zile ndogo wanafikiliria zipo salama wamedanganyika eeh.
Wanazifunika nusunusu wamefanya hivyo makusudu ili waamushe kiu ya maji usidanganyjike eeh!

Ndugu jihadhari na maji ya rahisi kachimbe kisima wewe mwenyewe ukiwa na kiu uyanywe maji uliypoyachimba heri.
Dawa ya mdudu hawajaipata wanaitafuta kotekote umwamini Yesu akuokoea amalize kiu

Unaweza kusikiliza wimbo hapa chini

Mithali 5: 15 – 19
Unywe maji ya birika lako mwenyewe, na maji yenye kububujika kwenye kisima chako.
Chemichemi yako ibarikiwe nawe umfurahia mke wa ujana wako!

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Lazarus umenifurahisha sana yaani ikanibidi nicheze naye. Wimbo mzuri sana Jumapili Njema kaka.

Lazarus Mbilinyi said...

Dada Yasinta,

Kaka Munishi nimependa sana hilo fumbo lake.
Jitahidi kutunza Kisima ili wadudu wapite mbali.

Upendo daima!