"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, May 13, 2009

Ni Bank Account

Ndoa au Mahusiano Yoyote ya Kimapenzi
ni mfano wa Bank Account tulizonazo.
Unapopata mwenzi wako ni kama vile umefungua Bank Account na katika kuendelea na maisha au relationship kila siku unafanya transaction ambazo ni either Kuweka pesa (Deposits) au Kutoa pesa (Withdraw)

Pia ni muhimu sana kujua hali ya Account yako bank ipoje; kwani unaweza kwenda kuchukua pesa ukakuta hakuna kitu, kumbe huko nyuma uli-overwithdraw zaidi kuliko ulivyotakiwa.
Hakikisha kila Wakati Account Yako Ina Pesa ndipo uzichukue pesa zako.
Love Bank Account ni muhimu sana katika maisha ya kila siku ya mahusiano na kama vile mti au mmea wowote unahitaji kutunzwa ili uweze kustawi na Love bank Account pia inahitaji kuwa na Pesa muda wote ili iweze kudumu.Unapomkubali mtu kuwa mwenzi wako (Soulmate) maana yake umefunguwa Love Bank Account kwake.

Ni jukumu lako kuhakikisha kila siku Kuna Balance ya pesa za kutosha ili inapotokea unahitaji kufanya manunuzi yoyote basi kuna akiba ya kutosha.
Unapompa feelings (hisia) nzuri za kukuhitaji wewe zaidi maana yake unafanya deposits, unaweka pesa za kutosha.
Kuna mambo mengine katika mahusiano watu hudhani ni vitu vidogo sana lakini ni muhimu sana na vina maana kubwa,
Unapo mwamini (trust),
unapompa zawadi haijalisha ni nini na kiasi gani,
unapompa muda, unapo mpa busu,
unampa maneno ya sifa na kutia moyo,
unampomsikiliza,
na kumjali hapo
unafanya Deposit na Account yako kwake inajaa.
Lakini unapokuwa humjali, unampa maneno mazito na magumu yanayoumiza (criticism),
Ignore, hutunzi ahadi zako wala kumlinda na kumpa kile anahitaji
hapo una withdraw kwa kiasi kikubwa na inawezekana unafanya over withdraw ya hiyo Account na siku mambo yakiwa mambo kuna kuwa hakuna balance, na zogo linaanza.
Please Hakikisha Love Bank Account ya Mkeo, Mumeo, Mchumba Wako, Mpenzi Wako Umeifanyia Deposits za Uhakika then Tutajua wewe Unajua Kupenda.
Ubarikiwe na Bwana!

2 comments:

Mwanasosholojia said...

Nakiri kuwa nilibanwa mkuu nikawa napita hapa kibarazani kwani kwa kasi kila mara, sasa angalau kidogo nina ahueni. Mada hii imenivutia sana ndugu yangu, nafurahi kuona hukosi jipya lakuliwaza nyoyo zetu na kuchangamsha akili zetu! Hongera sana. Hii dhana ya bank account naona kwa sasa ndiyo inachukua nafasi, ingawa kuna wengine nafikiri wanaitumia vibaya. Wao wanaitumia kipesa/ kiuwezo zaidi hali ambayo inapelekea mahusiano kuwa na maana ya "kama huna kitu hakuna penzi". Tukiichukulia kama ulivyo eleza, nina uhakika matatizo ndani ya mahusiano yatapuungu kama si kwisha kabisa!

Lazarus Mbilinyi said...

Asante sana kaka kwa kupita hapa!

Mwenyewe nipo na kazi fulani na wengine taaluma zetu ni kufanyia upasiaji miti na miti mingi inapatikana porini so inakuwa kazi kweli.

Upendo daima