"Marriage is our last, best chance to grow up."

Saturday, May 2, 2009

Ni moto

Sex ni zawadi murua kutoka kwa Mungu yenye makusudi ya ajabu.
Sex hutufanya kuzaliana, kujenga upendo (mutual love au one flesh) pia ili tujisikia raha (pleasure).
Sex ni God given drive kama vile tunavyojisikia njaa, ili tule Mungu aliweka ndani yetu kujisikia njaa. Na ili tuzaliane, kujenga upendo na ku-enjoy kati ya mume na mke katika ndoa Mungu aliumba sex, Mungu ndiye ame-innovate sex si binadamu.
Sex ni kitu ambacho kina nguvu sana na uwezo wa ajabu (powerful) kinachoweza kuharibu na pia kupotoshwa na binadamu.

Sex ni kama moto, uweza kukufanya ujisikie joto kama kuna baridi ila huo moto ukishindwa kuithibiti unaweza kuchoma nyumba yako au misitu na kuweza kukuua.
Watu wengi sasa wamekufa kwa sababu ya sex kama vile magonjwa ya zinaa kama UKIMWi, Kisonono, Kaswende nk.

Wengine wameachwa na wake zao au waume zao na kuzifikisha familia nje ya ndoto zao na maumivu makali wka watoto.
Wengine wamekatwa mapanga na wengine kupata ngeu za kila aina kwenye miili yao.
Wengine hawana amani maana siri walizoziweka ndani ya mioyo yao kuhusiana na sex zinawatafuna kila siku.
Ni kama vile aibu kuona watu wanapata maafa na wengine kufa kutokana na bado decisions kuhusian na sex.

Kama hujaolewa au kuoa kumbuka kusubiri (abstinence) ni uamuzi wa busara kuliko kujiingiza kwenye mapenzi kabla ya ndoa.
Kama umeoa au kuolewa kumbuka mapenzi nje ya ndoa ni janga kubwa kuliko unavyofikiria.

Kwa Mungu hakuna lisilowezekana:

(Luka 1:37)

2 comments:

Anonymous said...

kaka lazarus, uko sahihi kabisa inawezekana kuvumilia mpk siku ifike, but lazma uwe mtu mwenye hofu ya Mungu, vinginevyo hutaweza.
mdogo wako Grace

Lazarus Mbilinyi said...

Mdogo wangu Grace,

Ni kweli maisha bila hofu ya Mungu hufiki popote na ukiingia kwenye mahusiano ndo zaidi kwani kumjua Mungu na kuishi sawasawa na mapenzi yake ndiyo ufunguo wa maisha bora ya mahusiano au ndoa.

Upendo daima