"Marriage is our last, best chance to grow up."

Friday, May 29, 2009

Tunaenda ICU!

Baadhi ya Wanaume baada ya tendo la ndoa hujikuta hoi bin taabani.
Na wanawake wengi hulalamika sana na hii tabia ambapo mwanaume akishamaliza tu hujikoka usingizi na kuanza kukoroma within seconds.
Na hali huwa mbaya zaidi kwani kabla ya sex mwanamke hakuandaliwa kwa muda wa kutosha na mwanaume anamaliza haraka hata kabla mwanamke hajafikishwa popote na kitu cha ajabu zaidi mwanaume akimaliza analala fofofo.

Pia Wanaume wenyewe hawawezi kuondokana na hili kwani ni suala la kisaikolojia na lipo nje ya uwezo.
Hata hivyo akijifunza anaweza kuwa tofauti.

Mwanaume huweza kutengeneza mbegu (semen) kila baada ya masaa 42 hadi 72 na hiki kitendo husababisha mgandamizo wa kimwili wa kutaka kuzitoa kwa njia ya sex.
Pia wanasayansi wanasema kwamba kila drop moja la majimaji ya mbegu za kiume (seminal fluid) huwa kunakuwa na zaidi ya mbegu za kiume milioni 300 na mwanaume ana uwezo wa kutoa hizo mbegu kupitia sex (ejaculation) mara 2 au 3 kwa siku.

Kitendo cha kutoa hizo mbegu huhusisha nguvu za kimwili na kihisia na huwa na pressure kubwa sana wakati zinatoka na kumfanya mwanaume kuwa hoi kabisa.
Huo utoaji wa nguvu ni kama mlipuko wa nje wa bomu (outward explosion) tofauti na mwanamke ambaye kwake huwa internal/ inward/inside explosion.

MENGINEYO
Pia wanaume wanaoishi vijijini Utafiti unaonesha kwamba wao hushiriki tendo la ndoa mara nyingi zaidi kuliko wanaume wa mijini, hii ni kutokana na wanaume wa mijini kukumbana na misukosuko ya maisha na kuathirika kisaikolojia hivyo kuathiri mwili kutaka sex.

Wanaume huwa frustrated sana na wanawake kwa sababu wanawake mara nyingi hawapendi sex.
Wanawake nao huwa frustrated sana na wanaume kwa sababu wanaume kila wakati wao wanataka sex.
Wanawake wanawalaumu wanaume kwa sababu hawajui kupenda.
Wanaume nao wanawalaumu sana wanawake kwa sababu wanaongelea sana upendo lakini hawataki kuweka katika vitendo (sex)
Binadamu hufanya mapenzi kwa sababu ya homoni ya testosterone ambayo kwa kiasi kikubwa ni kwa wanaume.
Mwanaume wa kawaida huzalisha hii homoni mara 20 kuliko mwanamke, ndiyo maana mwanaume anakuwa na drive kubwa ya sex.
Hii ina maana kwamba jinsi mwanaume anavyojisikia kukosa sex kwa siku moja ni sawa na mwanamke anavyojisikia kukosa sex kwa siku 20.

Mwanaume anaweza kuzalisha mtoto kila anapofanya mapenzi wakati mwanamke anaweza kuzaa watoto kwa kila baada ya miaka miwili, hii ina maana kwamba mwanamke anatakiwa kuchagua nani anatakiwa kuwa baba wa mtoto.Wanaume siku zote wanatafuta quantity wakati wanawake siku zote wao ni kutafuta quality.

Ndiyo maana wanaume hutafuta sex kwenye mahusiano na wanawake hutafuta upendo.
Kwa mwanamke upendo ni proof kwamba mwanaume atabaki kwake na kuwa naye wakati wanaume wao baada ya sex ndiyo hujisikia mwanamke anampenda.

Men fall in love through sex; women fall in sex through love.

9 comments:

Anonymous said...

Hap solution ni kuto kuwaoa kabisa ,hawa warembo. kumbe vurugu zao zote za kutaka kuolewa kumbe mambo si hivyo. Heri wakae bila kuolewa kuliko kusumbua watu kiasi hiki. eti wana taka kupedwa kwa maneno ,pengine busu la mdomoni tuu. Basi wanawake matatizo matupu, kuzaa kimbembe, kitandani nako ndoo kabisa sasa wanataka nini kwa wanaume. Lipstick? zakutokea kwenda kupiga umbea jinsi alivyo mwekea ngumu mumewe mumewe?
pia nimesikia wanaume wengi wanalalamika kuwa wanawake wanataka kupednwa bila wao kupenda? hivi hivi viumbe kweli vimeanza kupotea.
Kweli kazi ipo ningekuwa na ngazi ndefu ningeenda kumwuliza aliye tuumba.
Edmund.

Lazarus Mbilinyi said...

Kaka Edmund,

Usinichekeshe sana, hakuna kitu kizuri kama mwanamke asilimia kubwa inatokana na wewe mwanaume ulivyo, ukiwa ovyo unatengeneza mwanamke ovyo na ukiwa smart unatengeneza mwanamke smart so "A man creates a woman"
Ila wakati mwingine hawa viumbe kuwaelewa mwanaume unahitaji kuwa na hekima na busara ya ajabu kwani wengi wanaishi miaka hata 30 bado anakuwa hajui mke wake anataka kitu gani katika maisha.
Pia wanaume tunadhani kumpa kumpa mwanamke nyumba nzuri, gari zuri, mahitaji yote ya pesa bila wewe kuwa karibu naye basi upo romantic, ni kweli ni vizuri kufanya hayo yote ila bila kuwa karibu na yeye kihisia, kimwili na kumpa upendo na kubembelezana hahahaha hapo ni muhimu zaidi,
Wewe Edmund nahisi unatakiwa uoe mke wa kizungu uone habari yake kwani wapo ambao hata sex lazima uandike apllication letter hata hivyo siku ukifika anakugomea vilevile huku mzee unajikunja na kazi zote ndani nna nje hahaha kidding!

Ni kweli hakuna ngazi inafika huko sana sana ametupa Bible hapo ukisoma utapata majibu yote.

Upendo daima

Anonymous said...

Mh!
Sidhani kama mada ililenga kuwakanda wanawake. Nafikiri ilikuwa ni kujua mahitaji ya wanawake ili pindi ukimtimizia mambo yawe shwari. Ni kweli baadhi ya wanawake hawapendi sex kwa sababu wanaume wanaofanya nao hawajui kuwaridhisha. Utakuta janaume likisha paramia dakika 2 haziishi kashamaliza unamuachia mwenzio shombo tu. Kwa hiyo its obvious sex haitakuwa na maana kwake.
Sasa endapo wanaume wataweza kuwafanya wanawake waenjoy sex mbona shwari tu.... kama unabisha muulize jamaa yangu jinsi ninavyoiomba mwenyewe.

UPENDO DAIMA...!
Dada M.

Lazarus Mbilinyi said...

Dada M,

Upo sahihi kabisa, si kwamba wanawake hawapendi sex, tatizo ni wanaume (baadhi si wote) wanakuwa focused kwenye sex kuliko kuwapenda wake zao.
Tukumbuke kwamba kila mwanaume anafanya kabla ya kwenda chumbani na mke wake ni muhimu kuliko kile kinachofanyika chumbani wakiwa faragha.

Upendo daima

Simon. said...

hi;
nice blog you have out there..
i real like it and will be droping daily to check whats up in here..
you can also check mine at
http://samvande.blogspot.com
regards.

Lazarus Mbilinyi said...

Kaka Simon,

Thank you so much for the comments, Nimepita kwako I real appreciate your detailed informative blog.
I have added in my list for anybody to view it.

Love Always!

Anonymous said...

sina namba ya simu dada M.Ningemwuliza sasa hivi kama sijaambiwa maajabu. Lakini poa kama unawezea ni kazi njema. Kaza buti.
Lakini hata hivyo sijaelewa hata kidogo. Acheni uvivu, uvivu hata kwenye asali, maajabu haya!!.
Edmund.

Anonymous said...

Wapendwa taratibu mambo yatanyoka!!!. Unajifanya kocha nenda kavae buti tukuone unavyo rukaruka kihasara uwanjani, kama hatuja kutoa hata bila kugusa mpira!!!
simon

Anonymous said...

halo hahaaaa haha hahah!!, you have made my day!!! nilikuwa sijasoma, ati application mapema kupata hizo pilipili!!!!, na CV je sio muhimu????.
Basi kwaheli!!! ,Hiyo dunia ya marriage ni yenu wenyewe.
edmund.