"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, May 20, 2009

Usimfananishe na wengine!

James (si jina lake halisi) ana mshangaa mke wake ambaye baada ya kuzaa mtoto ambaye sasa ana miaka miwili amekuwa akikwepa kuvua nguo na kubaki uchi wakiwa pamoja chumbani wakati haikuwa kawaida yake.
Bila kusita James anaamua kumuuliza mke wake mpenzi
vipi mbona siku hizi ni kama unanikwepa nisikuone upo uchi?”
Mke wake Beatrice anajibu
Naogopa utaniona nilivyo na umbo baya kwani nimenenepa sana na najisikia hutanifurahia kuniona na hizi nyama uzembe nilizonazo”

James kwa mshangao huku ana tabasamu anamjibu
Sikutegemea kama unaweza kuwaza hivyo kwani mwili wako ni wa thamani sana kwani umenizalia mtoto mzuri sana hivyo ni faraja na najisikia fahari sana kuuona mwili wako katika umbo lolote kwani nikiuona mwili wako najiona fahari kwani kwa mwili wako tumepata mtoto mzuri sana duniani"

Je, ni wanawake wangapi wanaweza kutegemea majibu ya hekima kama ya James kutoka kwa waume zao hasa pale wakiwa wamebadilika maumbo yao?

John baada ya kuona mke wake amenenepa ghafla baada ya kuzaa watoto wawili akaaamua kununua jarida (magazine) linaloonesha wanawake wembamba wanamitindo na akaliweka kitandani ili akiona asome na ajifunze na kama inawezekana aweze kufanya juhudi kuiga au kurudi kwenye umbo lake zamani na kuonekana sawa na wale wanawake kwenye jarida.

Je, unadhani approach aliyotumia John kuweka jarida ambalo litaonesha wanawake wembamba itasaidia mke wake kujirekebisha?

Jambo la msingi si kutaka kuwaridhisha au kuwapa kichwa wanawake ambao hunenepa baada ya kuzaa na kwamba waridhike na kujiachia, hapana jambo la msingi ni kwamba approach ambayo mwanaume hutumia inaweza kufanya mwanamke kujisikia amedharauliwa na huishia kuumia na kukwazika.

Kutumia kipimo cha wanawake wa kwenye majarida si sahihi kwani wengi hawajawahi kuzaa hata mtoto mmoja na wengine wamefanyiwa plastic surgery baadhi ya viungo vyao kama matiti na hips, na pia picha zao hupitia processs za kuzisafisha ili zionekane nzuri zaidi na kuvutia hivyo ukitaka mke awe kama hao una kazi ya kufanya na si kumsukumia gazeti asome awe kama wao.

Pia ifahamike kwamba ukitaka kufikisha ujumbe mara nyingi kwa mwanamke jambo la msingi ni jinsi unavyowakilisha ujumbe wako unaweza kuwa na nia nzuri hata hivyo jinsi unavyowakilisha huweza kufikisha ujumbe mwingine ambao matokeo ni kuumizana hisia.
Wapo wanaume ambao huenda mbali zaidi kwa kuwalinganisha na wanawake wengine kwa mfano
"Huoni mwenzako Anna sasa amepungua na wewe bado umebaki umenenepeana"
Hakuna kitu kinaumiza kama hicho!
Kuwa positive huweza kusaidia kutatua tatizo kuliko kuwa negative au kulalamika tu,
anyway kwanza ni mke wako hata aweje ni wewe uliyekubali kusema "hadi kifo kitakapo tutenganisha!"
Hivyo kitunze kidumu na kipendeze na si kwa kulaumu na kumlalamikia tu bila kusaidiana.
"Usione vinaelea vimeundwa kwa mawazo positive na kwa upendo wa kweli"

No comments: