"Marriage is our last, best chance to grow up."

Tuesday, June 30, 2009

God, the best maker of all marriages,
Combine your hearts into one.-
William Shakespeare

Ni utamaduni tu!

Fikiria wewe ni mwanamke; mume wako mpenzi amesafiri kwa mwaka mmoja au miwili na umemmiss kweli, una hamu naye, huhitaji chochote ula unamtaka yeye maana ni haki yako na ni wako, bahati nzuri au mbaya siku anafika wewe ndo umeanza siku zako (MP)

Je, utahakikisha unafanya unaloweza kuhakikisha mnakuwa mwili mmoja au ndo kula jiwe hadi siku tano ziishe?

UTANGULIZI:
Kuwa mwili mmoja wakati mwanamke yupo MP kunahusisha mila, desturi na tamaduni zenye mawazo tofauti baadhi ya tamaduni ni marufuku kubwa (mwiko) au ni unajisi kujihusisha na kuwa mwili mmoja wakati mwanamke yupo MP, hata hivyo kuna wanawake (na wanaume) na madaktari wengi wanaothibitisha kwamba hakuna tatizo na badala yake kuna faida kubwa.

Kwa wastani mwanamke huwa na siku 500 za MP katika maisha yake hii inatokana kuwa na siku 5 kwa wastani kati ya siku 28 za mwezi mmoja; hii ina maana kwamba zoezi hili litakumbana na siku ambazo suala la sex kwake linaweza kuleta usumbufu kwani atakuwa anahitaji kujishusisha ila atajikuta yupo MP.

JE, ZIPI NI FAIDA ZA KUWA MWILI MMOJA WAKATI WA MP?
Mwanamke akifikia kileleni (orgasm) hutoa homoni za endorphins ambazo ni natural pain killer na mood enhancer hivyo huweza kupunguza maumivu ya MP, kichwa na msongo wa mawazo pia husaidia flow ya damu kwa siku zinazofuata (Dr Monique Rainford - gynaecologist).

Mwanamke hujisikia raha zaidi (pleasurable) kwani uke na kisimi huwa sensitive zaidi na kuguswa kidogo tu mwanamke husisimka kwa hisia kali zaidi ni moja ya nyakati ambazo mwanamke libido huwa juu.

JE, NINI HASARA ZA KUWA MWILI MMOJA WAKATI WA MP?
Kisaikolojia baadhi ya wanawake hujiona ni wachafu (messy) na hujisikia vibaya (uncomfortable) hivyo hawezi kufurahia kuwa mwili mmoja.
Kama mwanamke au mwanaume ana maambukizi inakuwa rahisi kuambukizana magonjwa kwani viungo vya mwanamke vinakuwa delicate na rahisi kuambukizwa.
Pia ana uwezekano mkubwa wa kuambukizwa fungus (yeast) na bacteria (candidiasis) kwa kuwa pH ya uke huwa na kiwango kidogo cha acid.

JE, MWANAMKE ANAWEZA KUPATA MIMBA KUWA MWILI MMOJA WAKATI YUPO MP?
Ndiyo kuna uwezekano wa kupata mimba ikiwa tu mwanamke ana mzunguko mfupi sana ambao siku anayokuwa fertile ndo siku anaanza siku zake.
Pia sperms zinaweza kukaa zaidi ya siku 5 na kuweza kurutubisha yai baada ya siku kumalizika.

Kuchukua tahadhari kuwa mwili mmoja wakati wa mwanamke kuwa katika siku zake ni jambo la msingi zaidi na hupelekea tendo kuwa la raha na wapo wanawake wanakubali kwamba sex wakati huo huwa na raha ya ajabu na kupunguza maumivu ya kuwa kwenye siku zake (menstrual cramps)

Hata hivyo kila ndoa ina aina yake ya kuwa mwili mmoja hivyo kumfahamu vizuri mpenzi wako au mwenzi wako ndilo jambo la msingi kwani mnaweza kukwazana na ikaleta mzozo mkubwa.

Ubarikiwe na Bwana.

Monday, June 29, 2009

"The most wasted day is that in which we have not laughed."

Sunday, June 28, 2009

Nimenunua jipya, niendeshe vipi?

Mimi ni ijana wa kiume mwenye umri wa miaka 27 natagemea kuoa miezi miwili ijayo kwa ndoa takatifu.
Napenda kujua nini cha kufanya kumwandaa mwanamke siku nikiwa honeymoon kwani hii itakuwa mara yangu ya kwanza kuwa na mwanamke (mwili mmoja)
Je, unaweza kunipa tips muhimu kumuandaa mwanamke kabla ya tendo la ndoa?


Kwanza nakupongeza sana kwa kuwa umegundua umuhimu wa kumwandaa mwenzi wako (foreplay) ambaye kwanza ni kifaa kipya kabisa na hii itakuhakikisha anapata muda wa ku-relax na kuwa na mood kwa ajili ya tendo takatifu na matokeo wewe pamoja na mwenzi wako mtafurahia.
Kitu cha msingi kabla kuwanza kuwa mwili mmoja ni vizuri kuwa na maombi kwanza kwa sababu ndo yako ni takatifu.
Kumbuka wewe mwanaume ndiyo kiongozi, mnaweza kuanza kwa kila mmoja kuomba mwenyewe kwanza then baada ya muda unaweza kumsogelea mwenzi wako na kumshika mikono ya kuanza kuomba pamoja (kushukuru kwa Mungu kufanikisha ndoa yenu na zaidi kuombeana ili muweze kuwa mwili mmoja.)
Baada ya kushikana mikono unaweza kuendelea kumkumbatia huku mnaendelea kuombeana hadi mnamaliza sala yenu.
Baada ya hapo kuna njia panda unaweza kuendelea naye hadi mnakuwa mwilim mmoja au mnaweza kumaliza maombi na kuendelea na processs za hapa chini.

Kumwandaa mwanamke kuwa mwili mmoja huanza kwa maneno, ongea kile ambacho kitamfanya damu yake kuwa hot.
Pia matendo huweza kufanya kitu cha maana zaidi kuliko maneno, wakati unampa maneno mguse kwa kupalaza (lightly) kwenye mwili wake wanawake husisimka kwa kuguswa wakati wanaume kwa kuona; tembeza mkono kama mawimbi unapoongea au kutoa zile hadithi zako za kumtengeneza mood, huku ukiwa karibu kiasi cha nywele zake kugusa uso wako.

Wakati wa maongezi mguse kwa wororo (tenderly) anza kuingilia himaya yake (siyo sehemu za siri – private parts) bali private space.
Unaweza kugusa mkono wake au kuondoka kitu chochote kwenye nywele zake au uso wake (hata kama hakipo we si unajua unafanya kitu gani) au unaweza kushika mikono yake (au vidole ) na kufanya massage kiana kwa kutumia vidole vyako.

Anza kumsifia jinsi alivyo ukianza na nguo au kitu chochote amevaa (hapo ndipo ugonjwa wa wanawake wengi ulipo) sifia sura yake na vile alivyo kama vile nywele, kucha, lips na vingine unavyovijua wewe, sifia kwa uhakika na kiukweli anyway ni kweli ur wife is so beautiful ndo maana upo naye hapo.

Jihusishe naye zaidi kwa kumgusa (touching) katika njia ambayo si ya kuashiria unataka sex pia kwa hatua kama hii usithubutu kumbusu yeye bali yeye ndo utakuomba umbusu.

Maongezi yako yanatakiwa sasa kuwa ya kimahaba zaidi, tumia sexy words, mwambie unavyojisikia kihia (feelings) ongea kwa ulaini ili akuelewe kirahisi, unapoongea mnong’oneze kwenye makisio yake kama vile unamwambia siri hata kama mpo chumbani wawili tu.
Wakati unamnong’oneza sogeza zaidi lips za mdomo wako kwenye masikio yake na kugusisha na kumpa kabusu ka kiaina halafu achia kumruhusu yeye kujiachia kwako zaidi na kukung’ang’ania zaidi.
Ukiona anakuegemea zaidi ongeza kabusu kengine kwenye sikio huku ukimwambia maneno matamu na yanayovutia ya kimahaba.
Ukiona joto lake linazidi sasa usifanye kosa anza kusambaza mikono yako na kumgusa kila eneo la mwili wake (kiwanja kizima) lakini usiguse matiti, au chini (sehemu za siri) bali tumbo, mgongo, shingo, mikono, miguu, kidevu nywele nk.

Anza kusambaza busu lako kuanzia kwenye lile sikio, shingo, kinywa huku yeye akiendelea kukuinamia na wewe unaendelea kumpoa soft kisses baada ya hapo naamini moto maji yataanza kuchemka kiasi kwamba kupoa itakuwa kazi nzito na ukiona hakuna kitu anza square one au soma hapa.

Saturday, June 27, 2009

If you love something, set it free.
If it comes back to you, it's yours. If it doesn't, it never was.

We do not possess anything in this world, least of all other people.
We only imagine that we do.
Our friends, our lovers, our spouses, even our children are not ours; they belong only to themselves.
Possessive and controlling friendships and relationships can be as harmful as neglect.

Friday, June 26, 2009

Ukibomoa moja, jenga tano!

“Nimepoteza hisia za kumpenda, zimepotea na zimepotea kabisa.
Simpendi kabisa Julia na hata sifahamu kama kweli niliwahi kumpenda; nashangaa na sihitaji kuwa naye tena, sijisikii chochote linapokuja suala na hisia zangu kwake naamini ndoa imefika mwisho” James aliongea kwa mshangao mbele ya Julia

Julia naye akajibu kwa kusema “hata sielewi tumefikia vipi hatua hii.
Tunaongea mara chache sana na hata tukiongea hatuongea jema lolote, (machozi yanaanza kumiminika kwenye mashavu) ni kulaumiana, kudharauliana, kusutana, kila mmoja anampuuza mwenzake, ndoto zimeyeyuka na hakuna ladha ya maisha.
Hapa nina maumivu makali.
Hivi inawezekana mtu ukashindwa kabisa kumpenda mtu ambaye alikuwa bila yeye maisha hayana maana?

Hali kama hii huwakuta wanandoa wengi na watu wengi walio katika mahusiano; haijalishi ni miaka mingapi au mlikuwa mnapendana kiasi gani na bila kujifahamu vizuri na kutumia busara na hekima kumaliza hili tatizo ndoa au mahusiano huweza kujikuta yameangukia kwenye shimo lefu mno.

Kila ndoa ina positive na negative moments, mwanandoa mmoja akiwa anamwangalia mwenzake kwa negatives tu itafika mahali ataanza kuji – withdraw na kujiweka mbali na automatically ataanza kujisahau kuwa caring. Wakati mmoja anajiweka mbali na mwenzake huyu mwingine huanza ku-panic na kuanza kutoa lawama kwamba hupendwi. Wanavyozidi kusuguana ndivyo wanazidi kusababisha mafuriko ya lawama emotionally na matokeo ni kuwa disconnected katika emotions na feelings.
Guess what?
Moto huo hautazimika!

Kuna bwana mmoja anaitwa Gottman yeye na rafiki zake walifanya utafiti kuhusiana na positives na negatives kwenye suala la ndoa na mahusiano na kutoa jumuisho kwamba quality ya emotions ilizonazo kwa mwenzi wako ni muhimu sana.
Ni simple lakini muhimu sana katika mahusiano.

Kama positives zitakuwa nyingi kuliko negatives unavyomchukulia mwenzi wako basi mahusiano yatakuwa bora sana, haleluya Kubwa!
Na kama negatives zitakuwa nyingi kuliko positives katika hisia kwa mwenzi wako basi shughuli nzito inakuja mbele yenu!

Ukweli ni kwamba negatives moja huhitaji positive tano ili kufanya balance ya ndoa au mahusiano kuwa katika hali nzuri (feelings).
Hii ina maana ukimbomoa mwenzi wako mara moja basi inabidi umjenge mara tano zaidi ili ku- balance ule uharibifu umefanya mara moja.
Kila negative moja unahitaji positive tano ili emotions na feelings za mapenzi yenu kurudi kuwa katika hali ya kawaida.

Thursday, June 25, 2009


Great Sex
It’s not about frequency of sex; it’s about eroticism.
It’s not about technique; it’s about integrating your head, heart, and spirit with your genitals, it’s about your frame of mind and emotional connection with your spouse.

The who I am that I bring to our sexual interactions will determine the depth of our intimacy, passion and eroticism.

Wednesday, June 24, 2009

Anavuma hata usingizini!

Ni jambo la kawaida kwa wanandoa katikati ya usiku mmoja kumtaka mwenzake tendo la ndoa hata hivyo je, mwenzi wako huwa anakuwa ameamka kabisa au bado huwa usingizini na kuendelea kuwa mwili mmoja?

Wapo watu ambao huweza kuamka usiku na kutembea umbali mrefu na kufanya vitu tofauti na vya ajabu huku hawajielewi hawa kwa kingereza wanajulikana kama sleep walker.

Hata hivyo linapokuja suala la kufanya mapenzi wapo watu ambao husisimka kimapenzi wakiwa usingizini na kuanza kufanya mapenzi huku wakiwa hawajijui na hawana uwezo wa kuthibiti hicho kitendo.
Kitaalamu hali hii hujulikana kama sexsomia.
Wapo ambao wakiwa katika hali ya kawaida kufanya tendo la ndoa kwa mapozi lakini wakiwa katika hali hii ya usingizini huwa hawana utani na hufanya kwa umaridadi zaidi hadi wenzi wao huwashangaa hata hivyo asubuhi akiulizwa ili apewe appreciation yake kwa kufanya kazi nzuri huruka na kukataa kwamba si kweli na yeye alilala usingizi fofofo na anaonewa, kweli haya makubwa!

Hata hivyo wataalamu wengi wanahusanisha na watu wenye matatizo ya kutembea wakiwa usingizini.
Pia watu wenye hali ya sexsomia wamekuwa wakitumia kama defence mahakamani hasa wakipatikana na kosa la kubaka.
Kwa maelezo zaidi ya kesi hii soma hapa

Tuesday, June 23, 2009

Huweza kuvunjika!

Unaweza kuvunja uume:
Ingawa uume hauna mfupa unaweza kuvunjika; kitendo cha uume kuvunjika kwa kingereza huitwa (penile fracture) hii ni ajali ambayo hutokea mara chache sana wakati wa kufanya mapenzi na inapotokea huweza kutoa kamlio fulani huku uume ukigeuka rangi na kuwa mweusi au blue na maumivu makali ya kufa mtu.

Hii ajali huwapata wanaume vijana (miaka 30 kwenda chini) ambao uume kukisimama hunyoka sana na kuwa mgumu pia wanapofanya mapenzi huwa hawatulii ni kama vita.
Mwanaume anaposugua kwa nguvu kwenye uke (in and out) na kugusa pubic bone kwa mwanamke kama yupo rough au style ya mwanamke kuwa juu ya mwanaume na hasa mwanamke akiwa wild (nyege zilizokithiri) wakati wa sex basi ajali inaweza kutokea.

Uume huwa na maamuzi yake (Own mind)
Inawezekana (kama ni mwanaume) kuna wakati umegundua kwamba uume hufanya vitu tofauti na unavyotaka na umeku - let down baadhi ya siku.
Ni kweli unao uamuzi kidogo sana kuhusiana na uume kuliko viungo vingine vya mwili kama mkono au mguu hii ni kwa sababu uume hujibu taarifa kutoka kwenye ubongo kupitia mfumo wa fahamu (nervous system) ambao haupo chini ya ufahamu au uwezo wako, uume hutumia mfumo wa fahamu ambao ni automatic (automatic nervous system) hii ni pamoja mapigo ya moyo na Blood pressure.

Kusisimka kimapenzi (kusimamisha) mara nyingi si voluntary ni involuntary (kama hukusoma biology ya kidato cha pili au tatu utajijua) ndiyo maana uume husimama wakati umelala.
Pia uume huweza kusisima wakati wa kuinua vitu vizito au wakati wa kutoa haja kubwa.
Pia uume hukua au kuongezeka bila wewe kuamua na wakati mwingine husinyaa bila wewe kuamua.

Kiwango cha kusinyaa kwa uume hutofautiana kati ya mwanaume na mwanaume (Drogo Montague, MD, a urologist at the Cleveland Clinic anasema).
Uume ukiwa kwenye maji baridi au hewani huweza kusinyaa bila wewe kuamua.
Pia kuwa na stress huwa na matokeo sawa kwenye uume kama maji baridi.
Unapojisikia vizuri uume huwa mkubwa kuliko ukiwa na stress hata kama umesinyaa.
Swali
Je, wanaume ambao hujikuta wanafanya vitu vya ajabu kwenye daladala na kushikwa na mfadhaiko huwa wanaonewa kupelekwa polisi?
Jibu
Uzuri ni kwamba ukipelekwa kwenye chomba cha sheria au polisi wao hawajui kama uume wako upo involuntary au unatumia automatic nervous system so huna defence kwamba hukufanya makusudi kwani wao wanajua mmiliki wa mpini ndo amesababisha ambaye ni mwanaume, hivyo hujaonewa.
Anyway soma kitabu cha Warumi sura ya 8 yote.

Uume wako unaweza kuwa Grower au shower:
Kwa wanaume kuna tofauti kubwa sana kwa uume unapokuwa umesimama au umesinyaa wapo ambao uume ukisimama huwa hauongezeki kiwango kikubwa (grower) na wanaume ambao uume ukisimama huongezeka kidogo sana (showers)
Hata hivyo jambo la msingi ni kwamba kwa mwanaume huwezi ku-judge kimpini chake wakati hajasimamisha kwani anaweza kufanya surprise ukashangaa.

Asilimia kubwa ya wanaume duniani hawajatahiriwa.
Ripoti ya WHO pamoja na UNAIDS inasema ni asilimia 30 tu ya wanaume wenye miaka 15 kwenda juu ndiyo wametahiriwa duniani.
Pia kutahiriwa kunategemea sana dini ya mtu.
Suala la wanaume kutahiriwa limekuwa gumzo duniani hata hivyo WHO na UNAIDS wanapendekeza kwamba ni muhimu kwa wanaume kutahiriwa ili kupunguza maambukizi ya UKIMWI.

Monday, June 22, 2009

Ni heri!

Ni heri wanandoa ambao wamegundua changamoto zinazoridhisha kutoka kwa mwenzake kwa maana kila mmoja atakuwa na uhakika na mwenzake bila kuwa na hofu au mashaka.

Heri wanandoa ambao wanaweza kushirikisha huzuni za ndani kutoka kwa mwenzake kwa maana hakuna atakaye jisikia mpweke wakati wa shida, matatizo au janga na ugumu wa aina yoyote katika maisha ya ndoa.

Heri wanandoa ambao kila mmoja ameonja utamu wa upendo wa mwenzake na kwamba uzuri wa upendo huendelea kudumu na kudumu na kila siku hujisikia kuwa mwenzake ni mpya.

Heri wanandoa ambao upendo ni imara kiasi cha kushirikisha wengine kwa maana kwao maisha hayawezi kuwa hayana maana tena.

Heri wanandoa ambao imani waliyonayo kati yao huleta matumaini na kutia moyo wengine kwa maana watu watawaongelea na kuwaambia
“ Ni wanandoa wenye furaha na waliobarikiwa”

Heri wenye ndoa ambao wanauhusiano na Mungu kila mmoja binafsi na wote kwa pamoja kwa maana maisha yao yatakuwa na utajiri wa furaha na hakuna ambalo halitawezekana kwao.

Marriage is possible because it combines the maximum of temptation with the maximum of opportunity.
By
George Bernard Shaw

Sunday, June 21, 2009

Be careful!

(Picha kwa hisani ya www.blisstree.com)Mtengenezaji keki mmoja aliambiwa aandae kike na kuyaweka maandiko ya Biblia kutoka 1Yohana 4: 18 kwa uzembe akaenda kutengeneza keki na kuweka maneno ya Biblia kutoka Yohana 4:18

Hivyo basi keki ilisomeka:
Kwa maana umeshakuwa na wanaume watano na mwanamume unayeishi naye sasa si mume wako!’’
Yohana 4: 18

Badala ya
Katika upendo hakuna hofu.
Lakini upendo ulio kamili huitupa nje hofu, kwa sababu hofu inahusika na adhabu.
Kila mwenye hofu hakukamilika katika upendo.
1Yohana 4: 18

Hapo si kutaka maneno na kuharibu sherehe za watu.

Wanaume tu!

(Picha kwa hisani ya www.ralphmag.org) Kuishi na mwanamke kunahitaji mwanaume kuwa makini na jinsi unavyoishi naye pamoja na unavyoongea naye na mawasiliano yote kwa ujumla.
Mawasiliano ni ufunguo kwa mwanamke kumfurahia mume wake.
Ukiongea na mke wako kama mwanamke mrembo naye atajiona ni mrembo ukiongea na mke wako kama vile ni jimama lililopitwa na wakati ni kweli anajiona amezeeka na kupitwa na wakati.

Jambo la kwanza msifie kwa jinsi anavyoonekana (physical appearance) yaani nguo alizovaa, nywele, viatu na hata perfume, anyway vitu hivi anavaa kwa ajili yake na wewe pia.
Kwa kumpa compliment basi atakuwa na confidence na kwamba umevutiwa na atajisikia vizuri. Suala la nguo ni kitu muhimu sana kwa mwanamke ndiyo maana hata wenyewe kwa wenyewe huweza kupeana sifa,
je wewe mwenye mali naamini si zaidi?
Unavyozidi kumsifia mwanamke kwa mwonekano wake, jinsi anavyofanya vizuri kitandani, jinsi alivyo, tabia njema na kila kitu anafanya naye atajitoa zaidi kuhakikisha anakupa huduma za uhakika.
Jambo la msingi hapa unaanda akili yake kwa ajili ya kuwa mwili mmoja baadae (naamini umenielewa)

Jambo la pili ni muhimu sana kumuuliza jinsi alivyoshinda hasa ukikutana naye jioni baada ya kazi.
Hata hivyo unatakiwa kuwa makini sana na jibu la swali kwani kama alikuwa na siku mbaya anaweza kukumwagia kopo zima la worms. Pia unatakiwa kuwa na tactics za kuhakikisha unabadilisha mambo mabaya anayokwambia na kuwa mazuri au kubadilisha somo.
Kumbuka lengo lako ni kutaka kutengeneza mazingira ya yeye kuwa na mood nzuri kwa ajili ya kuwa mwili mmoja.

Jambo la tatu hakikisha anajifahamu jinsi unavyojisikia kuhusu yeye na pia ni jinsi gani unajisikia vizuri kufanya mapenzi, tendo la ndoa au kuwa mwili mmoja na yeye.
Kama umezoea kuwa na utaratibu unaojirudiarudia (routine) unatakiwa kubadilisha. Ikiwezekana kuanzia sasa kila touch mwilini mwake kuanzia mwanzo hadi mwisho hakikisha unamwambia unavyojiskia raha. Hakikisha amejifunza na anafahamu unavyojisikia unapombusu, mkumbatia, mpenda, mshika, mnusa, muonja nk zaidi mhakikishie jinsi unavyojisikia akikupa mahaba.

Jambo la nne hakikisha unamsifia mbele za watu au mbele za rafiki zako na zaidi sana ukiwa chumbani hakikisha unamuandaa hadi yeye analilia wewe kumuingia ili kuwa mwili mmoja hiyo ina maana kwamba utakuwa umemuandaa vya kutosha, tumia mwendo wa kobe na si cheater.

Jambo la tano, hujawahi ambiwa na mke wako kwamba “ hujawahi nipeleka hata Bagamoyo tu: hii ina maana kwamba anataka siku moja upange muwe na outing ya uhakika wewe na yeye tu, maana yake anataka romance. Hivyo fanya kweli maisha ni sasa!

Hii ilikuwa kwa ajili ya wanaume tu, nashangaa wewe ni mwanamke na umesoma hadi mwisho, ok haina shida nenda kamwambie mumeo basi!

Friday, June 19, 2009

Kimara stop over- Dar es Salaam Tanzania "Relationships, marriages are ruined where one person continues to learn, develop and grow and the other person stands still. "
Catherine Pulsifer,

Si kweli!

Hapa hakuna kitu kinaitwa "kufanya makosa" Kuna msemo wa kingereza kwamba “someone is better than “No one’” ni uwongo kwani “No One” is better than a relationship that lack respect

Wapo watu ambao (hasa wanawake wale ambao wanaona muda unaenda bila kuwa na mchumba au mpenzi wa kuwa naye katika maisha) huamua kushikana na bora mwanaume kwa kudhania kwamba ni heri kuwa na huyo mmoja kuliko kutakuwa naye kabisa.

Subiri kidogo nikwambie!
Kujiingiza kwa wanaume ambaye moyo wako hauko radhi eti kwa sababu unataka na wewe uonekana una mpenzi au una mchumba au una mume au una boyfriend ni kuumiza hisia zako.
Hata kama unaamini utafanikisha matakwa yako bila kuunganishwa emotionally, intellectually au affectionally utaishia kuumizwa.

Wengi wanajuta kwa sababu ya kuamini kwamba "someone is better than no one, hata hivyo waliokiri kwamba "no one is better than a relationship that lack respect" wanapeta.
Tafakari kwa makini!

Pia kujua ni yeye soma hapa

Thursday, June 18, 2009

Ana akili za kitoto!

Kwa kuchangamkiana hivi unaweza dhania umepata mchumba,
hata hivyo fikiria mbali zaidi ukitaka uishi naye hadi kifo...
(picha imepigwa na Lazarus Mbilinyi)
Mke wangu alikuwa mzuri, mrembo, mchekeshaji, anayependeza na kuvutia kila wakati katika mazungumzo na vitendo.
Hivi karibuni amekuwa mzembe na naona anakuwa na akili ya kitoto na jinsi tunavyoendelea na maisha naona habadiliki na hii inanipa shida sana pia nimegundua kwamba IQ level yake ndogo sana.

Je, nifanyeje?

Kwanza ulimuoa kwa sababu alikuwa mzuri, mrembo, mchekeshaji, anayependeza na kuvutia kwa maneno na matendo hivyo leo ndo unaona hafai kwa sababu ana akili ya kitoto ambayo wakati huo hukuiona?

Hata hivyo IQ si kipimo kizuri cha maisha ya ndoa kwani wapo ma-genius kibao ambao pamoja na uwezo walionao kwenye ku-solve paper bado likija suala la ndoa ni zero.
IQ haina nguvu sana Linapokuja suala la kutumia common sense kwenye maisha ya kijamii.
Kama unaona hakui na anaendelea kuwa na tabia za kitoto hutakiwa kulalamika kwani huyo ndiye uliyemuoa kwa mbwembwe na uhakika na si wewe tu wapo wengi tu ambao baada ya kipindi Fulani hujikuta wanakutana na mauzauza kwa wenzi wao.

Naamini hakuwahi kukudanganya ila wewe ulimpenda kwa vitu vya nje ambavyo ni vya muda hukuangalia mambo ya msingi na ya kudumu ulimpenda kwa sababu ya uzuri wa muda.
Anyway hiyo ni hatua mojawapo ya ndoa hivyo mpende zaidi

Kwa maelezo zaidi bonyeza hapa

Wednesday, June 17, 2009

Mamia Wawania Kumuoa Milionea Anayetafuta Mume Kwenye Internet

Takribani wanaume 400 wa Korea Kusini wanapigana vikumbo kujaribu bahati yao ya kumuoa mwanamke milionea wa nchini humo ambaye ametangaza kutafuta mume kwenye internet.
Je, kwa wanaume kufanyiwa interview baada ya shortlist itamsaidia huyu mama milionea kupata mume sahihi?

Kwa habari zaidi soma hapa
Source: Nifahamishe

Utafanyeje!

Unamka asubuhi unakuta mwenzi wako kamwagilia mashuka kwa mikojo utafanyeje?Fikiria umekuwa na ndoto za kupata mwenzi na umefanikiwa na ile kuanza kuishi pamoja katika ndoa unakuja kugundua kwamba mwenzako ni kikojozi.
Utafanyeje?

Ukweli inabidi umkubali na zaidi umpende kwa kiwango cha juu kuliko wakati wowote na kumpa uhakika kwamba wewe ndiye mtu sahihi ambaye unaweza kumchukulia na kuishi naye katika huo udhaifu alionao kwani hata yeye hafanyi kwa kutaka au kupenda au makusudi imekuwa hivyo.

Je, kikojozi ni nani?
Kikojozi ni mtu ambaye akiwa amelala huweza kutoa mkojo bila yeye kujua inaweza kuwa usiku au mchana pia anaweza kuwa mtoto au mtu mzima, lakini hapa tunazungumzia mtu mzima au mwenzi wako.
Kitu cha msingi ni kwamba hakuna anayependa kuwa kikojozi kwani hiki kitendo hufanyika bila hiari au kupenda (involuntary).

Mara nyingi ukitamka neno kikojozi wengi huhusisha watoto hata hivyo wapo watu wazima (kwenye ndoa pia) ambao ni vikojozi.
Pia ifahamike kwamba kuwa kikojozi si tatizo serious la kimatibabu bali huwa ngumu kuishi kama kikojozi wewe mwenyewe na pia yule au wale unaishi nao.

Je, kuwa kikojozi husababishwa na nini?
Kuna evidence kwamba tabia ya kuwa kikojozi unaweza kurithi kutoka kwa wazazi mojawapo, kama una wazazi ambao mmoja alikuwa au ni kikojozi basi una asilimia 77 za kuwa kikojozi.
Pia vikojozi wengi wanaonekana wana kiwango kidogo cha homoni ya ADH (antidiuretic) ambayo husaidia figo kuzalisha kiasi kidogo sana cha mkojo usiku na hupelekea mtu kulala usingizi bila kusumbuliwa na mkojo.
Pia imajulikana kwamba vikojozi wengi ni wanaume
(Huu utafiti una walakini maana hautoi sababu ni zipi hata hivyo uzoefu unaonesha kwamba watoto wa kiume huchelewa sana kuacha kukojoa vitandani ukilinganisha na wenzao wa kike)

Kuwa na kibofu kidogo kiutendaji ni sababu mojawapo ya mtu mzima kuwa kikojozi. Kabla taarifa haijafika kwenye ubongo kibofu kinakuwa kimeshafanya vitu vyake.
Misuli ya kibofu hushndiwa kushika mkojo kabla ya kuamriwa na ubongo.

Pia kuutwika (pombe) huweza kusababisha kalowanisha mashuka kwani mipombe husaidia kuzalisha kiwango kikubwa cha mkojo pia kupunguza utendaji wa misuli ya kibofu.
Pia kisukari, maambukizi kwenye kibofu, matatizo ya maumbile ya kibofu, cancer ya kibofu nk huweza kusababisha mtu mzima kuwa kikojozi.

Jinsi ya kuthibiti kuwa kikojozi
Kupunguza kiwango cha vimiminika hasa baada ya mchana na usiku kabla ya kwenda kulala.
Hii haina maana kwamba usinywe maji au juisi kwani kunywa maji ni muhimu sana kwa afya, jambo la msingi ni timing ya wakati gani unywe na wakati gani usinywe.

Mazoezi ya kibofu kwa kunywa kiwango kikubwa cha vimiminika na kupunguza baada ya masaa 2 – 3.
Kutumia alarm kuamshwa hizi ni pamoja na zile zinazofungwa kwenye nguo ya ndani na ikianza kulowa tu lazima utaamka maana itakutetemesha na kukupigia kelele.
Kuamshana na yule unalala naye au ishi naye.
Na zaidi kutumia cover kitandani ambalo halilowanishi godoro.
Na mwisho muombee kwani kwa Mungu hakuna lisilowezekana

Tuesday, June 16, 2009

Wengine huwaangamiza..................

Ndoa huweza kuwa ndicho kitu chenye furaha ya ajabu au kuwa kitu kinacholeta huzuni.
Mungu aliweka ndoa ili kumuunganisha mwanaume na mwanamke ili kila mmoja kati yao ampe mwenzake kila hana hata hivyo hizo tofauti zilizopo zinaweza kuwa sababu kubwa ya hawa wawili kuwa vipande badala ya kitu kimoja.
Kumpenda na kuhisi na mwenzi wako ni kazi ya kujitolea kila siku na zaidi kufanya mema kwa ajili ya mwenzi wako.

Matatizo au migogoro au kutofautiana katika ndoa ni kitu cha kawaida na huweza kuleta matokea mazuri kwani wanandoa wanaotatua matatizo vizuri hujikuta wanafahamiana na matokeo hujuana na hujenga ndoa imara.

Ukweli kama kuna ndoa ambayo wanadai hawana hata tofauti au kupishana kwa njia yoyote basi mmoja ya wanandoa amekufa ni mfu au wameamua kula jiwe tofauti zilizopo huku moyoni kila mmoja akiumia kwa jina la amani.

Kwa migogoro katika ndoa wengine ni faida na wengine huwaangamiza

Mmoja anakuwa ametoka katika familia ambayo wakati wa migogoro na zogo wazazi wake walikuwa wanaishughulikia vibaya kama si kuikwepa au kuiacha.
Hivyo hata baada ya kuishi na mke au mume huamini njia waliyotumia wazazi wake ni sahihi. Unapoamua kuoa au kuolewa unatengeneza ndoa mpya duniani ambayo inahitaji njia sahihi ili kutatua matatizo na migogoro.

Inawezakana mmoja au wote wanaamini kukitokea mgogoro wowote wa ndoa ni kitu kibaya, wanaamini wakijaribu kutatua hawataweza.
Migogoro hutokea kwa sababu ya toafuti za kimawazo na kuijaribu kuitatua kwa upendo na hekima kila mmoja akijaribu kuwa sehemu ya suluhisho hujenga ndoa

Wanaamini amani ni pamoja na kutunza matatizo bila kuyaongelea au kutatua. Wanaogopa kuzungumzia matatizo na tofauti zilizopo kwani wanaweza kuwasha moto wasioweza kuuzima.
Hakuna kitu kibaya kama kutunza jambo moyoni ni sawa na magari mawili ambayo yanaelekea kwenye ahead on collision siku ikifika enough is enough hapatatosha.

Wanafahamiana juu juu tu na hivyo kuyajadili matatizo yanayojitokeza ni kuingilia business ambazo ni kuingilia others stuff.
Ukiingia kwenye ndoa kila kitu ni deep hakuna cha others stuff kwani kujuana ni pamoja na udhaifu na uimara na kwa njia hii hujenga intimacy.

Hawajiamini (insecure) hivyo mgogoro ukijitokeza wanaongea sana ili kujilinda badala ya kusikiliza na kujua watatue vipi.
Tatizo lolote au mgogoro wowote ukijitokeza ni muhimu kila mmoja kutulia na kusikiliza kwa makini kabla ya kuanza kuongea.
Wapo wanaume (si wote) mke hata kama hajamaliza kuongea yeye hudakia na kusema “najua unataka kusema kitu gani” Mke hujiona hajasikilizwa na mgogoro huweza kupanda kutoka kichuguu na kuwa mlima kilimanjaro.

Kila mmoja analenga kushinda au kwamba yeye ni sahihi kuliko mwenzake matokeo yake wanashindwa kutatua na wanaongeza tatizo kuwa kubwa zaidi.
Kumbuka hakuna mtu ambaye yupo sahihi kila siku au siku zote; ni muhimu kutambua kwamba kuna wakati tunakosea na tukubali tumekosa na tuombe msamaha.

Ukitaka kujifunza zaidi kuhusu kutatua matatizo katika ndoa soma hapa

Monday, June 15, 2009

Ogopa na epuka!

Siyo mkataba ni Agano!
(Picha hisani ya lateralaction.com) Uwongo
Ndoa ni mkataba (contract) na kwa kuwa ni mkataba basi unaweza kuvunjwa.
Ukweli:
Ndoa ni agano (covenant) lililowekwa na Mungu.
Ilikuwa ni mpango wa Mungu hata kabla ya binadamu kuweka mikataba ya kisheria kuhusu ndoa. Mungu ana define ndoa ni agano na agano halijajikita katka msingi ya kupokea zaidi ya unavyotoka (quid pro quo)

Uwongo:
Unaoa au kuolewa ni yeye tu hakuna uhusiano na familia yake
Ukweli:
unapooa au kuolewa si mwenzi tu bali ni pamoja na package ya familia yale.

Uwongo:
Naweza kumbadilisha mwenzi wangu:
Ukweli:
Huwezi kumbadilisha, unachoweza ni kumuathiri na tabia zako.
Kama unaamini utaweza kumbadilisha mwenzi wako unanidanganya na zaidi utakuja kukatishwa tamaa kwa hali ya juu sana.

Uwongo:
Tupo tofauti sana ndoa haiwezi kufika popote
Ukweli:
Tofauti zinazokuwepo kati ya mke na mume haziwezi kuiua ndoa bali jinsi tofauti zinavyoshughulikiwa ndicho kitu kinachoweza kuleta maafa.
Hakuna familia mbili ambazo hufanana kila kitu na hakuna watu wawili wanaweza kwenda sawa kwa kila kitu hivyo lazima kutakuwa na tofauti kati ya mke na mume.
Kumbuka ukikutanisha vitu viwili katika mwendo (moving) lazima msuguano utatokea na mke na mume ni watu na watu ni moving object hivyo tofauti na kusuguana lazima.

Uwongo:
Nimepoteza zile hisia za kumpenda tena na zimepota kabisa, Haitawezekana kumpenda tena.
Ukweli:
Hisia za kumpenda huweza kurejeshwa.
Ukielekeza katika positive kuliko negative unaweza kurejesha mapenzi kama mwanzo.
Kuwa na kiwango kikubwa cha negative kwa mwenzi wako hupelekea kujiweka mbali (emotional distance) na kupoteza upendo ingawa siri ni kuendelea kuangalia upande wa positive.

Uwongo:
Siwezi kubadilika hivyo nichukue kama nilivyo au niache.
Ukweli:
Unaweza kubadilika ingawa unahitaji hamu ya kutaka kubadilika, utiifu katika kutaka kubadilika na uwezo wa kutaka kubadilika.
Kwako binafsi ni vigumu kubadilika ila kwa uwezo wa Mungu Inawezekana kubadilika

Uwongo:
Mwenzangu amenisaliti kwa kutoka nje ya ndoa hivyo jibu ni talaka
Ukweli:
kutoka nje ya ndoa huumiza na huangamiza lakini si zaidi ya kushindwa kufanya marekebisho na upatanisho.
Ni jambo la msingi kujua sababu ya affair ilikuwa ni nini, then kwa msaada wa Mungu kusameheana, kutubu na kujitolea kuacha na kubadilika.
Kumbuka katika Biblia hakuna sehemu inayoruhusu talaka bali kusameheana na upatanisho.
Hii haina maana kwamba unaruhusiwa kuwa na affair kwa sababu kuna kusamehewa na kupatanishwa.

Uwongo:
Ndoa imefika mahali ambapo hatuwezi kuirejesha tena:
Ukweli:
Bado hamjachelewa, kwa Mungu hakuna lisilowezekana.
Je, hata ndoa ambayo imekufa inaweza kufufuliwa? Ni kweli Inawezekana kwani Mungu wetu ni Mungu wa muujiza.
Kama Mungu hawezi kufanya kile ametuahidi atakuwa Mungu gani? Mungu anaweza kubadilisha mioyo na kutoa njia na mwelekeo mpya kabisa katika ndoa na mahusiano.

Sunday, June 14, 2009

It takes step of faith to believe that God has good plan for us especially when things are not happening.

"For I know the plans I have for you," declares the LORD, "plans to prosper you and not to harm you, plans to give you hope and a future."
Jeremiah 29:11

Saturday, June 13, 2009

Kuwa na Malengo

Mwaka 1954 aliamini anaweza, akashangaza ulimwengu!Utangulizi
Kuwa na malengo ni namna mtu unatumia muda; hii ni pamoja na kutengeneza mpango maalumu jinsi ya kuyafikia hayo malengo.
Malengo ni ndoto ambazo zimewekewa deadline.

Jambo la msingi kabisa katika kufanikisha malengo ni kuwa na imani ndani yako (believing in yourself), Kujiamini mwenyewe hata pale wengine hawaamini kile unataka kufanya.

MFANO
Ilijulikana kwamba hapa duniani haitawezekana akatokea binadamu ambaye ataweza kukimbia mile 1 chini ya dakika 4.
Hii ilitokana na tafiti mbalimbali za wanasayansi (neurologist, doctors, trainers) hata wanariadha wenyewe.
Hawa wanasayansi walikiri kwamba hatatokea binadamu ambaye ataweza kuuvunja hii rekodi hasa kutokana na mpangilio ya bones mwilini, uwezo wa mapafu na vizuizi vya upepo unapokimbia.

Hivyo attitude ya wanariadha ilikuwa imewekwa kuamini kwamba huwezi kukimbia mile 1 chini ya dakika 4 na wakaamini, wakashindwa kukimbia chini ya dakika 4 all became failure.

Hata hivyo mwaka 1954 mwanariadha wa Uingereza Roger Bannister alivunja rekodi kwa kukimbia mile 1 chini ya dakika 4 baada ya kuweka malengo na kuyafanikisha na kuweka historia duniani kinyume na imani ya watu wengi (out of crowd).
Aliamini katika uwezo wake, akaweka malengo (revolutionary ideas) ili kuweka kufanikisha malengo yake.

"If you believe in yourself there is nothing you cant accomplish".

Kwa miaka 35 zaidi ya wanariadha 300 wameungana na Roger Bannister kuuvunja hii rekodi hata hivyo bila Roger Bannister kuuvunja rekodi attitude ya wanariadha ingekuwa palepale kwamba haiwezekani.

"If you are defeated in mind you are already lost the battle".

Hivyo basi panua uwezo wako wa kufikiria na Fikiria katika usahihi (positive) kwani kufikiria kinyume kunaweza kukukosesha kupokea Baraka za Mungu ambazo amekuwekea hapa duniani.

Think small, believe small, expect small then wonder why nothing big happens.

Tutaendelea……………………………………

No one wins the comparison game:
Your relationship must be evaluated based on your own needs,

not on the relative relationship success of those around you.

Don’t let yourself play this comparison game.

Friday, June 12, 2009

Wakufanana Naye!

Tafiti nyingi zinafanana na zinakubali kwamba ndoa nyingi imara ni zile ambazo mke na mume huwa na sifa nyingi zinazofanana.
Kundi la watafiti lilikusanya ndoa 35 (wanawake na wanaume 70) ambazo ziliwekwa katika makundi matatu kundi la kwanza lilikuwa la wale ambao ndoa zako zilikuwa za furaha, kundi la pili zile zilikuwa ni zile wanandoa walikuwa na wakati mgumu kuishi pamoja na kundi la tatu la wale walikuwa njiani kuachana.

Majibu yalikuwa ni kwamba wale walioishi kwa furaha walifanana sana katika mambo mengi (general activities), walikuwa marafiki na walifanana katika kujihusisha binafsi na mwenzake.
Wale ambao hawakuwa na furaha kuishi pamoja hawakufanana katika utendaji wa mambo yao kila siku, pia hawakufanana linapokuja suala la mwitikio wa hisia zao.
Wale waliokuwa wanataka kuachana kila mmoja alikuwa na sifa nyingi zisizofanana kabisa.

Kiwango cha furaha katika ndoa huweza kujieleza kutokana na kufanana kwa wanandoa katika sifa binafsi walizonazo.
Hii ina maana wanandoa wakifanana kiuchumi, tabia, mazingira, tamaduni, matumizi ya pesa, kiwango cha energy, uwezo wa kuongea na kusikiliza, kiimani, kihisia nk inakuwa rahisi kila mmoja kutegemea nini kutoka kwa mwenzake.

Hivyo ukitaka kuwa na ndoa imara ni muhimu kuwa na balance account ambayo kufanana ni zaidi ya tofauti kwa sbabu kila tofauti iliyopo inahitaji kupatanisha na kuweka kuikubali hata kwa maumivu.

BWANA Mungu akasema,
Si vema huyu mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.
Mwanzo 2:18

Walevi wa kazi!

Retirement HomeKama mwanamke una mume ambaye ni mlevi wa kazi jambo la msingi ni kukumbuka kwamba haina haja kuanza kuzozana au kukefyakefya kila usiku akichelewa kirudi, au kumkasirikia au kumnunia au kupigishana kelele.
Why?
Kwa sababu siku inayofuata anaweza akalala hukohuko ofisini kukwepa kelele zako.

Hakuna mwanaume anayeoa mke ili akirudi nyumbani apigiwe kelele, au anuniwe au akute mke amevimba mashavu kwa hasira, kwa nini asiende pangoni ?
Utafanyeje kama mume ni mlevi wa kazi?
Jambo la kwanza ni muhimu kufahamu kwanza sababu za yeye kuchelewa;
Je, anataka kupata promotion kazini?
Anafanya overtime?
Au amepata deal la kazi kwa muda au bosi amempa kazi ambayo ina deadline?
Je, mume wako ni boss kazini so inabidi ahakikishe kazi zimefanywa?
Je ni kazi ya muda au muda mrefu?

Je, mume anakwepa kuwa nyumbani labda kuna tatizo katika mahusiano?
Au kuna kubishana kuhusu kipato hivyo anajitahidi aweze kufikia pale wewe unataka?
Au yupo addicted na kazi tu?

Inawezekana anatumia muda mwingi kazini kwa sababu ni majukumu na ni kwa faida yako na familia kwa ujumla.
Hivyo inabidi uwe makini kujua sababu kwanza kuliko kuanza kupiga kelele.

Jambo la pili na la msingi ni kukaa pamoja kama mke na mume kwa upendo na kuzungumza kwa pamoja na kwa upendo suala la yeye kuchelewa kurudi na zaidi kwamba familia ni muhimu.

Jambo la tatu ni kuhakikisha unawasiliana naye na kuimarisha mawasiliano katika ndoa.
Kama ni wakati wa kuwa na mawasiliano naye basi ni wakati huu kwani anatakiwa kujua anahitajika nyumbani pamoja na kupenda kazi kote na kwamba familia pia ni muhimu.

Pia ukigundua ni mlevi wa kazi na kwamba anawaza na anategemea raha ya maisha miaka 47 ijayo kwenye retirement home basi hakikisha unamwandalia chakula chake (dinner /supper)mapema sana ili akirudi late usiku akikute (kimeganda) kesho atawahi zaidi.

Ikishindikana, kama kuna retirement home tafuta weekend moja nenda naye na mkifika huko tafuta wale wazee wa pale; kaa nao na wawape uzuri na furaha ya maisha uzeeni usisahau kuwauliza jinsi wanavyo-enjoy kuwa mwili mmoja angalau mara 4 au 3 kwa wiki na pia jinsi wanavyofurahia kucheza na watoto wao; anaweza kupata mawazo mapya.

Zaidi ya yote Muombee kwa Mungu!

Thursday, June 11, 2009

Ni mali ya mtoto au mume au mke?

Matiti hutoa chakula cha mtotoLinapokuja suala la matiti wanaume wengi (si wote) hunyang'anyana hati miliki ya matiti na mtoto anayenyonya hata hivyo wanawake nao kila mmoja ana mtazamo wake tofauti, hebu angalia maoni ya wanawake hawa wa Nigeria wanavyojibu swali la nani ni mmiliki halali wa matiti ya mwanamke.

Mrs. Arogundade
Mume wangu ndiye anamiliki matiti yangu kwa sababu mume alikuja kabla ya mtoto.
Baada ya mtoto kunyonya kwa muda inakuwa zamu ya mume wangu kwani tunalala kitanda kimoja.
Mtoto wangu ana access ya matiti yangu kwa muda tu wakati mume wangu ni mali yake maisha yetu yote.
Matiti yangu ni kitu ambacho mume wangu huchezea na pia ni mto wake wa kulalia.
Ukweli ni kwamba mume wangu hujisikia wivu kama mtoto wangu ataendelea kunyonya zaidi ya muda aliopewa.
Linapokuja suala la matiti yangu mume wangu huwa anachanganyikiwa, hawezi kufanya ile kitu (sex) bila matiti yangu.
Mrs. Omisade
Mume wangu ni mmiliki ya matiti yangu.
Mume wangu akiyakamata tu matiti yangu basi huwa tunakuwa na mahaba ya nguvu katika uso wa dunia.
Mume wangu hawezi kuanza chochote bila kugusa matiti na pia hunisisimua sana kwa ajili ya kufanya mapenzi pia mume wangu huniambia huwa anamuazima mtoto wetu matiti na akimaliza anatakiwa kurudishiwa mali zake kutoka kwa mtoto.
Mrs. Alhaja Sadiku
Kitu kimoja ninachopenda kuhusu mume wangu ni pale anapochezea matiti yangu kama vile machungwa, pia huwa namruhusu mtoto wangu kuchezea matiti kwa kadri anavyoweza.
Najua mume wangu alilipa mahari kitu inachompa access ya mwili wangu wote.
Matiti ni kwa ajili ya chakula cha mtoto wangu.
Mrs. Olagbaju
Ukweli mume wangu ndiye anamiliki matiti yangu.
Ila lazima akubaliane nami kwamba wakati tunayonyesha mtoto lazima aache kwa ajili ya mtoto wetu.
Wakati ninaponyonyesha naweza kumruhusu mume wangu kuyachezea kwa mikono na si kunyonya.
Mume wangu anamiliki matiti yangu permanently na pia anamiliki kila kitu nilichonacho pamoja na matiti.
Mrs. Agunbiade
Mtoto wangu ndiye anamiliki matiti yangu.
Mume wangu ana mtazamo tofauti kwani huwa hapendi kabisa kuyanyonya, wakati nanyonyesha hapende kabisa hata kula chakula changu yeye hapendi kabisa harufu ya maziwa kutoka kwenye matiti yangu.

Mrs. Amadi
Mume wangu hawezi kufanya bila matiti, kabla kitu chochote kutokea yaani kufanya mapenzi lazima achezee matiti yangu na bila matiti siwezi kusisimka.
Mume wangu husahau huzuni zote akianza kunyonya matit yangu.

Mrs. Ganiu
Mume wangu ndiye anayemiliki matiti yangu, mtoto wangu hunyonya kwa muda tu, then automatically matiti hurudi kwa mume wangu.

Mrs. Daniel
Mume wangu anamiliki matiti yangu kwa sababu alinioa kihalali.
Tunapotaka kuwa kwenye huduma ya pamoja ya usiku kila mara ni utukufu, huanza kwa mume wangu kunichezea matiti yangu na kuyakandakanda halafu tendo huanza.
Mrs. Omole
Mume wangu aliniambia kwamba nilipokutana naye kwa mara ya kwanza matiti ndiyo kitu kilimvutia sana yeye, hivyo ni mali yake, najua matiti yangu ni sehemu ambayo mume wangu ni dhaifu, siwezi kumnyima mali zake, hata kama mtoto wangu anayanyonya, mume wangu bado huyanyonya na kuyachezea.
Mrs. Ojo
Kabla ya mtoto kuzaliwa matiti yangu yalikuwa ni toy la mume wangu kuchezea.
Baada ya mtoto matiti ni kwa ajili ya mtoto, mume wangu anaishia kuchezea tu si kuyanyonya.
Mrs. Alao
Mume wangu anamiliki matiti yangu kwa sababu tulikuwa pamoja kabla ya mtoto kuzaliwa.
Moto anaweza kuazima matiti kwa muda tu, mume wangu anamiliki matiti yangu permanently na mtoto huwa yake kwa muda.
Mrs Salome
Mume wangu ni owner wa matiti yangu.
Hawezi kufanya mapenzi bila matiti yangu.
Mume wangu huniambia matiti yangu ni chakaazi (succulent ).
Matiti yangu humpeleka mbali sana mume wangu na husisimka hadi kufika juu sana hata kabla hatujaanza kitu chenyewe.
Mtoto wangu ipo siku atayacha na kwenda kuanza nyumba yake hivyo lazima nimridhishe mume wangu kwa matiti yangu.Mungu alinipa matiti ili kumridhisha mume wangu katia suala la tendo la ndoa.
Siwezi kunyonyesha mtoto miezi 7 bila kuyarudisha kwa mmiliki wake ambaye ni mume wangu mpenzi.
Je, wewe kama ni mwanamke matiti yako ni mali ya nani?
Mtoto au mume wako?
Source: Modupe Okanlawon & Omowunmi Owoyomi
Daily Sun News, Sunday, June 8 , 2008


The past is not the future!

The past would be a good indicator of the future.
The same is not true for the relationships.


Your relationships history is not your relationships future.
Your relationships future is not limited by your experiences of the past or by disappointment of the past.

You can’t change the weather but you can change the relationships pattern, you can learn from your experiences and avoid mistakes of the past.

Tuesday, June 9, 2009

Ni baba vivuli!

Wanapenda kazi hadi kutamani kulala kazini!Wapo watu ambao ni walevi wa kupindukia linapokuja suala la kazi (hasa sisi wanaume na si wote). Huamka mapema kabla watoto hawajaamka na huchelewa kurudi baadaya watoto na mke wameshalala. Kama ni chakula (dinner) basi kwenye kimepoa hadi kikawa kipolo na mke husubiri hadi anachoka na kuamua kulala.

Ukiwauliza wanasema wanafanya hivyo kwa sababu ya future kwa maana kwamba anafanya kazi kama punda ili baadae aishi kama mfalme.
Mke huwa kama mlinzi wa nyumba.
Watoto wanakuwa wageni na baba yao kwani hawajawahi kujua raha ya baba na kucheza naye na kumuuliza maswali mbalimbali.

Huyu baba usiku akirudi anakuta watoto wamelala fofofo; huku akijiamini na yale anafanya huwagusa watoto kwa mikono na kuwaambia

Najua mnafahamu kwamba baba yenu najitahidi kufanya kazi usiku na mchana ili muwe na future”

Anawabusu na kwenda zake kulala huku yupo hoi yupo hoi.
Akifika kitandani kwa mkewe anamwambia
“ Unajua najitahidi sana kuhakikisha tunalipa bills na pia nikistaafu kazi tunakuwa na maisha mazuri (retirement home)
Hapa kuwa mwili mmoja ni ngumu kwani mke huwa kihisia amejipiga password, haingiliki maana anawaza jinsi alivyomsubiri na jinsi chakula kimepoa bila mume kuwepo cha dinner.
Hii haina maana kwamba mke na mume hawatakiwi kuwa na mipango ya muda mrefu na muda mfupi au kutowekeza kwa ajili ya future bali itakuwa haina maana na ujinga uliokithiri na wa hali ya juu kupoteza familia kwa sababu ya mipango ya baadae, anyway hata hiyo mipango ni kwa ajili ya nani wakati umepoteza familia?

Hata kama umechelewa dinner wahi nyumbani uonane na watoto na mke kabla hawajalala si vizuri watoto kuishi maisha kwa ufahamu kwamba baba ni kama kivuli tu ambacho hutoa busu kila siku wakati wameshalala na kabla hawajaamka asubuhi.
Huku ni kujidanganya, Eti unafanya kazi hadi kusahau familia ili uwe na maisha wakati umestafu kazi?
Familia gani?
Mke gani?
Wakati atakuwa ameshajichokea na kujizeekea kwa ulevi wako wa kazi, ata-enjoy wakati hata kuwa mwili mmoja (sex) kashajizeekea?
Na watoto wameshakuwa na maisha yao, huku kujidanganya!
Ishi sasa na pia panga mipango ya uhakika ya baadae.

Mke amekubali kukuoa kwa sababu anakuhitaji sasa, anahitaji upendo wako sasa, anahitaji maisha sasa anahitaji kukufaidi sasa, anahitaji satisfaction sasa, anahitaji umefikishe kwenye kilele cha raha ya ndoa sasa.
Ni kweli future ni muhimu na ni muhimu sana kufikiria kuhusu future tena nakutia moyo kwa hilo ila too much is harmful.

Maisha ni sasa na maisha lazima yawe na balance hata kama upo busy namna gani watoto wanakuhitaji baba na mke anakuhitaji.

Wapo ambao huishi mbali na mke au mume kutokana na kazi wanazofanya hata hivyo siku akirudi nyumbani hapatikani akiulizwa vipi mbona huna muda na sisi familia yako, majibu yake
“Nina mipango na rafiki zangu
sasa nani muhimu rafiki zako au mke na watoto?
Anyway ukipoteza watoto na mke rafiki zako watachukua nafasi yao?

“Your Marriage or Relationship is so Important, Please take Good Care of Yourself and Be Kind to Your Partner and Try to Keep Your Sense of Humor”

Jambo la msingi ni kuwa na ratiba kamili hata kama upo busy weka ratiba ambayo itakuwezesha kuwa na familia angalau mara 3 au 4 katika siku 7 za wiki.
Watoto wakufahamu na mke aridhike ndipo mipango yako itakuwa ya maana sana na Mungu atakubariki kwa hilo.

Je, ukiwa na mume mlevi wa kazi ufanyeje?

Tutaendelea...............................


Ni wazuri sana!

Ni mara chache sana utakutana na mwanaume akitoa chozi la uhakika hivi!
(http://www.democracyfornewmexico.com/)Wanawake kweli ni viumbe wa thamani ambao wakati mwingine hushangaza; hata hivyo yote ni kwa utukufu wa Mungu aliyetuumba tuwe tofauti ili kukamilishana.

Machozi ni moja ya vitu ambavyo mwanamke huhusika moja kwa moja hata katika malezi wazazi wetu walikuwa wanatuonya watoto wa kiume tusilie tukikutana na jambo kubwa au gumu kwani walisema kulia ni mwanamke na si mwanaume.

Mwanaumke huweza kutoa machozi akifurahi, akihuzunika, akikutana na rafiki au ndugu ambaye walioachana muda mrefu, hata wakati mwingine hutoa machozi ili kupata kitu na wakati mwingine hutoa machozi kwa kupoteza kitu katika miliki yake yaani moyo, na kwenye misiba basi huko usiseme maana ukichanganya na mila inakuwa shughuli nzito.
Kwa maelezo zaidi ya machozi na mwanamke soma hapa

Pia machozi ni moja ya silaha mwanamke hutumia hasa kujilinda kwani anaweza kujieleza kwamba tafadhari “Usiniambie mapungufu yangu la sivyo nitaaza kutoa machozi sasa hivi
Hata hivyo kazi kubwa ya mwanaume ni kutofautisha machozi ya hisia, msongo wa mawazo na uchoyo, ni kweli mwanamke ni emotional creature ambaye mwanaume lazima uwe makini to handle with care.

Hata hivyo Watafiti wengi wanakubaliana kwamba mwanamke anayetoa machozi ni mzuri sana lipokuja suala la hisia katika maeneo yote ya maisha hii ina maana kwamba mwanamke mwenye kumwaga chozi mara kwa mara ni mtamu chumbani kwa sababu anaweza kujieleza katika lugha ya mapenzi (love making, act of marriage) Na mwanamke mwenye macho makavu maana yake ni mgumu kuji –express wakati wa kuwa mwili mmoja.

Wanawake wenye machozi ni mara chache sana kuwa baridi (frigid) wakati wa kuwa mwili mmoja kwani ukimwandaa ni rahisi kuwa connected kihisia.

Pia kujua machozi ni dawa soma hapa

Sunday, June 7, 2009

Wanatumia moyo, tunatumia kichwa

Hii ndiyo highway wanaume hutumia kupita na hisia zaoWanawake sex ni moyoni na wanaume sex ni kichwani!
Watu wengi huamini kwamba sex ni kama cement inayowaunganisha mwanaume na mwanamke kuendelea kudumu katika mahusiano.
Baadhi ya tafiti zinaonesha kwamba wakati wa sex wanawake huzalisha kiwango kikubwa sana cha oxytocin homoni inayosisimua hisia na kufanya watu kupendana (fall in love).
Hii husaidia wanawake kuwa na mtandano mzuri unaohusanisha mwili mzima wakati wa sex.

Wanaume huzalisha kiwango kidogo sana cha homoni za oxytocin na hii huwezesha wao kufanya sex bila kuwa connected kihisia.
Kwa mwanamke sex ni emotions kwanza, kuwa na mood nzuri, kupendwa kwanza au kupokea upendo, caring na mwanaume kwanza, Linapokuwa suala la hisia wanawake ni sawa na barabara yenye njia 8 (8 lanes) wakati wanaume ni mfano wa barabara iliyotota inayoenda msituni (forest access road).

Wanaume sex ni suala la mwili kwa mfano mwanaume na mwanamke wakiwa chumbani kitendo cha mwanamke kuvua ngua kwa ajili ya kujiandaa kulala mwanaume tayari anakuwa amesisimka wakati mwanamke anachojua ni kupanda kitandani kulala na si vinginevyo.
Hii ina maana mwanaume tayari yupo tayari kuwa mwili mmoja wakati mwenzake mwanamke yupo tayari kulala usingizi.
Kuwa tayari kuwa mwili mmoja mwanamke huhitaji kupikwa katika hisia zake hata kabla ya Kuingia chumbani.

Zaidi soma hapa

Saturday, June 6, 2009

That is my Personal Stuff!

Itakuwa kichekesho kama utaingia kwenye elevator na kuamua kubaki first floor miaka nenda rudi!Kuna wakati wake zetu hutuuliza maswali ambayo huwa sisi wanaume tunashindwa kuwapa jibu kamili (si wanaume wote).
Atakuuliza unajisikiaje kwa kila kitu, Niambie kuhusu hiki na kile iliramradi swali na huwa tunaogopa sana kujibu kwani kuna wakati hatujui majibu na kuna wakati tunahisi wanauliza maswali ambayo ni ya ndani mno kiasi kwamba ni kuingilia personal stuff.

Ukweli ni kwamba ni kwa sababu hatujaweza kuwapa habari zetu zote kwa undani na kuwapa siri zetu za ndani kiasi cha wao Kujiona ni wenyeji katika maisha yetu, Kujiona si wageni tena, kutujua kwa undani na siri zetu za ndani yaani intimacy.

Intimacy
kwa mke na mume ni kujuana in deep, ni sharing ya mambo ya ndani, siri za ndani, innermost qualities za ndani ambazo ni ninyi wawili tu ndiyo mnapeana.
Intimacy si kufanya mapenzi au romance bali ni kupeana habari (core information) za ndani, mawazo ya ndani, hisia za ndani, ndoto za ndani, huzuni na furaha.
Kukiwa na intimacy basi tendo la ndoa huwa linaridhisha, mapenzi huwa matamu, romance huwa huleta raha.

Intimacy ni kumvumbua partner katika habari zake maalumu za ndani na kwamba ninyi wawili kila mmoja ni mali ya mwenzake.
Intimacy ni kutumia muda pamoja kujuana katika hali ya ndani kihisia kiasi cha kutengeneza bonding imara, huwezesha watu kuwa mwili mmoja na kuhitajiana, kuwa fused together, kuwa merged, welded together.

Intimacy ni hitaji muhimu la mwanamke katika mahusiano ili afungue moyo wake na kuwa tayari kuwa na mumewe kuridhishana kimwili.

Bila intimacy ni sawa na ndoa kuwa kwenye elevator na katika kusubiri kwenda floor ya 10 mnabaki floor ya kwanza na matokeo ni kuishia hapo miaka nenda rudi.

Hivyo basi ni muhimu sana sisi wanaume kuwaruhusu wake zetu kujua hizi personal stuff ili awe mwenyewe na si mgeni kwako.

Kwa maelezo zaidi unaweza kusoma hapa

Friday, June 5, 2009

Ripe fruits falls by itself, but does not fall in your mouth,

Haiba

Kuna mwingine ukimwangalia tu unajua kazi yako ni kumsikiliza tu!
(Picha kwa hisani ya DM)Haiba ni muunganiko wa tabia ambayo mtu anakuwa nayo kumtofautisha na mwingine na jinsi anavyojihusanisha na mazingira bonyeza hapa kuna maelezo ya ziada kuhusu maana ya haiba kama kaka Bwaya alivyoelezea.

Waajiri wengi huchunguza haiba ya mtu wakati wa usaili ili kupata mtu anayefaa kazi fulani, kwani haiba ya mtu wa kitengo cha Hesabu (ambaye hutakiwa kufuata sheria na kanuni) ni tofauti na mtu wa kitengo cha mapokezi ambaye hutakiwa kuwa social.

Pia katika ndoa suala la haiba huwa muhimu sana kwani wanapooana watu ambao haiba zao hufanana au kutofanana wakati mwingine huleta shughuli nzito katika ndoa.
Wataalamu wengi wanakubaliana kwamba kuna aina kubwa nne za haiba nazo ni kama ifuatavyo:-

Dominant:
Hii ni aina ya haiba ambayo mtu huwa na sifa ya kutoa maamuzi haraka sana.
Huwa hana mashaka sana na kitu chochote, anajiamini na maamuzi yake.
Pia watu wa kundi hili huchoshwa sana na kazi zinazojirudiarudia (routine tasks)
Huwa hawapendi kabisa kufuata details za vitu.
Mfano:
Kama amenunua Baiskeli ya mtoto ambayo haijaunganishwa yupo tayari kutumia masaa 3 akijijaribu kufanya kuunganisha hata kama inamshinda kuliko kutumia dakika 10 kusoma Instructions manual yake.

Influencer:
Ni watu ambao wapo social, wanaopenda marafiki, wanaongea sana.
Hupenda kujishirikisha na watu wenye mafanikio.
Kuwagundua ni rahisi kwani hata ukienda maofisini mwao au majumbani mwao utakuta wametundika vyeti vyao vya mafanikio kama vile Degrees na Awards mbalimbali walizopata.
Ni watu wachangamfu sana na wanapenda sana kuwakarimu wengine na kupata kibali kutoka kwao.
Wakiwa kwenye kitengo cha sales hupenda sana kufanya hiyo kazi maana ndiyo eneo lao.
Wapo warm na friendly.
Hawa watu nyumbani kwao huwa na wageni kila mara.

Supporter:
Hawa ni watu ambao ni watiifu sana na hufanya kazi kwa juhudi yote.
Huwategemea sana wengine yaani hawawezi kuwa wenyewe.
Wengi hata kama analipwa mshahara mdogo bado ataendelea na kazi hadi atastaafu hapohapo miaka yote.
Hawana uwezo wa kufikiria mambo mapya na kujaribu kufanya, ni tegemezi na waoga sana.
Ukitaka kuwajua; wao wakiwa kazini hutumia muda kadogo sana kwa ajili ya mapumziko.
Si rahisi kukuta wanagombana kwa maneno na mtu
Wapo tayari kufanya kazi ambazo wengine hawapendi kufanya.

Kwa njia hii wameweza kuwa na accomplishments ambazo wengine hawana.
Hawa wakioana na mtu yeyote ndoa huwa nzuri kwani hawana mambo makubwa.
Ili kuwatambua ni kitendo chao cha kukataa kabisa kutoa maamuzi.
Kama ni mwanamke akiulizwa na mumewe kwenda outing na akaulizwa twende wapi, basi mwanamke wa hili kundi atajibu “Wewe amua tu haina tatizo

Complaint:
Hawa ni Perfectionist.
Utawatambua kwa sababu wao hufuata sheria, kanuni taratibu na kila kinachotakiwa.
Huwa wanasikitika sana na kukatishwa tamaa pale wakiona sheria haifuatwi au taratibu zilizowekwa zinapuuzwa.
Kwenye ndoa hata kitendo cha kuweka nguo chumbani kina taratibu zake ukiweka tofauti ni zogo.
Mfano:
Mtu wa aina aina hii kama amenunua baiskeli mpya ambayo haijaunganishwa kwa ajili ya mtoto wake basi kwanza atakaa chini na kuanza kuchambua kila sehemu ya ile baiskeli kuanzia ndogo hadi kubwa then ataanza kama kuna kitu hakipo basi duka lililomuuzia siku hiyo wanashida, pili ataanza kusoma ile Instructions manual na kama kuna herufi imekosewa atarekebisha.
Hawa kama unawaajiri kazi basi wanafaa kufanya kazi kitendo cha Hesabu (finance & Accounting)

KATIKA NDOA
Kama Dominant akioana na Dominant nani atakubali uamuzi wa mwenzake ikiwa wote wanataka kuwa waamuzi?
Na ikiwa Influencer akaoana na influencer mwenzake nani atamsikiliza mwenzake ikiwa wote wanataka kuongea tu bila kusikiliza?
Na je, Complaint akioana na Influencer itakuwaje kama influencer kawaida yupo tayari kubadili taratibu na sheria ili kuridhisha watu wake akubaliane nao?

Tunamshukuru Mungu kwamba Kwake Yote yanawezekana na wawili wakiishi pamoja huweza kuathiriana na kuweza kufanana zaidi, hata hivyo uwe makini wakati unachagua mchumba.

Thursday, June 4, 2009

The selection you make of a marriage partner may well have more to do with the quality of you marriage than everything you do after getting married.

Malalamiko mengine! kazi

Mlipooana tu sex ilikuwa hot, exciting na full speed! Na mlikuwa mnasemezana kwamba hata siku moja haitakuja kubadilika hata hivyo baada ya watoto kuzaliwa na majukumu kuongezeka hata bila tahadhari tayari kila mmoja analalamika kisirisiri. Na mbaya zaidi wengine hulalamika kwa ndani hawasemi, ukweli unahitaji kukaa chini na mwenzi wako na kujadiliana na kumalizi kwani “small things matters”

Malalamiko yafuatayo mara nyingi hutawala ndoa nyingi si zote:

Mke wangu haniambii nini anahitaji tukiwa kitandani.
Kama wewe ni mwanamke ukweli ni kwamba mume wako hawezi kusoma kile kipo akilini mwako, “men read news papers not minds” kama ulikuwa umeota kuhusu yeye au ulikuwa unatamani akufanyie kitu chochote wakati wa kuwa mwili mmoja, au unahisi akifanya kitu Fulani utajisikia kusisimka zaidi; mwambie na yeye ataipata point yako na si kula jiwe.

Hataki kunyoa!
Baada ya kuwa na watoto, baadhi ya wanawake husahau kabisa kiwembe kinauzwa wapi au kimewekwa wapi, inawezekana wewe unayesoma hapa ni mojawapo (walewale), wewe mwenyewe ni shahidi hukuwa na msitu mnene kama wa ikweta hapa kabla; ni kweli upo busy na mumeo anajua upo busy hata hivyo kujiweka safi ni tabia njema, mumeo analalamika kimya kimya! Looo!

Chumbani anavaa kama yupo ofisini!
Wakati wa honeymoon ulikuwa unavaa nguo za chumbani chumbani na ofisini ofisini, sasa mbona ukiwa chumbani unajifunika nguo gubigubi, ni kweli tangu uzae watoto umebadilika sana, umenenepa na mumeo anajua hata hivyo anahitaji kuufurahia mwili wako kwa wewe kuvaa zile nguo za chumbani ili akufaidi, unaficha mwili wa nini wakati ni mali ya mumeo.

Anang’ang’ania mlalo mmoja tu!
Anapenda missionary position tuu, kama mwanzo wa ndoa alikuwa anajirusha style zote basi inawezekana libido imeshuka na ni dalili kwamba hana hamu tena, jibu ni kuanza upya yaani umchumbie upya, ukifanya mchezo ataanza kupena kusoma vitabu kuliko sex!

Hataki kulianza!
Yaani kila siku ni mimi mwanaume kuanza hata kama mpo hivyo inatakiwa angalau siku moja na wewe uniambia unanihitaji.
Inawezekana mwanaume hajui mwanamke anahitaji kitu gani katika mapenzi, mwanamke akiwa na mood nzuri anaweza kulianza, hata hivyo unachofanya na mkeo nje ya chumbani huweza kutoa npicha ya kile mtafanya mkiwa chumbani.

Anaogopa watoto watatusikia!
Kila siku tukitaka kuwa mwili mmoja mke hulalamika kwamba hadi watoto walale kwani watatusikia, nikifungua radio ili kumeza sauti za tunapokuwa mwili mmoja bado analalamika kwamba watasikia.
Mwanaume lazima ujue kwamba “everything in women’s life is wonderfully connected” ni kweli huwa anawaza watoto watasikia au mlango hujafunga vizuri na matokeo anaweza asipate raha kamili, ni jukumu la mwanaume kuhakikisha usalama na privacy kabla ya kuanza kung’ang’ania kuwa mwili mmoja.

Tuesday, June 2, 2009

Makosa Mkubwa - Usifanye

Unapotafuta mwenzi wa maisha si suala la kubahatisha kama vile kuwa kwenye chumba chenye giza totoro na kuanza kutafuta sindano sakafuni bali ni suala la kuhakikisha kuna mwanga wa kutosha kupata kabla ya kuingia kutafuta.

Ukweli ni kwamba dalili za ndoa kushindwa huweza kujulikana mapema hata kabla ya ndoa kufungwa hasa kutokana na jinsi mwenzi alivyopatikana

Usikubali kuoana haraka mno.
Kuwa wachumba kwa muda mrefu huwezesha ndoa yenye afya.
Hapa unatafuta mtu wa kuishi nawe maisha yako yote ina maana utalala naye chumba kimoja maisha, utakula naye chakula maisha yote, utakuwa naye katika matatizo ya kifedha maisha yako yote, utauguzana naye miaka yako yote, mtakumbana na kukatishwa tamaa pamoja maisha yako yote.
Kuamua haraka haraka kuoana ni kujitengenezea risk kubwa.

Usikubali kuoana wakati bado umri mdogo sana:
Oa au olewa wakati kwanza wewe mwenyewe unajijua vizuri.
Pia hakikisha unamfahamu vizuri yule unaoana naye.
Kuanzia miaka 24 kwenda mbele ni umri mzuri kuoa au kuolewa.
Kuwa na umri mdogo maana yake bado hujatimiza mambo ya msingi kama pamoja na kukomaa kiakili kuishi kama mke na mume.
Tafiti zinaonesha ndoa stable ni zile ambazo wanandoa walioana wakiwa na miaka kuanzia 28.

Usikubali kitu chochote, mazingira yoyote au mtu yeyote kukusukuma kuoa au kuolewa.
Hakikisha umetuliza akili zako ndipo ingie katika biashara za kuoana.
Inawezekana unataka kuoana haraka kwa sababu uliachwa na mchumba mwingine, au unajisikia mpweke, au anahisi ukiolewa suala la uchumi litakuwa limepata jibu.

Usikubali kumridhisha mtu yeyote na chaguo lako:
Ni wewe utakaye pata faida au hasara, raha au machungu, furaha au huzuni, utamu au kuumizwa na si muda mfupi bali hadi kifo kitakapowatenganisha.
Haina haja kuwafurahisha wazazi au marafiki, au mchungaji, au mchumba mwenyewe kwamba unaoa au unaolewa eti wawe very happy.
Hii haina maana kwamba hutakiwa kuwasikiliza katika ushauri wao kuhusu wewe kuoa/kuolewa bali hii ni ndoa ni yako a lifetime opportunity.
Wala usikubali mtu awaye yote akuchagulie au kukufanyia uamuzi hata kama anauzoefu namna gani.
Wewe ndiye unatakiwa kuwa na uamuzi wa busara hata baada ya kupokea ushauri wa kila aina kutoka kwa watu tofauti

Usikubali kuoana na mtu hadi uweze kumfahamu katika njia tofauti.
Unatakiwa kumfahamu vizuri huyo mwenzi wako mtarajiwa, mfahamu tabia zake kwa kadri unavyoweza.
Kutembea mmeshikana mikono miaka 10 ijayo kunategemea sana jinsi unavyomfahamu vizuri kabla ya kuingia naye kwenye ndoa.

Usiolewe au kuoa huku una matarajio makubwa sana (unrealistic):
Ndoa kimbilio la faraja; inahitahiji kazi ya maana ili ikupe faraja.
Usiingie kwenye ndoa umeweka matarajio ya juu sana as if ni solution kwa shida zako zote kifedha, kihisia na kimaisha.
Hata kama sasa kuna mapenzi ya juu sana na una matumaini makubwa uwe makini kwani kila kitu kinaweza kuyeyuka kama barafu kwenye jua.
Kama unataka kuwa an ndoa imara jiandae kwa kazi iliyombele, kujitoa kutakuwa na maumivu, kuvumiliana, utakutana na changamoto ambazo inabidi ushindi na kuthibitishwa ili kuwa na true love kwa mwenzi wako.

Usikubali kuoana na mtu ambaye tabia yake unahisi hutaweza kuivumilia maisha yako yote.
Kama kuna tabia Fulani ambayo hupendezwi nayo kama wivu, uchoyo, uchafu, hasira, uvivu, kutowajibika, siyo mkweli au msumbufu; jiulize kama utaweza kutumia maisha yako yote na yeye huku ukipambana na hiyo tabia.
Hiyo tabia mbaya kwake haitaondoka, kama unaomba muujiza abadili tabia hakikisha unatokea kabla hujaoana naye lakini si kuoana naye huku unajua kuna tatizo kubwa eti ukioana naye muujiza utatokea.
Siku njema.....................................

Monday, June 1, 2009

Kipara au Msitu?


Binadamu akifikia miaka 9 – 14 mwili huanza kubadilika. Hiki ni kipindi ambacho msichana au mvulana hubadilika kutoka utoto na kuwa mtu mzima na hiki kitendo huitwa balehe na moja ya dalili ni kuota kwa nywele kwenye makwapa, sehemu za siri nk.

Leo tunazungumzia nywele za sehemu za siri yaani mavuzi.
Hizi nywele kawaida huwa na rangi tofauti na nywele za sehemu zingine kama kichwani, zingine huwa na rangi nzito zaidi, zingine huwa ngumu zaidi, zingine hunyoka (straight), zingine hujisokota (curl)

Linapokuja suala kunyoa hizi nywele ni preference ya mtu, pia jambo la kushangaza ni kwamba wanawake ndio huzungumziwa zaidi kuliko wanaume ni kama vile wanaume hawana hizi nywele.
Imefika wanaume hujiuliza wenyewe je, mwenzangu unapenda mke kuwa na forest au kuwa na jangwa la sahara?
Kila mwanaume au mwanamke ana jibu lake.

Baadhi ya wanawake hujisikia more attractive wakiwa wamenyoa wakati wengine hujisikia raha wakiwa na thick forest.

Hata hivyo kama lilivyo suala la matiti au makalio (matako) wapo wanaume hufurahia na kujisikia excited zaidi kwa mwenzi wake kuwa na msitu wa asili wa uhakika wakati huohuo wapo wanaume ambao kwa mwanamke kuwa na msitu mnene kwake huona ni mwanamke mchafu na asiyejitunza kama anshindwa kujinyoa sehemu muhimu kama hiyo basi yupo careless na hajipendi.

Kunyoa au kutokunyoa ni suala la hiari yako na mpenzi wako hakuna sababu ya Kujiona upo sahihi au hupo sahihi pia wapo ambao hunyoana na nyakati kama hizo kwao ni faragha na kujuana.

Kutokupata information zinazotakiwa wakati mwingine huweza kusababisha mtu kuchukua hatua ambazo zinaweza kushangaza hata mpenzi wake.

FAIDA ZA KUACHA KUNYOA
(Kuwa na msitu)
Hizi nywele huwa zonashika homoni za pheromones ambazo zikisambaa huweza kuvutia mtu wa jinsi tofauti (attraction)
Huweza kuzuia msuguano (friction) wakati wa tendo la ndoa, Kumbuka viungo vya uzazi vipo delicate sana.
Husaidia kufanya maeneo ya sehemu za siri kuwa jotojoto (warm)
Huzuia na Kulinda sehemu za siri kama hasa vitu vidogo kama mavumbi Kuingia sehemu nyeti hasa wanawake kama zilivyo nywele za kawaida zinavyolinda kichwa.
Huonesha kukua kwa mtu (sexual maturity)

FAIDA ZA KUNYOA
(Kipara)
Huboresha tendo la ndoa hasa kwa wale wanaopenda Kipara.
Huboresha usafi; hizi nywele hushika harufu (odor) na kuweza kupelekea kutoridhishana kimapenzi, au kama muhusika hajaoga vizuri anaweza kukufukuza kwa harufu.
Kujisikia vizuri, kujiamini na kujisikia safi.

KUNYOA AU KUTOKUNYOA KATIKA NDOA
Kuwa na maeneo ambayo yanatunzwa ni moja ya njia ambayo mke na mume huweza kujisikia vizuri kwa mwenzake.
Wengine hujisikia vizuri zaidi kwa kila mmoja kuwa kipara na kufanya degree of intimacy kuwa juu zaidi (ngozi kwa ngozi hunoga zaidi)
Wanandoa wengi hukubaliana kunyoa au kunyoana kuliko kuacha msitu, sababu kubwa zikiwa
Kunyoa huleta ukaribu (intimacy)
Kuwa kipara (mwanamke) ni zaidi ya kuwa uchi kwani unakuwa kama umeondoa kile kinafuka uke hivyo mume huweza kuona kwa macho na kwa kugusa uzuri na jinsi Mungu alivyokuumba.
Pia wanandoa ambao hunyoana kuanzia honeymoon huwafanya kuwa karibu zaidi kwa kujuana zaidi.
Kunyoa ni usafi.
Agano la kale ilikuwa ni ishara ya kujitakasa.
Kunyoa mwanamke huonesha amejitoa kwa mumewe.

(Hesabu 8:7)
Katika Agano la kale ishara mojawapo ya kujitakasa ilikuwa ni kunyoa nywele zote katika mwili.

JE, KUNA STYLE ZA KUNYOA?
Wengine wanaponyoa huweka style mbalimbali just for fun.
Wengine hupunguza (trimming) na si kunyoa Kipara kabisa.
Wengine hunyoa pembetatu ili wakivaa bikini nywele zisionekane.
Wengine hutengeneza mstatili ambao huitwa “Chaplin Moustache” kwa raha zao mke na mume.
Wengine hupaka rangi nyekundu na kuchora umbo la moyo kama zawadi kwa mwenzi wake.