"Marriage is our last, best chance to grow up."

Thursday, June 18, 2009

Ana akili za kitoto!

Kwa kuchangamkiana hivi unaweza dhania umepata mchumba,
hata hivyo fikiria mbali zaidi ukitaka uishi naye hadi kifo...
(picha imepigwa na Lazarus Mbilinyi)
Mke wangu alikuwa mzuri, mrembo, mchekeshaji, anayependeza na kuvutia kila wakati katika mazungumzo na vitendo.
Hivi karibuni amekuwa mzembe na naona anakuwa na akili ya kitoto na jinsi tunavyoendelea na maisha naona habadiliki na hii inanipa shida sana pia nimegundua kwamba IQ level yake ndogo sana.

Je, nifanyeje?

Kwanza ulimuoa kwa sababu alikuwa mzuri, mrembo, mchekeshaji, anayependeza na kuvutia kwa maneno na matendo hivyo leo ndo unaona hafai kwa sababu ana akili ya kitoto ambayo wakati huo hukuiona?

Hata hivyo IQ si kipimo kizuri cha maisha ya ndoa kwani wapo ma-genius kibao ambao pamoja na uwezo walionao kwenye ku-solve paper bado likija suala la ndoa ni zero.
IQ haina nguvu sana Linapokuja suala la kutumia common sense kwenye maisha ya kijamii.
Kama unaona hakui na anaendelea kuwa na tabia za kitoto hutakiwa kulalamika kwani huyo ndiye uliyemuoa kwa mbwembwe na uhakika na si wewe tu wapo wengi tu ambao baada ya kipindi Fulani hujikuta wanakutana na mauzauza kwa wenzi wao.

Naamini hakuwahi kukudanganya ila wewe ulimpenda kwa vitu vya nje ambavyo ni vya muda hukuangalia mambo ya msingi na ya kudumu ulimpenda kwa sababu ya uzuri wa muda.
Anyway hiyo ni hatua mojawapo ya ndoa hivyo mpende zaidi

Kwa maelezo zaidi bonyeza hapa

No comments: