"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, June 24, 2009

Anavuma hata usingizini!

Ni jambo la kawaida kwa wanandoa katikati ya usiku mmoja kumtaka mwenzake tendo la ndoa hata hivyo je, mwenzi wako huwa anakuwa ameamka kabisa au bado huwa usingizini na kuendelea kuwa mwili mmoja?

Wapo watu ambao huweza kuamka usiku na kutembea umbali mrefu na kufanya vitu tofauti na vya ajabu huku hawajielewi hawa kwa kingereza wanajulikana kama sleep walker.

Hata hivyo linapokuja suala la kufanya mapenzi wapo watu ambao husisimka kimapenzi wakiwa usingizini na kuanza kufanya mapenzi huku wakiwa hawajijui na hawana uwezo wa kuthibiti hicho kitendo.
Kitaalamu hali hii hujulikana kama sexsomia.
Wapo ambao wakiwa katika hali ya kawaida kufanya tendo la ndoa kwa mapozi lakini wakiwa katika hali hii ya usingizini huwa hawana utani na hufanya kwa umaridadi zaidi hadi wenzi wao huwashangaa hata hivyo asubuhi akiulizwa ili apewe appreciation yake kwa kufanya kazi nzuri huruka na kukataa kwamba si kweli na yeye alilala usingizi fofofo na anaonewa, kweli haya makubwa!

Hata hivyo wataalamu wengi wanahusanisha na watu wenye matatizo ya kutembea wakiwa usingizini.
Pia watu wenye hali ya sexsomia wamekuwa wakitumia kama defence mahakamani hasa wakipatikana na kosa la kubaka.
Kwa maelezo zaidi ya kesi hii soma hapa

No comments: