"Marriage is our last, best chance to grow up."

Friday, June 5, 2009

Haiba

Kuna mwingine ukimwangalia tu unajua kazi yako ni kumsikiliza tu!
(Picha kwa hisani ya DM)Haiba ni muunganiko wa tabia ambayo mtu anakuwa nayo kumtofautisha na mwingine na jinsi anavyojihusanisha na mazingira bonyeza hapa kuna maelezo ya ziada kuhusu maana ya haiba kama kaka Bwaya alivyoelezea.

Waajiri wengi huchunguza haiba ya mtu wakati wa usaili ili kupata mtu anayefaa kazi fulani, kwani haiba ya mtu wa kitengo cha Hesabu (ambaye hutakiwa kufuata sheria na kanuni) ni tofauti na mtu wa kitengo cha mapokezi ambaye hutakiwa kuwa social.

Pia katika ndoa suala la haiba huwa muhimu sana kwani wanapooana watu ambao haiba zao hufanana au kutofanana wakati mwingine huleta shughuli nzito katika ndoa.
Wataalamu wengi wanakubaliana kwamba kuna aina kubwa nne za haiba nazo ni kama ifuatavyo:-

Dominant:
Hii ni aina ya haiba ambayo mtu huwa na sifa ya kutoa maamuzi haraka sana.
Huwa hana mashaka sana na kitu chochote, anajiamini na maamuzi yake.
Pia watu wa kundi hili huchoshwa sana na kazi zinazojirudiarudia (routine tasks)
Huwa hawapendi kabisa kufuata details za vitu.
Mfano:
Kama amenunua Baiskeli ya mtoto ambayo haijaunganishwa yupo tayari kutumia masaa 3 akijijaribu kufanya kuunganisha hata kama inamshinda kuliko kutumia dakika 10 kusoma Instructions manual yake.

Influencer:
Ni watu ambao wapo social, wanaopenda marafiki, wanaongea sana.
Hupenda kujishirikisha na watu wenye mafanikio.
Kuwagundua ni rahisi kwani hata ukienda maofisini mwao au majumbani mwao utakuta wametundika vyeti vyao vya mafanikio kama vile Degrees na Awards mbalimbali walizopata.
Ni watu wachangamfu sana na wanapenda sana kuwakarimu wengine na kupata kibali kutoka kwao.
Wakiwa kwenye kitengo cha sales hupenda sana kufanya hiyo kazi maana ndiyo eneo lao.
Wapo warm na friendly.
Hawa watu nyumbani kwao huwa na wageni kila mara.

Supporter:
Hawa ni watu ambao ni watiifu sana na hufanya kazi kwa juhudi yote.
Huwategemea sana wengine yaani hawawezi kuwa wenyewe.
Wengi hata kama analipwa mshahara mdogo bado ataendelea na kazi hadi atastaafu hapohapo miaka yote.
Hawana uwezo wa kufikiria mambo mapya na kujaribu kufanya, ni tegemezi na waoga sana.
Ukitaka kuwajua; wao wakiwa kazini hutumia muda kadogo sana kwa ajili ya mapumziko.
Si rahisi kukuta wanagombana kwa maneno na mtu
Wapo tayari kufanya kazi ambazo wengine hawapendi kufanya.

Kwa njia hii wameweza kuwa na accomplishments ambazo wengine hawana.
Hawa wakioana na mtu yeyote ndoa huwa nzuri kwani hawana mambo makubwa.
Ili kuwatambua ni kitendo chao cha kukataa kabisa kutoa maamuzi.
Kama ni mwanamke akiulizwa na mumewe kwenda outing na akaulizwa twende wapi, basi mwanamke wa hili kundi atajibu “Wewe amua tu haina tatizo

Complaint:
Hawa ni Perfectionist.
Utawatambua kwa sababu wao hufuata sheria, kanuni taratibu na kila kinachotakiwa.
Huwa wanasikitika sana na kukatishwa tamaa pale wakiona sheria haifuatwi au taratibu zilizowekwa zinapuuzwa.
Kwenye ndoa hata kitendo cha kuweka nguo chumbani kina taratibu zake ukiweka tofauti ni zogo.
Mfano:
Mtu wa aina aina hii kama amenunua baiskeli mpya ambayo haijaunganishwa kwa ajili ya mtoto wake basi kwanza atakaa chini na kuanza kuchambua kila sehemu ya ile baiskeli kuanzia ndogo hadi kubwa then ataanza kama kuna kitu hakipo basi duka lililomuuzia siku hiyo wanashida, pili ataanza kusoma ile Instructions manual na kama kuna herufi imekosewa atarekebisha.
Hawa kama unawaajiri kazi basi wanafaa kufanya kazi kitendo cha Hesabu (finance & Accounting)

KATIKA NDOA
Kama Dominant akioana na Dominant nani atakubali uamuzi wa mwenzake ikiwa wote wanataka kuwa waamuzi?
Na ikiwa Influencer akaoana na influencer mwenzake nani atamsikiliza mwenzake ikiwa wote wanataka kuongea tu bila kusikiliza?
Na je, Complaint akioana na Influencer itakuwaje kama influencer kawaida yupo tayari kubadili taratibu na sheria ili kuridhisha watu wake akubaliane nao?

Tunamshukuru Mungu kwamba Kwake Yote yanawezekana na wawili wakiishi pamoja huweza kuathiriana na kuweza kufanana zaidi, hata hivyo uwe makini wakati unachagua mchumba.

No comments: