"Marriage is our last, best chance to grow up."

Tuesday, June 23, 2009

Huweza kuvunjika!

Unaweza kuvunja uume:
Ingawa uume hauna mfupa unaweza kuvunjika; kitendo cha uume kuvunjika kwa kingereza huitwa (penile fracture) hii ni ajali ambayo hutokea mara chache sana wakati wa kufanya mapenzi na inapotokea huweza kutoa kamlio fulani huku uume ukigeuka rangi na kuwa mweusi au blue na maumivu makali ya kufa mtu.

Hii ajali huwapata wanaume vijana (miaka 30 kwenda chini) ambao uume kukisimama hunyoka sana na kuwa mgumu pia wanapofanya mapenzi huwa hawatulii ni kama vita.
Mwanaume anaposugua kwa nguvu kwenye uke (in and out) na kugusa pubic bone kwa mwanamke kama yupo rough au style ya mwanamke kuwa juu ya mwanaume na hasa mwanamke akiwa wild (nyege zilizokithiri) wakati wa sex basi ajali inaweza kutokea.

Uume huwa na maamuzi yake (Own mind)
Inawezekana (kama ni mwanaume) kuna wakati umegundua kwamba uume hufanya vitu tofauti na unavyotaka na umeku - let down baadhi ya siku.
Ni kweli unao uamuzi kidogo sana kuhusiana na uume kuliko viungo vingine vya mwili kama mkono au mguu hii ni kwa sababu uume hujibu taarifa kutoka kwenye ubongo kupitia mfumo wa fahamu (nervous system) ambao haupo chini ya ufahamu au uwezo wako, uume hutumia mfumo wa fahamu ambao ni automatic (automatic nervous system) hii ni pamoja mapigo ya moyo na Blood pressure.

Kusisimka kimapenzi (kusimamisha) mara nyingi si voluntary ni involuntary (kama hukusoma biology ya kidato cha pili au tatu utajijua) ndiyo maana uume husimama wakati umelala.
Pia uume huweza kusisima wakati wa kuinua vitu vizito au wakati wa kutoa haja kubwa.
Pia uume hukua au kuongezeka bila wewe kuamua na wakati mwingine husinyaa bila wewe kuamua.

Kiwango cha kusinyaa kwa uume hutofautiana kati ya mwanaume na mwanaume (Drogo Montague, MD, a urologist at the Cleveland Clinic anasema).
Uume ukiwa kwenye maji baridi au hewani huweza kusinyaa bila wewe kuamua.
Pia kuwa na stress huwa na matokeo sawa kwenye uume kama maji baridi.
Unapojisikia vizuri uume huwa mkubwa kuliko ukiwa na stress hata kama umesinyaa.
Swali
Je, wanaume ambao hujikuta wanafanya vitu vya ajabu kwenye daladala na kushikwa na mfadhaiko huwa wanaonewa kupelekwa polisi?
Jibu
Uzuri ni kwamba ukipelekwa kwenye chomba cha sheria au polisi wao hawajui kama uume wako upo involuntary au unatumia automatic nervous system so huna defence kwamba hukufanya makusudi kwani wao wanajua mmiliki wa mpini ndo amesababisha ambaye ni mwanaume, hivyo hujaonewa.
Anyway soma kitabu cha Warumi sura ya 8 yote.

Uume wako unaweza kuwa Grower au shower:
Kwa wanaume kuna tofauti kubwa sana kwa uume unapokuwa umesimama au umesinyaa wapo ambao uume ukisimama huwa hauongezeki kiwango kikubwa (grower) na wanaume ambao uume ukisimama huongezeka kidogo sana (showers)
Hata hivyo jambo la msingi ni kwamba kwa mwanaume huwezi ku-judge kimpini chake wakati hajasimamisha kwani anaweza kufanya surprise ukashangaa.

Asilimia kubwa ya wanaume duniani hawajatahiriwa.
Ripoti ya WHO pamoja na UNAIDS inasema ni asilimia 30 tu ya wanaume wenye miaka 15 kwenda juu ndiyo wametahiriwa duniani.
Pia kutahiriwa kunategemea sana dini ya mtu.
Suala la wanaume kutahiriwa limekuwa gumzo duniani hata hivyo WHO na UNAIDS wanapendekeza kwamba ni muhimu kwa wanaume kutahiriwa ili kupunguza maambukizi ya UKIMWI.

No comments: