"Marriage is our last, best chance to grow up."

Saturday, June 13, 2009

Kuwa na Malengo

Mwaka 1954 aliamini anaweza, akashangaza ulimwengu!Utangulizi
Kuwa na malengo ni namna mtu unatumia muda; hii ni pamoja na kutengeneza mpango maalumu jinsi ya kuyafikia hayo malengo.
Malengo ni ndoto ambazo zimewekewa deadline.

Jambo la msingi kabisa katika kufanikisha malengo ni kuwa na imani ndani yako (believing in yourself), Kujiamini mwenyewe hata pale wengine hawaamini kile unataka kufanya.

MFANO
Ilijulikana kwamba hapa duniani haitawezekana akatokea binadamu ambaye ataweza kukimbia mile 1 chini ya dakika 4.
Hii ilitokana na tafiti mbalimbali za wanasayansi (neurologist, doctors, trainers) hata wanariadha wenyewe.
Hawa wanasayansi walikiri kwamba hatatokea binadamu ambaye ataweza kuuvunja hii rekodi hasa kutokana na mpangilio ya bones mwilini, uwezo wa mapafu na vizuizi vya upepo unapokimbia.

Hivyo attitude ya wanariadha ilikuwa imewekwa kuamini kwamba huwezi kukimbia mile 1 chini ya dakika 4 na wakaamini, wakashindwa kukimbia chini ya dakika 4 all became failure.

Hata hivyo mwaka 1954 mwanariadha wa Uingereza Roger Bannister alivunja rekodi kwa kukimbia mile 1 chini ya dakika 4 baada ya kuweka malengo na kuyafanikisha na kuweka historia duniani kinyume na imani ya watu wengi (out of crowd).
Aliamini katika uwezo wake, akaweka malengo (revolutionary ideas) ili kuweka kufanikisha malengo yake.

"If you believe in yourself there is nothing you cant accomplish".

Kwa miaka 35 zaidi ya wanariadha 300 wameungana na Roger Bannister kuuvunja hii rekodi hata hivyo bila Roger Bannister kuuvunja rekodi attitude ya wanariadha ingekuwa palepale kwamba haiwezekani.

"If you are defeated in mind you are already lost the battle".

Hivyo basi panua uwezo wako wa kufikiria na Fikiria katika usahihi (positive) kwani kufikiria kinyume kunaweza kukukosesha kupokea Baraka za Mungu ambazo amekuwekea hapa duniani.

Think small, believe small, expect small then wonder why nothing big happens.

Tutaendelea……………………………………

No comments: