"Marriage is our last, best chance to grow up."

Tuesday, June 2, 2009

Makosa Mkubwa - Usifanye

Unapotafuta mwenzi wa maisha si suala la kubahatisha kama vile kuwa kwenye chumba chenye giza totoro na kuanza kutafuta sindano sakafuni bali ni suala la kuhakikisha kuna mwanga wa kutosha kupata kabla ya kuingia kutafuta.

Ukweli ni kwamba dalili za ndoa kushindwa huweza kujulikana mapema hata kabla ya ndoa kufungwa hasa kutokana na jinsi mwenzi alivyopatikana

Usikubali kuoana haraka mno.
Kuwa wachumba kwa muda mrefu huwezesha ndoa yenye afya.
Hapa unatafuta mtu wa kuishi nawe maisha yako yote ina maana utalala naye chumba kimoja maisha, utakula naye chakula maisha yote, utakuwa naye katika matatizo ya kifedha maisha yako yote, utauguzana naye miaka yako yote, mtakumbana na kukatishwa tamaa pamoja maisha yako yote.
Kuamua haraka haraka kuoana ni kujitengenezea risk kubwa.

Usikubali kuoana wakati bado umri mdogo sana:
Oa au olewa wakati kwanza wewe mwenyewe unajijua vizuri.
Pia hakikisha unamfahamu vizuri yule unaoana naye.
Kuanzia miaka 24 kwenda mbele ni umri mzuri kuoa au kuolewa.
Kuwa na umri mdogo maana yake bado hujatimiza mambo ya msingi kama pamoja na kukomaa kiakili kuishi kama mke na mume.
Tafiti zinaonesha ndoa stable ni zile ambazo wanandoa walioana wakiwa na miaka kuanzia 28.

Usikubali kitu chochote, mazingira yoyote au mtu yeyote kukusukuma kuoa au kuolewa.
Hakikisha umetuliza akili zako ndipo ingie katika biashara za kuoana.
Inawezekana unataka kuoana haraka kwa sababu uliachwa na mchumba mwingine, au unajisikia mpweke, au anahisi ukiolewa suala la uchumi litakuwa limepata jibu.

Usikubali kumridhisha mtu yeyote na chaguo lako:
Ni wewe utakaye pata faida au hasara, raha au machungu, furaha au huzuni, utamu au kuumizwa na si muda mfupi bali hadi kifo kitakapowatenganisha.
Haina haja kuwafurahisha wazazi au marafiki, au mchungaji, au mchumba mwenyewe kwamba unaoa au unaolewa eti wawe very happy.
Hii haina maana kwamba hutakiwa kuwasikiliza katika ushauri wao kuhusu wewe kuoa/kuolewa bali hii ni ndoa ni yako a lifetime opportunity.
Wala usikubali mtu awaye yote akuchagulie au kukufanyia uamuzi hata kama anauzoefu namna gani.
Wewe ndiye unatakiwa kuwa na uamuzi wa busara hata baada ya kupokea ushauri wa kila aina kutoka kwa watu tofauti

Usikubali kuoana na mtu hadi uweze kumfahamu katika njia tofauti.
Unatakiwa kumfahamu vizuri huyo mwenzi wako mtarajiwa, mfahamu tabia zake kwa kadri unavyoweza.
Kutembea mmeshikana mikono miaka 10 ijayo kunategemea sana jinsi unavyomfahamu vizuri kabla ya kuingia naye kwenye ndoa.

Usiolewe au kuoa huku una matarajio makubwa sana (unrealistic):
Ndoa kimbilio la faraja; inahitahiji kazi ya maana ili ikupe faraja.
Usiingie kwenye ndoa umeweka matarajio ya juu sana as if ni solution kwa shida zako zote kifedha, kihisia na kimaisha.
Hata kama sasa kuna mapenzi ya juu sana na una matumaini makubwa uwe makini kwani kila kitu kinaweza kuyeyuka kama barafu kwenye jua.
Kama unataka kuwa an ndoa imara jiandae kwa kazi iliyombele, kujitoa kutakuwa na maumivu, kuvumiliana, utakutana na changamoto ambazo inabidi ushindi na kuthibitishwa ili kuwa na true love kwa mwenzi wako.

Usikubali kuoana na mtu ambaye tabia yake unahisi hutaweza kuivumilia maisha yako yote.
Kama kuna tabia Fulani ambayo hupendezwi nayo kama wivu, uchoyo, uchafu, hasira, uvivu, kutowajibika, siyo mkweli au msumbufu; jiulize kama utaweza kutumia maisha yako yote na yeye huku ukipambana na hiyo tabia.
Hiyo tabia mbaya kwake haitaondoka, kama unaomba muujiza abadili tabia hakikisha unatokea kabla hujaoana naye lakini si kuoana naye huku unajua kuna tatizo kubwa eti ukioana naye muujiza utatokea.
Siku njema.....................................

9 comments:

Anonymous said...

Lakini sikuhizi si rahis zaidi maana hata internet wanapatikana wakubwaga.Ila huku ni vituko vitupu maana wengine wamefanya dating hata na ndugu zao.
Lakini swala la internet unalionaje maana halijaandikwa na limekuja let.
edmund.

~PakKaramu~ said...

Pak karamu reading your blog

fikirikwanza said...

somo jema sana hasa kwa kina fkirkwanza.

Lazarus Mbilinyi said...

Kukutana na mtu kwa njia ya internet ni sawa na kukutana na mtu mahali popote, issue isifanye makosa hakikisha unaepuka makosa tuliyojadili. Mfahamu muda wa kutosha, jua tabia zake pia hakikisha unapima na umeamua mwenyewe kwa hiari yako na ukiwa na akili timamu.

Upendo daima

Anonymous said...

My Blog
http://www.wretch.cc/blog/markacey
Nice to meet you
Hsinchu, Taiwan

Anonymous said...

kaka lazarus mi nina swali ni la kiroho zaidi, mbona isaka na rebeka walioana na hawakuwahi onana? Mungu alimwongoza na akapata mke wala haina kuchunguzana tena rebeka akasema msinikawilishe niende kwa bwana wangu, unaonaje hapo?

barikiwa

Lazarus Mbilinyi said...

Uliyeuliza kutumia model ya Isaka na Rebeka (kuoana bila kuchunguzana) ukweli unapotafuta mtu wa kuwa mke au mume ni wewe mwenyewe unaweza usichunguze hata kutoanana kabisa na huyo mchumba na mkaoana wala haina shida.
Hii ni hatua ya juu sana ya kiroho ambayo unakuwa umemwachia Mungu asilimia mia na wengi imewasaidia.

Hata hivyo dunia ya sasa na jinsi tunavyotafuta mke au mume kwa sasa tumebadilika sana na watu tunakutana tamaduni tofuati, imani tofauti (hata katika kundi la wanaoamini) hivyo unakuwa umepaki gari for your own risk kuoana bila hata kujua jina la pili la huyo unataka kuoana naye, anyway hii ni nafasi muhimu sana katika maisha na uamuzi wako utaathiri sana future yako, ila kama unaishi enzi za akina Rebeka na Isaka na tamaduni zenu zinafanana mpendwa keep on going na utafutahia ndoa yako, otherwise think twice!

Upendo daima

Anonymous said...

KAKA LAZARUS SHALOM!
NI KWELI KABISA NI HATUA YA JUU YA KIROHO ZAIDI, MIMI NDO NILETOA COMMENT YA REBEKA NA ISAKA, KUSEMA UKWELI MIMI NA MUME WANGU NDOA YETU NI PARADISE NA NILIAZIMIA BWANA ATANIONGOZA KUMPATA MUME WANGU KAMA ALIVYOFANYA KWA ISAKA NA REBEKA TULIKUWA HATUJUANI KABISA YEYE WA BARA JINGINE NAMI MTZ,LKN NASHANGAA BWANA AKAMLETA KWA NJOZI NA MAONO KUTHIBITISHA NDIE MUME WANGU MARA 3 KWA NYAKATI TOFAUTI.

KWA KWELI MUNGU WA AJABU SANA NINAISHI NA MUME WANGU MAISHA MATAMU SANA LKN YOTE NI KWA AJILI YA KUMPENDA KRISTO YESU. NDOA YETU NI PARADISO, ASANTE YESU YOTE YAWEKANA KWAKE YEYE AAMINIYE.

UBARIKIWE KAKA

Lazarus Mbilinyi said...

Mdau wa Ile njia ya Isaka na Rebeka Hongera sana,

Ni kweli kwa Mungu hakuna lisilowezekana na unapomwachia Mungu asilimia zaidi ya mia akupe mwenzi unampata mzima mzima huku hujui chochote kuhusu yeye na mnapooana ni kama vile kuna sauti inakwambia "huu ndio ubavu wako" na wengi ilitokea hivyo na hatukubisha na ndoa zipo paradiso hata hivyo unahitaji kumtegemea Mungu mia kwa mia.
Pia muhimu kutokubweteka kwani ndoa ni kazi inayoendelea kila mmoja kujitoa kwa ajili ya mwenzake na ukikosea kubali na omba msamaha na zaidi hakikisha ndoa ina vicheko mara kwa mara hahaha

Ubarikiwe na Upendo daima