"Marriage is our last, best chance to grow up."

Thursday, June 4, 2009

Malalamiko mengine! kazi

Mlipooana tu sex ilikuwa hot, exciting na full speed! Na mlikuwa mnasemezana kwamba hata siku moja haitakuja kubadilika hata hivyo baada ya watoto kuzaliwa na majukumu kuongezeka hata bila tahadhari tayari kila mmoja analalamika kisirisiri. Na mbaya zaidi wengine hulalamika kwa ndani hawasemi, ukweli unahitaji kukaa chini na mwenzi wako na kujadiliana na kumalizi kwani “small things matters”

Malalamiko yafuatayo mara nyingi hutawala ndoa nyingi si zote:

Mke wangu haniambii nini anahitaji tukiwa kitandani.
Kama wewe ni mwanamke ukweli ni kwamba mume wako hawezi kusoma kile kipo akilini mwako, “men read news papers not minds” kama ulikuwa umeota kuhusu yeye au ulikuwa unatamani akufanyie kitu chochote wakati wa kuwa mwili mmoja, au unahisi akifanya kitu Fulani utajisikia kusisimka zaidi; mwambie na yeye ataipata point yako na si kula jiwe.

Hataki kunyoa!
Baada ya kuwa na watoto, baadhi ya wanawake husahau kabisa kiwembe kinauzwa wapi au kimewekwa wapi, inawezekana wewe unayesoma hapa ni mojawapo (walewale), wewe mwenyewe ni shahidi hukuwa na msitu mnene kama wa ikweta hapa kabla; ni kweli upo busy na mumeo anajua upo busy hata hivyo kujiweka safi ni tabia njema, mumeo analalamika kimya kimya! Looo!

Chumbani anavaa kama yupo ofisini!
Wakati wa honeymoon ulikuwa unavaa nguo za chumbani chumbani na ofisini ofisini, sasa mbona ukiwa chumbani unajifunika nguo gubigubi, ni kweli tangu uzae watoto umebadilika sana, umenenepa na mumeo anajua hata hivyo anahitaji kuufurahia mwili wako kwa wewe kuvaa zile nguo za chumbani ili akufaidi, unaficha mwili wa nini wakati ni mali ya mumeo.

Anang’ang’ania mlalo mmoja tu!
Anapenda missionary position tuu, kama mwanzo wa ndoa alikuwa anajirusha style zote basi inawezekana libido imeshuka na ni dalili kwamba hana hamu tena, jibu ni kuanza upya yaani umchumbie upya, ukifanya mchezo ataanza kupena kusoma vitabu kuliko sex!

Hataki kulianza!
Yaani kila siku ni mimi mwanaume kuanza hata kama mpo hivyo inatakiwa angalau siku moja na wewe uniambia unanihitaji.
Inawezekana mwanaume hajui mwanamke anahitaji kitu gani katika mapenzi, mwanamke akiwa na mood nzuri anaweza kulianza, hata hivyo unachofanya na mkeo nje ya chumbani huweza kutoa npicha ya kile mtafanya mkiwa chumbani.

Anaogopa watoto watatusikia!
Kila siku tukitaka kuwa mwili mmoja mke hulalamika kwamba hadi watoto walale kwani watatusikia, nikifungua radio ili kumeza sauti za tunapokuwa mwili mmoja bado analalamika kwamba watasikia.
Mwanaume lazima ujue kwamba “everything in women’s life is wonderfully connected” ni kweli huwa anawaza watoto watasikia au mlango hujafunga vizuri na matokeo anaweza asipate raha kamili, ni jukumu la mwanaume kuhakikisha usalama na privacy kabla ya kuanza kung’ang’ania kuwa mwili mmoja.

No comments: