"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, June 17, 2009

Mamia Wawania Kumuoa Milionea Anayetafuta Mume Kwenye Internet

Takribani wanaume 400 wa Korea Kusini wanapigana vikumbo kujaribu bahati yao ya kumuoa mwanamke milionea wa nchini humo ambaye ametangaza kutafuta mume kwenye internet.
Je, kwa wanaume kufanyiwa interview baada ya shortlist itamsaidia huyu mama milionea kupata mume sahihi?

Kwa habari zaidi soma hapa
Source: Nifahamishe

4 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Kwa mimi naona ni upuuzi tu kwani mtu unaoa au kuolewa na mtu kwa vile umempenda kwa dhati si unazipenda pesa.Hiyo ni mimi!!!

Lazarus Mbilinyi said...

Dada Yasinta upo sahihi,
Hata hivyo pesa si jibu la mambo yote kuna vitu vingi sana katika maisha pesa imeshindwa kutoa jibu na matokeo watu wamejikuta wapo katika upweke uliokithiri.

Upendo daima

Anonymous said...

kaka lazarus siajabu ukakuta huyo mama wanaume wanamuogopa kwa kuwa milionea najua hata wengi wa kaka zangu wa kitz wapo hivyo either kama mwanamke ana pesa sana, ni kale ka nishai flani tu kapo kwa wanaume, lkn zaidi ya yote mume na mke hata kama unaweka profile kwa internet lazma Mungu ashirikishwe kikamilifu ili mtu apate mume au mke alie chaguo toka kwa Mungu.

barikiwa sana

Lazarus Mbilinyi said...

Mpendwa,
Hapo hakuna kitu ndoa ni institution ambayo upo invented na Mungu hivyo Mungu ni namba moja (unaweza kupinga na ukipenda andamana ila huo ndiyo ukwweli) jamii yoyote ambayo imemuweka mbali jehova basi ndoa zao zinasuasua na kiwango cha talaka kina tisha hata sasa hakuna kitu kinaitwa family tree bali family web kwa sababu mwanaume mmoja au mwanamke mmmoja anazaa watoto na wanandoa tofauti na kujikuta tunapoteza ile family tree kwani koo zinavulugana.
Pesa si jibu la mambo yote ingawa maskini wengi wanaamini wakiwa na pesa watamaliza matatizo yote.

Hapo hakuna lolote wanaume wanataka hizo pesa za huyo mama ila zitawatokea puani.

Upendo daima