"Marriage is our last, best chance to grow up."

Tuesday, June 9, 2009

Ni baba vivuli!

Wanapenda kazi hadi kutamani kulala kazini!Wapo watu ambao ni walevi wa kupindukia linapokuja suala la kazi (hasa sisi wanaume na si wote). Huamka mapema kabla watoto hawajaamka na huchelewa kurudi baadaya watoto na mke wameshalala. Kama ni chakula (dinner) basi kwenye kimepoa hadi kikawa kipolo na mke husubiri hadi anachoka na kuamua kulala.

Ukiwauliza wanasema wanafanya hivyo kwa sababu ya future kwa maana kwamba anafanya kazi kama punda ili baadae aishi kama mfalme.
Mke huwa kama mlinzi wa nyumba.
Watoto wanakuwa wageni na baba yao kwani hawajawahi kujua raha ya baba na kucheza naye na kumuuliza maswali mbalimbali.

Huyu baba usiku akirudi anakuta watoto wamelala fofofo; huku akijiamini na yale anafanya huwagusa watoto kwa mikono na kuwaambia

Najua mnafahamu kwamba baba yenu najitahidi kufanya kazi usiku na mchana ili muwe na future”

Anawabusu na kwenda zake kulala huku yupo hoi yupo hoi.
Akifika kitandani kwa mkewe anamwambia
“ Unajua najitahidi sana kuhakikisha tunalipa bills na pia nikistaafu kazi tunakuwa na maisha mazuri (retirement home)
Hapa kuwa mwili mmoja ni ngumu kwani mke huwa kihisia amejipiga password, haingiliki maana anawaza jinsi alivyomsubiri na jinsi chakula kimepoa bila mume kuwepo cha dinner.
Hii haina maana kwamba mke na mume hawatakiwi kuwa na mipango ya muda mrefu na muda mfupi au kutowekeza kwa ajili ya future bali itakuwa haina maana na ujinga uliokithiri na wa hali ya juu kupoteza familia kwa sababu ya mipango ya baadae, anyway hata hiyo mipango ni kwa ajili ya nani wakati umepoteza familia?

Hata kama umechelewa dinner wahi nyumbani uonane na watoto na mke kabla hawajalala si vizuri watoto kuishi maisha kwa ufahamu kwamba baba ni kama kivuli tu ambacho hutoa busu kila siku wakati wameshalala na kabla hawajaamka asubuhi.
Huku ni kujidanganya, Eti unafanya kazi hadi kusahau familia ili uwe na maisha wakati umestafu kazi?
Familia gani?
Mke gani?
Wakati atakuwa ameshajichokea na kujizeekea kwa ulevi wako wa kazi, ata-enjoy wakati hata kuwa mwili mmoja (sex) kashajizeekea?
Na watoto wameshakuwa na maisha yao, huku kujidanganya!
Ishi sasa na pia panga mipango ya uhakika ya baadae.

Mke amekubali kukuoa kwa sababu anakuhitaji sasa, anahitaji upendo wako sasa, anahitaji maisha sasa anahitaji kukufaidi sasa, anahitaji satisfaction sasa, anahitaji umefikishe kwenye kilele cha raha ya ndoa sasa.
Ni kweli future ni muhimu na ni muhimu sana kufikiria kuhusu future tena nakutia moyo kwa hilo ila too much is harmful.

Maisha ni sasa na maisha lazima yawe na balance hata kama upo busy namna gani watoto wanakuhitaji baba na mke anakuhitaji.

Wapo ambao huishi mbali na mke au mume kutokana na kazi wanazofanya hata hivyo siku akirudi nyumbani hapatikani akiulizwa vipi mbona huna muda na sisi familia yako, majibu yake
“Nina mipango na rafiki zangu
sasa nani muhimu rafiki zako au mke na watoto?
Anyway ukipoteza watoto na mke rafiki zako watachukua nafasi yao?

“Your Marriage or Relationship is so Important, Please take Good Care of Yourself and Be Kind to Your Partner and Try to Keep Your Sense of Humor”

Jambo la msingi ni kuwa na ratiba kamili hata kama upo busy weka ratiba ambayo itakuwezesha kuwa na familia angalau mara 3 au 4 katika siku 7 za wiki.
Watoto wakufahamu na mke aridhike ndipo mipango yako itakuwa ya maana sana na Mungu atakubariki kwa hilo.

Je, ukiwa na mume mlevi wa kazi ufanyeje?

Tutaendelea...............................


No comments: