"Marriage is our last, best chance to grow up."

Monday, June 22, 2009

Ni heri!

Ni heri wanandoa ambao wamegundua changamoto zinazoridhisha kutoka kwa mwenzake kwa maana kila mmoja atakuwa na uhakika na mwenzake bila kuwa na hofu au mashaka.

Heri wanandoa ambao wanaweza kushirikisha huzuni za ndani kutoka kwa mwenzake kwa maana hakuna atakaye jisikia mpweke wakati wa shida, matatizo au janga na ugumu wa aina yoyote katika maisha ya ndoa.

Heri wanandoa ambao kila mmoja ameonja utamu wa upendo wa mwenzake na kwamba uzuri wa upendo huendelea kudumu na kudumu na kila siku hujisikia kuwa mwenzake ni mpya.

Heri wanandoa ambao upendo ni imara kiasi cha kushirikisha wengine kwa maana kwao maisha hayawezi kuwa hayana maana tena.

Heri wanandoa ambao imani waliyonayo kati yao huleta matumaini na kutia moyo wengine kwa maana watu watawaongelea na kuwaambia
“ Ni wanandoa wenye furaha na waliobarikiwa”

Heri wenye ndoa ambao wanauhusiano na Mungu kila mmoja binafsi na wote kwa pamoja kwa maana maisha yao yatakuwa na utajiri wa furaha na hakuna ambalo halitawezekana kwao.

Marriage is possible because it combines the maximum of temptation with the maximum of opportunity.
By
George Bernard Shaw

4 comments:

Anonymous said...

Kaka, Umenena vema hapo na mungu akubariki sana kwa kuwatia nguvu, moyo, kuwajaza maarifa na kumtegemea mungu wanandoa wote wamtegemeao na wasiomtegemea Mungu. Msafiri

fikirikwanza said...

Usinikumbuke hapa jijini london(no nimekosea ikelo).

Anonymous said...

kaka lazarus naomba uliza ulishawahi toa mada wanandoa lazma wapeane taarifa mapema kabla ya tendo na kama ni usiku ili akili iwe sawa kujua nini kitaendelea usiku, swalilangu sasa, kama nimeamka katikati ya usiku alafu nahisi kufanya tendo sasa nifanyeje nijikaushe tu mpk asb mume wangu akiamka au? msaada plz.

mdogo wako Grace

Lazarus Mbilinyi said...

Dada Grace asante kwa swali zuri.
Wanandoa hupeana taarifa mapema kuhusiana na mambo ya kuwa mwili mmoja kwa sababu ya mood kwa maana kwamba maandalizi mazuri huwezesha kuwa na tendo la ndoa linaloridhisha kwani sex ni ubongo na maandalizi mazuri husaidia kuliko kushituana hasa mwanamke.
Hata hivyo kila ndoa au wanandoa ni tofauti na wengine na kila ndoa ina aina yake ya kuwasiliana kuhusiana na kuwa mwili mmoja, pia kila mmoja kati ya wanandoa ana aina yake ya kuwakilisha ujumbe kwamba anataka kuwa mwili mmoja, hivyo usiweke sheria kwamba kwa kuwa wanasema lazima utoe taarifa kabla basi ukitaka kuwa mwili mmoja usiku (baada ya kunyegeka ghafla basi ule jiwe) jambo la msingi unaweza kuongea na mwenzi wako au unaweza kutoa ishara kwamba unataka vitu (hahaha) aki-respond basi fanya kweli.
Jambo la msingi hakikisha unajua aina ya ndoa mliyonayo linapokuja suala la kuwa mwili mmoja. Wengine hupenda ya kushtuana na wengine hadi taarifa ikiwezekana wiki kabla au siku kabla hata.
Mfahamu sana mwenzi wako na wewe mwenyewe na uwe huru na muwazi kwa mpenzi wako then enjoy.

Upendo daima