"Marriage is our last, best chance to grow up."

Tuesday, June 30, 2009

Ni utamaduni tu!

Fikiria wewe ni mwanamke; mume wako mpenzi amesafiri kwa mwaka mmoja au miwili na umemmiss kweli, una hamu naye, huhitaji chochote ula unamtaka yeye maana ni haki yako na ni wako, bahati nzuri au mbaya siku anafika wewe ndo umeanza siku zako (MP)

Je, utahakikisha unafanya unaloweza kuhakikisha mnakuwa mwili mmoja au ndo kula jiwe hadi siku tano ziishe?

UTANGULIZI:
Kuwa mwili mmoja wakati mwanamke yupo MP kunahusisha mila, desturi na tamaduni zenye mawazo tofauti baadhi ya tamaduni ni marufuku kubwa (mwiko) au ni unajisi kujihusisha na kuwa mwili mmoja wakati mwanamke yupo MP, hata hivyo kuna wanawake (na wanaume) na madaktari wengi wanaothibitisha kwamba hakuna tatizo na badala yake kuna faida kubwa.

Kwa wastani mwanamke huwa na siku 500 za MP katika maisha yake hii inatokana kuwa na siku 5 kwa wastani kati ya siku 28 za mwezi mmoja; hii ina maana kwamba zoezi hili litakumbana na siku ambazo suala la sex kwake linaweza kuleta usumbufu kwani atakuwa anahitaji kujishusisha ila atajikuta yupo MP.

JE, ZIPI NI FAIDA ZA KUWA MWILI MMOJA WAKATI WA MP?
Mwanamke akifikia kileleni (orgasm) hutoa homoni za endorphins ambazo ni natural pain killer na mood enhancer hivyo huweza kupunguza maumivu ya MP, kichwa na msongo wa mawazo pia husaidia flow ya damu kwa siku zinazofuata (Dr Monique Rainford - gynaecologist).

Mwanamke hujisikia raha zaidi (pleasurable) kwani uke na kisimi huwa sensitive zaidi na kuguswa kidogo tu mwanamke husisimka kwa hisia kali zaidi ni moja ya nyakati ambazo mwanamke libido huwa juu.

JE, NINI HASARA ZA KUWA MWILI MMOJA WAKATI WA MP?
Kisaikolojia baadhi ya wanawake hujiona ni wachafu (messy) na hujisikia vibaya (uncomfortable) hivyo hawezi kufurahia kuwa mwili mmoja.
Kama mwanamke au mwanaume ana maambukizi inakuwa rahisi kuambukizana magonjwa kwani viungo vya mwanamke vinakuwa delicate na rahisi kuambukizwa.
Pia ana uwezekano mkubwa wa kuambukizwa fungus (yeast) na bacteria (candidiasis) kwa kuwa pH ya uke huwa na kiwango kidogo cha acid.

JE, MWANAMKE ANAWEZA KUPATA MIMBA KUWA MWILI MMOJA WAKATI YUPO MP?
Ndiyo kuna uwezekano wa kupata mimba ikiwa tu mwanamke ana mzunguko mfupi sana ambao siku anayokuwa fertile ndo siku anaanza siku zake.
Pia sperms zinaweza kukaa zaidi ya siku 5 na kuweza kurutubisha yai baada ya siku kumalizika.

Kuchukua tahadhari kuwa mwili mmoja wakati wa mwanamke kuwa katika siku zake ni jambo la msingi zaidi na hupelekea tendo kuwa la raha na wapo wanawake wanakubali kwamba sex wakati huo huwa na raha ya ajabu na kupunguza maumivu ya kuwa kwenye siku zake (menstrual cramps)

Hata hivyo kila ndoa ina aina yake ya kuwa mwili mmoja hivyo kumfahamu vizuri mpenzi wako au mwenzi wako ndilo jambo la msingi kwani mnaweza kukwazana na ikaleta mzozo mkubwa.

Ubarikiwe na Bwana.

No comments: