"Marriage is our last, best chance to grow up."

Tuesday, June 9, 2009

Ni wazuri sana!

Ni mara chache sana utakutana na mwanaume akitoa chozi la uhakika hivi!
(http://www.democracyfornewmexico.com/)Wanawake kweli ni viumbe wa thamani ambao wakati mwingine hushangaza; hata hivyo yote ni kwa utukufu wa Mungu aliyetuumba tuwe tofauti ili kukamilishana.

Machozi ni moja ya vitu ambavyo mwanamke huhusika moja kwa moja hata katika malezi wazazi wetu walikuwa wanatuonya watoto wa kiume tusilie tukikutana na jambo kubwa au gumu kwani walisema kulia ni mwanamke na si mwanaume.

Mwanaumke huweza kutoa machozi akifurahi, akihuzunika, akikutana na rafiki au ndugu ambaye walioachana muda mrefu, hata wakati mwingine hutoa machozi ili kupata kitu na wakati mwingine hutoa machozi kwa kupoteza kitu katika miliki yake yaani moyo, na kwenye misiba basi huko usiseme maana ukichanganya na mila inakuwa shughuli nzito.
Kwa maelezo zaidi ya machozi na mwanamke soma hapa

Pia machozi ni moja ya silaha mwanamke hutumia hasa kujilinda kwani anaweza kujieleza kwamba tafadhari “Usiniambie mapungufu yangu la sivyo nitaaza kutoa machozi sasa hivi
Hata hivyo kazi kubwa ya mwanaume ni kutofautisha machozi ya hisia, msongo wa mawazo na uchoyo, ni kweli mwanamke ni emotional creature ambaye mwanaume lazima uwe makini to handle with care.

Hata hivyo Watafiti wengi wanakubaliana kwamba mwanamke anayetoa machozi ni mzuri sana lipokuja suala la hisia katika maeneo yote ya maisha hii ina maana kwamba mwanamke mwenye kumwaga chozi mara kwa mara ni mtamu chumbani kwa sababu anaweza kujieleza katika lugha ya mapenzi (love making, act of marriage) Na mwanamke mwenye macho makavu maana yake ni mgumu kuji –express wakati wa kuwa mwili mmoja.

Wanawake wenye machozi ni mara chache sana kuwa baridi (frigid) wakati wa kuwa mwili mmoja kwani ukimwandaa ni rahisi kuwa connected kihisia.

Pia kujua machozi ni dawa soma hapa

5 comments:

Anonymous said...

kaka napenda sana sana makala zako!!!!zinanifanya najiskia muruuuuaaaaaa!keep it up!

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Mbilinyi asante sana kwa soma hili kwa kweli kuna mengi nimejifunza.
Ubarikiwe kakangu

Lazarus Mbilinyi said...

Dada Yasinta na mdau mwingine,
Asante sana kwa comments na kunitia moyo, kitu cha msingi ni muhimu kujifunza ili tuwe partner wazuri kwa wale tunawapenda na zaidi mahusiano yawe mazuri na yenye kuridhisha.

Upendo daima!

Simon. said...

ni kweli kabisa kaka ulichokiongea kwenye makala yako..
nimeipenda sana hii makala mkuu..
tuko pamoja mzee,siku zote

Lazarus Mbilinyi said...

Hata hivyo inabidi mwanaume kuwa makini mwanamke anapotoa machozi wengine huwa lethal weapon kukumaliza maana anajua akitoa machozi utapata huruma furani, You have to know this stuff in and out.

Uwende lipwela