"Marriage is our last, best chance to grow up."

Sunday, June 28, 2009

Nimenunua jipya, niendeshe vipi?

Mimi ni ijana wa kiume mwenye umri wa miaka 27 natagemea kuoa miezi miwili ijayo kwa ndoa takatifu.
Napenda kujua nini cha kufanya kumwandaa mwanamke siku nikiwa honeymoon kwani hii itakuwa mara yangu ya kwanza kuwa na mwanamke (mwili mmoja)
Je, unaweza kunipa tips muhimu kumuandaa mwanamke kabla ya tendo la ndoa?


Kwanza nakupongeza sana kwa kuwa umegundua umuhimu wa kumwandaa mwenzi wako (foreplay) ambaye kwanza ni kifaa kipya kabisa na hii itakuhakikisha anapata muda wa ku-relax na kuwa na mood kwa ajili ya tendo takatifu na matokeo wewe pamoja na mwenzi wako mtafurahia.
Kitu cha msingi kabla kuwanza kuwa mwili mmoja ni vizuri kuwa na maombi kwanza kwa sababu ndo yako ni takatifu.
Kumbuka wewe mwanaume ndiyo kiongozi, mnaweza kuanza kwa kila mmoja kuomba mwenyewe kwanza then baada ya muda unaweza kumsogelea mwenzi wako na kumshika mikono ya kuanza kuomba pamoja (kushukuru kwa Mungu kufanikisha ndoa yenu na zaidi kuombeana ili muweze kuwa mwili mmoja.)
Baada ya kushikana mikono unaweza kuendelea kumkumbatia huku mnaendelea kuombeana hadi mnamaliza sala yenu.
Baada ya hapo kuna njia panda unaweza kuendelea naye hadi mnakuwa mwilim mmoja au mnaweza kumaliza maombi na kuendelea na processs za hapa chini.

Kumwandaa mwanamke kuwa mwili mmoja huanza kwa maneno, ongea kile ambacho kitamfanya damu yake kuwa hot.
Pia matendo huweza kufanya kitu cha maana zaidi kuliko maneno, wakati unampa maneno mguse kwa kupalaza (lightly) kwenye mwili wake wanawake husisimka kwa kuguswa wakati wanaume kwa kuona; tembeza mkono kama mawimbi unapoongea au kutoa zile hadithi zako za kumtengeneza mood, huku ukiwa karibu kiasi cha nywele zake kugusa uso wako.

Wakati wa maongezi mguse kwa wororo (tenderly) anza kuingilia himaya yake (siyo sehemu za siri – private parts) bali private space.
Unaweza kugusa mkono wake au kuondoka kitu chochote kwenye nywele zake au uso wake (hata kama hakipo we si unajua unafanya kitu gani) au unaweza kushika mikono yake (au vidole ) na kufanya massage kiana kwa kutumia vidole vyako.

Anza kumsifia jinsi alivyo ukianza na nguo au kitu chochote amevaa (hapo ndipo ugonjwa wa wanawake wengi ulipo) sifia sura yake na vile alivyo kama vile nywele, kucha, lips na vingine unavyovijua wewe, sifia kwa uhakika na kiukweli anyway ni kweli ur wife is so beautiful ndo maana upo naye hapo.

Jihusishe naye zaidi kwa kumgusa (touching) katika njia ambayo si ya kuashiria unataka sex pia kwa hatua kama hii usithubutu kumbusu yeye bali yeye ndo utakuomba umbusu.

Maongezi yako yanatakiwa sasa kuwa ya kimahaba zaidi, tumia sexy words, mwambie unavyojisikia kihia (feelings) ongea kwa ulaini ili akuelewe kirahisi, unapoongea mnong’oneze kwenye makisio yake kama vile unamwambia siri hata kama mpo chumbani wawili tu.
Wakati unamnong’oneza sogeza zaidi lips za mdomo wako kwenye masikio yake na kugusisha na kumpa kabusu ka kiaina halafu achia kumruhusu yeye kujiachia kwako zaidi na kukung’ang’ania zaidi.
Ukiona anakuegemea zaidi ongeza kabusu kengine kwenye sikio huku ukimwambia maneno matamu na yanayovutia ya kimahaba.
Ukiona joto lake linazidi sasa usifanye kosa anza kusambaza mikono yako na kumgusa kila eneo la mwili wake (kiwanja kizima) lakini usiguse matiti, au chini (sehemu za siri) bali tumbo, mgongo, shingo, mikono, miguu, kidevu nywele nk.

Anza kusambaza busu lako kuanzia kwenye lile sikio, shingo, kinywa huku yeye akiendelea kukuinamia na wewe unaendelea kumpoa soft kisses baada ya hapo naamini moto maji yataanza kuchemka kiasi kwamba kupoa itakuwa kazi nzito na ukiona hakuna kitu anza square one au soma hapa.

8 comments:

Anonymous said...

woow!
kaka lazarus hii hukuwahi niambia lkn roho wa bwana alifunulia hii before kufaya tendo lazma kuomba na after kushukuru, kaka ulieuliza swali hiyo iwe ndo destruri yenu ya kuomba before na after tendo isiishie honeymoon tu, naamini mtainjoy mno maana kumtanguliza bwana unapata raha ya ajabu sana. barikiwa mtumishi

ni grace hapa.

Anonymous said...

hongera sana kaka muuliza swali jua ndoa ni paradiso usisikilize mafundisho ya kishetan yasemwayo na watu wasiojua neno la bwana kusema ndoa ni ndoano.

asante pia kwa kaka lazarus kuendelea kutufundisha kila siku hapa bloguni Mungu akubariki sana.

napenda tu kusema kwamba ndoa isimame vizur lazma muwe wana maombi kweli kweli, tena usije jidanganya mke/mume wangu mtumishi kama hutasimama kuomba umechemka, ila hutachemka kwa damu ya YESU.

nakuja kwenye maombi haswa pekee kwa ndoa.lazma ufanye toba kwa ajili ya mke wako na wewe mwenyewe mume, then umshukuru bwana kwa kukupa mke/mume mwema.

sasa teka moyo /ufahamu kwa mamlaka ya damu ya Yesu na ufunge kabisa moyo/ufahamu usione binadamu awaye yeyote kwa jina la Yesu bali moyo wake ukupende wewe tu, pia teka nyara macho yake na yafunge kwa super glue ya damu ya Yesu yasione kiumbe yeyote isipokuwa wewe ndo uonekane wa maana kwake kwa jina la Yesu. fanya kwako pia teka ufaham/moyo/macho yafunge kwa mamlaka kama ulivyofanya kwa mkeo. vunja vunja roho za magomvi,vita,dharau,chuki kwenye ndoa yenu kwa damu ya YESU. izindike ndoa yako kwa damu ya Yesu kila siku tena nakushauri mda mzur wa kuomba ni usiku wa manane hakika utaona mkono wa bwana.

msisahau kuombea watoto wenu pia hata kama bado hawajazaliwa waombee baraka kila iitwayo leo, omba Mungu awape watoto, wazur wazima,wacha Mungu wenye adabu,utii ,wenye akili etc.

alafu endelea kujifunza maswala ya mapenzi toka kwa kaka lazarus hapa, utakuwa tu unashangaa watu wanalia ooh ndoa yangu jaman imenishinda wewe hayo magumu na majuto hutayaona kabisa, kila siku itakuwa honeymoon kwenu na upendo kila siku bwana atakuwa anauongeza kwenu na ndoa yenu itakuwa mbingu ndogo, yote yanawezekana kwake yeye aaminiye

ubarikiwe sana

Ms GBennett

Lazarus Mbilinyi said...

Dada Grace,

Ili kufurahia kuwa mwili mmoja ni muhimu sana kumuomba Mungu kwanza kwani yeye ndiye aliye invent sex hivyo ili kuwa na tendo linaloridhisha na kutupa raha ya ajabu tunazidi kumhusisha zaidi na zaidi na zaidi hata baada ya kumaliza tunashukuru vilevile na pia tunaombeana kila mmoja kumuombea mwenzake ili awe mtamu zaidi na shetani ashindwe si uanjua raha iliyopo kuomba kifuani kwa mwenzi wako!

Ubarikiwe na Bwana

Upendo daima

Lazarus Mbilinyi said...

Dada Ms GBennett,

Nimependa sana maoni yako yaani natamani siku moja nikusanye wanandoa utoe semina ya uhakika ili kuponya hii institution.

Yote umeongea ni muhimu sana na ni vizuri kila mwanandoa kuyafanyia kazi kwani ndoa kama ilivyo haina tatizo na tatizo kubwa ni sisi tunaounda ndoa hata hivyo tukiwa chini ya uwezo wa Mungu hakuna lisilowezekana hata wale ambao wanasema "mimi ndivyo nilivyo siwezi kubadilika" huo usemi umepitwa na wakati kwani kwa Mungu hakuna lisilowezekana hata kama ndoa ipo kwenye shimo tayari Bwana Yesu anaweza kuirudisha kwenye kwenye hali ya wanandoa kuishi kwa raha na upendo wa ajabu.

Upendo daima

Anonymous said...

shalom kaka lazarus!
roho wa Mungu alinisukuma kuandika juu ya nguvu ya kuzindika ndoa kwa damu ya YESU ,najua haya maoni yataponya wengi sana, nimefurahi kusikia hivyo kwa kweli kama wanandoa wote wangekuwa wanazindika ndoa zao kwa damu ya YESU kungekuwa hakuna ma yatima ambao wameachwa na wazazi waliokufa na ukimwi, hakuna kusalitiana i mean vimada na mahawara. ila tabu ya watu wengi ufahamu umefungwa na shetan na hawaombi jinsi ipasavyo, maana maombi ya ndoa si kama yale tumezoea kuombea chakula, Mungu turehemu sana.

nina njozi baadae ya kuwa natoa semina khs ndoa au kuandika vitabu juu ya nguvu ya maombi kwenye ndoa, bwana akinipa kibali ntafanya hivyo wakati ukifika

ubarikiwe sana

MS GBennett

Lazarus Mbilinyi said...

MS GBennett,

Hongera sana na Mungu akubariki kwa kuwa una mzigo katika mwili wa Kristo kupitia huduma ya kujenga ndoa, tunakuombea Mungu azidi kukupa maono zaidi na ufanikiwe kwa kile Roho mtakatifu anakufunulia.

Ubarikiwe sana na Bwana

Anonymous said...

napenda kuongezea kaka muuliza swali unaingia kwenye ndoa kuna kitu kinaitwa WIVU, unatakiwa uwe na wivu mzuri wa kumpenda mkeo na kumwonyesha furaha uliyo nayo kwake, na wewe kama ni mwombaji haswa wa haya maombi nilioandika hapa ya kuzindika ndoa hupaswi kuwa na wivu mbaya, yani ule wivu unaopelekea mashaka, maana utakuwa unaharibu maombi yako sasa, sasa mwingine anaomba alafu anachunguza simu ya mumeo aone kama atafumania sms au kuangalia simu zipi zimepigwa sana.ukishaanza kuweka mashaka tayar umemruhusu shetan maana tukiomba tunaamini Yesu anatenda na ndo mlinzi tosha.

biblia inasema mwanamke atamlinda mwanamme si kwa sms au kuangalia mbona leo kachelewa sana kurud na kumhisia mabaya bali ni kwa maombi haswa, wanawake wenzangu tusibweteke kuomba kwa ajili ya waume zetu, wengi walizembea ndo maana unasikia mtumishi flani ameanguka kwa uzinzi lkn chanzo ni mkewe ambao haombi ipasavyo kumlinda mumewe.

mbarikiwe wandugu

MS GBennett

Anonymous said...

napenda kuongezea kaka muuliza swali unaingia kwenye ndoa kuna kitu kinaitwa WIVU, unatakiwa uwe na wivu mzuri wa kumpenda mkeo na kumwonyesha furaha uliyo nayo kwake, na wewe kama ni mwombaji haswa wa haya maombi nilioandika hapa ya kuzindika ndoa hupaswi kuwa na wivu mbaya, yani ule wivu unaopelekea mashaka, maana utakuwa unaharibu maombi yako sasa, sasa mwingine anaomba alafu anachunguza simu ya mumeo aone kama atafumania sms au kuangalia simu zipi zimepigwa sana.ukishaanza kuweka mashaka tayar umemruhusu shetan maana tukiomba tunaamini Yesu anatenda na ndo mlinzi tosha.

biblia inasema mwanamke atamlinda mwanamme si kwa sms au kuangalia mbona leo kachelewa sana kurud na kumhisia mabaya bali ni kwa maombi haswa, wanawake wenzangu tusibweteke kuomba kwa ajili ya waume zetu, wengi walizembea ndo maana unasikia mtumishi flani ameanguka kwa uzinzi lkn chanzo ni mkewe ambao haombi ipasavyo kumlinda mumewe,na kufanya hivyo hamna talaka wala kuchokana wala kutengana

mbarikiwe wandugu

MS GBennett