"Marriage is our last, best chance to grow up."

Monday, June 15, 2009

Ogopa na epuka!

Siyo mkataba ni Agano!
(Picha hisani ya lateralaction.com) Uwongo
Ndoa ni mkataba (contract) na kwa kuwa ni mkataba basi unaweza kuvunjwa.
Ukweli:
Ndoa ni agano (covenant) lililowekwa na Mungu.
Ilikuwa ni mpango wa Mungu hata kabla ya binadamu kuweka mikataba ya kisheria kuhusu ndoa. Mungu ana define ndoa ni agano na agano halijajikita katka msingi ya kupokea zaidi ya unavyotoka (quid pro quo)

Uwongo:
Unaoa au kuolewa ni yeye tu hakuna uhusiano na familia yake
Ukweli:
unapooa au kuolewa si mwenzi tu bali ni pamoja na package ya familia yale.

Uwongo:
Naweza kumbadilisha mwenzi wangu:
Ukweli:
Huwezi kumbadilisha, unachoweza ni kumuathiri na tabia zako.
Kama unaamini utaweza kumbadilisha mwenzi wako unanidanganya na zaidi utakuja kukatishwa tamaa kwa hali ya juu sana.

Uwongo:
Tupo tofauti sana ndoa haiwezi kufika popote
Ukweli:
Tofauti zinazokuwepo kati ya mke na mume haziwezi kuiua ndoa bali jinsi tofauti zinavyoshughulikiwa ndicho kitu kinachoweza kuleta maafa.
Hakuna familia mbili ambazo hufanana kila kitu na hakuna watu wawili wanaweza kwenda sawa kwa kila kitu hivyo lazima kutakuwa na tofauti kati ya mke na mume.
Kumbuka ukikutanisha vitu viwili katika mwendo (moving) lazima msuguano utatokea na mke na mume ni watu na watu ni moving object hivyo tofauti na kusuguana lazima.

Uwongo:
Nimepoteza zile hisia za kumpenda tena na zimepota kabisa, Haitawezekana kumpenda tena.
Ukweli:
Hisia za kumpenda huweza kurejeshwa.
Ukielekeza katika positive kuliko negative unaweza kurejesha mapenzi kama mwanzo.
Kuwa na kiwango kikubwa cha negative kwa mwenzi wako hupelekea kujiweka mbali (emotional distance) na kupoteza upendo ingawa siri ni kuendelea kuangalia upande wa positive.

Uwongo:
Siwezi kubadilika hivyo nichukue kama nilivyo au niache.
Ukweli:
Unaweza kubadilika ingawa unahitaji hamu ya kutaka kubadilika, utiifu katika kutaka kubadilika na uwezo wa kutaka kubadilika.
Kwako binafsi ni vigumu kubadilika ila kwa uwezo wa Mungu Inawezekana kubadilika

Uwongo:
Mwenzangu amenisaliti kwa kutoka nje ya ndoa hivyo jibu ni talaka
Ukweli:
kutoka nje ya ndoa huumiza na huangamiza lakini si zaidi ya kushindwa kufanya marekebisho na upatanisho.
Ni jambo la msingi kujua sababu ya affair ilikuwa ni nini, then kwa msaada wa Mungu kusameheana, kutubu na kujitolea kuacha na kubadilika.
Kumbuka katika Biblia hakuna sehemu inayoruhusu talaka bali kusameheana na upatanisho.
Hii haina maana kwamba unaruhusiwa kuwa na affair kwa sababu kuna kusamehewa na kupatanishwa.

Uwongo:
Ndoa imefika mahali ambapo hatuwezi kuirejesha tena:
Ukweli:
Bado hamjachelewa, kwa Mungu hakuna lisilowezekana.
Je, hata ndoa ambayo imekufa inaweza kufufuliwa? Ni kweli Inawezekana kwani Mungu wetu ni Mungu wa muujiza.
Kama Mungu hawezi kufanya kile ametuahidi atakuwa Mungu gani? Mungu anaweza kubadilisha mioyo na kutoa njia na mwelekeo mpya kabisa katika ndoa na mahusiano.

4 comments:

angel said...

hello,
jaman mbilinyi thanx a lot yaan umejubu maswali mengi yaliokua kichwan mwangu ambayo sikua na wa kumuuliza
be blessed brother
angel

fikirikwanza said...

uwongo: ukiwa na zaidi ya miaka 40 umechelewa kuoa.
Ukweli: hata ukiwa kikognwe ni haki yako kuoa au kuolewa!!!!

Lazarus Mbilinyi said...

Dada Angel,

Asante sana kwa kunitia moyo, ni kweli kuna vitu vingi tunaamini kuwa ni kweli katika ndoa na mahusiano hata hivyo ni kutokana na mfumo wa kijamii na si katika misingi iliyowekwa tangu mwanzo na Mungu.
Mungu ndiye aliye design ndoa pamoja na sex katika ndoa.

Ubarikiwe na Bwana

Lazarus Mbilinyi said...

Fikiri Kwanza,

Upo sahihi, umri ni namba tu hata kama ni kikongwe unaweza kuolewa au kuoa kwani unahitaji mwenzi.

Hakuna kitu kinaitwa nimechelewa kuoa au kuolewa ila kila jambo na wakati wake.

Upendo daima