"Marriage is our last, best chance to grow up."

Saturday, June 6, 2009

That is my Personal Stuff!

Itakuwa kichekesho kama utaingia kwenye elevator na kuamua kubaki first floor miaka nenda rudi!Kuna wakati wake zetu hutuuliza maswali ambayo huwa sisi wanaume tunashindwa kuwapa jibu kamili (si wanaume wote).
Atakuuliza unajisikiaje kwa kila kitu, Niambie kuhusu hiki na kile iliramradi swali na huwa tunaogopa sana kujibu kwani kuna wakati hatujui majibu na kuna wakati tunahisi wanauliza maswali ambayo ni ya ndani mno kiasi kwamba ni kuingilia personal stuff.

Ukweli ni kwamba ni kwa sababu hatujaweza kuwapa habari zetu zote kwa undani na kuwapa siri zetu za ndani kiasi cha wao Kujiona ni wenyeji katika maisha yetu, Kujiona si wageni tena, kutujua kwa undani na siri zetu za ndani yaani intimacy.

Intimacy
kwa mke na mume ni kujuana in deep, ni sharing ya mambo ya ndani, siri za ndani, innermost qualities za ndani ambazo ni ninyi wawili tu ndiyo mnapeana.
Intimacy si kufanya mapenzi au romance bali ni kupeana habari (core information) za ndani, mawazo ya ndani, hisia za ndani, ndoto za ndani, huzuni na furaha.
Kukiwa na intimacy basi tendo la ndoa huwa linaridhisha, mapenzi huwa matamu, romance huwa huleta raha.

Intimacy ni kumvumbua partner katika habari zake maalumu za ndani na kwamba ninyi wawili kila mmoja ni mali ya mwenzake.
Intimacy ni kutumia muda pamoja kujuana katika hali ya ndani kihisia kiasi cha kutengeneza bonding imara, huwezesha watu kuwa mwili mmoja na kuhitajiana, kuwa fused together, kuwa merged, welded together.

Intimacy ni hitaji muhimu la mwanamke katika mahusiano ili afungue moyo wake na kuwa tayari kuwa na mumewe kuridhishana kimwili.

Bila intimacy ni sawa na ndoa kuwa kwenye elevator na katika kusubiri kwenda floor ya 10 mnabaki floor ya kwanza na matokeo ni kuishia hapo miaka nenda rudi.

Hivyo basi ni muhimu sana sisi wanaume kuwaruhusu wake zetu kujua hizi personal stuff ili awe mwenyewe na si mgeni kwako.

Kwa maelezo zaidi unaweza kusoma hapa

No comments: