"Marriage is our last, best chance to grow up."

Friday, June 26, 2009

Ukibomoa moja, jenga tano!

“Nimepoteza hisia za kumpenda, zimepotea na zimepotea kabisa.
Simpendi kabisa Julia na hata sifahamu kama kweli niliwahi kumpenda; nashangaa na sihitaji kuwa naye tena, sijisikii chochote linapokuja suala na hisia zangu kwake naamini ndoa imefika mwisho” James aliongea kwa mshangao mbele ya Julia

Julia naye akajibu kwa kusema “hata sielewi tumefikia vipi hatua hii.
Tunaongea mara chache sana na hata tukiongea hatuongea jema lolote, (machozi yanaanza kumiminika kwenye mashavu) ni kulaumiana, kudharauliana, kusutana, kila mmoja anampuuza mwenzake, ndoto zimeyeyuka na hakuna ladha ya maisha.
Hapa nina maumivu makali.
Hivi inawezekana mtu ukashindwa kabisa kumpenda mtu ambaye alikuwa bila yeye maisha hayana maana?

Hali kama hii huwakuta wanandoa wengi na watu wengi walio katika mahusiano; haijalishi ni miaka mingapi au mlikuwa mnapendana kiasi gani na bila kujifahamu vizuri na kutumia busara na hekima kumaliza hili tatizo ndoa au mahusiano huweza kujikuta yameangukia kwenye shimo lefu mno.

Kila ndoa ina positive na negative moments, mwanandoa mmoja akiwa anamwangalia mwenzake kwa negatives tu itafika mahali ataanza kuji – withdraw na kujiweka mbali na automatically ataanza kujisahau kuwa caring. Wakati mmoja anajiweka mbali na mwenzake huyu mwingine huanza ku-panic na kuanza kutoa lawama kwamba hupendwi. Wanavyozidi kusuguana ndivyo wanazidi kusababisha mafuriko ya lawama emotionally na matokeo ni kuwa disconnected katika emotions na feelings.
Guess what?
Moto huo hautazimika!

Kuna bwana mmoja anaitwa Gottman yeye na rafiki zake walifanya utafiti kuhusiana na positives na negatives kwenye suala la ndoa na mahusiano na kutoa jumuisho kwamba quality ya emotions ilizonazo kwa mwenzi wako ni muhimu sana.
Ni simple lakini muhimu sana katika mahusiano.

Kama positives zitakuwa nyingi kuliko negatives unavyomchukulia mwenzi wako basi mahusiano yatakuwa bora sana, haleluya Kubwa!
Na kama negatives zitakuwa nyingi kuliko positives katika hisia kwa mwenzi wako basi shughuli nzito inakuja mbele yenu!

Ukweli ni kwamba negatives moja huhitaji positive tano ili kufanya balance ya ndoa au mahusiano kuwa katika hali nzuri (feelings).
Hii ina maana ukimbomoa mwenzi wako mara moja basi inabidi umjenge mara tano zaidi ili ku- balance ule uharibifu umefanya mara moja.
Kila negative moja unahitaji positive tano ili emotions na feelings za mapenzi yenu kurudi kuwa katika hali ya kawaida.

2 comments:

Anonymous said...

shalom kaka,

hapo chanzo kama wanandoa hawaombi ndo matokeo yake , tena si maombi tu ya kukubabaisha unanielewa kaka, yale ya kukumbatia ndio yanayoweka ndoa iwe imara na upendo wakati wote. vinginevyo kazi ipo.Yesu tusaidie

Lazarus Mbilinyi said...

Upo sasa mpendwa,

Maombi nia msingi wa wanandoa kuimarisha feelings zao na kuwa connected, kwani kuomba pamoja hasa kwa kukumbatiana huleta matokeo ya ajabu mno.

Ubarikiwe na Bwana.

Upendo daima