"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, June 17, 2009

Utafanyeje!

Unamka asubuhi unakuta mwenzi wako kamwagilia mashuka kwa mikojo utafanyeje?Fikiria umekuwa na ndoto za kupata mwenzi na umefanikiwa na ile kuanza kuishi pamoja katika ndoa unakuja kugundua kwamba mwenzako ni kikojozi.
Utafanyeje?

Ukweli inabidi umkubali na zaidi umpende kwa kiwango cha juu kuliko wakati wowote na kumpa uhakika kwamba wewe ndiye mtu sahihi ambaye unaweza kumchukulia na kuishi naye katika huo udhaifu alionao kwani hata yeye hafanyi kwa kutaka au kupenda au makusudi imekuwa hivyo.

Je, kikojozi ni nani?
Kikojozi ni mtu ambaye akiwa amelala huweza kutoa mkojo bila yeye kujua inaweza kuwa usiku au mchana pia anaweza kuwa mtoto au mtu mzima, lakini hapa tunazungumzia mtu mzima au mwenzi wako.
Kitu cha msingi ni kwamba hakuna anayependa kuwa kikojozi kwani hiki kitendo hufanyika bila hiari au kupenda (involuntary).

Mara nyingi ukitamka neno kikojozi wengi huhusisha watoto hata hivyo wapo watu wazima (kwenye ndoa pia) ambao ni vikojozi.
Pia ifahamike kwamba kuwa kikojozi si tatizo serious la kimatibabu bali huwa ngumu kuishi kama kikojozi wewe mwenyewe na pia yule au wale unaishi nao.

Je, kuwa kikojozi husababishwa na nini?
Kuna evidence kwamba tabia ya kuwa kikojozi unaweza kurithi kutoka kwa wazazi mojawapo, kama una wazazi ambao mmoja alikuwa au ni kikojozi basi una asilimia 77 za kuwa kikojozi.
Pia vikojozi wengi wanaonekana wana kiwango kidogo cha homoni ya ADH (antidiuretic) ambayo husaidia figo kuzalisha kiasi kidogo sana cha mkojo usiku na hupelekea mtu kulala usingizi bila kusumbuliwa na mkojo.
Pia imajulikana kwamba vikojozi wengi ni wanaume
(Huu utafiti una walakini maana hautoi sababu ni zipi hata hivyo uzoefu unaonesha kwamba watoto wa kiume huchelewa sana kuacha kukojoa vitandani ukilinganisha na wenzao wa kike)

Kuwa na kibofu kidogo kiutendaji ni sababu mojawapo ya mtu mzima kuwa kikojozi. Kabla taarifa haijafika kwenye ubongo kibofu kinakuwa kimeshafanya vitu vyake.
Misuli ya kibofu hushndiwa kushika mkojo kabla ya kuamriwa na ubongo.

Pia kuutwika (pombe) huweza kusababisha kalowanisha mashuka kwani mipombe husaidia kuzalisha kiwango kikubwa cha mkojo pia kupunguza utendaji wa misuli ya kibofu.
Pia kisukari, maambukizi kwenye kibofu, matatizo ya maumbile ya kibofu, cancer ya kibofu nk huweza kusababisha mtu mzima kuwa kikojozi.

Jinsi ya kuthibiti kuwa kikojozi
Kupunguza kiwango cha vimiminika hasa baada ya mchana na usiku kabla ya kwenda kulala.
Hii haina maana kwamba usinywe maji au juisi kwani kunywa maji ni muhimu sana kwa afya, jambo la msingi ni timing ya wakati gani unywe na wakati gani usinywe.

Mazoezi ya kibofu kwa kunywa kiwango kikubwa cha vimiminika na kupunguza baada ya masaa 2 – 3.
Kutumia alarm kuamshwa hizi ni pamoja na zile zinazofungwa kwenye nguo ya ndani na ikianza kulowa tu lazima utaamka maana itakutetemesha na kukupigia kelele.
Kuamshana na yule unalala naye au ishi naye.
Na zaidi kutumia cover kitandani ambalo halilowanishi godoro.
Na mwisho muombee kwani kwa Mungu hakuna lisilowezekana

1 comment:

Anonymous said...

Hi brother, Hii ni msg nzuri sana ila hapa umenena vema (Na mwisho muombee kwani kwa Mungu hakuna lisilowezekana) http://www.mwakasege.org/mafundisho/jina-la-Yesu/uweza-5.htm mbarikiwe sana.
Msafiri