"Marriage is our last, best chance to grow up."

Friday, June 12, 2009

Wakufanana Naye!

Tafiti nyingi zinafanana na zinakubali kwamba ndoa nyingi imara ni zile ambazo mke na mume huwa na sifa nyingi zinazofanana.
Kundi la watafiti lilikusanya ndoa 35 (wanawake na wanaume 70) ambazo ziliwekwa katika makundi matatu kundi la kwanza lilikuwa la wale ambao ndoa zako zilikuwa za furaha, kundi la pili zile zilikuwa ni zile wanandoa walikuwa na wakati mgumu kuishi pamoja na kundi la tatu la wale walikuwa njiani kuachana.

Majibu yalikuwa ni kwamba wale walioishi kwa furaha walifanana sana katika mambo mengi (general activities), walikuwa marafiki na walifanana katika kujihusisha binafsi na mwenzake.
Wale ambao hawakuwa na furaha kuishi pamoja hawakufanana katika utendaji wa mambo yao kila siku, pia hawakufanana linapokuja suala la mwitikio wa hisia zao.
Wale waliokuwa wanataka kuachana kila mmoja alikuwa na sifa nyingi zisizofanana kabisa.

Kiwango cha furaha katika ndoa huweza kujieleza kutokana na kufanana kwa wanandoa katika sifa binafsi walizonazo.
Hii ina maana wanandoa wakifanana kiuchumi, tabia, mazingira, tamaduni, matumizi ya pesa, kiwango cha energy, uwezo wa kuongea na kusikiliza, kiimani, kihisia nk inakuwa rahisi kila mmoja kutegemea nini kutoka kwa mwenzake.

Hivyo ukitaka kuwa na ndoa imara ni muhimu kuwa na balance account ambayo kufanana ni zaidi ya tofauti kwa sbabu kila tofauti iliyopo inahitaji kupatanisha na kuweka kuikubali hata kwa maumivu.

BWANA Mungu akasema,
Si vema huyu mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.
Mwanzo 2:18

2 comments:

Anonymous said...

nashukuru sana mwandishi wa mada hii mm ninapendakukuliza sasa kama mtu tayari umeshaoana na mtu msiyefanana ktk mambo mengi tufanye nini? maana unatamani hata bora ukae peke yako bila mke eu mume yaani unaishi maisha ambayo hayana raha kabisa naomba nisaidie katika hili yaani nimechoka.

Lazarus Mbilinyi said...

Kama umeoana na mtu ambaye baada ya kuanza kuishi mnajikuta mnatofautiana sana katika mambo mengi kitu cha kufanya ni kusherehekea hizo tofauti na kuzikubali hata kama ni mbaya kiasi gani kwani tofauti zipo na zitakuwepo na jambo la msingi ni kuzikubali na kuweka mkazo katika mambo mazuri ambayo anaweza kufanya na si katika mambo mabaya (positive Vs Negative.
Naamini umenishangaa kwa kile nimekisema hapo juu ila ndo hivyo, kwani wakati mnaoana mlivutiana kwa kitu gani? na hizo sifa zimeishia wapi kama si ninyi wenyewe mmeamua kufocus kwenye negative na kuacha positives?

Kama hujanielewa kabisa wasliana nami kwa simu 0767 03 44 41